Search This Blog

Tuesday, June 19, 2012

KENYA YAMTIMUA KOCHA WA TIMU YA TAIFA FRANCIS KIMANZI

Makocha wanaajiriwa ili kufukuzwa (Coaches are hired to be fired)


Wiki kadhaa baada ya Tanzania kumfukuza kazi aliyekuwa kocha wa timu wa timu ya taifa Jan Poulsen na kumpa kazi aliyekuwa kocha wa timu ya vijana Kim Poulsen, leo majirani zetu Kenya nao wamefuata mfano wa Tanzania baada ya kumfukuza kazi Francis Kimazi na benchi lote la ufundi la timu ya taifa ya nchi hiyo Harembee Stars.

Katika jitihada za kujiokoa, shirikisho la nchi hiyo ambalo limekuwa kwenye presha kubwa kutoka wapenzi wa soka wa nchi hiyo waliotaka mabadiliko kwenye timu kufuatiwa kuwa na mfululizo wa matokeo mabaya kwenye michuano ya kufuzu African Cup of Nations na Kombe la Dunia.

Kimanzi alikuta barua ya kufukuzwa kazi inamsubiri muda mchache baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta akitokea Togo, alipoenda kuiongoza Harembee Stars kucheza dhidi ya Togo na kufungwa kwa bao 1-0, hivyo kupelekea timu hiyo kupoteza matumaini ya kucheza michuano ya African Cup of Nations in 2013.

Mbadiliko hayo yamehitimisha utawala wa Kimanzi ambaye aliingia Harembee tangu November 1, 2011, akichukua nafasi ya Zedekiah Otieno Zico.


Lakini katika makubaliano ya kusitisha kibarua chake, Kimanzi amakubaliana na KFF kwamba atashushwa cheo na kuwa mkurugenzi wa ufundi huku nafasi ya ukocha kwa sasa ikiwa ipo wazi.

No comments:

Post a Comment