Search This Blog

Tuesday, June 19, 2012

HILI NDILO TAMKO LANGU RASMI JUU YA TUHUMA ZILIZOELEKEZWA KWANGU NA MZEE IBRAHIM AKILIMALI!

Siku ya Jumatatu, tarehe 18, June, 2012, majira ya mchana, Katibu wa Baraza la Wazee wa klabu ya Yanga aliitisha mkutano wa waandishi wa habari kwenye makao makuu ya klabu bingwa ya Afrika Mashariki na Kati yaliyopo eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam.

 Katika mkutano wake huo na waandishi wa habari jana Mzee Ibrahim Akilimali aliongelea mambo mengi yanayoihusu Yanga lakini pia aliniongelea mimi Shaffih Dauda. Akiwa na akili timamu na nina uhakika bila kulazimishwa na mtu, Mzee Akilimali alinitupia shutuma nzito ambazo nadiriki kuziita za uongo ambazo kwa kweli zinaweza au zimeshafanikiwa kuharibu jina langu kama mwandishi wa habari pia kama binadamu wa kawaida tu.

Hivyo kuniharibia sifa yangu nzuri ambayo nimejijengea kwa kutumia nguvu kuifanya vizuri kazi yangu. Mzee Akilimali alinukuliwa akisema kwamba mimi (Shaffih Dauda) nimekuwa ndio kikwazo cha ujio wa kocha wa kimataifa wa Brazil, Marcio Maximo kuja kuifundisha klabu ya Yanga. Aliendelea kusema kwamba mimi nimekuwa na mawasiliano na Maximo nikimwambia mambo mengi ya uongo kuhusu Yanga ili niweze kutimiza lengo langu la kumuona kocha huyo asije kuifundisha Yanga.

Allinukuliwa akisema kwamba nimekuwa nikimtumia ujumbe mfupi wa simu, barua pepe na kumpigia simu Marcio Maximo nikimwambia asije Yanga kwa kuwa timu hiyo ni maskini na wana madeni hivyo asijaribu kuja Yanga. Katibu huyo wa Baraza la Wazee la Yanga aliendelea kusema kwamba Maximo amewatumia ujumbe akiwaambia mimi namsumbua sana juu ya suala hilo hivyo sasa anaogopa mpaka kupokea simu za Tanzania kwa ajili ya usumbufu wangu Shaffih Dauda. Kiukweli hizi ni tuhuma nzito na chafu dhidi yangu, kamwe siwezi kukaa kimya na kuliacha hili lipite hivi hivi, hivyo nimeona bora nilitolee majibu.

Tuhuma za Mzee Akilimali sio tu zinaweza kunichafua bali pia zinanigombanisha na mamilioni ya wapenzi na wanachama ya klabu Yanga pamoja na wapenzi wote wenye kupenda maendeleo ya mchezo wa soka hapa nchini. Binafsi pamoja na wana sports xtra wenzangu tumekuwa mstari wa mbele kupigania maendeleo ya michezo hapa nchini hususani mchezo wa soka, ujio wa Marcio Maximo hapa nchini kuja kuifundisha Yanga naamini ungeweza kuisaidia klabu iyo pamoja na nchi kwa ujumla,sasa iweje nimzuie kuja nchini kufanya jambo la maendeleo kama hilo ?

Pia tuhuma hizi zinaweza kuniharibia kazi yangu kupitia vipindi vya michezo vya Sports Extra na Sports Bar ambavyo siku zote kwa pamoja na wenzangu tumekuwa tukifanya kazi ya kuhabarisha pamoja na kutoa mawazo yetu kuhakikisha soka na michezo kwa ujumla inapiga hatua kuelekea mbele. Mwisho baada ya kusema yote hayo nimefikia uamuzi wa kumpa siku saba (7) Mzee Akilimali kutoa ushahidi au vielelezo vya shutuma alizonitupia alivyodai anavyo ili kuweza kuthibitisha madai yake dhidi yangu,na kama akishindwa basi itabidi aitishe tena mkutano wa waandishi wa habari kama alivyofanya wakati akitoa tuhuma zake dhidi yangu na akanushe aliyoyasema na kuniomba radhi la sivyo sheria itachukua mkondo wake. Huu ndo ushahidi wa alichokizungumza mzee wangu Akilimali.

53 comments:

  1. Kaka ntafurahi sana kama utamshtaki uyu mzee baada ya izo siku7 mana sio siri KAKUPA TUHUMA NZITO sanaaa tena toka kwa club yenye wapenz wengi..sio siri prove it wrong..jisafishe kaka.PIA ntashangaa sana afta izo siku7 ukikaa KIMYA!,izo tuhuma nzito braza tek zem serious!..do smthng i mean MPELEKE MAHAKAMANI BILA KUSITA AFTA 7DAYS akikaa kimya.:
    mkufunzjr.

    ReplyDelete
  2. Shaffih hata kama aliichoongea mzee akilimali hakina ukweli,wewe ulishajihariibia siku nyingi sio tu kwa yanga bali wapenda soka wengi,umekuwa kwa kujua au kutokujua ukitumiwa kwa mambo ya binafsi kama kujifanya wewe ndio kamati ya ligi,nidhamu na msemaji wa TFF,kwangu wewe sio mhandishi,ni shabiki uliyepata nafasi ya kuwa mrusha maoni yako

    ReplyDelete
  3. kaka lazima huyu mzee alipe fidia tena ya maana,, si anazo milioni 750. usimwache kabisa tuone hao wanao mtumia kama watamsaidia mzee huyu mlopokaji,! ukiwa mjinga shida sana ye aliona raha sana kulopoka tu mbele ya mic

