Search This Blog

Thursday, September 8, 2011

TOKA KWENYE KIPIGO CHA BELFAST HADI KUITEKA ULAYA NA DUNIA NZIMA

Mwezi Septemba tarehe 6 mwaka 2006 Soka la Hispania lilifikia kiwango cha chini kuliko siku zote katika histoaria yake. Kipigo cha mabao 3-2 toka kwa Ireland ya Kaskazini huko Belfast kilikuwa kipigo kibaya zaidi kwa timu ambayo inatazamwa na watu kama timu inayotisha lakini haikuwahi kudhihirisha uwezo wake kwenye michuano mikubwa.
Ni wachache ambao wangeweza kutabiri kilichotokea baada ya hapo.
Miaka mitano baadae Timu ya taifa ya Hispania imekuwa bingwa wa ulaya na bingwa wa dunia na ni nani wa kusimama njiani wakielekea kutwaa ubingwa mwingine wa Ulaya, hakika hakuna.
Ushindi dhidi ya Lichteinstein umewahakikishia kufuzu kwa kombe ambalo wanaenda kulitetea na umewafanya watimize miaka mitano tangu walipofungwa na mabao matatu ya David Healy.
Usiku ule kwenye uwanja wa Windsor Park ambapo David Healy alifunga ‘Hat-trick’ ulikuwa usiku wa mapinduzi makubwa kwa aliyekuwa kocha Luis Aragones .Huku kazi yake ikiwa hatarini , mabadiliko yalilazimika kufanyika kwenye timu ya Hispania.
Akiwa ndio kwanza ametoka kwenye kashfa ya ubaguzi wa rangi baada ya kumtolea maneno ya kibaguzi Thierry Henry , kocha huyu wa Hispania alikuwa na maamuzi magumu ya kufanya.
Na katika maamuzi hayo gumu kuliko lote ilikuwa kumuacha mshambuliaji mkongwe na nahodha Raul Gonzalez. Usiku ule jijini Belfast ulikuwa wa mwisho kumuona Raul akiichezea timu ya taifa . Kama shuti lake alilopiga mwishoni mwa mchezo lisingegonga mwamba basi pengine tungeendelea kumuona Raul akiwa mchezaji wa timu ya taifa, lakini mambo yalienda kombo kwake.
Kuwekwa kando kwa Raul kulizua maswali mengi. Raul alikuwa kipenzi cha wengi na katika miaka yake yote ya kuichezea timu ya taifa hakuwahi kutwaa ubingwa wowote akiwa na timu hiyo.
Mwaka baadae kocha Aragones alilipuka kwa hasira alipouliza kuhusu Raul .’unajua Raul amecheza kwenye kombe la dunia mara ngapi?? Aragones aliuliza , Akajibiwa mara tatu, Akauliza tena ,amewahi kutwaa kombe hilo mara ngapi?? Akajibiwa kuwa hajawahi Akauliza tena na Kombe la Ulaya je?? Akajibiwa mara mbili , na amewahi kushinda mara ngapi?? Hajawahi.
Si lawama zote zinamwendea Raul , lakini mshambuliaji huyu wa Real Madrid amekuwa akicheza chini ya kiwango kwa muda mrefu kwenye timu ya taifa na mpaka kufikia kipindi hicho ilionekana kuwa muda umefika kwa Hispania kusonga mbele na kumuacha Raul. Inasemekana kuwa Raul alikuwa sababu ya mgogoro kwenye kambi ya kombe la dunia huko ujerumani mwaka 2006 ambako Hispania ilitolewa kwenye hatua ya raundi ya pili na Ufaransa
Mchezo huo ulichezwa huko Hannover mwezi juni lakini Hispania wlaibaki na Hangover mpaka mwezi septemba . Kufuatia kipigo dhidi ya Ireland ya kaskazini , na vipigo vingine dhidi ya Sweden na Romania Hispania waling’aa wakicheza mechi 35 bila kufungwa ambapo Hispania walitwaa ubingwa ulaya chini ya Aragones na wakaendelea kutwaa ubingwa wa dunia chini ya Vicente Del Bosque.
Wakati Aragones aliondoka alisema kuwa ili Hispania itwae ubingwa wa dunia ni lazima icheze kwa kutawala sehemu ya kiungo huku ikitumia mchezo wake wa kupiga pasi nyingi . Kiungo mwenye nguuv nyingi Marcos Sennna aliitwa kwenye timu kuongezea kwenye akili za viungo Xavi na Iniesta na mbele akaletwa David Villa kwenye nafasi iliyoachwa na Raul Gonzalez ambapo Villa aliunda safu ya ushambuliaji sambamba na Fernando Torres huku Villa akifunga mabao manne na Torres akifunga moja kwenye fainali ya EURO 2008 dhidi ya ujerumani .

Aragones aliachia ngazi baada ya euro 2008 ila Hispania walikuwa wazuri zaidi chini ya Del Bosque wakicheza soka la kuvutia machoni huku wakiiga mfumi unaotumika Barcelona na kutawala dunia kwa kutwaa kombe la Dunia afrika kusini .
Mpaka kufikia wakati huo Sergio Busquets na Pedro walikuwa wameongezwa na beki mwingine Gerard Pique ambaye alirudi Hispania toka Man United . Hispania ikawa timu iliyokamilika kuliko zote ulimwenguni ambayo mpaka hii leo wameendelea kutawala soka la dunia hii .

YANGA YAISHINDA TFF,YAENDELEA KUBURUZA MKIA

Yanga jana kwa mara ya kwanza walivaa jezi za mdhamini wa Ligi Kuu Vodacom, lakini zikiwa na alama nyeusi badala ya alama nyekundu


Hapo jana Yanga ililazimishwa sare ya bila kufungana na Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom.

Wakati huo huo bao la Gervais Kago liliipa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Villa Squard kwenye uwanja wa Mkwakwani Mkoani Tanga.






TENGA: SAHAUNI WAZO LA KAMPUNI KUENDESHA LIGI KUU YA TZ BARA.

Raisi wa TFF Leodegar Tenga amezitaka klabu za Ligi Kuu kusahau habari ya ligi kusimamiwa na kampuni na sasa yupo mbioni kuunda chombo kitakachoendesha ligi hiyo.
Tenga anadai migogoro inayoendelea katika nchi za Kenya na Uganda ni kwasababu ya ligi ya nchi hizo kuendeshwa na kampuni.
Akasisitiza kamati ya utendaji ya TFF ndio itakayoteua majina ya viongozi watakaounda chombo maalum cha kusimamia Ligi Kuu na Ligi daraja la kwanza ili kuwe na uwiano sawa.

Wednesday, September 7, 2011

Mbinu mbovu za mazoezi za timu za England ndio zinazoua wachezaji kwa majeraha .Kwa mujibu wa mtaalamu wa Kidachi Raymond Verheijen.

