Wachezaji wengi wa kileo wanaweza kuwa wametimiza ndoto zao kwa vitu vingi , kama vile kazi ya kufanya ambayo ni ndoto ya maisha yake , akaunti ya benki inayosoma vizuri na vitu vingine vingi vinavyomfanya awe kwenye mazingira mazuri ya kufanyia kazi kuliko ilivyokuwa zamani.
Lakini tatizo kuu linalomkabili ni mbinu za mazoezi ambazo zimeegemea sana kwenye sayansi na teknolojia ya kisasa . Huu ni mtazamo wa mtaalamu wa masuala ya viungo wa Kidachi Raymond Verheijen.
Verheijen amewahi kufanya kazi kwenye timu za taifa za Uholanzi,Korea ya Kusini na Urusi pamoja na Vilabu kama Barcelona,Manchester City na Chelsea pamoja na chama cha soka cha Uholanzi.
Kwa mtazamo wake mazoezi ya kisasa hayapaswi kuzingatia sana ugumu wa mazoezi ya viungo na muda mrefu wa kuyafanya.
Yeye anasema kuwa mazoezi yanapaswa kuwa machache kwenye upande wa viungo ili kuwaweka wachezaji Fit kuchezea mpira kwa muda mrefu.
Raymond anasema siku hizi Kuna tofauti kubwa kwenye mbinu za kufundisha mpira ukilinganisha na zamani , tatizo ni kwamba watu wengi wanadhani kufanya mazoezi mengi na kwa muda mrefu ni kitu bora.
Kiasili anasema watu wanaamini kuwa kabla ya mechi unapaswa kuuandaa na kuujenga mwili.
Wanawasukuma wachezaji kufanya mazoezi wakati mwingine zaidi ya kiwango chao cha kawaida cha kufanya mazoezi ili mradi tu wawe fit kwa kuwa wanaiga mbinu za mazoezi toka kwenye michezo mingine.
Kiukweli kwenye michezo mingine kama Riadha, Mbio za baiskeli na kuogele kufanya mazoezi mengi ni vizuri lakini siyo kwenye soka.
Watu wanaufanya mchezo kuonekana mgumu pasipo na faida yoyote. Kwa sababu ya mapinduzi haya ya kisayansi watu wanaacha kufikiri kama wanadamu wa kawaida na wanaacha kufanya mambo kwa kufuata misingi.
Neno soka limeingiliwa na hili suala la Fitness na ndiyo maana mimi huwa nasema ni vyema kurudi kwenye mambo ya msingi.
Inawezekana vipi timu 10 tofauti zina makocha kumi tofauti wa masuala ya fitness na wanatumia mbinu 10 tofauti? Haiwezekani, wachezaji wanakuwa wahanga wa fitness. Mbinu za kufanya mazoezi hazipaswi kuegemea kwenye mawazo ya mtu mmoja au uzoefu wake .
Mazoezi ya soka yanapaswa kuwa ya soka na si kuongeza vitu toka mazoezi ya michezo mingine kama Hockey na Riadha.
Verheijen ambaye maisha yake ya soka yalikatishwa na jeraha la paja alilopata akiwa na umri wa miaka 17, amesomea masuala ya physiology na saikolojia ya michezo kwenye chuo cha Free Huko Amsterdam na mawazo yake yametumika kwenye kozi za kufundishia ukocha na ualimu wa michezo kwa jumla nchini kwao uholanzi.
Mtaalamu huyu mwenye umri wa miaka 39 ambaye ana Leseni ya ukocha daraja la A inayotambulika na UEFA anasema kuwa makocha wengi wa masuala ya fitness hawana histoaria ya mchezo wa soka na ametoa mifano mingi sana ya timu ambazo zina historia ya kuwa na wachezaji walioko fiti sana na wasioumia umia kila leo . Anatolea mfano timu ya Korea ya kusini ambayo amefanya nayo kazi kwenye michuano ya kombe la dunia mara 3 .
Nilipoanza kufanya kazi na Guus , nilimuuliza kwanini aliniita kufanya kazi na timu ile .Hawa watu tayari wako fit alisema , ila ngoja uone mechi yao ya kwanza ya kirafiki alisema Guus. Kwenye mchezo wao wa kwanza waliweza kucheza vyema kwenye dakika 60 za kwanza lakini baada ya hapo walichoka sana.
Kama Guus angekuwa amemleta mtu ambaye ni mtaalamu wa mazoezi angemwambia kuwa wachezaji wa Korea ya kusini wanakosa pumzi na hivyo angewakimbiza kuzunguka uwanja raundi kadhaa au angewakimbiza msituni au mlimani ili kuwapa pumzi. Ila mimi sikutafsiri tatizo la wakorea kama hivyo, kwangu niliona kuwa wakorea hawawezi kucheza kwa mtindo mmoja kwa muda wa dakika 90. Hii inamaanisha kuwa unapaswa kutumia lugha ya mchezo wa Soka kufafanua tatizo na si vinginevyo .
