Real Madrid imefanikiwa kumsajili kijana Takuhiro Nakai maarufu kwa jina la "Pipi," kijana huyo ana umri wa miaka 9.
Kwa mujibu wa gazeti la Marca la nchini Hispania, Nakai kwa mara ya kwanza alionekana nchini Japani kwenye kipindi cha Televisheni akionyesha kipaji chake.
Kwa kumsajiili kijana huyo Madrid ni kama vile imewalipa mahasimu wao Barcelona ambao hivi karibuni walimsajili pia kijana raia wa Japani Takefusa Kubo "Japanese Messi," mwenye umri wa miaka 11.
HUYU NDO KIJANA TAKUHIRO NAKAI
Search This Blog
Wednesday, October 9, 2013
Dennis Bergkamp ATAMANI KUREJEA ARSENAL
Dennis Bergkamp amedhibitisha nia yake ya kurejea siku moja kwenye benchi la ufundi la klabu ya Arsenal.
Gwiji huyo wa Gunners ambaye alistaafu mwaka 2006 baada ya kuitumikia miaka 11 amesema akimaliza mkataba na klabu ya Ajax angependa kujiunga na Arsenal yenye makazi yake kaskazini mwa jiji la London.
‘Kila kitu wakati nikiwa Arsenal kilikuwa safi,muda wote nilikuwa na furaha,sikuwahi kugombana na mtu yeyote na imebaki kwenye moyo wangu tangu nimeondoka, Najiona siku zijazo kuwa sehemu ya benchi la ufundi la Arsenal kwasababu naipenda sana kazi ya kufundisha hasa kuwafundisha washambuliaji namna ya kufumania nyavu. Nalikumbuka sana bao nililolifunga kwenye mchezo dhdi ya Newcastle UTD,litabaki kuwa bao bora kabisa kwangu’.
‘Kila kitu wakati nikiwa Arsenal kilikuwa safi,muda wote nilikuwa na furaha,sikuwahi kugombana na mtu yeyote na imebaki kwenye moyo wangu tangu nimeondoka, Najiona siku zijazo kuwa sehemu ya benchi la ufundi la Arsenal kwasababu naipenda sana kazi ya kufundisha hasa kuwafundisha washambuliaji namna ya kufumania nyavu. Nalikumbuka sana bao nililolifunga kwenye mchezo dhdi ya Newcastle UTD,litabaki kuwa bao bora kabisa kwangu’.
CHAGUA LIPI BAO KALI KATI YA HAYA MABAO 10 YA TIK TAK.
Van Der Vaart alilifunga bao hili kwenye dakika ya 17 kwenye mchezo dhidi ya Nurnberg likiwa bao lake la nne msimu huu wa BUNDESLIGA ,pia ushindi huu wa mabao 5-0 ulikuwa kwa kwanza kwa kocha Bert van Marwijk tangia ajiunge na Hamburg.
Camilo Sanvezzo
Kinda raia wa Brazil Camilo Sanvezzo aliifungia Vancouver Whitecaps bao la kusawazisha kwenye mchezo MLS dhidi ya Portland uliomalizika kwa timu hizo kufungana mabao 2-2.
Paolo Di Canio
Paolo Di Canio alifunga moja ya mabao bora ktk historia ya Premier League mnamo mwezi machi mwaka 2000 akiwa na Westham Utd kwenye mchezo dhidi ya Wimbledon.
Radamel Falcao
Radamel Falcao amefunga mabao kadhaa mazuri lakini bao alilofunga kwenye mchezo wa kirafiki dhidi America de Cali mnamo mwezi may mwaka 2012 litabaki kuwa bao bora kabisa mpaka sasa miongoni mwa mabao mengi aliyowahi kuyafunga.
Xherdan Shaqiri
Moja ya vitu vilivyoishawishi Bayern Munich kumsajili Xherdan Shaqiri kwa ajili ya msimu wa 2012-13 ni uwezo wake mkubwa aliounyoshe akiwa na FC Basel, hili ni moja mabao bora alilolifunga kwenye mchezo dhidi FC Luzern mnamo April 2012.
Pa-Moudou Kah
Zlatan Ibrahimovic ( ENGLAND Vs SWEDEN )
Wayne Rooney ( MANCHESTER UTD Vs MANCHESTER CITY )
Carlos Vela ( REAL SOCIADAD Vs MALAGA )
Trevor Sinclair ( QPR Vs Burnsley )
Tuesday, October 8, 2013
HATIMAYE RAISI WA CAMEROON AMSHAWISHI SAMUEL ETO'O KUTOSTAAFU SOKA LA KIMATAIFA
Rais wa Cameroon Paul Biya amemshawishi mwanasoka Samuel Eto'o kutafakari upya mipango yake ya kujizulu kutoka soka ya kimataifa
Mshambulizi huyo wa Chelsea alikutana na waakilishi wa Rais mjini Yaounde kujadili mustakabali wa mchezaji huyo kuhusu soka ya kimataifa.
Sasa atakwenda Ufaransa kujiunga na timu ya taifa inayojiandaa kucheza dhidi ya Tunisia katika michuano ya kufuzu kwa kombe la Dunia Brazil mwaka 2014. Baada ya kukutana na Eto'o, alikubali kuchezea Cameroon kwa mara nyingine.
Etoo mwenye umri wa miaka 32 aliwambia wenzake kuwa hatacheza tena soka ya nyumbani punde tu baada ya Cameroon kuicharaza Libya na kuingia katika awamu ya pili ya kufuzu kwa kombe la dunia.
