Search This Blog
Tuesday, October 8, 2013
KOCHA ALIYEIPA ZAMBIA UBINGWA WA AFRIKA AACHIA NGAZI NA KUJIUNGA NA KLABU YA SOCHAUX
Zambia imempa idhini kocha Herve Renard kuyaacha majukumu yake katika timu ya taifa ya nchi hiyo ili kuchukua jukumu lake jipya la kuwa kocha wa klabu ya Ufaransa ya FC Sochaux.
Kocha huyo alikuwa ameanza muhula wa pili wa mkataba wake kuwa kocha wa timu ya taifa ya Zambia.
Zambia sasa imempa kazi ya muda Patrice Beaumelle kuwa kocha wa Chipolopolo. Lakini Zambia ilikuwa na wakati mgumu mwaka huu kiasi cha kuondolewa nje ya michuano ya kufuzu kwa kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil.
Beaumelle, amekuwa akifanya kazi kama kocha wa muda, na atashikilia wadhifa wa kocha mkuu wakati Chipolopolo watapocheza mechi ya kirafiki na Brazil mjini Beijing tarehe 15 Oktoba.
Shirikisho la soka nchini humo katika taarifa yake lilisema kuwa kocha "Herve Renard ameachishwa majukumu yake ili kumruhusu kuiongoza timu ya Ufaransa.''
Renard, mwenye umri wa miaka 45, alichukua wadhifa huo wa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Zambia mwaka 2008 na aliiongoza timu hiyo hadi kufika robo fainali za kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2010.
Baadae alikuwa kocha wa timu ya Angola na USM Alger kwa muda kabla ya kurejea kuwa kocha wa Zambia na kutimiza ndoto yake ya kuiongoza Zambia kunyakua kombe la taifa bingwa Afrika mwaka 2012.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment