Search This Blog

Tuesday, June 19, 2012

ENGLAND VS UKRAINE: MECHI YA KWANZA YA ROONEY - NA INAWEZA IKAWA YA MWISHO KWA SHEVCHENKO



Wayne Rooney atarudi kwenye kikosi cha England leo usiku baada ya kumaliza adhabu yake ya kusimamishwa mechi mbili . Anategemewa kucheza sambamba na mchezaji mwenzake wa Man United Danny Welbeck, ingawa Andy Carroll pia anaweza akaanza baada ya kucheza vizuri dhidi ya Sweden.

Theo Walcott, pamoja na kuondoka mazoezini Jumapili akiwa na majeruhi kidogo ya misuli ya nyuma ya paja, lakini anaweza kaanza leo baada kuanya vizuri baada ya kuingia kwenye mchezo dhidi ya Sweden. Winga huyo wa Arsenal, ikiwa atachaguliwa anategemewa kumbadili James Milner, huku England wakitumia mfumo wa 4-2-3-1, lakini pia Milner anaweza kurudi kwenye upande wa kushoto kumbadili Ashley Young ambaye bado hajaonyesha kiwango kikubwa mpaka sasa  kwenye michuano hii.

Andry Shevchenko ni mtu ambaye ana mashaka makubwa kucheza kutokana na majeruhi ya goti lakini bado anapewa ya kucheza ikiwa atapasi vipimo vya afya katika mechi ambayo Ukraine inabidi washinde ili kusonga mbele. Ikiwa hatoweza kucheza, Oleg Blokhin anategemewa kumbadili na Artem Milevskiy au Marko Devic kucheza pamoja na Andriy Veronin.

Blokhin amechezesha safu ya ulinzi na kiungo ile ile katika michezo miwili ya kwanza, huku Antoliy Tymoshchuk akiulinda ukuta wa nyuma huku Serhiy Nazarenko, Yevhen Konoplyanka na Andriy Yarmolenko wakisaidia mashambulizi na washambuliaji.

JE WAJUA

England na Ukraine wamekutana mara mbili katika mechi za mashindano, huku kila timu ikishinda mechi moja walipokutana kwenye michuano ya kufuzu kombe la dunia 2006.

Pia timu hizi zimeshakutana mara mbili kwenye mechi za kirafiki, huku England wakishinda mechi zote mbili, wakifunga mabao 5 na kuruhusu moja.

Andy Carroll alifunga dhidi Sweden lakini pia alikuwa na asilimia chache ya pasi zilizokamilika kuliko mchezaji yoyote wa England. Carroll alimaliza mchezo wote akiwa kapiga pasi 19 tu katik ya 41 alizojaribu.

England wanahitaji japo sare tu kuweza kufuzu kwa robo fainali, lakini wanahitaji kuyazidi matokeo ya France dhidi ya Sweden ili kuweza kuwa viongozi wa group. Timu zote mbili zina pointi sawa lakini England wamezidiwa kwa goli moja na France.

Ukraine watakuwa timu mwenyeji ya tano kutoka kwenye hatua ya makundi tangu  michuano hiyo ilipoanza kushirikisha timu 16 mwaka 1996, ikiwa watashindwa kuwafunga England.

Mchezo wa Jumanne unaweza ukawa wa mwisho wa Andriy Shevchenko kuichezea nchi yake. Mpaka sasa yeye ndiye mfungaji bora wa muda wote wa nchi hiyo akiwa tayari ameshafunga mabao 48 katika mechi 110.

Ukraine watacheza mara mbili na England kwenye michuano ya kufuzu kombe la dunia nchini Brazil 2014.

No comments:

Post a Comment