Wachezaji wengi wa kileo wanaweza kuwa wametimiza ndoto zao kwa vitu vingi , kama vile kazi ya kufanya ambayo ni ndoto ya maisha yake , akaunti ya benki inayosoma vizuri na vitu vingine vingi vinavyomfanya awe kwenye mazingira mazuri ya kufanyia kazi kuliko ilivyokuwa zamani.
Lakini tatizo kuu linalomkabili ni mbinu za mazoezi ambazo zimeegemea sana kwenye sayansi na teknolojia ya kisasa . Huu ni mtazamo wa mtaalamu wa masuala ya viungo wa Kidachi Raymond Verheijen.
Verheijen amewahi kufanya kazi kwenye timu za taifa za Uholanzi,Korea ya Kusini na Urusi pamoja na Vilabu kama Barcelona,Manchester City na Chelsea pamoja na chama cha soka cha Uholanzi.
Kwa mtazamo wake mazoezi ya kisasa hayapaswi kuzingatia sana ugumu wa mazoezi ya viungo na muda mrefu wa kuyafanya.
Yeye anasema kuwa mazoezi yanapaswa kuwa machache kwenye upande wa viungo ili kuwaweka wachezaji Fit kuchezea mpira kwa muda mrefu.
Raymond anasema siku hizi Kuna tofauti kubwa kwenye mbinu za kufundisha mpira ukilinganisha na zamani , tatizo ni kwamba watu wengi wanadhani kufanya mazoezi mengi na kwa muda mrefu ni kitu bora.
Kiasili anasema watu wanaamini kuwa kabla ya mechi unapaswa kuuandaa na kuujenga mwili.
Wanawasukuma wachezaji kufanya mazoezi wakati mwingine zaidi ya kiwango chao cha kawaida cha kufanya mazoezi ili mradi tu wawe fit kwa kuwa wanaiga mbinu za mazoezi toka kwenye michezo mingine.
Kiukweli kwenye michezo mingine kama Riadha, Mbio za baiskeli na kuogele kufanya mazoezi mengi ni vizuri lakini siyo kwenye soka.
Watu wanaufanya mchezo kuonekana mgumu pasipo na faida yoyote. Kwa sababu ya mapinduzi haya ya kisayansi watu wanaacha kufikiri kama wanadamu wa kawaida na wanaacha kufanya mambo kwa kufuata misingi.


Neno soka limeingiliwa na hili suala la Fitness na ndiyo maana mimi huwa nasema ni vyema kurudi kwenye mambo ya msingi.
Inawezekana vipi timu 10 tofauti zina makocha kumi tofauti wa masuala ya fitness na wanatumia mbinu 10 tofauti? Haiwezekani, wachezaji wanakuwa wahanga wa fitness. Mbinu za kufanya mazoezi hazipaswi kuegemea kwenye mawazo ya mtu mmoja au uzoefu wake .

Mazoezi ya soka yanapaswa kuwa ya soka na si kuongeza vitu toka mazoezi ya michezo mingine kama Hockey na Riadha.
Verheijen ambaye maisha yake ya soka yalikatishwa na jeraha la paja alilopata akiwa na umri wa miaka 17, amesomea masuala ya physiology na saikolojia ya michezo kwenye chuo cha Free Huko Amsterdam na mawazo yake yametumika kwenye kozi za kufundishia ukocha na ualimu wa michezo kwa jumla nchini kwao uholanzi.

Mtaalamu huyu mwenye umri wa miaka 39 ambaye ana Leseni ya ukocha daraja la A inayotambulika na UEFA anasema kuwa makocha wengi wa masuala ya fitness hawana histoaria ya mchezo wa soka na ametoa mifano mingi sana ya timu ambazo zina historia ya kuwa na wachezaji walioko fiti sana na wasioumia umia kila leo . Anatolea mfano timu ya Korea ya kusini ambayo amefanya nayo kazi kwenye michuano ya kombe la dunia mara 3 .
Nilipoanza kufanya kazi na Guus , nilimuuliza kwanini aliniita kufanya kazi na timu ile .Hawa watu tayari wako fit alisema , ila ngoja uone mechi yao ya kwanza ya kirafiki alisema Guus. Kwenye mchezo wao wa kwanza waliweza kucheza vyema kwenye dakika 60 za kwanza lakini baada ya hapo walichoka sana.

Kama Guus angekuwa amemleta mtu ambaye ni mtaalamu wa mazoezi angemwambia kuwa wachezaji wa Korea ya kusini wanakosa pumzi na hivyo angewakimbiza kuzunguka uwanja raundi kadhaa au angewakimbiza msituni au mlimani ili kuwapa pumzi. Ila mimi sikutafsiri tatizo la wakorea kama hivyo, kwangu niliona kuwa wakorea hawawezi kucheza kwa mtindo mmoja kwa muda wa dakika 90. Hii inamaanisha kuwa unapaswa kutumia lugha ya mchezo wa Soka kufafanua tatizo na si vinginevyo .
Tulilitatua tatizo hili kwa kucheza kwa kugawanya muda wa dakika kumi kumi, huku tukiongeza idadi ya makundi ya muda huo wa dakika kumi kumi taratibu kuanzia mara nne , tano , sita kabla ya kucheza kwa mtindo huu kwa muda wa dakika 90.


Unapaswa kuwalazimisha wachezaji kufanya masuala Fulani hata kama mwili unasema hapana , unapaswa kuwazoesha hivyo. Kama unataka kucheza mtindo Fulani kwa muda mrefu unapaswa kufanya mazoezi ya kuucheza mtindo huo uwanjani kwa muda mrefu.
Mbinu hii ya kugawanywa muda ilibuniwa na Mwalimu wa kirusi ili kuzuia kufanya mazoezi zaidi na kumfanya mchezaji aperform kwa kiwango cha juu.

Kama unataka kupiga hatua kama mchezaji kitu muhimu cha kufanyia kazi ni spidi ya vitu unavyofanya kama mchezaji. Na hili linaonyesha kuwa soka ni mchezo wa kiwango cha matukio na sio mchezo wa kuvumilia mateso ya mazoezi. Kwenye mchezo wa kuvumilia mazoezi magumu unapaswa kufanya mazoezi kwa muda mrefu lakini kwenye mchezo wa kiwango unapaswa kuzingatia kiwango cha mazoezi unayoyafanya.
Kama unataka kuongeza kasi ya matendo yako uwanjani uchovu ni adui yako namba moja . kwa kila kipindi cha mazoezi unapaswa kuwa fresh na kama unataka kuongeza kiwango kama mchezaji unahitaji pia kuwa fresh.


Kwa maneno mengine ‘chache ni zaidi’ . Njia pekee ambayo mchezaji atapiga hatua kwenye kiwango chake ni kwa kufanya mazoezi yaliyo bora na si kufanya mazoezi zaidi .
Mwangalie Arjen Robben ambaye ametumia muda mwingi akiwasumbua madkatari pale Stamford Bridge kuliko alivyokuwa anawasumbua mabeki kwa miaka yake mitatu aliyokuwa Stamford Bridge.

