Timu ya Senegal imefuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani shukrani kwa mabao mawili ya Moussa Sow na kuisaidia nchi yake kushinda 2-0 dhidi ya DR Congo, huku Misri ikiaga rasmini baada ya kufungwa 2-1 na Sierra Leone.
Mfungaji bora wa msimu uliopita wa Ligi Kuu ya Ufaransa Ligue 1 alionyesha thamani yake kwenye ardhi ya nyumbani baada ya kupachika mabao hayo mawili katika kipindi cha kwanza na kuamsha shangwe kwenye jiji la Dakar na kuifanya Senegal kuongoza Kundi E.
Wanaungana na Botswana, Burkina Faso na Ivory Coast kuunda timu 16 zitazocheza michuano hiyo pamoja na wenyeji wawili Equatorial Guinea na Gabon.
Burkina Faso ilifuzu hata kabla ya kuanza kwa mpira baada ya Namibia kuichapa Gambia 1-0 jijini Windhoek kwenye mechi iliyochezwa mapema.
Mafanikio ya Burkina Faso na Senegal yalifunika kwa ushindi wa Libya, ikicheza timu mpya chini ya bendera mpya ya taifa walifanikiwa kufufua matumaini yao.
Libya ilifanikiwa kuichapa Msumbiji kwa bao1-0 jijini Cairo katika mechi Kundi C iliyochezwa huku milango ya uwanja ikiwa imefungwa.
Mabingwa watetezi Misri wameutema ubingwa huo baada ya kuchapwa 2-1 ugenini na Sierra Leone, lakini walishaonyesha kukata tamaa kwa sababu ya kuwatumia kikosi cha wachezaji wa umri wa miaka 23 kwenye mchezo huo uliofanyika Freetown.
Cameroon ilitoa namachungu yake kwa kuinyuka Mauritius 6-0, nayo Ivory Coast walitoa salamu za pole kwa majeruhi Didier Drogba baada ya chipukizi Gervinho kuongoza mauaji ya mabao 5-0 dhidi Rwanda.
Mali ikiwa na kiungo wa Barcelona, Seydou Keita wamejiweka vizuri baada ya kushinda 3-0 nyumbani dhidi ya Cape Verde jijini Bamako huku Tunisia ikiweka njia panda baada ya kutoka suruhu na Malawi.
No comments:
Post a Comment