Wanasoka Diego Forlan wa Inter Milan na kiungo mpya wa Manchester City, Owen Hargreaves pamoja na mshambuliaji wa Chelsea, Romelu Lukaku ni miongoni mwa wachezaji walionguliwa kwenye vikosi vya timu zao kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa.
Forlan aliyesajiliwa na Inter hivi karibuni aliichezea Atletico Madrid kwenye kusaka tiketi ya Europa Ligi kabla ya kuhamia Italia.Mshambuliaji huyo wa Uruguay alichezea Atletico dhidi ya timu ya Norway ya Stromsgodset katika hatua ya tatu ya kusaka kufuzu kwa michuano ya Europa.
Alijiengua kwenye mchezo dhidi ya Vitoria Guimaraes wakati huo akiwa na mazungumzo na klabu hiyo ya San Siro, lakini sheria ya UEFA inamzuia mchezaji huyo aliyecheza Europe kuichezea Inter sasa labda hadi mwakani.
Inter imepagwa Kundi B pamoja na CSKA Moscow, Lille na Trabzonspor, lakini bado safu yao ya ushambuliaji ipo imara kwa kuwepo kwa Giampaolo Pazzini, Diego Milito, Mauro Zarate na chipukizi kwenye miaka 18, kutoka Uholanzi, Luc Castaignos .
Hargreaves na Lukaku pia wameachwa kwenye vikosi vyao kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa.
Hargreaves, 30, aliyejiunga na City wiki iliyopita akiwa na tumaini na kurudi kwenye kiwango chake baada ya kuachwa na Manchester United.
Kiungo huyo wa zamani wa England bado anakazi kubwa ya kurudi kwenye kiwango chake baada ya kuwa majeruhi ya goti kwa muda mrefu na City wameamua kutomweka kwenye orodha 17 watakaocheza Ligi ya Mabingwa.
Wachezaji wengine nane kati ya 25 ni lazima wawe ni wale wa akiba wa nyumbani au chipukizi.
Kuondolewa huko kwa Hargreaves kunamfanya hakose mechi mbili za Kundi A dhidi ya timu yake ya zamani Bayern Munich, wakati City itapocheza kwa mara ya kwanza michuano hiyo.
Hata hivyo, kocha wa City, Roberto Mancini anayo nafasi ya kumtumia kwenye kikosi chake cha Januari kama atafanikiwa kufuzu kwa hatua ya makundi.
Wakati huohuo, mshambuliaji wa kimataifa wa Ubelgiji, Lukaku pia ameondolewa kwa kushangaza kwenye kikosi cha Chelsea kwa ajili ya mashindano hayo hatua ya makundi.
Lukaku aliyesajiliwa kwa pauni 18 milioni kutoka Anderlecht mwezi uliopita, ataweza kucheza kwenye 16 bora, lakini Chelsea imewajumuisha wachezaji waliosajili siku ya mwisho ya usajili Oriol Romeu, Juan Mata na Raul Meireles kwenye kikosi chao cha wachezaji 22.
No comments:
Post a Comment