Akiwa Chelsea walimuita ‘the man of glass’ , mwaka jana alicheza Bayern Munich . Walichofanya pale ni kupunguza mazoezi aliyokuwa anayafanya . Alicheza kwenye kiwango cha juu sana na walitwaa mataji kwa sababu yake .
Ghafla Robben hakuwa majeruhi tena.


Swali ni kwamba Robben alikuwa ‘mchezaji wa glassi au makocha waliomfundisha ndio walikuwa makocha wa glassi? Wachezaji kama Robben na Va Persie hutumia nguvu kwenye matendo yao kuliko wachezaji wengine .
Wanapofanya mazoezi kama wachezaji wengine matumizi yao ya nguvu yanakuwa mara mbili zaidi hivyo ni lazima uwapunguzie mazoezi wafanye angalau asilimia 50 na ni kitu ambacho Bayern walifanya kwa Robben .

Unapokuwa umechoka ishara toka kwenye ubongo wako kwenda kwenye mwili wako inakuwa inasafiri taratibu kuliko kawaida . Kama ishara inakwenda taratibu inahatarisha viungo vyako kwakuwa unatumia nguvu nyingi kuliko uwezo wako wa kawaida na hivi ndio unasikia vitu kama magoti,enka,nyonga, nyama za paja na vingine ving vinaumia .

Timu nyingi za ligi kuu nchini England zinatumia teknolojia ya kompyuta kupima kiwango cha ‘perfomance ‘ ya mchezaji na hata kiwango cha uchovu . Pamoja na vipimo hivyo vya sayansi na teknolojia mpya bado kulikuwa na wachezaji karibu 108 ambao rekodi zilisoma kuwa hawakuwepo kwenye viwango vyao vya kawaida kwenye wikiendi ya desemba , nah ii ni sawa na asilimia 5.4 ya wachezaji kwenye kila timu, mahesabu haya yanaonyesha kuwa kuna tatizo kubwa.

Aston Villa na Tottenham ndio walioathirika sana kuliko wengine huku wakiwa na karibu wachezaji 11 wenye majeraha na Arsenal walimpoteza beki wao Kieran Gibbs kwa jeraha la Enka . Kwa ujumla timu hizi tatu ukitazama kwa undani ndio zenye tatizo la kuwapa wachezaji mazoezi magumu kuliko inavyotakiwa.

Sawa kuna watu waliowahi kuvunjia mifupa vibaya kama Eduardo na Ramsay lakini vipi kuhusu Robin Van Persie ambaye amekaa nje kuliko hata hawa wachezaji waliowahi kuvunjika vibaya , na Van Persie majeraha yake si ya kuvunjika mifupa , amekuwa na matatizo ya misuli san asana .

Verheijen anamtumia mchezaji mwingine wa kidachi Rafael Van Der Vaart kama mfano . Verheijen anakataa katakata imani ya Tottenham kuwa mchezaji huyu hayuko ‘fit’ .
Hana uzito usio wa kawaida , namjua tangu utoto wake , nilifanya naye kazi mwaka 2001 wakati nikisaidia kwenye timu ya Uholanzi ya Under 20 kwenye kombe la dunia huko Argentina na jinsi alivyokuwa kimwili .

Van Der Vart amekuwa na msimu mrefu sana na hakupumzika kwa kuwa alilazimika kucheza kwenye kombe la dunia ambako timu yake ilicheza mpaka fainali. Fitness yake ilikuwa juu lakini hakuwa Fresh kwa kuwa hakupata muda wa kutosha kupumzisha mwili wake.

Wachezaji wanaocheza kombe la dunia mara zote wanakuwa fiut lakini uchovu ndio adui yao, na uchovu huufanya mwili upoteze mawasiliano baina yake na ubongo na hapo ndio majeraha hasa ya misuli na nyama yanapokuja na kuwamaliza wachezaji hawa.
Wanachohitaji ni muda wa kutosha wa kupumzika na mazoezi ambayo yanazingatia hilo.


Mazoezi kwa kipindi kimoja kwa siku na mazoezi haya hayapaswi kuwa na lundo la mazoezi magumu ya viunngo na kunatakiwa kuwa na muda mwingi katikati ya vipindi vya mazoezi wa kuuruhusu mwili kurejea kwenye hali yake ya kawaida baada ya mazoezi.Verheijen anasema kuwa alitumia mfumo huu akiwa na Barcelona ya Frank Rijkaard mwaka 2004 baada ya michuano ya Euro.

Verheijen amewahi kufanya kazi kwenye ligi kuu ya England ambako alikuwa kwenye timu ya Man City chini ya Mark Hughes kwenye mzunguko wa pili wa msimu wa mwaka 2009.
Katika kipindi cha Julai na Novemba mwaka jana Man City walikuwa na rekodi bora kwenye ligi kuu ya wachezaji kutoumia.


Pia timu hii ilikuwa na takwimu bora kwenye mbio wakati wa mechi na walifanya mazoezi mara moja kwa siku.Mazoezi yalikuwa na kiwango bora na hayakuwa ya kuchosha , kwa muda wote huo Man City walikuwa na mchezaji mmoja tu aliyeumia na alikuwa Benjani ambaye Verheijen anakiri kuwa jeraha alilopata lingeweza kuzuilika

Alipokuja Roberto Mancini aliongeza mazoezi ya nguvu wakati alipokuja , jambo ambalo lilipingwa na wachezaji kama Craig Bellamy na Carlos Tevez. Mancini aliongeza mazoezi kutoka kwenye kipindi kimoja kwenda kwenye vipindi viwili na pia aliongeza muda wa mazoezi hayo toka kwenye dakika 75 hadi masaa mawili. Katika siku zake 10 za kwanza kulikuwa na wachezaji takribani 10 walioumia , hakuna mwandishi wa habari anayechambua suala hili, huu ni upuuzi.
Wakati Mancini alipokuja bado nilikuwa City japo si kwenye nafasi yangu niliyokuwa nayo wakati wa Hughes anasema Verheijen,.


Lakini baada ya wiki mbili na majeraha kwa wachezaji yakiongezeka niliamua kuondoka kwa kuwa watu walinihusisha na majeraha yale kwa wachezaji, anaongeza Verheijen.
City walilaumu kipindi cha Krismasi kuwa ndio kilisababisha majeraha kwa wachezaji , kwa mujibu wao majeraha yale yasingeweza kuzuilika.
Kwa sasa majeraha haya yamepungua kwa sababu wana mechi nyingi katikati ya wiki na hivyo wamelazimika kupunguza muda wa mazoezi kuwa mara moja na si mara mbili
Anachojaribu kueleza mtaalamu huyu ni timu hasa za nchini England kuondokana na dhana potofu kuwa ‘fitness’ ya mchezaji inaongezeka kwa vipindi virefu vya mazoezi magumu , wachezaji wanaumia kwa sababu hii na si sababu nyingine , maisha yao ya uchezaji yanakuwa mafupi kwa sababu hii na si sababu nyingine .
Makocha wengi wanafanya hivi , hawazingatii umri wa mchezaji na vitu vingine muhimu , kila mtu anataka mbinu hizi za mazoezi ambazo hazisaidii.
Mtaalamu huyu anafanya kazi ya kumuweka fit Craig Bellamy kwa siku mbili za wiki kwa gharama za mchezaji huyu , na amekuwa mstari wa mbele kujaribu kuleta mabadiliko kwenye mazoezi .

Mtwa Kiwhelu Akitaja kikosi chake Bora cha Yanga.





Steven Nemes
Alikuwa kipa mahiri na aliyetisha langoni. Hakuwa mtu aliyetaka masikhara uwanjani.

Mtwa Kihwelo
Mimi mwenyewe nilikuwa sitaki mzaha katika upande wa kulia na nilicheza kama beki wa kupanda na kushuka.

Ken Mkapa
Beki mrefu aliyekuwa katika fomu enzi zake na ambaye alikuwa roho ya Yanga upande wa kushoto. Alicheza soka la uhakika la kupanda na kushuka.

Willy Mtendamema
Alikuwa mahiri katika safu ya ulinzi na muda wote alionekana kuwakumbusha wenzake majukumu yao vema.

Issa Athuman
Marehemu kwa sasa. Alikuwa mchezaji tegemeo katika safu ya ulinzi. Namkumbuka kwa kuwa mkali sana kama ukifanya makosa ya kijinga.

Method Mogella
Marehemu kwa sasa. Alikuwa kiungo mtaratibu uwanjani huku akicheza sana soka la akili. Atakumbukwa na wengi kutokana na kipaji chake murua.

Zamoyoni Mogella
Alikuwa hana mfano uwanjani na alikuwa roho ya timu. Vile vile alikuwa mshauri mzuri kwa wachezaji wengine.

Steven Mussa
Marehemu kwa sasa. Alikuwa mchezaji mtaratibu lakini mshindani uwanjani. Alikuwa kiungo maridadi sana na aliweza kuunganisha timu muda wote bila ya kuchoka.

Said Mwamba
Marehemu kwa sasa. Wengi wanakifahamu kipaji cha Said. Alikuwa bora sana uwanjani na asiye na mzaha kama utafanya makosa ya kijinga.

Mohamed Hussein
Alikuwa mfungaji hodari wakati huo. Asingeweza kupoteza nafasi mbili za wazi kama washambuliaji wa kileo.

Edibily Lunyamila
Wote tunafahamu sifa za Edibily. Ndiye aliyekuwa nyota wa michuano ile. Alikuwa fiti sana Eddy na alitubeba kwa kiasi kikubwa.

NIZAR AMKABIDHI JEZI RAISI Dr JAKAYA KIKWETE




























Tuesday, September 6, 2011

MIKAEL ARTETA NA NJIA 5 ZA KUWA IMARA KIAKILI MCHEZONI



Kiungo mpya wa Arsenal Mikael Arteta anajaribu kutoa mafunzo ni jinsi gani ya kuwa imara kiakili kipindi cha michezo migumu.


1: FIKIRIA KUSHINDA

“Kitu muhimu zaidi kabla ya mechi ni kwenda uwanjani ukiwa mentality ya ushindi.Huwezi ku-control pressuere ya mchezo hivyo ni vizuri kuji-control mwenyewe na kitakachoenda kutokea mchezoni.Kama unajiamini, then kipaji chako kitaonekana tu na uta-perform vizuri.”


2: USIOGOPE WALA USIWE NA JAZBA BAADA YA KUCHEZEWA RAFU KWA MARA KWA MARA.

“Mpinzani wako anapokuchezea vibaya hakikisha anaadhibiwa mapema ili ajiadhari kupata red card.Kufanya hivyo, kutampeleka sehemu ambayo wewe unataka akufanyie madhambi, ndani au pembeni ya penati boksi.”


3: JINSI YA KUPIGA PENATI

“Kwa kawaida mpigaji penati uwa na advantage kubwa zaidi.Acha mambo yote ya nje uwanja pembeni, na akili yako yote iwe kwenye na mpira-jinsi ya kuupiga, wapi utaupiga na namna ya kufunga goli.”


4: KAMA MCHEZESHAJI, CHEZA KWA UTULIVU UKIWA UNATAFUTA GOLI.

“Usi-panic, cheza kwa utulivu ndani ya aina ya mchezo wa asili.Usijipe pressure kutoa pasi ya mwisho, wachezaji wengine uwanjani wanaweza kufanya hivyo pia.”


5: USIJARI MANENO YA MPINZANI WAKO

“Ukiwa unajari mno maneno anayoyatoa mpinzani wako kiwanjani, utakosa concentration uwanjani, na hilo ndilo lengo lake.Jibu maneno yake kwa kucheza vizuri.”

JKT Ruvu 3 Coastal Union 0,Nyoso apata timu South Afrika.


Klabu ya Simba inatarajia kuvuna mamilioni mengine kutoka kwa beki wake ambaye pia huchezea 'Taifa Stars', Juma Nyosso baada ya kufikia muafaka na Klabu ya Platnum Stars inayoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini, ambayo imeonesha nia ya kumsajili.

Hapo jana JKT Ruvu ilipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal union ushindi ambao uliwapeleka kileleni mwa msimamo wa ligi kuu y a VODACOM kwa kufikisha pointi 9.
mabao ya JKT Ruvu yalifungwa na Sostenes Manyasi,Rajabu Chau na Emmanuel Lucas.

MARSH AWAMWAGIA UPUPU MAKOCHA WA KIGENI




Kocha msaidizi wa timu ya soka ya taifa, Taifa Stars Syllvester Marsh amesema moja ya sababu inayochangia timu ya taifa kufanya vibaya ni ubishi wa makocha wa kigeni.

Akihojiwa na Sports xtra ya Clouds fm, Marsh alisema kuwa kitendo makocha wa kigeni kudharau ushauri wa wazawa kinatokana na wao kuamini wazawa hawajui chochote kuhusu masuala ya soka.

Alisema kuwa alibaini kuwepo kwa fikra hizo zilizotawala miongoni mwa makocha wazungu wakati alipokuwa akifanya kazi na aliyewahi kuwa kocha wa timu za taifa za vijana, Marcus Tino baada ya kumwambia kwamba anashangaa kuona Tanzania ina makocha wazuri.

"Niseme ukweli kwamba, kuna tabia ya makocha wakigeni wanaokuja hapa kudharau ushauri wa wazawa, hii inatokana na wao kuamini pengine sisi hatujui chochote kuhusu soka.

"Ukweli makocha wakigeni wanaamini kwamba mpaka wao wanachukuliwa maana yake labda hapa hakuna kocha mzuri, kumbe si hivyo, Congo juzi tu wamemtimua kocha wao kwa sababu hizo hizo kwamba hashauriki.

"Kwa mfano wakati ule nafanya kazi na Tinoco aliwahi kuniambia kwamba kumbe Tanzania kuna makocha wazuri akionekana kushangaa, lakini sio suala la kulaumu kwasababu pengine mazingira ndiyo wanayakuta yanawafanya wafikiri hivyo,"alisema Marsh.