Tulilitatua tatizo hili kwa kucheza kwa kugawanya muda wa dakika kumi kumi, huku tukiongeza idadi ya makundi ya muda huo wa dakika kumi kumi taratibu kuanzia mara nne , tano , sita kabla ya kucheza kwa mtindo huu kwa muda wa dakika 90.
Unapaswa kuwalazimisha wachezaji kufanya masuala Fulani hata kama mwili unasema hapana , unapaswa kuwazoesha hivyo. Kama unataka kucheza mtindo Fulani kwa muda mrefu unapaswa kufanya mazoezi ya kuucheza mtindo huo uwanjani kwa muda mrefu.
Mbinu hii ya kugawanywa muda ilibuniwa na Mwalimu wa kirusi ili kuzuia kufanya mazoezi zaidi na kumfanya mchezaji aperform kwa kiwango cha juu.
Kama unataka kupiga hatua kama mchezaji kitu muhimu cha kufanyia kazi ni spidi ya vitu unavyofanya kama mchezaji. Na hili linaonyesha kuwa soka ni mchezo wa kiwango cha matukio na sio mchezo wa kuvumilia mateso ya mazoezi. Kwenye mchezo wa kuvumilia mazoezi magumu unapaswa kufanya mazoezi kwa muda mrefu lakini kwenye mchezo wa kiwango unapaswa kuzingatia kiwango cha mazoezi unayoyafanya.
Kama unataka kuongeza kasi ya matendo yako uwanjani uchovu ni adui yako namba moja . kwa kila kipindi cha mazoezi unapaswa kuwa fresh na kama unataka kuongeza kiwango kama mchezaji unahitaji pia kuwa fresh.
Kwa maneno mengine ‘chache ni zaidi’ . Njia pekee ambayo mchezaji atapiga hatua kwenye kiwango chake ni kwa kufanya mazoezi yaliyo bora na si kufanya mazoezi zaidi .
Mwangalie Arjen Robben ambaye ametumia muda mwingi akiwasumbua madkatari pale Stamford Bridge kuliko alivyokuwa anawasumbua mabeki kwa miaka yake mitatu aliyokuwa Stamford Bridge.
Akiwa Chelsea walimuita ‘the man of glass’ , mwaka jana alicheza Bayern Munich . Walichofanya pale ni kupunguza mazoezi aliyokuwa anayafanya . Alicheza kwenye kiwango cha juu sana na walitwaa mataji kwa sababu yake .
Ghafla Robben hakuwa majeruhi tena.
Swali ni kwamba Robben alikuwa ‘mchezaji wa glassi au makocha waliomfundisha ndio walikuwa makocha wa glassi? Wachezaji kama Robben na Va Persie hutumia nguvu kwenye matendo yao kuliko wachezaji wengine .
Wanapofanya mazoezi kama wachezaji wengine matumizi yao ya nguvu yanakuwa mara mbili zaidi hivyo ni lazima uwapunguzie mazoezi wafanye angalau asilimia 50 na ni kitu ambacho Bayern walifanya kwa Robben .
Unapokuwa umechoka ishara toka kwenye ubongo wako kwenda kwenye mwili wako inakuwa inasafiri taratibu kuliko kawaida . Kama ishara inakwenda taratibu inahatarisha viungo vyako kwakuwa unatumia nguvu nyingi kuliko uwezo wako wa kawaida na hivi ndio unasikia vitu kama magoti,enka,nyonga, nyama za paja na vingine ving vinaumia .
Timu nyingi za ligi kuu nchini England zinatumia teknolojia ya kompyuta kupima kiwango cha ‘perfomance ‘ ya mchezaji na hata kiwango cha uchovu . Pamoja na vipimo hivyo vya sayansi na teknolojia mpya bado kulikuwa na wachezaji karibu 108 ambao rekodi zilisoma kuwa hawakuwepo kwenye viwango vyao vya kawaida kwenye wikiendi ya desemba , nah ii ni sawa na asilimia 5.4 ya wachezaji kwenye kila timu, mahesabu haya yanaonyesha kuwa kuna tatizo kubwa.
Aston Villa na Tottenham ndio walioathirika sana kuliko wengine huku wakiwa na karibu wachezaji 11 wenye majeraha na Arsenal walimpoteza beki wao Kieran Gibbs kwa jeraha la Enka . Kwa ujumla timu hizi tatu ukitazama kwa undani ndio zenye tatizo la kuwapa wachezaji mazoezi magumu kuliko inavyotakiwa.
Sawa kuna watu waliowahi kuvunjia mifupa vibaya kama Eduardo na Ramsay lakini vipi kuhusu Robin Van Persie ambaye amekaa nje kuliko hata hawa wachezaji waliowahi kuvunjika vibaya , na Van Persie majeraha yake si ya kuvunjika mifupa , amekuwa na matatizo ya misuli san asana .