Licha ya ripoti za yeye kuacha kucheza soka, kocha wa timu ya Cameroon Volker Finke alimteua Eto'o kuchezea timu ya taifa ya Cameroon dhidi ya Tunisia ingawa mwenyewe hakuwa ametoa taarifa rasmi.
Eto'o amekuwa na uhusiano tete na maafisa wa soka nchini Cameroon katika siku za nyuma ikiwemo hata kuongoza timu ya taifa kwenye mgomo uliosambaratisha mechi ya kirafiki dhidi ya Algeria.
Eto’o aliadhibiwa kwa kupigwa marufuku kucheza mechi 15 ingawa baada ya kukata rufaa alipunguziwa adhabu hadi mechi 8
Hata baada ya adhabu yake kumalizika alikataa kuichezea Cameroon kwa miezi kadhaa.
Pia sio mara ya kwanza kwa Rais Biya kuingilia kati na kumzuia mchezaji kujiuzulu kutoka katika majukumu ya kitaifa.
MAKALA: YANGA NI NZITO, SIMBA IPENI MUDA KIDOGO
Na Baraka Mbolembole
Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara, Yanga SC, iliifunga timu ya Mtibwa Sugar mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa siku ya ya jumapili, na kusogea hadi katika nafasi ya pili ya msimamo. Wakiwa wamekusanya pointi 14 katika michezo saba iliyopita, Yanga wapo nyuma ya vinara Simba kwa tofauti ya pointi tatu, na itasafiri hadi mjini, Bukoba kucheza na timu ya Kagera Sugar wikiendi ijayo.
Katika mchezo huo ambao ulishuhudia kwa mara nyingine kiwango kizuri kutoka katika safu ya ulinzi, kiungo na ile ya ushambuliaji. Yanga walionekana kucheza kwa maelewano makubwa, kitu ambacho walianza kukionesha katika mchezo wa wiki iliyopita dhidi ya Ruvu Shooting.
SAFU YA ULINZI
Imeonekana kupandisha kiwango chake cha kujilinda, tofauti na michezo mitano ya mwanzoni ambayo walijikuta wakiruhusu mabao saba. Wakiwa na safu kali ya mashambulizi, Yanga ilikuwa ikihitaji kuwa na safu imara ya ulinzi, pengine namna walinzi, Mbuyu Twite, David Luhende, Kelvin Yondani na Nadir Jaroub ilivyocheza katika mchezo dhidi ya Ruvu, na ule wa juzi dhidi ya Mtibwa, pengine wangeweza kushinda katika michezo yake ya Mbeya, dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons, walifunga mabao mawili katika michezo hiyo iliyokuwa migumu lakini walipoteza pointi nne ambazo zingeweza kuwapeleka juu zaidi.
Ila, safu yao ya ulinzi ilijikuta ikishindwa kuhimili kasi na uwezo wa wafungaji waliopo kwa sasa katika timu mbalimbali za ligi kuu. Ligi ni ngumu hasa, na pengine matokeo yanayotokea sasa ni kutokana na uwezo mzuri wa washambuliaji msimu huu. Namna walivyoweza kucheza na Azam na kuweza kufunga mabao mawli, na kuruhusu matatu katika lango lao ilitokana na kila timu kuwa na wachezaji wazuri. Mbuyu amekuwa na maendeleo mazuri tangu alipotoka katika majeraha yake, na ndivyo ilivyo kwa Kelvin. Luhende alifanya makosa mengi katika michezo ya Mbeya, ila amejitahidi kupunguza katika michezo miwili iliyopita, amekuwa akilaumiwa kwa makosa yake ya kuzingatia ushambuliaji pekee na kujisahau katika jukumu lake hasa, la ulinzi.
Kwa sasa safu hii ya ulinzi ndiyo itakuwa muokozi wa Yanga katika michezo inayofuata, kwa kuwa kila timu inaweza kufunga msimu huu, na zinaweza kufunga katika lango la timu zetu kubwa Yanga na Simba, iwe Taifa au viwanja vya mikoani. Yanga watakwenda kucheza na Kagera, timu ambayo inaweza kufunga bao moja au mawili katika mchezo huo, huu utakuwa ni mtihani mwingine kwa walinzi hao ambao wameonekana kucheza kwa maelewano mazuri mchezoni.
Unahitaji kuitazama timu iliyokamilika Tanzania, itazame Yanga, itazame wanavyokuwa wanacheza hata katika michezo migumu. Wana umoja ambao miaka iliyopita hawakuwa nao. Washambuliaji wana fanya majukumu yao, viungo wanachezesha timu na kuisaidia katika kujilinda, tatizo lilikuwa safu ya ulinzi, ila sasa linaonekana kuanza kuondoka taratibu, ila sasa wapo kina Them Felix wengi tu, ambao wanaweza kuzihadaa safu za ulinzi za timu pinzani na kufunga mabao. Yanga watakwenda kuvunja mwiko Kagera? Safu yao ya ulinzi inayo majibu. Sina shaka kuwa wanaweza kufunga mabao mawili au moja huko, watalilindaje kwa timu ambayo nayo inauwezo wa kufunga mabao?
KUHUSU SIMBA
Simba ilipunguzwa kasi na Ruvu Shooting, siku ya jumamosi iliyopita baada ya kulazimisha kusawazisha kwa mkwaju wa penati.
" Tulikuwa tukicheza na timu yenye akili timamu" alisema kocha msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo mara baada ya mchezo huo. Julio alisema hayo akitambua kuwa wapinzani wao walikuwa katika kiwango cha juu cha stamina, uwezo wa kumiliki mpira, na timu iliyokuwa na mbinu nyingi pamoja na kasi mchezoni. Hii ndiyo ligi ambayo tulikuwa tukiililia kwa muda mrefu.
