Search This Blog
Tuesday, October 8, 2013
SAKATA LA MALIPO YA OKWI: SIMBA SASA WADAI MIL.480 NA ASILIMIA 20 YA FEDHA ALIZOUZWA OKWI SC VILLA
UAMUZI wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), kumwidhinisha Emmanuel Okwi kuichezea SC Villa ya Uganda umeibua mapya Simba.
Katibu Mkuu wa Simba, ambaye kitaaluma ni mwanasheria, Evodius Mtawala alisema: “Hatukubali, madai yetu yamebadilika sasa tunadai mambo mawili, tupewe Dola 300,000 halafu watupe na asilimia 20 ya pesa watakayomuuza Okwi kwa SC Villa.”
Simba wameenda mbali zaidi na kudai mpaka Ijumaa wiki hii, Etoile du Sahel itawatambua wao ni nani, kwa kuwa Fifa itakuwa imeshashusha rungu lake dhidi ya timu hiyo ya Tunisia.
Mtawala alisema hawana shida na Okwi wanachohitaji sasa ni fedha zao tu ambazo ukizibadilisha kwa madafu zinakuwa Sh480 milioni.
“Tunataka salio tu, Okwi hawezi kwenda SC Villa bila ya Simba kushirikishwa. Villa wanajisumbua tu kwa kuwa mkataba wetu ambao tumeingia na Etoile du Sahel wakimuuza mchezaji lazima watupe asilimia 20 ya fedha wanayomuuza.”
Fifa imetoa baraka zake kwa Shirikisho la Soka Uganda (Fufa), kumwidhinisha Okwi kuichezea Villa kwa miezi sita, baada ya Fufa kutuma maombi Fifa wakitaka Okwi aruhusiwe kuichezea Villa kwa muda wakati sakata lake likitafutiwa ufumbuzi.
Fifa imelitaka Shirikisho la Soka la Tunisia (FTF), litoe leseni ya uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa Okwi kupitia mfumo wa kielektroniki (TMS).
SOURCE: MWANASPOTI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Sinba na fedha za okwi, nachanganyikiwa. Kwa jinsi mikataba ya sasa hivi ilivyo na uelewa wa watu wetu nina wasiwasi kama simba inadai kiasi hicho fedha, nahisi mkataba ulikuwa unahusisha performance ya mchezaji maana hainiingii akilini eti kwa kipindi chote hiki wasilipe hata shilingi. Naona villa wameona weekness wakaitumia, sasa haya maneno ya kina mtawala nayona ndo yaleyale.ya danganya toto, mara utasikia hanspope kawapandia ndege kweda dai hivi kweli biashara ishafanyika kulipwa hadi uende? wanatuzingua tu wameshalamba hela iposiku watasema
ReplyDeleteUsitoke povu bure, kwanza jiulize uelewa na elimu ya uongozi wa Simba. Huyu anayepiga kelele ni mwanasheria jina, lakini ki taaluma zero
ReplyDeleteTuliza boli!! Hata mshiko wa dogo Ngasa kulikuwa na maneno kama hayo lakini mwisho wa siku mzigo umetemwa! Cha muhimu je maandishi yapo? Na hayo maandishi yamesainiwa na watu akili timamu? pande zote? Kwa hiari bila kulazimishwa!! baada ya kuyaelewa!!!
ReplyDeleteHi.. hiyo tuzo ya okwi mbona mzungu?tuwape tuzo zenye uasilia wa kiafrika
ReplyDelete