Marsh pia alizungumzia tabia ya makocha wa kigeni kutodumu muda mrefu kwa kusema kuwa, hilo linasababishwa hasa pale wanapokutana na mazingira tofauti na yale waliyoyategemea kuyakuta wakati wanatoka kwao.

"Mimi ni mzawa ninaweza kuvulimia kwasababu naijua vizuri hali halisi ya nchi yangu, lakini wao inakuwa vigumu kwasababu unakuta amezoea kupata kila kitu huko kwao sasa anapohitaji kitu fulani hasipotimiziwa hawezi kukaa,"alisema

Marsh amekuwa kocha msaidizi kwenye kikosi cha Taifa Stars kwa takribani miaka mitano tangu enzi za kocha Mbrazil Marcio Maximo, pia amewahi kuifundisha timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys akiwa kocha msaidizi wa Abdalah Kibadeni pamoja na kuzifundisha timu kadhaa za ligi kuu ikiwemo Kagera Sugar.



Monday, September 5, 2011

Washindi wa GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE




Washindi wa shindano la GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE waliopata nafasi ya kwenda nchini Afrika ya Kusini kuiwakilisha Tanzania:

014 - SULTAN MOHAMED SULTAN
- MANSOUR SEIF MANSOUR

003- HAFIDH MTORO MKAMBALA
- RAJAB SELEMAN RAJAB

011 - JUMA NASSOR JUMA
- MASUDI AMLANI MASUDI

002 - AMIRI ALLY AMIR
- IMAN JOSEPH MANDU

006 - NELSON ALLEN KESSY
- RAMADHANI RAMADHAN MTIBIRO

021 - LUKUBA GEORGE JOEL
- FREDY JORDAN NGULWA

007 - ALAWI OMAR RASHID
- ABDUL OMARI MADOHORA

009 - ALLY BIN ALLY MATUMBI
- RICK JOHN SANGA



















































MAPATO STARS v ALGERIA


Pambano la mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Equatorial Guinea na Gabon kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Algeria (Desert Warriors) limeingiza sh.148,220,000. Mechi hiyo ilichezwa Septemba 3 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mashabiki waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo ni 29,892. Viti vya kijani ambavyo kiingilio kilikuwa sh. 3,000 ndivyo vilivyovutia mashabiki wengi ambapo 17,650 ikiwa ni zaidi ya nusu ya mashabiki wote walinunua tiketi kwa ajili ya viti hivyo.

VIP A ambapo ndipo kulikokuwa na kiingilio cha juu cha sh. 30,000, jumla ya mashabiki 394 walinunua tiketi kwa ajili ya eneo hilo. Viti vya bluu ambapo kiingilio kilikuwa sh. 5,000, mashabiki walionunua tiketi walikuwa ni 8,166.

Viingilio vingine katika pambano hilo vilikuwa sh. 7,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 VIP C na sh. 20,000 VIP B.

TWIGA STARS YAPOTEZA MCHEZO WA KWANZA KWENYE ALL AFRICAN GAMES


Timu ya wanawake ya Taifa ya Tanzania (Twiga Stars) imepoteza mechi yake ya kwanza ya michezo ya All Africa Games (AAG) baada ya leo kufungwa mabao 2-1 na Ghana katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Machava, jijini Maputo.

Kwa mujibu wa Meneja wa Twiga Stars, Furaha Francis hadi mapumziko timu hiyo ilikuwa nyuma kwa bao 1-0. Mwanahamisi Shuruwa aliisawazishia Twiga Stars dakika ya 85, lakini Ghana ikapata bao la pili dakika tatu kabla ya filimbi ya mwisho.

Twiga Stars itacheza mechi yake ya pili Septemba 8 mwaka huu dhidi Afrika Kusini. Mechi ya mwisho katika hatua hiyo ya makundi itakuwa Septemba 11 mwaka huu dhidi ya Zimbabwe
.

LUKAKU, FORLAN NA HARGREAVES KUWA WATAZAMAJI KWENYE CHAMPIONS LEAGUE



Wanasoka Diego Forlan wa Inter Milan na kiungo mpya wa Manchester City, Owen Hargreaves pamoja na mshambuliaji wa Chelsea, Romelu Lukaku ni miongoni mwa wachezaji walionguliwa kwenye vikosi vya timu zao kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa.

Forlan aliyesajiliwa na Inter hivi karibuni aliichezea Atletico Madrid kwenye kusaka tiketi ya Europa Ligi kabla ya kuhamia Italia.Mshambuliaji huyo wa Uruguay alichezea Atletico dhidi ya timu ya Norway ya Stromsgodset katika hatua ya tatu ya kusaka kufuzu kwa michuano ya Europa.

Alijiengua kwenye mchezo dhidi ya Vitoria Guimaraes wakati huo akiwa na mazungumzo na klabu hiyo ya San Siro, lakini sheria ya UEFA inamzuia mchezaji huyo aliyecheza Europe kuichezea Inter sasa labda hadi mwakani.

Inter imepagwa Kundi B pamoja na CSKA Moscow, Lille na Trabzonspor, lakini bado safu yao ya ushambuliaji ipo imara kwa kuwepo kwa Giampaolo Pazzini, Diego Milito, Mauro Zarate na chipukizi kwenye miaka 18, kutoka Uholanzi, Luc Castaignos .

Hargreaves na Lukaku pia wameachwa kwenye vikosi vyao kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa.
Hargreaves, 30, aliyejiunga na City wiki iliyopita akiwa na tumaini na kurudi kwenye kiwango chake baada ya kuachwa na Manchester United.

Kiungo huyo wa zamani wa England bado anakazi kubwa ya kurudi kwenye kiwango chake baada ya kuwa majeruhi ya goti kwa muda mrefu na City wameamua kutomweka kwenye orodha 17 watakaocheza Ligi ya Mabingwa.

Wachezaji wengine nane kati ya 25 ni lazima wawe ni wale wa akiba wa nyumbani au chipukizi.

Kuondolewa huko kwa Hargreaves kunamfanya hakose mechi mbili za Kundi A dhidi ya timu yake ya zamani Bayern Munich, wakati City itapocheza kwa mara ya kwanza michuano hiyo.

Hata hivyo, kocha wa City, Roberto Mancini anayo nafasi ya kumtumia kwenye kikosi chake cha Januari kama atafanikiwa kufuzu kwa hatua ya makundi.

Wakati huohuo, mshambuliaji wa kimataifa wa Ubelgiji, Lukaku pia ameondolewa kwa kushangaza kwenye kikosi cha Chelsea kwa ajili ya mashindano hayo hatua ya makundi.

Lukaku aliyesajiliwa kwa pauni 18 milioni kutoka Anderlecht mwezi uliopita, ataweza kucheza kwenye 16 bora, lakini Chelsea imewajumuisha wachezaji waliosajili siku ya mwisho ya usajili Oriol Romeu, Juan Mata na Raul Meireles kwenye kikosi chao cha wachezaji 22.