Tulikuwa tunazihitaji timu kama Ruvu ambayo inaweza kucheza vizuri na Yanga kisha Simba ndani ya siku nne. Ni kweli Simba ilicheza soka la kiwango cha chini, kutokana na mazoea yetu ya kukariri ubora wa timu zetu kubwa na kuzinyima nafasi yoyote ya kushinda timu nyingine. Kinachotokea na kinachoendelea ndani ya Simba kwa sasa ni timu kutafuta kikosi cha kwanza, pengine hili lilitakiwa kuwa tayari machoni mwetu ila majeraha ya baadhi ya wachezaji yamekuwa yaivuruga mipango ya mwalimu. Nafikiri baada ya muda watu wataiona Simba inayoshambulia na kucheza mpira mzuri kama ilivyo kwa Yanga. Ipeni muda Simba, ila Yanga ni nzito.
Ila, safu yao ya ulinzi ilijikuta ikishindwa kuhimili kasi na uwezo wa wafungaji waliopo kwa sasa katika timu mbalimbali za ligi kuu. Ligi ni ngumu hasa, na pengine matokeo yanayotokea sasa ni kutokana na uwezo mzuri wa washambuliaji msimu huu. Namna walivyoweza kucheza na Azam na kuweza kufunga mabao mawli, na kuruhusu matatu katika lango lao ilitokana na kila timu kuwa na wachezaji wazuri. Mbuyu amekuwa na maendeleo mazuri tangu alipotoka katika majeraha yake, na ndivyo ilivyo kwa Kelvin. Luhende alifanya makosa mengi katika michezo ya Mbeya, ila amejitahidi kupunguza katika michezo miwili iliyopita, amekuwa akilaumiwa kwa makosa yake ya kuzingatia ushambuliaji pekee na kujisahau katika jukumu lake hasa, la ulinzi.
Kwa sasa safu hii ya ulinzi ndiyo itakuwa muokozi wa Yanga katika michezo inayofuata, kwa kuwa kila timu inaweza kufunga msimu huu, na zinaweza kufunga katika lango la timu zetu kubwa Yanga na Simba, iwe Taifa au viwanja vya mikoani. Yanga watakwenda kucheza na Kagera, timu ambayo inaweza kufunga bao moja au mawili katika mchezo huo, huu utakuwa ni mtihani mwingine kwa walinzi hao ambao wameonekana kucheza kwa maelewano mazuri mchezoni.
Unahitaji kuitazama timu iliyokamilika Tanzania, itazame Yanga, itazame wanavyokuwa wanacheza hata katika michezo migumu. Wana umoja ambao miaka iliyopita hawakuwa nao. Washambuliaji wana fanya majukumu yao, viungo wanachezesha timu na kuisaidia katika kujilinda, tatizo lilikuwa safu ya ulinzi, ila sasa linaonekana kuanza kuondoka taratibu, ila sasa wapo kina Them Felix wengi tu, ambao wanaweza kuzihadaa safu za ulinzi za timu pinzani na kufunga mabao. Yanga watakwenda kuvunja mwiko Kagera? Safu yao ya ulinzi inayo majibu. Sina shaka kuwa wanaweza kufunga mabao mawili au moja huko, watalilindaje kwa timu ambayo nayo inauwezo wa kufunga mabao?
KUHUSU SIMBA
Simba ilipunguzwa kasi na Ruvu Shooting, siku ya jumamosi iliyopita baada ya kulazimisha kusawazisha kwa mkwaju wa penati.
" Tulikuwa tukicheza na timu yenye akili timamu" alisema kocha msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo mara baada ya mchezo huo. Julio alisema hayo akitambua kuwa wapinzani wao walikuwa katika kiwango cha juu cha stamina, uwezo wa kumiliki mpira, na timu iliyokuwa na mbinu nyingi pamoja na kasi mchezoni. Hii ndiyo ligi ambayo tulikuwa tukiililia kwa muda mrefu.
Tulikuwa tunazihitaji timu kama Ruvu ambayo inaweza kucheza vizuri na Yanga kisha Simba ndani ya siku nne. Ni kweli Simba ilicheza soka la kiwango cha chini, kutokana na mazoea yetu ya kukariri ubora wa timu zetu kubwa na kuzinyima nafasi yoyote ya kushinda timu nyingine. Kinachotokea na kinachoendelea ndani ya Simba kwa sasa ni timu kutafuta kikosi cha kwanza, pengine hili lilitakiwa kuwa tayari machoni mwetu ila majeraha ya baadhi ya wachezaji yamekuwa yaivuruga mipango ya mwalimu. Nafikiri baada ya muda watu wataiona Simba inayoshambulia na kucheza mpira mzuri kama ilivyo kwa Yanga. Ipeni muda Simba, ila Yanga ni nzito.
MWANARIADHA WA ZAMANI LINFORD CHRISTIE AKIWA NA THIERRY HENRY.
Mnamo mwezi wa tano mwaka huu Arsenal ilisaini mkataba na PUMA wenye thamani ya paundi milioni 30 kwa mwaka, mkataba wa sasa wa Arsenal na kampuni ya NIKE uliosainiwa tangu mwaka 1994 unamalizika mwishoni mwa msimu huu.
Picha juu iliwekwa kwenye mtandao wa kijamii wa twitter na balozi wa PUMA Linford Christie inamuonyesha Thierry Henry akiwa ndani ya uzi mpya wa Arsenal wa msimu wa 2014-15,wengine kwenye picha hiyo ni nyota wa sasa Bacary Sagna na Olivier Giroud.