Verheijen anamtumia mchezaji mwingine wa kidachi Rafael Van Der Vaart kama mfano . Verheijen anakataa katakata imani ya Tottenham kuwa mchezaji huyu hayuko ‘fit’ .
Hana uzito usio wa kawaida , namjua tangu utoto wake , nilifanya naye kazi mwaka 2001 wakati nikisaidia kwenye timu ya Uholanzi ya Under 20 kwenye kombe la dunia huko Argentina na jinsi alivyokuwa kimwili .
Van Der Vart amekuwa na msimu mrefu sana na hakupumzika kwa kuwa alilazimika kucheza kwenye kombe la dunia ambako timu yake ilicheza mpaka fainali. Fitness yake ilikuwa juu lakini hakuwa Fresh kwa kuwa hakupata muda wa kutosha kupumzisha mwili wake.
Wachezaji wanaocheza kombe la dunia mara zote wanakuwa fiut lakini uchovu ndio adui yao, na uchovu huufanya mwili upoteze mawasiliano baina yake na ubongo na hapo ndio majeraha hasa ya misuli na nyama yanapokuja na kuwamaliza wachezaji hawa.
Wanachohitaji ni muda wa kutosha wa kupumzika na mazoezi ambayo yanazingatia hilo.
Mazoezi kwa kipindi kimoja kwa siku na mazoezi haya hayapaswi kuwa na lundo la mazoezi magumu ya viunngo na kunatakiwa kuwa na muda mwingi katikati ya vipindi vya mazoezi wa kuuruhusu mwili kurejea kwenye hali yake ya kawaida baada ya mazoezi.Verheijen anasema kuwa alitumia mfumo huu akiwa na Barcelona ya Frank Rijkaard mwaka 2004 baada ya michuano ya Euro.
Verheijen amewahi kufanya kazi kwenye ligi kuu ya England ambako alikuwa kwenye timu ya Man City chini ya Mark Hughes kwenye mzunguko wa pili wa msimu wa mwaka 2009.
Katika kipindi cha Julai na Novemba mwaka jana Man City walikuwa na rekodi bora kwenye ligi kuu ya wachezaji kutoumia.
Pia timu hii ilikuwa na takwimu bora kwenye mbio wakati wa mechi na walifanya mazoezi mara moja kwa siku.Mazoezi yalikuwa na kiwango bora na hayakuwa ya kuchosha , kwa muda wote huo Man City walikuwa na mchezaji mmoja tu aliyeumia na alikuwa Benjani ambaye Verheijen anakiri kuwa jeraha alilopata lingeweza kuzuilika
Alipokuja Roberto Mancini aliongeza mazoezi ya nguvu wakati alipokuja , jambo ambalo lilipingwa na wachezaji kama Craig Bellamy na Carlos Tevez. Mancini aliongeza mazoezi kutoka kwenye kipindi kimoja kwenda kwenye vipindi viwili na pia aliongeza muda wa mazoezi hayo toka kwenye dakika 75 hadi masaa mawili. Katika siku zake 10 za kwanza kulikuwa na wachezaji takribani 10 walioumia , hakuna mwandishi wa habari anayechambua suala hili, huu ni upuuzi.
Wakati Mancini alipokuja bado nilikuwa City japo si kwenye nafasi yangu niliyokuwa nayo wakati wa Hughes anasema Verheijen,.
Lakini baada ya wiki mbili na majeraha kwa wachezaji yakiongezeka niliamua kuondoka kwa kuwa watu walinihusisha na majeraha yale kwa wachezaji, anaongeza Verheijen.
City walilaumu kipindi cha Krismasi kuwa ndio kilisababisha majeraha kwa wachezaji , kwa mujibu wao majeraha yale yasingeweza kuzuilika.
Kwa sasa majeraha haya yamepungua kwa sababu wana mechi nyingi katikati ya wiki na hivyo wamelazimika kupunguza muda wa mazoezi kuwa mara moja na si mara mbili
Anachojaribu kueleza mtaalamu huyu ni timu hasa za nchini England kuondokana na dhana potofu kuwa ‘fitness’ ya mchezaji inaongezeka kwa vipindi virefu vya mazoezi magumu , wachezaji wanaumia kwa sababu hii na si sababu nyingine , maisha yao ya uchezaji yanakuwa mafupi kwa sababu hii na si sababu nyingine .
Makocha wengi wanafanya hivi , hawazingatii umri wa mchezaji na vitu vingine muhimu , kila mtu anataka mbinu hizi za mazoezi ambazo hazisaidii.
Mtaalamu huyu anafanya kazi ya kumuweka fit Craig Bellamy kwa siku mbili za wiki kwa gharama za mchezaji huyu , na amekuwa mstari wa mbele kujaribu kuleta mabadiliko kwenye mazoezi .
No comments:
Post a Comment