Search This Blog

Thursday, September 8, 2011

TOKA KWENYE KIPIGO CHA BELFAST HADI KUITEKA ULAYA NA DUNIA NZIMA

Mwezi Septemba tarehe 6 mwaka 2006 Soka la Hispania lilifikia kiwango cha chini kuliko siku zote katika histoaria yake. Kipigo cha mabao 3-2 toka kwa Ireland ya Kaskazini huko Belfast kilikuwa kipigo kibaya zaidi kwa timu ambayo inatazamwa na watu kama timu inayotisha lakini haikuwahi kudhihirisha uwezo wake kwenye michuano mikubwa.
Ni wachache ambao wangeweza kutabiri kilichotokea baada ya hapo.
Miaka mitano baadae Timu ya taifa ya Hispania imekuwa bingwa wa ulaya na bingwa wa dunia na ni nani wa kusimama njiani wakielekea kutwaa ubingwa mwingine wa Ulaya, hakika hakuna.
Ushindi dhidi ya Lichteinstein umewahakikishia kufuzu kwa kombe ambalo wanaenda kulitetea na umewafanya watimize miaka mitano tangu walipofungwa na mabao matatu ya David Healy.
Usiku ule kwenye uwanja wa Windsor Park ambapo David Healy alifunga ‘Hat-trick’ ulikuwa usiku wa mapinduzi makubwa kwa aliyekuwa kocha Luis Aragones .Huku kazi yake ikiwa hatarini , mabadiliko yalilazimika kufanyika kwenye timu ya Hispania.
Akiwa ndio kwanza ametoka kwenye kashfa ya ubaguzi wa rangi baada ya kumtolea maneno ya kibaguzi Thierry Henry , kocha huyu wa Hispania alikuwa na maamuzi magumu ya kufanya.
Na katika maamuzi hayo gumu kuliko lote ilikuwa kumuacha mshambuliaji mkongwe na nahodha Raul Gonzalez. Usiku ule jijini Belfast ulikuwa wa mwisho kumuona Raul akiichezea timu ya taifa . Kama shuti lake alilopiga mwishoni mwa mchezo lisingegonga mwamba basi pengine tungeendelea kumuona Raul akiwa mchezaji wa timu ya taifa, lakini mambo yalienda kombo kwake.
Kuwekwa kando kwa Raul kulizua maswali mengi. Raul alikuwa kipenzi cha wengi na katika miaka yake yote ya kuichezea timu ya taifa hakuwahi kutwaa ubingwa wowote akiwa na timu hiyo.
Mwaka baadae kocha Aragones alilipuka kwa hasira alipouliza kuhusu Raul .’unajua Raul amecheza kwenye kombe la dunia mara ngapi?? Aragones aliuliza , Akajibiwa mara tatu, Akauliza tena ,amewahi kutwaa kombe hilo mara ngapi?? Akajibiwa kuwa hajawahi Akauliza tena na Kombe la Ulaya je?? Akajibiwa mara mbili , na amewahi kushinda mara ngapi?? Hajawahi.
Si lawama zote zinamwendea Raul , lakini mshambuliaji huyu wa Real Madrid amekuwa akicheza chini ya kiwango kwa muda mrefu kwenye timu ya taifa na mpaka kufikia kipindi hicho ilionekana kuwa muda umefika kwa Hispania kusonga mbele na kumuacha Raul. Inasemekana kuwa Raul alikuwa sababu ya mgogoro kwenye kambi ya kombe la dunia huko ujerumani mwaka 2006 ambako Hispania ilitolewa kwenye hatua ya raundi ya pili na Ufaransa
Mchezo huo ulichezwa huko Hannover mwezi juni lakini Hispania wlaibaki na Hangover mpaka mwezi septemba . Kufuatia kipigo dhidi ya Ireland ya kaskazini , na vipigo vingine dhidi ya Sweden na Romania Hispania waling’aa wakicheza mechi 35 bila kufungwa ambapo Hispania walitwaa ubingwa ulaya chini ya Aragones na wakaendelea kutwaa ubingwa wa dunia chini ya Vicente Del Bosque.
Wakati Aragones aliondoka alisema kuwa ili Hispania itwae ubingwa wa dunia ni lazima icheze kwa kutawala sehemu ya kiungo huku ikitumia mchezo wake wa kupiga pasi nyingi . Kiungo mwenye nguuv nyingi Marcos Sennna aliitwa kwenye timu kuongezea kwenye akili za viungo Xavi na Iniesta na mbele akaletwa David Villa kwenye nafasi iliyoachwa na Raul Gonzalez ambapo Villa aliunda safu ya ushambuliaji sambamba na Fernando Torres huku Villa akifunga mabao manne na Torres akifunga moja kwenye fainali ya EURO 2008 dhidi ya ujerumani .

Aragones aliachia ngazi baada ya euro 2008 ila Hispania walikuwa wazuri zaidi chini ya Del Bosque wakicheza soka la kuvutia machoni huku wakiiga mfumi unaotumika Barcelona na kutawala dunia kwa kutwaa kombe la Dunia afrika kusini .
Mpaka kufikia wakati huo Sergio Busquets na Pedro walikuwa wameongezwa na beki mwingine Gerard Pique ambaye alirudi Hispania toka Man United . Hispania ikawa timu iliyokamilika kuliko zote ulimwenguni ambayo mpaka hii leo wameendelea kutawala soka la dunia hii .

No comments:

Post a Comment