Picha juu iliwekwa kwenye mtandao wa kijamii wa twitter na balozi wa PUMA Linford Christie inamuonyesha Thierry Henry akiwa ndani ya uzi mpya wa Arsenal wa msimu wa 2014-15,wengine kwenye picha hiyo ni nyota wa sasa Bacary Sagna na Olivier Giroud.
FURSA YA KIPINDI CHA TELEVISHENI NDIO ILIMTOA THEO WALCOTT.
Kocha mkongwe Harry Redknapp ametoa kitabu kinachoelezea maisha yake,gazeti la Dailymail la nchini Uingereza limekuwa likitoa baadhi ya stori zilizopo kwenye kitabu hicho,miongoni mwa alichokisema Redknapp ni namna mshambuliaji wa Arsenal na timu ya Taifa ya England Theo Walcott alivyopata nafasi mpaka kuwa mwanasoka wa kulipwa.
''Kwa mara ya kwanza nilikutana na Theo Walcott alipokuwa na umri wa miaka 12.
mchekeshaji Mike Osman,alikuwa ni mmoja wa wazalishaji wa kipindi cha Televisheni kilicholenga kuwashirikisha vijana wenye vipaji vya soka na kuwafuatilia maendeleo yao.
Mike Osman alitupa mwaliko mimi na Alan Ball wa kuwa wageni wa heshima ikiwa ni pamoja na kuwafundisha vijana wale,miongoni mwa vijana waliojitokeza alikuwa ni Theo Walcott,alinivutia na kilichofuata ni kumpeleka timu ya watoto ya Southampton.
Anampa nafasi: Harry Redknapp alimpa Theo Walcott nafasi ya kucheza mechi yake ya kwanza akiwa na umri wa miaka 16 na siku 143.
Redknapp alimuona Walcott alipokuwa na miaka 12 kwenye kipindi cha Televisheni cha mchekeshaji Mike Osman (juu).
SAKATA LA MALIPO YA OKWI: SIMBA SASA WADAI MIL.480 NA ASILIMIA 20 YA FEDHA ALIZOUZWA OKWI SC VILLA
UAMUZI wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), kumwidhinisha Emmanuel Okwi kuichezea SC Villa ya Uganda umeibua mapya Simba.
Katibu Mkuu wa Simba, ambaye kitaaluma ni mwanasheria, Evodius Mtawala alisema: “Hatukubali, madai yetu yamebadilika sasa tunadai mambo mawili, tupewe Dola 300,000 halafu watupe na asilimia 20 ya pesa watakayomuuza Okwi kwa SC Villa.”
Simba wameenda mbali zaidi na kudai mpaka Ijumaa wiki hii, Etoile du Sahel itawatambua wao ni nani, kwa kuwa Fifa itakuwa imeshashusha rungu lake dhidi ya timu hiyo ya Tunisia.
Mtawala alisema hawana shida na Okwi wanachohitaji sasa ni fedha zao tu ambazo ukizibadilisha kwa madafu zinakuwa Sh480 milioni.
“Tunataka salio tu, Okwi hawezi kwenda SC Villa bila ya Simba kushirikishwa. Villa wanajisumbua tu kwa kuwa mkataba wetu ambao tumeingia na Etoile du Sahel wakimuuza mchezaji lazima watupe asilimia 20 ya fedha wanayomuuza.”
Fifa imetoa baraka zake kwa Shirikisho la Soka Uganda (Fufa), kumwidhinisha Okwi kuichezea Villa kwa miezi sita, baada ya Fufa kutuma maombi Fifa wakitaka Okwi aruhusiwe kuichezea Villa kwa muda wakati sakata lake likitafutiwa ufumbuzi.
Fifa imelitaka Shirikisho la Soka la Tunisia (FTF), litoe leseni ya uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa Okwi kupitia mfumo wa kielektroniki (TMS).
SOURCE: MWANASPOTI
KOCHA ALIYEIPA ZAMBIA UBINGWA WA AFRIKA AACHIA NGAZI NA KUJIUNGA NA KLABU YA SOCHAUX
Zambia imempa idhini kocha Herve Renard kuyaacha majukumu yake katika timu ya taifa ya nchi hiyo ili kuchukua jukumu lake jipya la kuwa kocha wa klabu ya Ufaransa ya FC Sochaux.
Kocha huyo alikuwa ameanza muhula wa pili wa mkataba wake kuwa kocha wa timu ya taifa ya Zambia.
Zambia sasa imempa kazi ya muda Patrice Beaumelle kuwa kocha wa Chipolopolo. Lakini Zambia ilikuwa na wakati mgumu mwaka huu kiasi cha kuondolewa nje ya michuano ya kufuzu kwa kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil.
Beaumelle, amekuwa akifanya kazi kama kocha wa muda, na atashikilia wadhifa wa kocha mkuu wakati Chipolopolo watapocheza mechi ya kirafiki na Brazil mjini Beijing tarehe 15 Oktoba.
Shirikisho la soka nchini humo katika taarifa yake lilisema kuwa kocha "Herve Renard ameachishwa majukumu yake ili kumruhusu kuiongoza timu ya Ufaransa.''
Renard, mwenye umri wa miaka 45, alichukua wadhifa huo wa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Zambia mwaka 2008 na aliiongoza timu hiyo hadi kufika robo fainali za kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2010.
Baadae alikuwa kocha wa timu ya Angola na USM Alger kwa muda kabla ya kurejea kuwa kocha wa Zambia na kutimiza ndoto yake ya kuiongoza Zambia kunyakua kombe la taifa bingwa Afrika mwaka 2012.
