Search This Blog

Wednesday, June 20, 2012

PAMOJA NA KUONEKANA NA MAJIVUNO: CRISTIANO RONALDO AAMUA KUOKOA MAISHA YA MTOTO WA MIAKA 9 KUMLIPIA MATIBABU YA KANSA

Nuhazet, mtoto wa miaka 9 kutoka Las Palmas, Spain, amekuwa akipambana na kansa tangu alipokuwa na mwaka mmoja. Alipokutana na Cristiano Ronaldo kabla ya mechi ya mwisho ya Real Madrid msimu uliopita mwezi May 2012,  ndoto yake ya kuonana na mchezaji huyo ilitimia na kwa mujibu wake baada ya kumuona Ronaldo alikuwa yupo radhi ya kufa baada ya kuvumilia mateso ya ugonjwa huo tangu udogo wake, lakini mungu si Athumani kukutana kwake na Cristiano kumeanzisha upya mapambano ya kutibiwa kwa ugonjwa wake kwa usaidizi wa Ronaldo pamoja na wakala wake Jorge Mendes.

Stori iliyoandikwa na Canaris Investiga reports kwamba mwezi Machi, MRI ilitoa taarifa kwamba kansa ya Nuhazet imeshambaa kwenye sehemu tatu kutoka kwenye sehemu ya fuvu mpaka kwenye uti wa mgongo. Madakatari waliwaambia wazazi wake kwamba hakuna kinachoweza kufanyika na wakawashauri waache kupoteza fedha kwenye matibabu kwa maana matibabu hayo yanamuumiza mtoto kuliko inavyobidi. Wazazi waliuliza kama kuna kitu chochote wanachoweza kufanya popte pale duniani ambacho kingeweza kumsaidia Nuhazet, lakini waliambiwa matibabu pekee yaliyobakia yatakuwa ni majaribio.

Hivyo kutimiza moja ya ndoto ya Nuhazet, binamu akaanza kuwatafuta moja ya marafiki wazito na mmoja wao alikuwa ni Jorge Mendes, moja ya mawakala wenye nguvu kwenye soka. Wakandaa trip ya familia kutoka katika visiwa vya Canary mpaka Madrid kwa ajili ya kuangalia mechi ya mwisho ya Real Madrid kwa msimu uliopita dhidi ya Mallorca.

Siku ya mchezo, Mendes na familia wakamfanyia suprise Nuhazet kwa kumkutanisha  na Ronaldo, ambaye walitaniana na wakapiga picha za pamoja kabla ya kumuhaidi mtoto huyo kwamba ikiwa atafunga goli siku hiyo basi litakuwa ni kwa ajili ya Nuhazet . Baada ya kukutana, Nuhazet alienda kuangalia mechi akiwa kwenye sehemu maalum ya kukaa wageni wa Ronaldo  akiwemo mchumba wa Ronaldo, Irina Shayk.

Real Madrid walifunga Mallorca 4-1 na kubeba kombe la La Liga kwa mara ya kwanza ndani ya miaka minne. Ronaldo alifunga goli la kwanza la mchezo huo ambalo alilitoa kwa ajili ya mtoto huyo kama alivyomuahidi. Siku iliyofuatia Mendes akiwa na Raisi wa Real Madrid Florentino Perez, ambaye wiki kadhaa baadae alimpoteza mkewe aliyekuwa akiumwa kansa ya mapafu, waliwaita madaktari wa Sanchinarro Hospital. Kwa haraka wakamchukua Nuhazet na kuanza matibabu mapya ambayo yalijumuisha madawa maalum kutoka Marekani huku Ronaldo na Mendes wakilipa kitu.

Stori hii imekuja siku chache baada Lionel Messi kuripotiwa kuamua kulipiwa huduma za matibabu ya mtoto wa miaka 12 Walees Kashash, ambaye anaugua ugonjwa wa upungufu wa homoni za ukuaji (ugonjwa ambao Messi aliugua alipokuwa mdogo),  mpaka atakapofikisha miaka 18. Taarifa hizo baadae zimekuja kugundulika kuwa sio za ukweli, lakini Messi tayari alishaonekana kwa mapana kama binadamu mwenye huruma na roho nzuri sana. Kwa kijana  anayeonekana  mwenye majivuno na mbinafsi kama Cristiano Ronaldo  ambaye tayari ni baba wa mtoto wa miaka miwili - jambp hili alilofanya ni jema sana na linaondoa taswira mbaya iliyojengeka miongoni mwa watu.

Wengine wanaweza kusema ni katika kutaka kujitafutia sifa na kumfanya Ronaldo apendwe, lakini jambo muhimu ni kwamba Nuhazet bado anaendelea na matibabu na anaweza kurudi nyumbani wiki kadhaa zijazo ataanza stage nyingine ya matibabu. Na yote yamefanyika kwa sababu ya soka.

Football is powerful

No comments:

Post a Comment