    ReplyDelete
  4. huyu mzee hana akili kabsaaaa hawezi tamka hayo maneno kwenye vyombo vya habari..ni kweli kabsaa ameharibu jina lako pia kuleta uadui kati ya wanachama wa yanga,na nafikiri kwa wanachama wenye uelewa wa kazi yako hawawezi kukutia lawamani...na yeye ni nani ktk yanga kuna watu wanamtuma yule mzee..kaka mpe hizo 7days akishindwa mpeleke mahakamani ye si ana Tsh mil 750 bwaaana..kwanza hazipatee wapii
    Mdau Oslo Norway

    ReplyDelete
  5. Kaka huyu mzee kafanya kitu kibaya sana kwanza anajua jinsi gani nchi yetu inavyopenda soka anaweza kukuhatarishia maisha yako ukashindwa hata kutembea mitaani kwa jinsi alivyoropoka watu wanaweza kukufanyia chuki, inabidi tu akuombe radhi tena kupitia vyombo vya habari vyote nchini kwenye tv,radio, na magazeti

    ReplyDelete
  6. Huyu mzee ni mlopokaji sawa lakini na wewe Daudi level yako ya uchambuzi ni duni sana! Kama huamini endelea na style hiyo hiyo matokeao utayaona. Kwa nn ushambuliwe wewe kuna waandishi wa michezo wangapi nchi hii mbona wasiambiwe maneno haya wengine. Something is wrong somewhere in your job bro.

    ReplyDelete
    Replies
    1. ukiona anatajwa yy sana ujue ndo yuko juu zaid ya hao wengine kwahyo wanatafta sababu za kumuangushA na hawatofanikiwa....nothing wrong to him though no one is perfect,hiz ftna zote zimeanza kisa alienda ujeruman mwandish peke ake tanzania nzima watu mawivu yamewajaaa na watakufa nayo.shafih we got ur back wembe ni uleule na badoooooo

      Delete
  7. Kaka,uyo mzee hajakutendea haki,binafs nimeshtushwa na hzo habari,lakin kaka kama ulvyohaidi..aspofanya mburuze mahakaman.pole mana ni changamoto za kazi lakin usilfumbie macho. By fardhil muhala.

    ReplyDelete
  8. Uamuzi uliouchukua huenda ukawa sahihi.Vilevile naomba ufahamu kuwa hakuna binadamu anayeweza kuishi hapa duniani na akakosa tuhuma ziwe za kweli ama vinginevyo.Huenda umemua kuchukua uamuzi huo kutokana na aina na uzito wa tuhuma yenyewe.Mimi ninashaka kwamba hata kama uamuzi wako utaleta majibu chanya kwako,bado baadaye zitazuka tena tuhuma nyingine za aina hii,hii inatokana na aina ya kazi unayoifanya na namna unavyoifanya.Siku zote ukweli hujitenga na uongo,kama maneno ya huyo mzee ni uongo hayawezi kukuchafua hata siku moja(kamwe).Frankly speaking the only problem with you is bias on your mind.i.e.Favouring the the tradional rivals of Young Africans in several issues.I am sure no body will react negatively against you, if you abandon bias on your works(presentations,analysis and reports).Most of Young Africans fans are not trusting you any more,therefore even if you have contributed a positive idea they dont accept it.To me your first enemy is your mind(thinking and reasoning) featuring your mouth(speeches/words) as well as your hand(writings).It is like colonialists,"You are sowing the seeds for your own destruction".Pole sana ka mkubwa.Malele,DUCE.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Namuunga mkono huyu jamaa. Yanga fans hawataweza ku appreciate chochote utakachosema kuhusu Yanga kwa sababu uchambuzi wako mwingi unaishambulia sana Yanga na kuisifia Simba. In fact, this is common to most Clouds FM presenters wa Sports programmes. Iam sure mashabiki wa Yanga did not like kejeli za jana (19-06-2012) za presenters wa Jahazi wakati wa "michapo ya michezo". Zilikuwa comments za washabiki not wandishi wa habari ambao wanatakiwa kuwa neutral. Kuhusu tuhuma zilizotolewa na Mzee Akilimali, I doubt kama ana ushahidi wowote.

      Delete
  9. siku saba nyingi huyu mzee ni kmfungulia mashataka moja kwa moja ajibu tuhuma.baadala ya kushindwa kumleta maximo sasa wanatafutwa mchawi wa kumuangushia mzigo.hana jipya akalee wajukuu zake.kaniudhi sana akili matope.

    H.sato

    ReplyDelete
  10. hata kuongea hilo zee halijui had jina la shafih kaandikiwa kwenye karatas...matapish uliyotapika lazma uyale tena hayo utajutaaaa.

    ReplyDelete
  11. kaka Shaffih,
    Ushauri wangu umfungulie mashtaka huyu mzee Akilimali na akulipe fidia.
    Hata kama itakuwa ndogo iwe ni fundisho kwa wengine. Haiwezekani kitendo kama hichi cha kudhalalisha kikafumbiwa macho.

    ReplyDelete
  12. Sisimami upande wa Mzee Akilimali wala mashabiki wa yanga au wako wewe Dauda, lakini hilo unaloliita TAMKO lako hapo juu linamapungufu mengi sana na baada ya watu kulisoma tu na kutafakari huwenda wengine wakaanza kumuamini huyu mzee juu ya shutuma anazokutupia, amabapo huyu mzee amekushutumu kuwa wewe unawasiliana na Maximo kwa simu, msg na email na kumwambia kuwa asije Tanzania kuifundisha Yanga maana ni masikini. Hivyo mimi nilitegemea kwanza katika hilo tamko lako ukili kutokufanya/kufanya hivyo (kama madai ya huyo mzee yanavyosema)kabla ya wewe pia kumtupia lawama huyo mzee kuwa anakusingizia na kukuchafua. Sasa sisi upande wa tatu tutajua nani mkweli kama mtupiwa lawama hajakili ukweli/uongo wa hizo lawama na badala yake na yeye natupia lawama upande wa mwenzake.
    THIBITIA au KANUSHA kabla ya kushutumu na kulaumu!