SENEGAL, IVORY COAST WATANGULIA EQUATORIAL GUINEA AND GABON, MISRI WAVULIWA TAJI



Timu ya Senegal imefuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani shukrani kwa mabao mawili ya Moussa Sow na kuisaidia nchi yake kushinda 2-0 dhidi ya DR Congo, huku Misri ikiaga rasmini baada ya kufungwa 2-1 na Sierra Leone.

Mfungaji bora wa msimu uliopita wa Ligi Kuu ya Ufaransa Ligue 1 alionyesha thamani yake kwenye ardhi ya nyumbani baada ya kupachika mabao hayo mawili katika kipindi cha kwanza na kuamsha shangwe kwenye jiji la Dakar na kuifanya Senegal kuongoza Kundi E.

Wanaungana na Botswana, Burkina Faso na Ivory Coast kuunda timu 16 zitazocheza michuano hiyo pamoja na wenyeji wawili Equatorial Guinea na Gabon.

Burkina Faso ilifuzu hata kabla ya kuanza kwa mpira baada ya Namibia kuichapa Gambia 1-0 jijini Windhoek kwenye mechi iliyochezwa mapema.

Mafanikio ya Burkina Faso na Senegal yalifunika kwa ushindi wa Libya, ikicheza timu mpya chini ya bendera mpya ya taifa walifanikiwa kufufua matumaini yao.

Libya ilifanikiwa kuichapa Msumbiji kwa bao1-0 jijini Cairo katika mechi Kundi C iliyochezwa huku milango ya uwanja ikiwa imefungwa.


Mabingwa watetezi Misri wameutema ubingwa huo baada ya kuchapwa 2-1 ugenini na Sierra Leone, lakini walishaonyesha kukata tamaa kwa sababu ya kuwatumia kikosi cha wachezaji wa umri wa miaka 23 kwenye mchezo huo uliofanyika Freetown.

Cameroon ilitoa namachungu yake kwa kuinyuka Mauritius 6-0, nayo Ivory Coast walitoa salamu za pole kwa majeruhi Didier Drogba baada ya chipukizi Gervinho kuongoza mauaji ya mabao 5-0 dhidi Rwanda.

Mali ikiwa na kiungo wa Barcelona, Seydou Keita wamejiweka vizuri baada ya kushinda 3-0 nyumbani dhidi ya Cape Verde jijini Bamako huku Tunisia ikiweka njia panda baada ya kutoka suruhu na Malawi.

GUINESS FOOTBALL CHALLENGE YAZINDULIWA DAR


Wapenzi wa kinywaji mahiri cha Guinness na mashabiki wakubwa wa mpira wa miguu nchini Tanzania, kwa mara ya kwanza leo wamekusanyika katika viwanja vya Leaders kwa ajili ya kushiriki katika GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ ambayo imezinduliwa leo katika viwanja hivyo.

Washiriki wengi wamejitokeza ili kujisajiri na kuonyesha maajabu ya mpira wa miguu katika kipindi hiki kabambe cha Televisheni ambacho kinaangaliwa na kuwavutia watu wengi barani Afrika,Shindano hili litawapatia mashabiki nchini Tanzania nafasi ya kujitokeza na kuonyesha mapenzi yao ya dhati katika mpira wa miguu na kushindana na mashabiki wakubwa wa mpira wa miguu kutoka Kenya na Uganda huku kujishindia mamilioni ya fedha.

Katika picha juu kushoto ni Meneja wa kinywaji cha Guinness Moris Njowoka akumuelekeza jambo Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Serengeti Breweriers Ephraim Mafuru wakati wa shindano hilo leo.

Baada ya kupatika na timu nane zitakazokuwa na watu wawiliwawili , timu hizo zikishiriki katika shindano hilo kupitia Luninga (Television) likirushwa mara moja kila wiki Televisheni kwa muda wa wiki nane, na kila wiki atapatikana mshindi mmoja atakayejishindia Dolla za Kimarekani 50,000.


HAPA NIKIWA NA MKURUGENZI WA MASOKO WA SERENGETI BREWERIERS EPHRAIM MAFURU PAMOJA NA MENEJA WA KINYWAJI CHA GUINESS MORIS NJOWOKA.
WALIODHURIA PIA WALIBURUDIKA NA VINYWAJI KUTOKA GUINESS

MATCH REVIEW: TAIFA STARS VS ALGERIA



Timu ya taifa ya Tanzania imecheeza dhidi ya Algeria mchezo ambao umeisha kwa sare ya bao moja kwa moja .

Mwanzoni mchezo ulionekana kama umetawaliwa na watanzania kwa kiasi kikubwa hasa ukizingatia kuwa uwanjani walikuwepo wachezaji wasiopungua watano ambao wanaocheza soka la kimataifa kwa upande wa Tanzania , kingine ambacho kilionekana labda kuwachagiza wachezaji wa Tanzania kucheza vizuri ilikuwa umuhimu wa mechi yenyewe ambapo Tanzania ilikuwa na pointi 4 ikihitaji ushindi na kutazama matokeo ya mechi kati ya Moroco na Jamhuri ya Afrika ya kati ili kufufua matumaini ya kufuzu kwa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika .

Wachezaji wa Stars walionekna kuonana vizuri kipindi cha kwanza huku wachezaji wote wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi wakionekana kung’aa sana hasa Nizar Khalfan na Mbwana Sammata ambao walishirikiana kuipa Stars bao la kuongoza huku Mbwanna Sammata akifunga bao lake la nne katika mchezo wake wanne akiwa na timu ya taifa ya wakubwa .

Kulikuwa na maelewano mazuri sana baina ya mabeki wawili wa kati kwenye kipindi cha kwanza na hili lilichangiwa na Walgeria kutumia kipindi hicho kuwasoma wapinzani wao na kutumia kipindi cha pili kama wakati wao wa kutawala mchezo , na pia Mlinda lango Juma Kaseja alikuwa salama na maelekezo yake kwa mabeki wake kwenye jinsi ya kujipanga na kukaba yalionekana kueleweka sana .

Wakati kipindi cha kwanza kilipoisha mchezaji wa Algeria anayecheza soka la kulipwa kwenye klabu ya Milwall Hamer Bouzza aliamka kwenye benchi na kwenda kupasha misuli moto uwanjani huku wenzie wakienda kwenye chumba cha kubadili nguo , mwalimu msaidizi wa Algeria alionekana akimpa maelekezo ya peke yake wakati huo huku akiwa karibu nae akionekana kumuonyesha vitu Fulani kutoka kwenye ubao mdogo aliokuwa ameushikilia mkononi.

Hii ilitoa ishara ya kuwa Hamer Bouazza hajakaa benchi kama mchezaji baki wa ziada la hasha bali alikaa benchi kama silaha muhimu ya siri kwa Algeria na Watanzania walitambua hilo dakika chache baada ya kipindi cha pili kuanza kwani huyu jamaa alifunga bao jepesi akitumia uwezo mkubwa wa kusoma mgongano wa mawasiliano baina ya mabeki wawili wa kati Aggrey Morris na Juma Nyosso mgongano wa mawazo uliotokea sambamba na uwezo mdogo wa vijana hawa wa kuusoma mchezo kwenye nafasi yao. Bouazza hakufanya ajizi , aliukwamisha mpira wavuni na kusawazisha kwa upande wa timu yake huku akiwaacha watanzania 11 uwanjani na wengine takribani 30,000 kwenye majukwaa wakiwa hawana la kufanya huku wengine wakimtupia lawama mwamuzi kwa kudhani labda mfungaji aliotea lakini hakuwa ameotea na lilikuwa bao safi.

