Na Baraka Mbolembole
Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara, Yanga SC, iliifunga timu ya Mtibwa Sugar mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa siku ya ya jumapili, na kusogea hadi katika nafasi ya pili ya msimamo. Wakiwa wamekusanya pointi 14 katika michezo saba iliyopita, Yanga wapo nyuma ya vinara Simba kwa tofauti ya pointi tatu, na itasafiri hadi mjini, Bukoba kucheza na timu ya Kagera Sugar wikiendi ijayo.
Katika mchezo huo ambao ulishuhudia kwa mara nyingine kiwango kizuri kutoka katika safu ya ulinzi, kiungo na ile ya ushambuliaji. Yanga walionekana kucheza kwa maelewano makubwa, kitu ambacho walianza kukionesha katika mchezo wa wiki iliyopita dhidi ya Ruvu Shooting.
SAFU YA ULINZI
Imeonekana kupandisha kiwango chake cha kujilinda, tofauti na michezo mitano ya mwanzoni ambayo walijikuta wakiruhusu mabao saba. Wakiwa na safu kali ya mashambulizi, Yanga ilikuwa ikihitaji kuwa na safu imara ya ulinzi, pengine namna walinzi, Mbuyu Twite, David Luhende, Kelvin Yondani na Nadir Jaroub ilivyocheza katika mchezo dhidi ya Ruvu, na ule wa juzi dhidi ya Mtibwa, pengine wangeweza kushinda katika michezo yake ya Mbeya, dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons, walifunga mabao mawili katika michezo hiyo iliyokuwa migumu lakini walipoteza pointi nne ambazo zingeweza kuwapeleka juu zaidi.
Ila, safu yao ya ulinzi ilijikuta ikishindwa kuhimili kasi na uwezo wa wafungaji waliopo kwa sasa katika timu mbalimbali za ligi kuu. Ligi ni ngumu hasa, na pengine matokeo yanayotokea sasa ni kutokana na uwezo mzuri wa washambuliaji msimu huu. Namna walivyoweza kucheza na Azam na kuweza kufunga mabao mawli, na kuruhusu matatu katika lango lao ilitokana na kila timu kuwa na wachezaji wazuri. Mbuyu amekuwa na maendeleo mazuri tangu alipotoka katika majeraha yake, na ndivyo ilivyo kwa Kelvin. Luhende alifanya makosa mengi katika michezo ya Mbeya, ila amejitahidi kupunguza katika michezo miwili iliyopita, amekuwa akilaumiwa kwa makosa yake ya kuzingatia ushambuliaji pekee na kujisahau katika jukumu lake hasa, la ulinzi.
Kwa sasa safu hii ya ulinzi ndiyo itakuwa muokozi wa Yanga katika michezo inayofuata, kwa kuwa kila timu inaweza kufunga msimu huu, na zinaweza kufunga katika lango la timu zetu kubwa Yanga na Simba, iwe Taifa au viwanja vya mikoani. Yanga watakwenda kucheza na Kagera, timu ambayo inaweza kufunga bao moja au mawili katika mchezo huo, huu utakuwa ni mtihani mwingine kwa walinzi hao ambao wameonekana kucheza kwa maelewano mazuri mchezoni.
Unahitaji kuitazama timu iliyokamilika Tanzania, itazame Yanga, itazame wanavyokuwa wanacheza hata katika michezo migumu. Wana umoja ambao miaka iliyopita hawakuwa nao. Washambuliaji wana fanya majukumu yao, viungo wanachezesha timu na kuisaidia katika kujilinda, tatizo lilikuwa safu ya ulinzi, ila sasa linaonekana kuanza kuondoka taratibu, ila sasa wapo kina Them Felix wengi tu, ambao wanaweza kuzihadaa safu za ulinzi za timu pinzani na kufunga mabao. Yanga watakwenda kuvunja mwiko Kagera? Safu yao ya ulinzi inayo majibu. Sina shaka kuwa wanaweza kufunga mabao mawili au moja huko, watalilindaje kwa timu ambayo nayo inauwezo wa kufunga mabao?
KUHUSU SIMBA
Simba ilipunguzwa kasi na Ruvu Shooting, siku ya jumamosi iliyopita baada ya kulazimisha kusawazisha kwa mkwaju wa penati.
" Tulikuwa tukicheza na timu yenye akili timamu" alisema kocha msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo mara baada ya mchezo huo. Julio alisema hayo akitambua kuwa wapinzani wao walikuwa katika kiwango cha juu cha stamina, uwezo wa kumiliki mpira, na timu iliyokuwa na mbinu nyingi pamoja na kasi mchezoni. Hii ndiyo ligi ambayo tulikuwa tukiililia kwa muda mrefu.
Tulikuwa tunazihitaji timu kama Ruvu ambayo inaweza kucheza vizuri na Yanga kisha Simba ndani ya siku nne. Ni kweli Simba ilicheza soka la kiwango cha chini, kutokana na mazoea yetu ya kukariri ubora wa timu zetu kubwa na kuzinyima nafasi yoyote ya kushinda timu nyingine. Kinachotokea na kinachoendelea ndani ya Simba kwa sasa ni timu kutafuta kikosi cha kwanza, pengine hili lilitakiwa kuwa tayari machoni mwetu ila majeraha ya baadhi ya wachezaji yamekuwa yaivuruga mipango ya mwalimu. Nafikiri baada ya muda watu wataiona Simba inayoshambulia na kucheza mpira mzuri kama ilivyo kwa Yanga. Ipeni muda Simba, ila Yanga ni nzito.

Ahsante, Baraka Mbolembole! Napenda jinzi unavyoongeza viwango vyako vya kuzichambua na kuzidadavua timu zetu kiviwango na ubora. Unajua siyo waandishi wote wanao huo uwezo japo wote wanaweza kuandika. Endelea kutumia kalamu yako kutupa aina hizi za midadavuo - napenda uandishi wako!
ReplyDeleteKitu kimoja ambacho nongeshauri katika kunogesha chambuzi baraka aka our last born,jaribu kuongeza na upande wa maamuzi maana waamuzi nao ni sehemu ya mchezo,mfano kwenye game za simba na ruvu,mtibwa na yanga nilikua shuhuda,niliona makosa mengi ya kmaamuzi,mfano refa wa simba na ruvu alilimudu pambano kwa dakika 20 tu za mwanzoni baada ya hapo alishindwa kumudu kabisa na alipotoa penalti kwa simba akapoteza kujiamini kabisa,pia refa wa yanga na mtibwa nae kwa asilimia zaidi ya 70 alishindwa kumudu pambano,kweli ligi ngumu ila marefa wanaiharibu,but big up bro
ReplyDelete