Monday, October 7, 2013
UCHAGUZI UTAFANYIKA OKTOBA 27- TENGA
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amewahakikishia
Watanzania kuwa uchaguzi wa kupata Kamati mpya ya Utendaji ya shirikisho
utafanyika Oktoba 27 mwaka huu kama ilivyopangwa.
“Wazungu
wanasema ije mvua au jua, uchaguzi utafanyika. Isipokuwa tunachotaka
kuhakikisha ni kuwa unakuwa uchaguzi huru na wa haki,” amesema Rais Tenga
wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za TFF leo mchana
(Oktoba 7 mwaka huu).
Amesema
mchakato unakwenda vizuri kilichobaki ni revision (mapitio) na rufani, masuala
ambayo yako mbele ya Kamati ya Rufani ya Maadili na Kamati ya Rufani ya
Uchaguzi.
Rais
Tenga amesema lengo la hatua hizo si kuzuia watu wasigombee kwani ni lazima
mambo ya msingi ikiwemo sifa za wagombea yaangaliwe, lakini kwenye haki ni
lazima kuhakikisha inatendeka hata kama ni kwa mtu mmoja.
Mchakato
wa uchaguzi ulivutia waombaji 58 ambapo watatu wamekata rufani Kamati ya Rufani
ya Uchaguzi kupinga kuondolewa na Kamati ya Uchaguzi wakati wengine wanane
masuala yao yamepelekwa Kamati ya Rufani ya Maadili kwa njia ya mapitio
(revision) ili kupata mwongozo wa utekelezaji.
Mwongozo
huo umeombwa na Sekretarieti ya TFF kwa Kamati ya Rufani ya Maadili kwa vile
Kamati ya Maadili iliwaona waombaji wanane wa uongozi waliofikishwa mbele yake
kwa makosa ya kimaadili kutokuwa na hatia, lakini wakati huo huo ikitambua
kuondolewa kwao kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi kulikofanywa na Kamati ya
Uchaguzi.
MRADI WA
FOOTBALL FOR HOPE KUFUNGULIWA OKTOBA 13
Mradi
wa Football for Hope kusaidia watoto na wasiojiweza kupitia mpira wa miguu
uliofadhiliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) mkoani Iringa
utafunguliwa rasmi Oktoba 13 mwaka huu.
FIFA
hutoa mradi huo kwa baadhi ya nchi kwa kuzingatia mambo mbalimbali ikiwemo
utawala bora, lakini kwa kupitia taasisi zisizo za kiserikali (NGOs) ambapo kwa
Tanzania umepatikana kupitia taasisi ya Iringa Development of Youth, Disabled
and Child Care (IDYDCC).
Rais
wa TFF, Leodegar Tenga ameishukuru FIFA kwa msaada huo, kwani ni mkubwa na kuongeza
kuwa ni matumaini yake utatumika kwa lengo lililopangwa.
Amesema
mradi huo wa FIFA ambao ni wa kusaidia watoto kielimu na wasiojiweza kwa
kupitia mpira wa miguu haukupita moja kwa moja TFF ni mzuri kwani moja ya mambo
uliofanikisha ni kuwepo jengo na sehemu ya watoto kucheza.
Ni
wastani wa nchi kumi tu duniani kwa mwaka zinapata mradi huo kutoka FIFA, jambo
ambalo Rais Tenga amesema linachangiwa pia na uhusiano na ushirikiano uliopo
kati ya Tanzania na shirikisho hilo.
KAMATI YA
WANAWAKE, TWFA YAPONGEZWA
Kamati
ya Mpira wa Miguu wa Wanawake ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na
Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) wamepongezwa kwa
kuhakikisha akina mama wanacheza mashindano mbalimbali.
Pongezi
hizo zimetolewa na Rais wa TFF, Leodegar Tenga ambapo amesema timu za wanawake
zimekuwa zikishiriki katika mashindano mbalimbali licha ya ukweli kuwa hadi
sasa hakuna udhamini kwenye mchezo huo.
Amesema
mpira wa miguu unaendeshwa na udhamini na kuchangia, jambo ambalo
linafanikishwa kwa kiasi kikubwa na uwazi katika matumizi ya fedha, jambo ambalo
hivi sasa lipo ndani ya TFF.
Rais
Tenga amesema baada ya kuanzisha Kamati ya Ligi, hivi sasa TFF inapata asilimia
4.5 tu ya mapato ya mechi za ligi kutoka asilimia 33 iliyokuwa ikipata wakati
anaingia madarakani mwaka 2004.
Amesema
asilimia hiyo 4.5 haiwezi kuendesha mpira na ndiyo maana nguvu zinaelekezwa
katika kutafuta wadhamini na kuchangia. Pia TFF inatoa zaidi ya asilimia 15 ya
Fedha za Msaada wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FAP) kutoka FIFA kwenye mpira
wa miguu wa wanawake ambapo ni nchi chache zinazofikia kiwango hicho.
Hivyo,
ametoa mwito kwa kampuni kujitokeza kudhamini au kuchangia timu za Taifa za
mpira wa miguu za wanawake ambazo zinashiriki mashindano mbalimbali mwaka huu,
kwani gharama za kuziendesha ni kubwa.
Timu
ya wakubwa (Twiga Stars) inacheza mashindano ya mchujo ya Fainali za Afrika
(AWC) zitakazofanyika mwakani nchini Namibia wakati ile ya chini ya miaka 20
inacheza mashindano ya Dunia ambayo fainali pia zitachezwa mwakani nchini
Canada.