    Yangu ni hayo,
    Kazi njema na Blog yako idumu daima na daima!

    ReplyDelete
  13. mzee alinifurahisha alivyotamka neno e mail.

    ReplyDelete
    Replies
    1. haHAHAHAHHAHAHA Hata mimi alinichekesha sana!

      Delete
  14. LAZIMA UKUBALI KAKA SHAFII KUWA UANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO HUKUANZA LEO. WEWE ULIELETA CHACHU YA MICHEZO KTK CLOUDS RADIO NA BAADAE CLOUDS TV. HAKUNA ANAEKATAA KUWA WEWE UNAKIPAJI CHA UCHAMBUZI NA WENGI WAMEIGA STAILI YAKO. TULIKUPENDA, NA ULIWANIKIWA KUCHOTA MASHABIKI LUKUKI KATIKA TASNIA YA HABARI ZA MICHEZO. TULIKUWA TUKIISHI VIJINI TULISIKILIZA RTD NA RADIO ONE SI KAMA TULIPENDA KUSIKIZA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA HUKO BALI TULIKOSA UTAMU NA KUSHINDWA KUIKAMATA CLOUDS RADIO. NILIPO KIDATO CHA TANO PALE AZANIA NDIPO NILIPOANZA KUONA NA KUSIKIA KITU NYETI CHA KIMICHEZO KUTOKAA KWAKO. NAVIKUMBA VIONJO MBALIMBALI VINAPIGWA KUASHIRIA MDA WA HABARI MICHEZO. KWELI VILINISISIMUA. NAVIKUMBUKA SANA NA NATAMANI NIKUIMBIE VILIVYO TAMBA TANGU 2003 HADI SASA.WEWE NI GWIJI WA HABARI ZA MICHEZO.
    LAKINI KAKA YANGU KUNA TATIZO LA BAADHI YA WATU WANAOTAKA KUKUCHAFULIA HAIBA NA MAPENZI KWA WATU. SIO SIRI SHAFII MWANZO ULIKUWA MTAIFA , MZALENDO WA TAIFA LAKO HASA KATIKA MICHEZO. ULIKUA ZITO KABWE KATIKA MICHEZO
    LAKINI SASA UMEKUWA MZALENDO WA SIMBA. SIKUZOTE UNARUHUSU KIPISI CHA SIGARA KUWAKA HATIMA YAKE NYUMBA HUUNGUA. ULIWARUHUSU SANA VIONGOZI WA SIMBA KUKUTUMIA NA UKASHINDWA KUTAMBUA VILABU VYETU VYA SIMBA NA YANGA NI FITNA SANAAAA. UKIRUHUSU KUVIHUDUMIA UMERUHU SU KUCHAFULIWA. HAKUNA ANAE KATAA KUWA RAGE ATAZIKOSAA KURA NYINGI ZA WANA YANGA TABORA PINDI AKITHUBUTU KUGOMBEA TENA UBUNGE. HII NDO FITNA YA TANZANIA. ACHA WATU WAKUHISI TU LAKINI USITHUBUTU KUJICHANGANYA. HIVI UNAJUA ZITO KABWE NI SMBA MBOWE NI YANGA, LIPUMBA NI YANGA, LAKINI WANASOMA ALAMA ZA NYAKATI. LINI ULISIKIA WATU HAWA WAKITUMA ANGALAU UJUMBE MDOGO WA KUITAKIA SIMBA AU YANGA USHINDI PINDI WANAPOCHEZA. UTAWAONA WAKISHIRIKI LABDA KWENYE TIMU ZA TAIFA. WANAJUA HALI ZA VILABU VYETU AKUJIPELEKA KWAO KIDOGO WATAKUTUMIA MPAKA LIHARIBIKE JINA LAKO KWA WATANZANIA. MAMBO HAYA WACHIE WENYEWE KINA MKAMIA, AMOSI MAKALA, RIDHIWANI KIKWETE. WAPOTEZE MAPENZI KWA WATANZANIA WOTE KWA KUENDEKEZA USIMBA NA UYANGA. KWELI KAKA MZEE AKILI MALI AMEONGEA KITU KISICHO NA BUSARA ILA MZEE YULE HAKUZALIWA LEO NA WALA WEWE HUKUANZA UANDISHI WA HABARI LEO. LAZIMA KUNA KITU KILICHOMSUKUMA KUSEMA VILE. NI KWELI KAKA UMETEZA MAPENZI KWA KIASI KIKUBWA KWA WANAYANGA. MZEE AKILI MALI NA KICHAKA TU WANAYANGA WANAJIFICHA PALE, YEYE NI MSEMAJI TU, WALIO PELEKA HABARI HIZO NI VIJANA WAO NA WAPENZ WAZURI WA CLOUDS RADIO. USISHABIKIE HIZI MESEJI ZA ZINAZO KUUNGA MKONO HAWA NI WAZANDIKI WANAFIKI WANAKUUNGA MKONO KWA KUWA MTUHUMIWA NI KIONGOZI WA YANGA. KUMBUKA YA NDIMBO ALIPOAMUA KUWA SIMBA MOJA KWA MOJA LEO YUKO WAPI? ACHANA NAE LUIS SANDEU ALIACHA TBC NA KWENDA YANGA NAE KITAMKUTA MUDA SI MREFU. USHABIKI HAUKATAZWI KAKA ILA WEWE UMEZIDISHA HATMA YAKE UNAPOTEZA MASHABIKI WAKO KWA KUENDEKEZA SIMBA ILIYOMSHINDA BAHARESA NA KUUNDA TIMU YAKE YA AZAM. MM BINAFSI NIMEHAMIA CAPITAL RADIO TANGIA NILIPOANZA KUSIKA KASHFA ZAKO ILA SITAACHA KUTEMBELEA BLOG YAKO KILASIKU HATA KAMA UTAKA NILIPIE NISINGE AMA. BADILIKA KAKA WEWE NI WETU WOTE. KABURU NA RAGE HAWATA KUPELEKA POPOTE. WENYEWE WANAKUPENDA SASA KUTOKANA UMAHIRI WAKO WA HABARI ZA MICHEZO. KAMA WANGEKUWA NA SHIDA WEWE KWA NINI WAKUNG'ANG'ANIE SASA. HESHIMU KAZI YAKO KAKA. MZEE AKILI MALI SI MWENDA WAZIMU ANA AKILI TIMAMU. NA JUA ANACHO KISEMA. KAMA NI MROPOKAJI KWA NINI AROPOKE LEO NA SI TANGU ZAMANI AU SHAFII UMEANZA KAZI LEO?

