Search This Blog

Wednesday, June 15, 2011


Kwanini vilabu vikubwa ulaya vinauana kumpata?
Alexis Sanchez ni mchezaji mwenye umri wa miaka 22 . Sanchez ni raia wa Chile na anacheza kwenye klabu ya Serie A Udinese. Ulimwengu ulimshuhudia Sanchez kwa mara ya kwanza akipeperusha bendera ya taifa lake la Chile kwenye Kombe la dunia mwaka jana ambako Chile ilifika hatua ya 16 bora.

Tangu hapo Sanchez amepiga hatua mara dufu , msimu huu ulioisha Sanchez alifunga mabao 12 kwenye michezo 31 ikiwemo mechi moja dhidi ya Palermo ambapo alitupia bao nne na hatimaye kuisaidia Udinese kufuzu kucheza ligi ya mabingwa barani ulaya .

Mabingwa wa England mashetani wekundu Manchester United na jirani zao Manchester City hivi sasa wapo kwenye ushindani mkubwa sana wa kuipata saini ya Alexis Sanchez huku Barcelona , Real Madrid na Inter Milan wote wakimtazama kwa karibu japo United wanaonekana kuongoza mbio za kumsajili baada ya Sanchez mwenyewe na wengi wa washauri wake na watu wa karibu kumshauri aende kwa ‘babu fergie’.
Sanchez kwa asili ni winga lakini ana uwezo wa kucheza katikati nyuma ya mshambuliaji na anatumia miguu yote .

Uwezo gani hasa?
Watu wengi wamekuwa wakisema kuhusu uwezo wa Sanchez na karibu msimu mzima wa Serie A ulioisha hivi karibuni kivutio kikubwa kilikuwa uwezo wake wa kuwapita mabeki na kumiliki mpira bila wasiwasi na hakika Sir Alex Fergusson ameyasikia yaliyosemwa .
Sanchez alianza kucheza soka kama winga wa kulia lakini kadri alivyoendelea kupata uzoefu amekuwa akitumika kwenye maeneo mengi kwenye upande wa juu wa uwanja.

Alexis sio mshambuliaji kabisa ni aina ya watu ambao nchini uholanzi wanaitwa “mshambuliaji wa uongo” (yaani mtu anayetumika kama mbadala wa mshambuliaji –mara nyingi kiungo mwenye uwezo wa kufunga) ila anaweza kucheza kati nyuma ya mshambuliaji mkuu na kwa United mfano wa anavyocheza Wayne Rooney United .
Sanchez anaonekana kama Cristiano ronaldo mwingine. Hii ni kwa jinsi anavyopenda vibaiskeli na pia analijua goli lilipo na uwezo wake wa kufunga unajulikana kama unabisha waulize Palermo
.



Sanchez Ni Ronaldo mwingine?
Wengi wamemtazama Alexis Sanchez kama Cristiano Ronaldo mwingine na kama ukichukua muda wako kutazama clip ambazo tumeziweka hapa kwenye blog utaona kwanini .
Ana mtindo flani wa kuchezea mpira kama wa CR7 japo kwenye ligi ya Italia wengi walimfananisha na Lionel Messi kwa jinsi alivyo na miguu yenye kasi lakini Sanchez mwenyewe hapendi kufanishwa na wachezaji hao wawili ila kama ataiteka ligi kuu ya England kama alivyofanya Ronaldo Manchester patakuwa mahala sahihi .

Je amekamilika kuikabili ligi ya England?
Vilabu viwili vya Manchester pengine vinatambua kwa uthibitisho na ushahidi wa kutosha juu ya hatari zinazowakabili wachezaji wenye asili ya amerika ya kusini pindi wanapokuja England.
Nyota wa Uruguay Diego Forlan alishindwa kuwika United wakati Carlos Tevez ameweza kun’gaa akiwa United na City.


Robinho aliyekuja Man City kwa thamani ya paundi million 32.5 alikuwa tatizo huko Eastlands .
Sanchez mwenyewe angependelea kubakia Italia au kwenda Barcelona ila Manchester United wanaweza kumfanya abadili mawazo yake .

Kwa umbo lake la futi 5 na nchi 6 ni dhahiri mabeki wa England kina Gary Cahill na Christopher Samba watampa wakati mgumu kwa mabuti yao ya hatari ila watalikoga vumbi la kutosha kutokana spidi aliyo nayo , pamoja na umbo dogo alilonalo Sanchez ana nguvu na ufupi wake mara nyingi unamuongezea stamina na balance ya kuhimili rafu .

Ataenda wapi mwisho wa siku?
Alama za nyakati zinaashiria kuwa Man United watawazidi mahasimu wao Man City kete kwa kumnasa Sanchez kwa sababu kwa kitita cha fedha ambacho kimiwekwa kwa ajili ya Barcelona kufanya usajili ni dhahiri hakitatosha kumnasa na hata Barca wakikomaa na kumsajili Sanchez ataenda kucheza wapi zaidi ya kukalia benchi jambo ambalo hata yeye mwenyewe asingependa kulipitia , Madrid wana mipango mingine na hawajajihusisha kabisa na Sanchez , Manchester City wameweka ubaoni kitita cha paundi million 30 na wanaweza kuongeza wakihitajika kufanya hivyo lakini ushawishi mkubwa wa Manchester United kupitia mafanikio waliyo nayo nambinu ujanja wa Sir Alex Fergusson na mkurugenzi wake bwana David Gill ni dhahiri vitatosha kumleta Sanchez Old Trafford

UKWELI WA JUMA KASEJA KWENDA YANGA.


