Search This Blog

Sunday, October 6, 2013

LIVE SCORE VPL: YANGA SC 2 - 0 MTIBWA SUGAR FULL TIME


Dk 90+2 FULL TIME! Yanga 2-0 Mtibwa. 

Dk 90 Juma Liuzio anapiga shuti kali langoni kwa Yanga lakini mipra unatoka nje.  

Dk 86 Mtibwa inapata kona lakini Kisiga anacheza faulo. 

Dk 82 Salim Abdallah anamchezea faulo Said Bahanuzi. 

Dk 80 SUB: Yanga inafanya mabadiliko ametoka Kiiza ameingia Said Bahanuzi. 

Dk 78 Kisiga anapiga shuti kali katika lango la Yanga lakini kipa Barthez anaokoa mpira na kuwa kona. Yanga wanaokoa kona. 

Dk 76 SUB: Yanga inafanya mabadiliko ametoka Mbuyu Twite ameingia Juma Abdul. 

Dk 73 Yanga wanaokoa kona na wakati huo huo Ngalema anamchezea rafu Ngassa. 

Dk 73 Mtibwa inapata kona 

Dk 68 Mbuyu Twite wa Yanga anaumia na mwamuzi anasimamisha mpira kwa muda. 

Dk 66 SUB: Mtibwa inafanya mabadiliko ametoka Mgosi ameingia Juma Liuzio. 

Dk 64 Cannavaro anamchezea faulo Hassan Ramadhan wa Mtibwa. 

Dk 63 Yanga inapata kona mbili hapa. 

Dk 58 SUB: Yanga inafanya mabadiliko ametoka Msuva ameingia Nizar Khalfan. 

Dk 56 Ally Shomari wa Mtibwa anamchezea vibaya Msuva wa Yanga. Faulo inapigwa lakini Mtibwa wanaokoa. 

Dk 56 Mtibwa inapata kona lakini Yanga wanaokoa. 

Dk 53 Luhende anamchezea Hassan Ramadhan na faulo inapigwa kuelekea lango la Yanga. 

DDk 50 Yanga inafanya shambulizi kali na Kiiza anakosa bao la wazi 

Dk 46 Mtibwa inapata kona lakini Yanga wanaokoa 

Dk 45 Kipindi cha Pili Kimeanza! 

Dk 45 HALF TIME! Yanga 2-0 Mtibwa. 

Dk 43 Azam TV wanafunga tena mitambo yao ili waweze kupiga picha za mchezo huu. 

Dk 42 Ngassa anakosa bao baada ya Mtibwa kujichanganya katika kuokoa. 

Dk 36 SUB: Mtibwa inafanya mabadiliko ametoka Vincent Barnabas ameingia Masoud Mohamed. 

Dk 34 YELLOW CARD! Hassan Ramadhan wa Mtibwa anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya Msuva. 

Dk 32 SUB: Mtibwa wanafanya mabadiliko ametoka Salvatory Ntebe ameingia Dickson Daudi. 

Dk 31 YELLOW CARD! Vincent Barnabas wa Mtibwa anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya Domayo. 

Dk 29 Ngalema anamchezea rafu Hamis Kiiza wa Yanga lakini mwamuzi Isihaka Shirikisho hajaiona faulo hiyo. Mtibwa wanacheza fair play ili Kiiza atibiwe. 

Dk 26 Mtibwa wanapiga faulo langoni kwa Yanga lakini kichwa cha Vincent Barnabas kinatoka nje. 

Dk 24 GOOOOOO....! Kavumbagu anaipatia Yanga bao la pili akiunganisha vyema pasi nzuri ya Ngassa. Yanga 2-0 Mtibwa. 

Dk 19 Chuji anamchezea rafu Awadhi Juma na Shaban Kisiga anapiga faulo na mpira unadakwa na Barthez. 

Dk 18 Kavumbagu anakosa bao baada ya kupiga shuti kali na mpira kugonga mwamba na kurudi uwanjani na mashabiki waliamini mpira unaingia wavuni. 

Dk 16 Cannavaro anaokoa mpira uliokuwa unaelekea langoni kwa Yanga. 

Dk 13 Yanga inapata kona lakini Mtibwa wanaokoa. 

Dk 10 Paul Ngalema anamchezea rafu Simon Msuva. 

Dk 9 Yanga wamezinduka na kutawala sehemu ya kiungo. 

Dk 6 GOOOOOO.....! Mrisho Ngassa anaipatia Yanga bao la kwanza akimalizia pasi safi ya Didier Kavumbagu. Yanga 1-0 Mtibwa. 

Dk 4 Mafundi wa Azam TV wanaendelea na zoezi la kuvitoa vifaa vyao uwanjani baada ya Yanga kukataa mechi hii kurekodiwa au kuonyeshwa live. 

Dk 3 Frank Domayo anamchezea rafu Awadhi Juma wa Mtibwa. 

Dk 2 Awadh Juma wa Mtibwa anapiga shuti kali langoni kwa Yanga lakini kipa Ali Mustapha 'Barthez' anaudaka mpira. 

Mpira umeanza uwanja wa taifa baina ya mabingwa watetezi Yanga SC vs Mtibwa Sugar ya Morogoro.

5 comments:

  1. Hi...unaweza kutupatia progress ya mechi zingine zinazoendelea mbali ya hii "Live Match" hapa N/Stadium Salidarama?

    ReplyDelete
  2. shafii acha ushabiki, mbona jana hukutupa live match ya simba vs ruvu shooting?

    ReplyDelete
  3. Hii Mr Daudi inakuaje, Yanga hapo si wanakiuka Sheria?
    Mmh hili shirikisho linaweza watoza fine Yanga?
    Kweli Supersport wangevumilia? Na ndo hawa leaders of Dar Young Africans want to bring in changes ...?
    Hahah! What kind of transformation are they going to make?
    TFF is required to create conducive environment for investment as well as insuring safety of these investors otherwise small clubs won't tolerate anymore in covering club's expenses .

    ReplyDelete
  4. Hii Mr Daudi inakuaje, Yanga hapo si wanakiuka Sheria?
    Mmh hili shirikisho linaweza watoza fine Yanga?
    Kweli Supersport wangevumilia? Na ndo hawa leaders of Dar Young Africans want to bring in changes ...?
    Hahah! What kind of transformation are they going to make?
    TFF is required to create conducive environment for investment as well as insuring safety of these investors otherwise small clubs won't tolerate anymore in covering club's expenses .

    ReplyDelete