    ReplyDelete
  15. Ndio tatizo la soka ya bongo upumbafu m2pu...,na nyinyi mashabiki wa Yanga muwe mnayapima wanayoongea hao wazee wenu wa hiyo team mengine mnayashabikia wakati ni upupu na hayaendani na uzee wao,,mkimsikiliza Jaji Mkwawa jana mtanielewa namaanisha nini!!hv katika akili ya darasa la saba huyu shafii anaweza kumkataza kocha mwenye ujuzi kuifundisha team ulani???aache ajenda zake za kishabiki awaeleze wana Yanga kwanini Maximo kagoma kuja na sio kuja na weak reasons kama hiyo.

    ReplyDelete
  16. WAANDISHI WA HABARI MMEZIDI SANA ULITUMWA UMPIGIE SIMU NYOKKKOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

    ReplyDelete
    Replies
    1. matusi ya nini tena

      Delete
    2. ninachokulaumu Shafii nikuwa umesahau usemi wa kiswahili kuwa jambo unalolifahamu halikusumbui. maoni uliyotoa hapa yatakuletea matusi zaidi. Mzee nitarumbet tu. mpigaji yupo nyuma. kumbuka kuwa silika moja kubwa ya mzee ni kuaema na kutisha bila soni. alipopigwa mwamuzi mzee na aali zake walisema nini? walimsingizia nani? Suala la maximo ni kampeni halina ukweli. ili kudanganya watu itakapodhihirika kuwa maximo haji, lazima apatikane mtu aliyesababisha ili awe ndiyo adui wa Yanga.huyu usijibizane naye. Yeye na swahiba zake kama waliweza kumsingizia mtu kqa kosa la mwasyika alilotenda hadharani, kwa nini wasikufanye mchawi kwa jambo ambalo haliwezi kuthibitika? Nakushauri achana nao!!!!! ndivyo walivyo.

      Delete
  17. shaffih ni binaadamu kama binaadamu wengine na yawezekekana kabisa kukawa na mapungufu katika uchambuzi wake, kwahiyo hilo lisiwaumize kichwa kama mwajua ya kwamba hakuna mkamilifu. lakini pia isiwe sababu ya kutothamini mchango wake katika tasnia ya michezo, kwangu sioni upendeleo wa aina yeyote katika uandishi wake, na shaffih yupo karibu na watu wote wa mpira bila kujali ni wa yanga au simba au azam, ila mashabiki wasiojua nini maana ya uandishi au wameamua kujitoa fahamu, yaani hawataki kabisa kusikia kitu kinachoitwa ukweli na kuamua kucomment upuuzi, jitu kubwa kama nyumba eti linaandika mzee akilimali sio mwendaazimu mpaka aseme vile, sasa swali langu ni kwamba shaffih ni mwendaazimu alietaka uthibitisho? maaana email pamoja na sms ni vitu ambavyo vipo muda wote sasa atajiamini vipi kuomba ushahidi ikiwa hakufanya hayo mambo? washabiki wa yanga mlitakiwa muwe na mji wenu maalum wa kuishi kwani mnatia kichefuchefu kabisa!

    ReplyDelete
  18. Uadui wako na wanayanga(sio wote ni baadhi yao tena ni wale wasiotaka mabadiliko na washamba wa soka) ni kuwakosoa na wewe kuwa mkweli, watu hawa wa yanga hawataki kukosolewa kabisa sielewi wao wamekuwa akina nani, ila usikate tamaa wewe jembe na endeleza mapambano...!

    ReplyDelete
  19. Sawa kabisa Mkuu Dauda ili iwe fundisho siku nyingine waache kuropoka mambo pasipo kujua madhara yake mchukulie hatua, kama alikuwa anakuchukulia poa basi ajue si kila mtu unaweza kumropokea tu.Kama wanataka kukutoa chambo kwa kushindwa kumleta Maximo basi wajue wamegonga mwamba.
    Ila Tanzania ina mashabiki wa mpira wa ajabu sana, watu wanataka Vilabu vyao visifiwe tu hata kama wanafanya mambo ya kipuuzi, mtu akikosoa wanapiga kelele na kukuwekea bifu ukiwasifia basi wao roho zao kwatu kazi ipo kwa kweli.
    Bila kuwa na nia ya kuthihaki ila MASHABIKI WA YANGA WENGI WAO HAWANA AKILI NI MASHABIKI WAKIHUNI NA WASIOJUA MPIRA;Kama watachukia wachukie, I dont care.
    Mdau
    Mike.

    ReplyDelete
  20. Mkuu Dauda huyu mzee si wa kumtolea tamko kupitia vyombo ya habari, huyu unatakiwa umpelekee barua kupitia kwa wakili ukimpa hizo siku saba athibitishe au akusafishe na kama kweli hukufanya hicho alichokutuhumu inabidi umpe siku saba za kukusafisha na sio kuthibitisha na kama hatafanya hivyo inabidi umpeleke mahakamani kwa defamation, hii issue sio ya kuchukulia kijuujuu maana kumbuka Yanga ina washabiki wengi wapo wenye akili zao na wengine walioshikiwa akili zao hivyo wenye akili za kushikiwa wanaweza waamue lolote juu yako wakijua wewe ndo kikwazo cha Maximo kuja.