Hapo jana majira ya saa nne za usiku nilipost taarifa ya usajili wa Juma Kaseja na Haruna Niyonzima Kumalizana na klabu ya Yanga,hii ilikuwa baada ya kupata taarifa hizo kutoka kwa mmoja wa wajumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga ambaye hakupenda jina lake liandikwe hapa.

Kwa Mujibu wa Chanzo hicho ambacho kilisema Yanga walimpatia Kaseja kiasi cha shilingi milioni 30 ili ajiunge na Mabingwa hao wa Tanzania bara baada ya Kaseja kuwa amemaliza Mkataba wake na Simba.

Aidha chanzo hicho kiliendelea kwa kusema kuwa Usajili wa Kaseja umekuja baada ya Yanga kuonekana kushindwa kuhimili dili la kumasjili Shaban Kado kutoka Mtibwa Sugar ambaye tayari alikuwa amepewa shilingi Milioni 20 na klabu yake ya Mtibwa kutaka Milioni 35 jambo ambalo Yanga waliona litakuwa ni gharama kubwa kwao.

Lakini kwa taarifa ambazo nimezithibitisha asubuhi ya leo kutoka vyanzo tofauti ni kwamba JUMA KASEJA ana mkataba wa miaka miwili wa kuendelea kuitumikia klabu yake ya SIMBA siku chache zilizopita na Yanga baada ya kuona Kaseja ana Mkataba wa Miaka miwili wakaamua kuachana na suala la kumsajili Kaseja kwani waliona kuvunja mkataba wa Miaka miwili aliyonayo lilikuwa kinyume na Matarajio yao.

Hivyo napenda kuwajulisha rasmi kuwa taarifa za Juma Kaseja kwenda Yanga zilikuwa ni tetesi zilizokaribia Ukweli lakini Ukweli halisi ni kwamba Kaseja ni Mali ya Simba kwa Miaka Miwili Ijayo na atakuwa mmoja wa wachezaji wa Simba watakao ondoka hapo kesho asubuhi kwenda nchini DRC CONGO kuwavaa DC Motema Pembe kwenye Mchezo wa marudaiano.

Jamani hata tetesi muda mwingine huwa na Ukweli ndani yake hivyo lieleweke hivyo.

HABARI ZA USAJILI BARANI ULAYA

United yakaribia kumsajili Sanchez kwa ada ya £27million,
Manchester United ipo tayari kutoa kitita cha paundi milioni 27 kukamilisha dili la kumsajili Alexis Sanchez kutoka Udinese.na kuzipiga bao klabu za Manchester City na Barcelona.
Mtendaji mkuu wa Man United David Gill alikwea pipa hapo jana kwenda jijini Barcelona kukutana na viongozi wa Udinese. Kambi ya Alexis Sanchez inaitaka Man utd Kuiliko Man city.




Guus akaribia kurejea the Blues.
GUUS HIDDINK anakaribia kabisa kurejea Chelsea baada ya hapo jana usiku raisi wa chama cha soka nchini Uturuki Mahmut Ozgener kudhibitisha kung’atuka mwishoni mwa mwezi huu.


Arsenal itatumia £30MILLION kwenye usajili.
Arsene Wenger anataraji kuwapoza mashabiki wa tiku yake baada ya kusema atatumia kiasi cha paundi milioni 30 kwa ajili ya usajili.
Kocha huyo wa ‘The Gunners’ Wenger anakaribia kumnyakua mshambuliaji Gervinho raia wa Ivory Coast kwa ada ya paundi milioni 12.
Boss huyo wa Arsenal pia anawafuatilia mabeki wa kati nahodha wa Blackburn Christopher Samba ama beki wa Bolton Gary Cahill.
Naye mtendaji mkuu Ivan Gazidis amesema hawana uwezo wa kuwapatia mishahara ambayo wanaitaka kiungo Samir Nasri na beki Gael Clichy, badala yake sasa wenger anawasaka mshambuliaji Leandro Damiao anayeichezea Internacional ya nchini Brazil pamoja na beki wa kushoto AIK na timu umri chini ya 21 ya Sweden,Alexander Milosevic.









Tuesday, June 14, 2011

BREAKING NEWS! HARUNA NIYONZIMA,JUMA KASEJA WAMALIZANA NA YANGA

HARUNA NIYONZIMA (JEZI YA NJANO) AKIJARIBU KUMTOKA JUMA NYOSO





TAARIFA NILIZOZIPA HIVI PUNDE KUTOKA NDANI YA YANGA,KIUNGO WA APR YA RWANDA HARUNA NIYONZIMA' FABREGAS' PAMOJA NA GOLIKIPA JUMA KASEJA WAMEJIUNGA RASMI NA YANGA KWA AJILI YA MSIMU UJAO.