MECHI YA
YANGA, MTIBWA YAINGIZA MIL 97/-
Mechi
ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) iliyochezwa jana (Oktoba 6 mwaka huu) Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam kati ya Yanga na Mtibwa Sugar imeingiza sh. 97,557,000.
Watazamaji
waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo namba 46 lililochezeshwa na Isihaka
Shirikisho kutoka Tanga walikuwa 17,313. Yanga ilishinda mabao 2-0.
Viingilio
katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku
kila klabu ikipata mgawo wa sh. 23,453,748.95 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani
(VAT) iliyolipwa ni sh. 14,881,576.27.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 11,925,635.06, gharama ya
kuchapa tiketi ni sh. 3,171,190 wakati gharama za mchezo ni sh. 7,155,381.04.
Kamati
ya Ligi sh. 7,155,381.04, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 3,577,690.52
na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 2,782,648.18.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Sunday, October 6, 2013
KILIMANJARO PREMIUM LAGER YAZINDUA “NANI MTANI JEMBE” KAMPENI KABAMBE KWA MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA
Evodius Mtawala, Aden Rage, George Kavishe, Mohammed Bhinda na Mwalusako wakishindana kuvuta kamba
Kavishe akiongea kwenye uzinduzi wa NANI MTANI JEMBE leo
Mashabiki wakicheza
Viongozi wa Yanga na Simba wakicheza fussball
Dar
es Salaam:
Bia ya Kilimanjaro Premium Lager imeleta
msisimko mpya katika utani wa jadi kati ya mashabiki wa Simba na Yanga nchi nzima kupitia kampeni
yake mpya ijulikanayo kama NANI MTANI JEMBE iliyozinduliwa leo jijini Dar es
salaam na itadumu kwa muda wa miezi miwili.
Akiongea kwenye uzinduzi, George Kavishe, Meneja
wa bia ya Kilimanjaro Premium Lageramesema NANI MTANI JEMBE itawapa fursa ya
aina yake mashabiki wa Simba na Yanga kuonyesha mapenzi yao kwa Simba na Yanga
kupitia kampeni hiyo itakayoendeshwa kwa sms ambapo Shilingi milioni 100
zitagawanywa kati ya Simba na Yanga halafu fedha hizo zitawekwa katika benki
maalum mtandaoni.
Kama nilivyosema awali, NANI MTANI JEMBE itahusisha mashabiki wa
klabu za Simba na Yanga.
Kilimanjaro Premium Lager imetenga kiasi cha shilingi milioni 100
ambazo zitashindaniwa Simba na Yanga kupitia mashabiki wake.
Kampeni itakapoanza kila klabu itatengewa kiasi cha shilingi milioni
50.
Katika kipindi hicho chote mteja ambaye ni Mtani Jembe akibandua
ganda la kizibo cha bia ya Kilimanjaro Premium Lager ataona namba. Ataandika
jina la timu yake (SIMBA au YANGA) ikifuatiwa na namba hiyo ya kwenye kizibo
kasha atatuma kwenda namba 15440 na kuipa shavu timu yake. Baada ya hapo
atapata ujumbe wa kuthibitisha kwamba meseji yake imepokelewa. Kwa kufanya
hivyo atakuwa amepunguza kiasi cha shilingi 1,000 kwenye akaunti ya klabu pinzani na kuiongezea klabu yake kiasi
hicho cha sh. 1,000.
Mwisho wa kampeni kama mashabiki wa Simba walipiga kura zaidi na
kuichangia zaidi basi Simba itapata milioni 60 na Yanga itapata milioni 40. Na
vilevile mwisho wa kampeni kama mashabiki wa Yanga walipiga kura zaidi na
kuichangia zaidi basi Yanga itapata milioni 60 na Simba itapata milioni 40.
Mteja anayetuma SMS atachajiwa kiwango cha kawaida cha kutuma sms na
baada ya kutuma sms atapata sms ya uthibitisho kwamba ameipigia kura timu yake
na kufanikiwa kuichangia kiasi cha shilingi 1,000. Kutokana na upigaji kura wa
mashabiki, akiba ya timu wanayoshabikia itakuwa ikiongezeka au kupungua
kulingana upigaji kura.
Mwisho wa kampeni fedha hizo zitakabidhiwa
kwa uongozi wa kila timu kulingana na matokeo ya kura na klabu zitajiamulia
namna ya kutumia fedha hizo katika miradi yake ya maendeleo.
Kampeni hii inatarajiwa kuongeza chachu ya
ushindani kati ya mashabiki wa Simba na Yanga kwa kuwapa fursa kuonyesha
mapenzi yao kwa timu zao. Mbali na kampeni ya SMS, kutakuwepo na shilingi milioni
2 ambazo mashabiki watajishindia kila wiki kwa wiki kumi kwa mashabiki
watakaoshiriki zaidi. Vilevile Nani Mtani Jembe itawaburudisha mashabiki wa
Simba na Yanga kupitia matukio mbalimbali mabonanza, promosheni zitakazofanyika
barabarani, kwenye bar na kwenye matawi ya Simba na Yanga. Kampeni hii itafika
kileleni tarehe 14 Disemba 2013 ambapo mechi ya hisani itachezwa kati ya klabu
hizo mbili kwenye Uwanja wa Taifa mbele ya maelfu ya mashabiki wa timu hizo.
LIVE SCORE VPL: YANGA SC 2 - 0 MTIBWA SUGAR FULL TIME
Dk 90+2 FULL TIME! Yanga 2-0 Mtibwa.
Dk 90 Juma Liuzio anapiga shuti kali langoni kwa Yanga lakini mipra unatoka nje.