    ReplyDelete
  21. Shaffih dauda ni mwandishi wa habari? Umesomea? Una vyeti gani? Mimi siamini mwandishi wa habari anaweza kuwa biased kama Shaffih.. Mpaka anatia aibu yaani..

    ReplyDelete
  22. ww unajidanganya tu,huyo mzee nyuma yake kuna watu wazito,ss angalia usijekwenda mahakamani kushtaki ukaishia jela ww mwenyewe hapo ndipo utaamini inchi hii pesa ipo juu ya sheria

    ReplyDelete
  23. yanga msitusumbue na huyo maximo wenu c mumfuate huko huko, tatizo nyie nao ni wapuuzi wote pamoja na uongozi wenu bado mnamikataba ya kizamani ya kupigiana simu msitusumbue wapenda michezo kwanza naona hizi timu za wavaaa vikofia bora ziishe, mzee akilimali tunakueshimu sana tukomeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  24. Huyo mzee kaka chizi kabisa, wala asikupe tabu hata kidogo, wazee wa yanga wana tapatapa hawajuwi pakwenda ndio wanatafuta umaarufu tu,,,,achana na machizi we piga kazi tu.

    ReplyDelete
  25. Pole sana Dauda hilo ndio soka la Bongo nadhani hakuna sababu ya kushindana na huyu Mzee angalia mbele sio kurudi nyuma. Kwa mtazamo wangu finyu ulitakiwa kukanusha tu sio kufikishana mpaka Lupango. Elewa Mzee (Yanga) bado wana shida nawe na una shida zako kwao, kwanini wanaokuweka mjini uanze kuwaharibia kumbuka kutia kitumbua chao mchaka cha kwako kitapotea kabisa. Mimi binafsi nakukubali na nathamini sana mchango wako uliotukukuka katika tasnia ya Michezo Tanzania na kwa kweli haupimiki. Chapa kazi kaka achana na Matokeo ya Kampeni za Uchaguzi za Yanga. Hilo lilikuwa deal la mtu limeharibika anatafutwa mchawi.

    Gola.
    Dodoma

    ReplyDelete
  26. SHAFII ULIJIJENGEA HESHMA KUBWA KWA WAPENDA SOKA TZ LAKINI TOKA UANZE KUTUMIA RADIO NA TV CLOUDS KUIPONDA YANGA NA KUISIFIA SIMBA UMEJISHUSHIA HADHI YAKO KAKA..
    UMESAHAU JUKUMU LAKO UKIWA NYUMA YA MIC UMEWEKA UNAZI WAKO WA SIMBA MBELE KULIKO KULIKO JUKUMU LA KAZI YAKO,,

    UMESAHAU KAMA CLOUDS NI YA WATU WOTE SIO YA SIMBA PEKE YAO...WEWE UNATAKA KUIGEUZA CLOUDS IWE YA SIMBA TU....UNAHARIBU KAKA JIREKEBISHE

    JEFF ANAONGEAGA VITU VYA MSINGI SANA LAKINI WEWE HUWA UNAJIFANYA KUMPINGA MARA KWA MARA

    ReplyDelete
  27. Hao wanaokudis wanakukubali kiaina coz wanafuatilia hadi blog yako!so wasikutishe, huwezi kuwa mwandishi wa habari za michezo kama wewe sio shabiki wa michezo.

    ReplyDelete
  28. ASSALAM ALAYKUM, KAKA NAAMINI LISEMWALO LIPO NA KAMA HALIPO LAJA! JIULIZE KWANINI WEWE NA SIYO MAESTRO,JEFF AU ABDUL? JIULIZE MARA MBILI KWANINI WAITWE WAANDISHI WA HABARI ULAUMIWE WEWE! KIUNGWANA KAKA JIANGALIE TENA HII INAONESHA WEWE YANGA ASILIMIA KUBWA HAWAKUKUBALI NA IMANI IMEJENGEKA KWAMBA WEWE UNAIKANDIA YANGA SANA!
    MIMI NI MPENZI MKUBWA WA YANGA NA MARA ZOTE NIKIWA HAPO BONGO NAKUJA TAIFA KUANGALIA GEM IWE YA SIMBA AU YANGA AU YA TAIFA, MARA ZOTE NAKAA VIP B KARIBU KABISA WANAPOSIMAMA WAANDISHI KUCHUKUA PICHA AMBAPO HATA WEWE KUNA WAKATI UNASIMAMA PALE. UPANDE HUU WA YANGA HUWA WANAKULAANI SANA HASA BAADA YA TUKIO LA KUPIGWA MWAMUZI MECHI YA AZAM NA WEWE ULIVYOKUWA UKILIELEZEA JAMBO LILE KATIKA VIPINDI VYAKO VYA MICHEZO UKIONEKANA KULIVALIA NJUGA SUALI LILE! HII IMEPELEKEA KUONEKANA RADIO YENU INAISHAMBULIA YANGA!
    KWA MAONI YANGU KUJIBU SHUTUMA SI KUTENGENEZA JINA ILA UNAONGEZA MAADUI.... KAMA MUUNGWANA AKIVUKWA NA NGUO HUCHUTAMA HAKIMBII,, SASA NA WEWE PUNGUZA MAJIBIZANO NA JICHUNGUZE ULIPOTOKA NA UNAPOKWENDA KLWANINI WEWE? THERE IS SOMETHING WRONG BRO MAY BE URE WORDS COAST SOME MEMBER'S OF YANGA ON THEIR PERSONAL INTREST!
    JIPANGE KAKA KAMA UNANIA YA KUBADILI NA KUSIMAMIA SOKA LA TANZANIA AMBALO LINA MASLAHI YA WATU WACHACHE LISONGE MBELE....AMINI UNAANZISHA VITA NA WALAFI WA PESA ZA SOKA HIVYO JIPANGE NA UAMUE KWELI KUPAMBANA!