Mwalimu wa Taifa Stars Jan Poulsen alifanya mabadiliko kwa kumtoa Danny mrwanda na kumuingiza Mrisho Ngassa . Mabadiliko haya yalikuwa na walakini ndani yake kwa sababu kuu mbili . Kwanza Mrwanda hakuwa amechoka na alikuwa akielewana vyema tu na wenzie huku tatizo pekee lililokuwa likimkabili likiwa kimo kidogo huku akipambana na wapinzani wenye vimo vikubwa hali iliyokuwa inamlazimu kutumia nguvu nyingi ambazo zilikuwa zikitumiwa na Walgeria kujiangusha na kupata faulo nyingi. Pili kama mwalimu alifanya mabadiliko kwa kuzingatia tatizo hili basi hakulisuluhisha kwa kumuingiza Ngassa ambaye kama ilivyo kwa Mrwanda hana kimo zaidi tu ya kuinyima timu mtu ambaye ana uwezo wa kupiga mashuti na kumuingiza mtu ambaye hakuwa na uwezo wa kupiga mashuti na hivyo kuinyima timu mabao ambayo pengine yangewezwa kwa mtindo huu.

Kulikuwa na mabadiliko mengine ambapo Shaban Nditi alitolewa na akaingia Athumani Machupa, labda ingeeleweka kama kwenye nafasi ya Mrwanda angeingia machupa na si Ngassa . Kwa mtazamo wa kiufundi ingekuwa na faida kama labda angepumzishwa Abdi Kassim Babi na si Mrwanda .

Kwa upande wa wapinzani mabadiliko yaliyofanywa yalikuwa makini na yaliyozingatia utaalamu mkubwa wa kuusoma mchezo na nini kilihitajika kutoka kwenye mchezo huo . Aliingia Bouazza ambaye ni mfungaji na alifanya kazi yake kwa kufunga goli na kutengeneza nafasi zaidi za kufunga lakini aliingia mchezaji mwingine aliyekuwa ameletwa ili kusaidia umiliki wa mpira ambao Algeria walikuwa nyuma kipindi cha kwanza na hilo kweli lilitokea kwani Algeria walimiliki mpira kipindi cha pili .

Wachezaji wa Taifa Stars wanaocheza nje ya nchi walikuwa kivutio kikubwa kwa jinsi walivyoonyesha mabadiliko makubwa yanayoleta matumaini kwa upande wa Tiafa Stars . Wote kwa pamoja wlaionekana kuleta kitu tofauti kwenye timu huku wakijaribu kutumia uzoefu wanaoupata kutoka huko wanakocheza.

Upande wa mtu aliyeonekana kulemewa kidogo na mechi ilikuwa kwa nahodha na kaka mkuu wa timu Shadrack Nsajigwa Fusso ambaye kidogo alionekana kuwa na kasi tofauti na ile ya mchezo kwa ujumala , ya wenzie kwenye timu nay a wapinzani. Labda ni uchovu unaotokana na kucheza mechi nyingi kwenye kipindi kifupi pasipo kupumzika lakini pengine saa imeanza kusoma tofauti kidogo yaani pengine umefikia wakati wa kupumzika kwa majukumu ya kuichezea timu ya taifa kwa mkongwe huyu.

Kwa jinsi timu ilivyocheza kwanza faida kubwa ya kucheza nje ya nchi imeonekana nap engine hii ni changamoto kwa viongozi wa timu kuwa wepesi wa kuwatafutia wachezaji wao wanaocheza hapa nyumbani timu za kucheza nje ya nchi lakini tatizo kubwa limeendelea kuwa kukosa umakini mchezoni na hili ni tatizo litakaloendelea kuihukumu timu ya tiafa ya Tanzania . Kipindi cha pili kuna nafsi kama tatu za uhakika za kufunga zilizotengenezwa lakini kwanini wavu haukucheka ni wachezaji wa Taifa stars tu ndio wanaojua lakini kama umakini ungekuwepo ubao wa matokeo ungesoma tofauti kidogo.

MATCH REVIEW

Sunday, September 4, 2011

TAIFA STARS ILICHEZA VIPI DHIDI YA ALGERIA

Taifa Stars imetoka sare ya 1-1 dhidi ya Algeria katika mchezo wa kutafuta nafasi ya kucheza kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2012 litakalofanyika Gabon na Equatorial Guinea. Wachezaji wanaocheza soka nje ya nchi walionekana kung’aa sana kuliko wenzao kwenye mchezo huu. Tutazame jinsi wachezaji hawa walivyocheza kila mmoja kwa ubinafsi wake .




1: Juma Kaseja.




Mwanzoni alionekana kuwapanga vizuri mabeki wake kama ilivyo kawaida yake , akiwapigia kelele na kuwapongeza katika nyakati tofauti kadri ilivyostahili . Kazi yake nzuri iliharibiwa na jinsi mabeki wake wa kati Aggrey Morris na Juma Nyosso walivyomuangusha kwa kushindwa kuusoma mchezo na kuruhusu bao la kusawazisha , kwenye kipindi cha kwanza hakuwa mchezoni sana kwa kuwa muda mrefu mchezo ulitawaliwa na Taifa Stars na kwenye kipindi cha pili kwa nyakati tofauti alikuwa akitoka na kuipanga safu yake ya mabeki vyema hasa baada ya kufungwa bao .







2: Shadrack Nsajigwa.




Huu ulikuwa mchezo mgumu sana kwake kwa kuwa alionekana kupambana sana mpaka kufikia kuchoka . Nsajigwa ni mtu ambaye silaha yake kubwa ni nguvu nyingi na juhudi binafsi . Kwa jinsi alivyocheza dhidi ya Algeria alionekana kuchoka sana na hili lilikuwa dhahiri kipindi cha pili kwa kuwa Algeria kama ilivyo kawaida kwa timu za uarabuni huwa wanabadilika na kasi ya mchezo na walitumia sana upande wake kwa kuwa waliona kabisa kuwa umelemewa na mara nyingi kiungo Nizar Khalfan alikuwa anakuja kumpa tafu . Pengine ni ishara kwa kocha kuanza kumtafuta mbadala wa kaka fusso mapema kwani anaonekana kuwa mbali na siku zake za kuisaida timu ya taifa kama mchezaji kamili wa kimataifa , umefikia wakati kwake kuchagua kupunguza uzito wa timu ya taifa na kubaki na klabu yake ya Yanga .







3: Amir Maftah.




