Evodius Mtawala, Aden Rage, George Kavishe, Mohammed Bhinda na Mwalusako wakishindana kuvuta kamba
Kavishe akiongea kwenye uzinduzi wa NANI MTANI JEMBE leo
Mashabiki wakicheza
Viongozi wa Yanga na Simba wakicheza fussball
Dar
es Salaam:
Bia ya Kilimanjaro Premium Lager imeleta
msisimko mpya katika utani wa jadi kati ya mashabiki wa Simba na Yanga nchi nzima kupitia kampeni
yake mpya ijulikanayo kama NANI MTANI JEMBE iliyozinduliwa leo jijini Dar es
salaam na itadumu kwa muda wa miezi miwili.
Akiongea kwenye uzinduzi, George Kavishe, Meneja
wa bia ya Kilimanjaro Premium Lageramesema NANI MTANI JEMBE itawapa fursa ya
aina yake mashabiki wa Simba na Yanga kuonyesha mapenzi yao kwa Simba na Yanga
kupitia kampeni hiyo itakayoendeshwa kwa sms ambapo Shilingi milioni 100
zitagawanywa kati ya Simba na Yanga halafu fedha hizo zitawekwa katika benki
maalum mtandaoni.
Kama nilivyosema awali, NANI MTANI JEMBE itahusisha mashabiki wa
klabu za Simba na Yanga.
Kilimanjaro Premium Lager imetenga kiasi cha shilingi milioni 100
ambazo zitashindaniwa Simba na Yanga kupitia mashabiki wake.
Kampeni itakapoanza kila klabu itatengewa kiasi cha shilingi milioni
50.
Katika kipindi hicho chote mteja ambaye ni Mtani Jembe akibandua
ganda la kizibo cha bia ya Kilimanjaro Premium Lager ataona namba. Ataandika
jina la timu yake (SIMBA au YANGA) ikifuatiwa na namba hiyo ya kwenye kizibo
kasha atatuma kwenda namba 15440 na kuipa shavu timu yake. Baada ya hapo
atapata ujumbe wa kuthibitisha kwamba meseji yake imepokelewa. Kwa kufanya
hivyo atakuwa amepunguza kiasi cha shilingi 1,000 kwenye akaunti ya klabu pinzani na kuiongezea klabu yake kiasi
hicho cha sh. 1,000.
Mwisho wa kampeni kama mashabiki wa Simba walipiga kura zaidi na
kuichangia zaidi basi Simba itapata milioni 60 na Yanga itapata milioni 40. Na
vilevile mwisho wa kampeni kama mashabiki wa Yanga walipiga kura zaidi na
kuichangia zaidi basi Yanga itapata milioni 60 na Simba itapata milioni 40.
Mteja anayetuma SMS atachajiwa kiwango cha kawaida cha kutuma sms na
baada ya kutuma sms atapata sms ya uthibitisho kwamba ameipigia kura timu yake
na kufanikiwa kuichangia kiasi cha shilingi 1,000. Kutokana na upigaji kura wa
mashabiki, akiba ya timu wanayoshabikia itakuwa ikiongezeka au kupungua
kulingana upigaji kura.
Mwisho wa kampeni fedha hizo zitakabidhiwa
kwa uongozi wa kila timu kulingana na matokeo ya kura na klabu zitajiamulia
namna ya kutumia fedha hizo katika miradi yake ya maendeleo.
Kampeni hii inatarajiwa kuongeza chachu ya
ushindani kati ya mashabiki wa Simba na Yanga kwa kuwapa fursa kuonyesha
mapenzi yao kwa timu zao. Mbali na kampeni ya SMS, kutakuwepo na shilingi milioni
2 ambazo mashabiki watajishindia kila wiki kwa wiki kumi kwa mashabiki
watakaoshiriki zaidi. Vilevile Nani Mtani Jembe itawaburudisha mashabiki wa
Simba na Yanga kupitia matukio mbalimbali mabonanza, promosheni zitakazofanyika
barabarani, kwenye bar na kwenye matawi ya Simba na Yanga. Kampeni hii itafika
kileleni tarehe 14 Disemba 2013 ambapo mechi ya hisani itachezwa kati ya klabu
hizo mbili kwenye Uwanja wa Taifa mbele ya maelfu ya mashabiki wa timu hizo.
Yaani kampeni ya kulifanya taifa liwe la walevi, duuu kwa umasikini wa watanzania si na watoto wataingia hapa? So sad serikali inaangalia tu
ReplyDeleteUmelazimishwa kucheza? Mtoto wako umchunge dhidi ya majanga yote! Wizi, filamu za ngono, uongo, sigara.Huo ni wajibu wako Sio kilevi tu.Acha wapenzi wa soka waendelee na juhudi za kuinua Soka!!!
ReplyDelete