    ReplyDelete
  29. By the way watu hatuna kumbukumbu nzuri,kuna kipindi Shaffih alituhumiwa anaiongea vibaya SIMBA na watu wakatuaminisha kuwa yeye ni YANGA nakumbuka mpaka alipost kwenye wall ya SPORTS EXTRA FB kulalamika ukigeu geu wetu,na katika kila kitu ukiogopa kuwa mkweli basi hufai ktk jamii,naamini yote yanamkuta coz ktk ukweli huwa hafichi kitu,kama ni NYEKUNDU atasema sio kutuambia RANGI YA CHUNGWA.Kiukweli YANGA inapotezwa inapopelekwa,watapata mafanikio ya mda mfupi ila machungu watakayokuja kukutana nayo sio ya kuisha leo na lazma kuna hatari ya uvunjifu wa amani utatokea mda si mrefu.kiufupi INTEREST za MANJI ktk klabu hiyo sidhani kama zina malengo mazuri,mazuri kwa wasio na werevu na kinachoendelea,sitaki kuamini viongozi wote wa YANGA walioshinda uchaguzi kwa kupitia yeye hakuna hatari waliyokua wanaiona mpaka wawe wanashindwa kuelewana nae mbeleni,werevu wa LLOYD NCHUNGA ktk sheria naamini ni mkubwa sana kuliko maelfu ya wengi hapo JANGWANI,lazma kuna hatari aiyoiona na ndio maana wakapishana na naamini ni ktk mfumo wa kibiashara 2.Back to Topic MAXIMO kuzuiwa kuja kufanya kazi YANGA hizo ni ndoto tena na mtu baki kama SHAFIH,yule ni mjasiriamali kupitia kazi yake na huwa wana sifa ya kuwa RISK taker,hata kama YANGA wangekua wanapigana anaona,wakimwekea FUNGU+MKATABA unaoeleweka lazma aje coz anajua at last wakishindwana anaorudi ktk mkataba wake kudai chake,na mwisho anawakala wake,hiyo ni moja ya maeneo MAWAKALA wanapata hela kupitia kuhamisha mteja,kama kuna maslahi atamshawishi tu kuja bila kujali lolote

    ReplyDelete
  30. Ninyi mnaomtuhumu mzee Akilimali na kumkingia kifua Shaffih mmeshaupata ukweli au ndo ushabiki unawasumbua,na je? Huyo mzee Akilimali akitoa vielelezo vinavyoonesha ukweli kuhusu Mwandishi huyu mta-comment nini? Msikurupuke kumtuhumu mtu kabla ukweli hamjaujua.Binafsi nipo neutral mpaka itakapobainika Shaffih amesingiziwa au la!

    ReplyDelete
  31. Kama kweli huyo mzee kasema ushaidi upo ngojeni tudubiri ndani ya hizo siku 7 atawasilisha kwa waandishi na la sivyo kiroho safi aombe tu msamaha aseme tu niliteleza.
    Shaffih katika maisha changamoto nijambo la kawaida so usikate tamaaaa

    ReplyDelete
  32. mimi napenda kutoa onyo kwa ninyi vijana wa clouds, kuanzia Hando, Kibonde, wewe mwenye Shaffii pamoja na wengine. mlikuwa mnaanza kupendwa na kuheshimika sana kutokana na kazi zenu (japokuwa tunajua hamjaenda shule vizuri wala kusomea uandishi wa habari) ila acheni ushabiki wa kipuuzi. wasikilizaji wa redio yenu ni wapenzi wa timu zote mbili na msisahau yanga na simba wanagawana mashabiki hapa nchini, acheni kuishambulia yanga na kutoa comment personal kwenye media. Watu wengi tu wameacha kusikiliza clouds kwa sababu ya kuchoshwa na mambo yenu ya unazi. kimsingi mna haribu biashara ya Joseph Kusaga na inapaswa awaonye ama awawajibishe.mimi ni mmoja wa watu waliokuwa wanakuheshimu sana wewe kijana nikizingatia ulikotoka na ninavyokufahamu ila sasa unapotoka. Ndugu zangu wanayanga tunapaswa kutoa tamko juu ya hawa vijana wanachafua sana timu yetu na najua ni wengi tu hatupendi hii hali iendelee....

    ReplyDelete
    Replies
    1. AnonymousJune 20, 2012 11:06 PM
      Umenifurahisha sana nimetoka kutoa comments zangu juu ya hawa vijana na unazi wao then wakati napitia pitia comments nimekutana na hii yako mbapo umeenda sawa na nilivyokuwa nawaza mimi, binafsi sifurahii wanavyoonyesha unazi wao na kuisemea mabaya YANGA kweli ni lazima Kusaga achukue hatua laasivyo ulewaji sifa wa hawa vijana unaweza kumuharibia kampuni yake, ajaribu kusikiliza RADIO ONE aone akina KITENGE kama wanaweka mapenzi ya timu zao kwenye kipindi.

      Delete
    2. Bwana Shaffii nakushauri utoe tamko tena hapa kwenye ukurasa wako kuonyesha uko active. na zingatia maoni ya wadau na pia waambie na wenzako. this is not good for your career as well as clouds media group. huwa media zinaanza kufa kwa namna kama hii. nakumbuka magazeti ya motomoto, uwazi etc yalikufa kwasababu ya malalamiko ya stakeholders. tumieni hizi feedback kujirekebisha remember hii taswira ya usimba ikijengeka na akatokea mtu mwingine akafungua neutral program ama redio you guys will be in deep shiit!!!