Kwa uwezo wa asili Amir ni moja ya wachezaji wenye uwezo mkubwa sana na kipaji halisi . Tatizo kubwa la Amir ni ‘mambo’ yake mengi aliyo nayo anapokuwa uwanjani , mambo ambayo yanamfanya ashindwe kutekeleza majukumu yake ya msingi kama beki wa pembeni . Kwa kawaida beki wa pembeni hupaswa kuipandisha timu na kurudi kukaba lakini Amir hupanda sana na anajisahau na hili linampunguzia alama kwa watu wanaosoma mchezo wake . kwa mchezo dhidi ya Algeria alicheza vyema lakini tatizo hili lilionekana .




4: Juma Nyoso.




Moja ya mabeki shupavu ambao nchi hii inao kwa sasa. Anajua sana kukaba na pale anapocheza na mtu anayejua jinsi ya kumtuma na kumuelekeza cha kufanya basi Nyoso ni namba 4 mzuri sana . Tatizo lake ambalo linaonekana anapoichezea timu ya taifa ni uwezo wake mdogo wa kuusoma mchezo . Mara nyingi sana huwa anaingiliana na beki mwenzie na pia ana tatizo la kutegea hali ambayo ilisababisha bao la kusawazisha ambapo yeye na beki mwenzie na hasa yeye kwa kuwa alikuwa mkabaji huku mwenzie akisimama kwenye ‘free role’ walishindwa kusoma malengo ya wapinzani wao . Laiti kama Nyoso angeelewa haraka anachokuja kufanya Bouazza angemkaba ‘zero distance’ na pengine bao la kusawazisha lisingetokea .




5: Aggrey Morris.




Ni moja ya mabeki wenye umakini wa hali ya juu sana . Wakati Victor Costa alipoumia na kukaa nje kwa muda mrefu mbadala wake alikuwa mtu huyu . Pengine uzoefu mdogo wa michezo ya kimataifa umemhukumu kwenye mechi dhidi ya Algeria kwani yeye kama ilivyo kwa Nyosso anaingia lawamani kwa kuruhusu goli kupita kwenye njia aliyopaswa kuilinda kama beki . Labda si kwa kuwepo kama ‘man-marker’ lakini kwa kumuelekeza mwenzie ambaye kukaba ndio jukumu lake kufanya hivyo.




6: Henry Joseph.




Alicheza vizuri kwenye eneo lake hasa kwenye kipindi cha kwanza lakini baadae alionekana kulemewa hasa baada ya wimbi la mchezo kugeukia upande wa timu yake pale ambapo Algeria walifanya mabadiliko ambayo yalifanya kasi ya mchezo kubadilika kabisa na hivyo kuonekana amechoka . Bado anaendelea kuwa mchezaji muhimu kwenye timu hii ya taifa.




7: Nizar Khalfan.




Kama Taifa stars ingeshinda mchezo huu basi Nizar alipaswa kuwa Man Of The Match kuwa kuwa alionyesha ukomavu wake kama ‘proffessional player’. Nizar alikuwa akitimzia majukumu yake ipasavyo na hata kusaidia wenzie ambao walionekana kuelemewa kama ilivyokuwa kwa Nsajigwa.Pasi yake ilisababisha goli lililowekwa wavuni na Mbwana Samatta zaidi ya hapo alionyesha kujituma kwa aina yake na pia hakuwa anapoteza pasi kizembe na hata ilipotokea kafanya hivyo basi alihakikisha anahangaika na kuupata tena . Nizar ni lulu ambayo Taifa Stars inajivunia kuwa nayo .




8: Shabaan Nditi.




Uzoefu wake umeendelea kumlinda kwenye nafasi anayocheza , japo alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Athumani Machupa alionekana kucheza vizuri akiituliza timu na kuiendesha ipasavyo , tatizo lake ni kuwa na mtazamo mmoja kwenye mchezo wake na pia kukosa kasi ambayo labda inasababishwa na umri wake kuwa mkubwa lakini bado uzoefu wake ni wa thamani kubwa kwenye timu .




9: Mbwana Samatta.




Ndiye mchezaji bora ambaye Taifa Stars inaweza kujivunia kuwa naye . Mbwana ana sifa nyingi za mchezaji aliyekamilika kwa nafasi yake . Ameendeleza rekodi yake nzuri ya kufunga kwenye kila mechi ‘competitive’ ya Taifa Stars ambayo amecheza . Kiwango chake bado kipo juu sana japo ana mengi ya kujifunza kama vile kuweka akili yake mchezoni muda wote na si pale mpira unapokuwa mguuni kwake tu . Ana uwezo mkubwa sana kwa kuwa ni mfungaji mzuri na ni mtengenzaji mzuri kwa wenzie . Ni mtu ambaye Taifa Stars inamtazama kama mwokozi wa sasa na kwa muda mrefu ujao.




10: Danny Mrwanda .




Kama ilivyokuwa kwa wachezaji wenzie toka nje ya nchi alicheza vizuri huku akijituma sana kutokana na uzoefu alio nao wa kucheza Taifa Stars kwa muda mrefu na pia kucheza nje ya nchi. Danny ni mpambanaji na hilo lilionekana kwenye mchezo dhidi ya Ageria kwani alikuwa hakubali kirahisi pale alipokuwa akikumbana na miili ya kina Hassan Yebda , Karim Ziani na wengine ambao wana miiili iliyomzidi . Hakumaliza dakika 90 lakini kwa zile chache alizocheza alionyesha uwezo mkubwa.




11: Abdi Kassim .




Kwa muda mrefu Abdi amekuwa nje ya timu ya Jan Poulsen lakini alirejea kwenye mchezo dhidi ya Algeria . Alionyesha uwezo wake aliozoeleka nao na pia ukomavu wa kuwa mchezaji wa kimataifa ulionekana, alikuwa akipiga mipira yake ya mbali kama kawaida yake . Kwenye kipindi cha pili alipiga ‘free kick’ moja ambayo almanusra iwe bao la pili kama si umahiri wa mlinda lango wa Algeria . Baadaye alionekana kuchoka na kuwa kwenye kasi tofauti na ile ya mchezo .




Wachezaji Walioingia.




Mrisho Ngassa aliingia kuchukua nafasi ya Danny Mrwanda , kwa dakika chache alizoingia alibadili mpira kidogo japo wachezaji wa Algeria walimsoma na kumdhibiti kirahisi . Aliwahadaa wapinzani kwa chenga zake lakini mawasiliano mabovu baina yake na wenzie yaliinyima Stars magoli na pia uwezo wake mdogo wa kupiga mashuti ya mbali ulikuwa tatizo kwani alikuwa anapata nafasi za kupiga mashuti na aliishia kutoa pasi kwa kuwa hana uwezo wa kupiga .







Athumani Machupa.




Alipata dakika 13 tu za kuonyesha uwezo wake na sio zaidi ya hapo. Hakukugusa mpira mara zaidi ya tano na mara nyingi alikuwa akikimbiza vivuli vya mabeki wa Algeria , pengine swali la kuwauliza TFF kwanini mchezaji anatoka Sweden na kuja kucheza dakika 13 tu?