Dk 86 Mtibwa inapata kona lakini Kisiga anacheza faulo.
Dk 82 Salim Abdallah anamchezea faulo Said Bahanuzi.
Dk 80 SUB: Yanga inafanya mabadiliko ametoka Kiiza ameingia Said Bahanuzi.
Dk 78 Kisiga anapiga shuti kali katika lango la Yanga lakini kipa Barthez anaokoa mpira na kuwa kona. Yanga wanaokoa kona.
Dk 76 SUB: Yanga inafanya mabadiliko ametoka Mbuyu Twite ameingia Juma Abdul.
Dk 73 Yanga wanaokoa kona na wakati huo huo Ngalema anamchezea rafu Ngassa.
Dk 73 Mtibwa inapata kona
Dk 68 Mbuyu Twite wa Yanga anaumia na mwamuzi anasimamisha mpira kwa muda.
Dk 66 SUB: Mtibwa inafanya mabadiliko ametoka Mgosi ameingia Juma Liuzio.
Dk 64 Cannavaro anamchezea faulo Hassan Ramadhan wa Mtibwa.
Dk 63 Yanga inapata kona mbili hapa.
Dk 58 SUB: Yanga inafanya mabadiliko ametoka Msuva ameingia Nizar Khalfan.
Dk 56 Ally Shomari wa Mtibwa anamchezea vibaya Msuva wa Yanga. Faulo inapigwa lakini Mtibwa wanaokoa.
Dk 56 Mtibwa inapata kona lakini Yanga wanaokoa.
Dk 53 Luhende anamchezea Hassan Ramadhan na faulo inapigwa kuelekea lango la Yanga.
DDk 50 Yanga inafanya shambulizi kali na Kiiza anakosa bao la wazi
Dk 46 Mtibwa inapata kona lakini Yanga wanaokoa
Dk 45 Kipindi cha Pili Kimeanza!
Dk 45 HALF TIME! Yanga 2-0 Mtibwa.
Dk 43 Azam TV wanafunga tena mitambo yao ili waweze kupiga picha za mchezo huu.
Dk 42 Ngassa anakosa bao baada ya Mtibwa kujichanganya katika kuokoa.
Dk 36 SUB: Mtibwa inafanya mabadiliko ametoka Vincent Barnabas ameingia Masoud Mohamed.
Dk 34 YELLOW CARD! Hassan Ramadhan wa Mtibwa anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya Msuva.
Dk 32 SUB: Mtibwa wanafanya mabadiliko ametoka Salvatory Ntebe ameingia Dickson Daudi.
Dk 31 YELLOW CARD! Vincent Barnabas wa Mtibwa anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya Domayo.
Dk 29 Ngalema anamchezea rafu Hamis Kiiza wa Yanga lakini mwamuzi Isihaka Shirikisho hajaiona faulo hiyo. Mtibwa wanacheza fair play ili Kiiza atibiwe.
Dk 26 Mtibwa wanapiga faulo langoni kwa Yanga lakini kichwa cha Vincent Barnabas kinatoka nje.
Dk 24 GOOOOOO....! Kavumbagu anaipatia Yanga bao la pili akiunganisha vyema pasi nzuri ya Ngassa. Yanga 2-0 Mtibwa.
Dk 19 Chuji anamchezea rafu Awadhi Juma na Shaban Kisiga anapiga faulo na mpira unadakwa na Barthez.
Dk 18 Kavumbagu anakosa bao baada ya kupiga shuti kali na mpira kugonga mwamba na kurudi uwanjani na mashabiki waliamini mpira unaingia wavuni.
Dk 16 Cannavaro anaokoa mpira uliokuwa unaelekea langoni kwa Yanga.
Dk 13 Yanga inapata kona lakini Mtibwa wanaokoa.
Dk 10 Paul Ngalema anamchezea rafu Simon Msuva.
Dk 9 Yanga wamezinduka na kutawala sehemu ya kiungo.
Dk 6 GOOOOOO.....! Mrisho Ngassa anaipatia Yanga bao la kwanza akimalizia pasi safi ya Didier Kavumbagu. Yanga 1-0 Mtibwa.
Dk 4 Mafundi wa Azam TV wanaendelea na zoezi la kuvitoa vifaa vyao uwanjani baada ya Yanga kukataa mechi hii kurekodiwa au kuonyeshwa live.
Dk 3 Frank Domayo anamchezea rafu Awadhi Juma wa Mtibwa.
Dk 2 Awadh Juma wa Mtibwa anapiga shuti kali langoni kwa Yanga lakini kipa Ali Mustapha 'Barthez' anaudaka mpira.
Mpira umeanza uwanja wa taifa baina ya mabingwa watetezi Yanga SC vs Mtibwa Sugar ya Morogoro.
SIMBA SC NA RUVU SHOOTING ZAINGIZA MILLIONI 75
Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya wenyeji Ruvu Shooting na Simba lililochezwa jana (Oktoba 5 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 75,692,000.
Watazamaji waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo namba 43 la VPL msimu wa 2013/2014 lililomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 walikuwa 13,395.
Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 17,983,902.31 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 11,546,237.29.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 9,144,357.11, tiketi sh. 3,183,382, gharama za mechi sh. 5,486,614.26, Kamati ya Ligi sh. 5,486,614.26, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,743,307.13, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) sh. 1,066,841.66 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,066,841.66.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Saturday, October 5, 2013
AZAM YATOKA SARE NA WAGOSI COASTAL UNION - MECHI YATAWALIWA NA VURUGU
Leo golikipa wa Azam Mwadini Ally alikuwa na wakati mgumu sana, ingawa bahati haikuwa ya Wagosi.