      Delete
  33. Kibonde, Shaffi, na Hando acheni unazi kwenye taaruma na sio tu kwa simba bali hata comments zenu huko ulaya ni za kishabiki

    ReplyDelete
  34. Tayari Yanga wote adui zako!! unalipokeaje hili? hebu tupe CV zako za uandishi wa habari ili tuweze kuchanganua mambo, mwisho hebu tuambie ukweli unawsiliana na Maximo au la?(iwe kwa mema au mabaya)

    ReplyDelete
  35. wewe Shafii huwezi kumfanya kito CHOCHOTE huyu mzee na wewe unajua hilo vizuri moyoni mwako. nenda kamuulize Nchunga. sana sana hata wewe unaweza kuishia kufukuzwa kazi hapo Coulds

    ReplyDelete
    Replies
    1. kwan unazan shafii anatishika na uchaw wa huyo mzee!....Mungu tu anaamininiwa

      Delete
    2. uchawi nini bwana hiyo ni dini yake,atajijua mwenyewe huyo mzee lakini cha msingi kizimbani kama hatatoa ushahidi wa kutosha,kama uchawi ni huko Yanga.

      Delete
  36. Nafikiri ni hatua Nzuri ya kujisafisha kwa Mzee Akilimali kama hana Ushahidi wa Maongezi ya simu barua pepe au txt sms..Ni muhimu kuchukua hatua za kisheria kwa kumfikisha mahakamani. likewise

    ReplyDelete
  37. why make big deal out of this, tatizo la Shafii huwa unajisahau sana, tunajua Joe Kusaga ni simba, you are not forced to be a simba fan just becouse your top boss is supporting it. Leo uko hapo kesho haupo, waliondoka kina Kipanya utakuwa wewe? kuwa professional basi

    ReplyDelete
  38. elimu hamna kichwani,anapambana na waandishi wa habari badala atafute njia mbadala ya kuleta maendeleo ktk klabu yake kiukweli ameniudhi sana huyu mzee kuropoka vi2 bila kuwa na uhakika/ushahidisasa waliomtuma wape tena maneno ya kujibu ndani ya hizo cku saba!

    ReplyDelete
  39. Shaffih leo ni mara yangu ya kwanza kuaandika comment kwenye web yako, na hii imenipelekea kufanya hivi baada ya kusoma utetezi wako juu ya tuhuma zilizoelekezwa kwako na bwana Akilimali juu ya ujio wa kocha Maximo.
    Kwanza nikupongeze kwa kazi nzuri wewe pamoja na wanaspoti wenzako, pili lazima niwe muwazi kwenu na kwa kipindi chenu na kwa RADIO STATION yenu nzima ya CLOUDS, i hope mkisikiliza maoni ya wadau na mkayafanyia kazi basi ni dhahiri mtakuwa juu sana zaidi ya hapa mlipo.
    Binafsi huwa nachukizwa sana na ushabiki mlionao nyinyi watu wa kipindi cha sports extra, kiukweli mmeshindwa kuweka pembeni hisia na mapenzi yenu kwa timu fulani jina kapuni na kuonyesha upendeleo wa wazi kabisa kwa kuponda maendeleo, mafanikio hata shughuli za kila siku za hasimu mkubwa wa timu mnayoishabikia, Lakini pia napaswa kukubali kuwa siku moja moja mmekuwa mkimsemea mazuri huyo mpinzani wenu lakini kiukweli mmekuwa mkimsemea mazuri kwa kebehi na hili linajiziirisha through sauti zenu mnapotangaza, mmekuwa wanazi kupita kiasi na kuonyesha kebehi za nje nje n'way sitaki kulizungumzia sana hilo lakini my point ni kwamba:- Unapokuwa attacked na mtu mzima kama huyu na tuhuma zilizoelekezwa kwako ni nzito ambazo zinaweza kukufanya ukachukiwa au hata kudhuriwa kwa namna moja au nyingine na wapenzi wa YANGA kutokana na ukweli kwamba mashabiki wa timu hizi kubwa hapa nchini za SIMBA na YANGA always wamekuwa si watulivu once inapotokea hali fulani ambayo inaweza kutibua hali ya hewa kwenye timu yao fanya reference kwa NCHUNGA, Nilifikiria ingekuwa vyema ukamtafuta mzee AKILIMALI personal kwanza kabla ya kutoa malalamiko yako humu na kutoa commandment kuwa asikanusha madai yako within 7days basi aite waandishi wa habari then akanushe aliyoyasema. Nafikiri hapa umetoka nje ya mstari kidogo, changanua na ukipata jibu utajua nini ninamaanisha hapa.
    Kwa kuwasaidia tu jaribuni kufanya reference na vipindi vya michezo kwenye radio stations nyingine muone wenzenu wanavyoweka unazi pembeni na wanasimamia uhalisia hakika mtajiona wapi mnapopotoka.
    Nina mengi sana ya kueleza lakini kama unahitaji more advice just fine me personal
    Mdau

    ReplyDelete
  40. Niliposikia suala hilo nilicheka sana. Mtu mwenye akili timamu hawezi kuwa na visingizio eti MAXIMO hataki kuja YANGA sababu fulani anamwelezea mazingira ya kazi. Kila kocha huwa ana mazingira ya kazi yake, lazima awe watu wanaofanya kazi ya kuchunguza kule anakokwenda. Bahati nzuri MAXIMO aianijua vizuri YANGA kwahiyo kauli ya mzee huyo ni kama wale watu wenye tabia ya kulalamika/walalamishi lakini hawajui kuchukua uamuzi.
    KIHISIA; Labda iwe kweli SHAFII unatumiwa na MAXIMO katika kumwelezea mazingira ya kazi anayotaka kuja kufanya. je yale yanayosemwa kuhusu mazingira hayo kama mabaya na yanaonekana kosa lako liko wapi wakati ni jukumu mwajiri kuhakikisha mwajiriwa anafanya kazi katika mazingira bora?

    Mimi niliamua kuweka namba ya simu ya MAXIMO kwenye ukurasa wangu wa facebook, nilichukizwa jinsi habari za uongo zilivyokuwa zinatolewa na kuwalisha wasomaji uongo. Kwanini uwadanganye watu? Hilo ndilo ninaloona kwamba mtu mwenye akili timamu hawezi kutoa visingizio eti kocha hakuajiriwa sababu SHAFII alikuwa anampigia simu au kumtumia ujumbe wa baruapepe, hayo mambo inabidi uwaambie watu waliolazwa hospitali ya MILEMBE kule dodoma, ndio wataelewa. Haiwezekani mtu anayeijua YANGA eti asije sababu ya fulani akiwa SHAFII. Mimie sisikilizi CLOUDS FM wala SPOTRS EXTRA au SPORTS BAR. Wala sina ukaribu wowote na SHAFII DAUDA zaidi ya kusoma maandiko yake tu kwenye majarida na mara kadhaa nimemuona TBC. Simjui naye hanijui, lakini katika msingi LOGIC, wazee wa YANGA watakiwa kuelewa kuwa zama hizi SOCIAL INFORMATEC huwezi kumficha mtu kila jambo. watu wana simu ya MAXIMO. Maximo anawasiliana na Ikulu. kwanini alipokuwa na Rais Kikwete kule Brazil wazee wa Yanga hawajasema kuwa Rais Kikwete ameharibu dili? Ina maana MAXIMO hajui hali ya YANGA? Ubabaishaji, uelewa mdogo, ukosefu wa mikakati, mipango na matokeo yake watafukuza kila kocha, watafukuza kila kiongozi na mwisho itabaki habari za kuifunga SIMBA kwishaaaa. miaka 75 sasa wazee wetu wanataka tuendelee kudanganya ama mzee kasema? MAXIMO anao marafiki wangapi hapa nchini? MAXIMO anawasiliana na watu wangapi hapa nchini? huu mzaha sana.
    TANGU MWANZO nilijua MAXIMO hawezi kuja YANGA. Ingawa vyombo vya habari vinaandika kuwa anafundisha DEMOCRATA FC, ni uongo ile inaitwa ES DEMOCRATA GV. Pale Brazil kuna mradi wa ligi ya majimbo kwaajili ya kutafuta wachezaji bora watakao teuliwa kuungana na wengine wa timu ya taifa kwa ajili ya kombe la dunia 2014. ligi hiyo msichanganye na le ya majimbo ya kila msimu.
    SHAFII huna sababu ya kupoteza muda wako kulumbana na wazee kama hao. kama alitumwa na uongozi wa timu ya YANGA waulize, vinginevyo hakuna sababu ya kuwatisha eti sheria itachukua mkondo wake. MUHIMU; weka MWANASHERIA, CHUKUA HATUA, TUJUE UKWELI SIO KUKANUSHA TU, MAANA HATA IKIKANUSHWA HUKU PEMBENI ITAENDELEA KUAMINIWA TU NI KWELI. NAFIKIRI TUNAHITAJI KUFUNDISHANA UTARATIBU, MAHAKAMA ZIPO WAZI SHAFII ni wewe na roho yako.


    Markus Mpangala
    Dar es salaam,
    Juni 21, 2012.

    ReplyDelete
  41. akili za mwewe!,changanya na zako.

    ReplyDelete
  42. Yaani huyu jamaa asikatize mtaani kwetu utala kichapo cha fisi aaliyebomoa nyumba ya mfugaji na kuchukua mfugo akakutilizwa bado anakula. NASHINDWA JUA CLAUD HIYO NAYO NI NINI KA KIJIWE CHA WAMBEA FULANI HIVI IGINE RADIO ONE TBC CAPITAL MICHEZO INAPENDWA SANA Msijitoe akili MTAFA SIKU BADO haya weye Dauda tangu uunze shika maiki badi yanga tumekuwa hatuna raha, nikiwa na rafiki zangu shabiki wa simba huwa inabidi nisepe ili kipindi kiishe ndio nirudi na nikirudi basi wanasema umetoroka. KWANINI UNINYIME RAHA SHAFFIII MTAAANI KWETU NIMEKULIA HAPO, KWANINI UNITENGANISHE NA MARAFIKI ZANGU MAANA KIKIANZA KIPINDI CHAKO TUUUUUU YAWA HUZUI JE IMEKUWA VIBAYA MIE KUWA MPENZI WA YANGA. HERI WE KUONDOKA HAPO UFANYE KAZI INGINE KULIKO ILIVYO SASA WANAYANGA SIE. HUTAKIWE UPENDELEEEE TIMU DAUDA KUWA MSAWA MAANA WATU TUNAUMIA SANA. KWANNI NIKOSE RAHA MTAANI KWANGU.
    ACHA KAZI HIYO HUIWEZI DAUDA UTAFA BUREEEEEE MAANA WATU TUNAPENDA MICHEZO KA NINI HALAFU WEYE WAJA NA UPENDELEO WAKO HAPA.

    INANIUMA HASA NILIVYOTENGANA NA RAFIKI YANGU SHABIKI WA SIMBA SABABU YAKO, SABABU HUWA ANANITANIA SANA KWA MANENO YAKO DAUDA.
    SASA TENA JAMANI KUHUSU MAXIMO ULITUMWA JAMANI MBONA KIHEREHERE SANA JAMANI WEWE HUWAONI AKINA KITENGE JAMANI MBONA WAKO TOFAUTI MIE NAONA VIPINDI VYOTE VYA MICHEZO WAPEWE WATU WENYE BUSATA MAANA HAWA MABRAZAMENI WANATUNYIMISHA RAHA SANA NA WATANI WETU. RAHA YA WATANI MTANIANE MCHEKE YAISHE ILA NIPONDWE HUKU NAWE REDIO WAONGEZA NAUMIA SANA
    ACHANA NA HIYO KAZI DAUDA YAAANI USIKATIZE WEYE YAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAANI

    ReplyDelete