Yayo Kato akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Azam FC.
Nahodha Jerry Santo akikunjuka nje kidogo ya lango la Azam, ingawa shuti lake halikuleta madhara.
Kocha wa Coastal Union, Hemed Moroco akiwabwatukia wachezaji wake wacheze kama alivyowafunza.
Hili ndilo bao la kipindi cha pili walilokosa Coastal Union, ambapo shuti la Selembe lilipita mikononi mwa Mwadini Ally na kugonga mwamba.
SULUHU ya bila kufungana kati ya Coastal Union na Azam FC katika uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga imezidi kuwaongezea idadi ya suluhu Wagosi wa kaya katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Mchezo huo uliokuwa na presha kubwa kwa mashabiki na wachezaji ulimuweka katika wakati mgumu mwamuzi Andrew Shamba kutoka Pwani, kutokana na kushutumiwa kuwapendelea Azam FC.
Kipindi cha kwanza timu zote zilicheza kwa nguvu zikihakikisha zinapata mabao ya mapema na kujihakikishia ushindi lakini hakuna hata timu moja iliyofanikiwa kuona lango la mwenzake.
Kipindi cha pili kilianza kwa Azam FC kushambulia kwa kasi huku wakimiliki mpira hali iliyowachanganya wachezaji wa Coastal Union wakaanza kupoteana na kucheza bila kufuata mfumo. Hali hiyo ilizidi kuwachanganya Wagosi wa Kaya hasa baada ya mwamuzi kuanza kutoa maamuzi ya utata, kwani katika dakika ya sabini alitoa kona kwa Azam wakati ilikuwa ni goal kick.
Mashabiki wakaanza kuhamaki na kutaka kuvuruga mchezo baada ya mwamuzi kuzidisha kutoa maamuzi ya utata kama faulo zisizoeleweka na kona za utata. Hali hiyo ilimtisha mwamuzi na kusimamisha mchezo mara kwa mara ili kuwataka wasimamizi wa mchezo huo kuwatuliza mashabiki.
Tukio lililotokea kipindi cha kwanza ambapo mwamuzi wa pembeni alipigwa na kitu kisichojulikana kutoka jukwaa la 'Rasha' lilitaka kujirudia kipindi cha pili baada ya chupa na mawe kutupwa uwanjani baada ya mwamuzi kutoa faulo nje kidogo ya 18 upande wa Coastal Union.
Dakika ya 65 mwalimu Hemed Moroco alifanya mabadiliko na kumtoa Pius Kisambale akaingia Suleiman Kassim 'Selembe'. Mabadiliko hayo yaliongeza uhai kwa Wagosi hasa kutokana na aina ya uchezaji wa Selembe kutumia mipira ya kasi.
Azam FC walianza kuelemewa kutokana na Mganda, Yayo Kato kutumia vema mwili wake mfupi na wenye nguvu kuwashambulia mabeki wa Azam, hali hiyo iliwafanya Azam kubadilika na kucheza mpira wa hovyo uliowapa nafasi Coastal Union kupiga mipira mirefu ambapo ilipofika dakika ya 75 kipindi cha pili katika jukwaa la African Sports, Wagosi walikosa bao la wazi baada ya Selembe kupiga krosi iliyopenya ngome ya Azam akiwemo mlinda mlango Mwadini Ally na kugonga mwamba.
Kutokana na piga nikupige ya lala salama kufika dakika ya 74 mwamuzi alimnyooshea mlinzi wa kulia wa Coastal Union, kinda Hamadi Juma 'Basmat', kadi nyekundu baada ya kubadilishiana maneno na mchezaji wa Azam, Kipre Tchetche.
Tukio hilo lilianzia kwa Kipre kumpiga Hamadi kiwiko cha shingo hali iliyomfanya kinda huyo kumfuata kwa jazaba huku akimuuliza kwanini amemfanyia hivyo. Mwamuzi baada ya kuona Hamadi amemuelekezea kichwa Kipre akadhani kinda huyo anapigana ndipo akatoa kadi ya moja kwa moja.
Baada ya kadi hiyo hali ya uwanja ilichafuka ambapo mashabiki walikuwa wakipiga kelele huku wachezaji wakitaka kupigana, ndipo mchezaji mwingine wa Coastal Union beki wa kushoto Othman Tamim akapewa kadi ya njano papo hapo.
Baadaye mchezo ulirudi katika hali yake lakini ngome ya Coastal Union ilikuwa imepwaya hali iliyomfanya Juma Said 'Nyoso' kuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha ngome yao inakuwa imara.
Ilipofika dakika ya 84 mwlimu Moroco alifanya mabadiliko kwa kumtoa Uhuru Suleiman na kumuingiza Yusuf Chuma. Ambapo kinda huyo alionyesha uwezo mkubwa na kurudisha uhai wa safu ya ulinzi.
Mpaka mwamuzi wa leo anapuliza kipyenga cha mwisho matokeo yaliendelea kusomeka hivyo hivyohivyo 0-0, na kuendelea kuibakisha Coastal Union katika nafasi ya nne ikiwa na point 11 nyuma ya Azam iliyo nafasi ya tatu yenye point 11 lakini ikiwa na mabao mengi ya kufunga.
Baada ya mechi ya leo Coastal Union itashuka dimbani wiki ijayo katika uwanja wa Chamazi dhidi ya Ashanti United wanaoshika mkia katika ligi.
HABARI NA PICHA KWA HISANI YA COASTAL UNION BLOG
Subscribe to:
Posts (Atom)