KWA MUJIBU WA CHANZO CHANGU CHA HABARI KIMESEMA NIYONZIMA AMEJIUNGA NA YANGA KWA MKATABA WA MIAKA MIWILI PAMOJA NA KIPENGELE CHA KUUZWA IWAPO ATAPATA KLABU NYINGINE AKIWA NDANI YA MKATABA.

HARUNA NIYONZIMA ATATAMBULISHWA RASMI MARA TU BAADA YA MKATABA WAKE NA APR KUMALIZIKA MWISHONI MWA MWEZI HUU WA SITA.

KARIBU TENA KASEJA...






KUHUSU KASEJA KUREJEA YANGA KWA MARA NYINGINE TENA KUMEKUJA BAADA YA KUWEPO USHINDANI MKALI WA NANI ASAJILIWE KATI YAKE NA GOLIKIPA SHABANI KADO, KWA MUJIBU WA CHANZO HICHO CHA HABARI KASEJA AMEFANIKIWA KUMPIKU KADO NA KUFANIKIWA KUMWAGA WINO WA KUICHEZEA YANGA MSIMU UJAO.

' mara ya mwisho kwenye kikao tulikubaliana asajiliwe kado na wahusika wamalizane na mtibwa na ikishindikana basi achukuliwe angalau kwa mkopo,lakini nimepigiwa simu na mjumbe mwenzangu akaniamba kaseja amesajiliwa rasmi leo' KILISEMA CHANZO HICHO.


LET'S WAIT AND SEE!!

Yanga waanza rasmi maandalizi ya msimu mpya hii leo.

Mabingwa wa soka Tanzania Bara,Dar Young Africans,hii leo wameanza mazoezi rasmi chini ya kocha Felix Minziro,
Kocha mkuu wa timu hiyo Sam Timbe anatarajia kutua nchini kesho akitokea nchini kwao Uganda tayari kwa maandalizi ya msimu mpya.

NANI ANAYAFAHAMU HAYA MAJEMBE ?

Juzi kati nilipost kikosi cha sigara nikaomba mnitajie majina ya kile kikosi, sikumpata mshindi kwakweli FIFTY yangu nikabaki nayo,
sasa kuna voucher ya 10,000 ya mtandao wowote kwa atakayekuwa wa kwanza kuwataja hawa jamaa na angalau kutoa wasifu wao kiduchu.

Usajili unaendelea Barani Ulaya.

Michael Essien

Wakala wa kiungo Michael Essien bwana Fabien Piveteau amesema kiungo huyo hana mpango wa kuihama timu yake ya Chelsea na kujiunga na kocha wa Real Madrid,Jose Mourinho.



AMAURI


Mshambuliaji wa kimataifa wa Italia Carvalho Amauri anawaniwa na vilabu kadhaa vya nchini England, kwa mujibu wa wakala wake.



Alexis Sanchez


Manchester City nayo imeingia kwenye mbio za kuwania saini ya winga wa Udinese, Alexis Sanchez.
Sanchez pia amekuwa akiwaniwa na vilabu kadhaa barani ulaya vikiwemo Barcelona na Manchester Utd.









TFF yaiagiza Villa Squard Kufanya uchaguzi mapema.

Shirikisho la Kandanda hapa nchini TFF imeitaka kamati ya Uchaguzi ya Villa Squad kufanya Uchaguzi wa klabu hiyo haraka iwezekanavyo kufuatia kukharishwa kwa Uchaguzi wa klabu hiyo jumapili iliyopita.

Katibu Mkuu wa TFF Angetile Osiah amesema Villa Sports Club ni mwanachama wa TFF hivyo kufuatia ibara ya 1 kifungu kidogo cha sita ambacho kinasema mwanachama wa TFF ni lazima aheshimu Katiba,maamuzi na maagizo yote ya TFF na kuhakikisha kuwa zinafuatwa,hivyo Villa kama mwanachama lazima atimize kwa vitendo ibara hiyo kwa kufanya Uchaguzi huo haraka iwezekanavyo.

HATIMAYE DROGBA AACHANA NA UKAPERA,ABRAMOVICH MWENYEKITI WA KAMATI YA HARUSI.

Hatimaye mchezaji maarufu wa Ivory Coast na Chelsea Didie Drogba alifunga pingu za maisha na mpenzi wake wa siku nyingi Lalla Diakite huko the Marie de Monaco, Monaco.
Inasemwa kuwa sherehe hii ilifanikishwa na mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abramovich na yeye ndiye alikuwa Chairman wa Shughuli nzima, huku wachezaji wenzake kama Salomon Kalou na Florent Malouda wakiwa ni wapambe wa Bwana Harusi. Mbali na hao mwanamuziki nyota wa R n B Akon pia alikuwa ni mmoja wa waalikwa ambapo Fally Ipupa alikuwa mmoja wa waliotumbuiza.
Habari zinasema kwamba Drogba aliupenda sana wimbo wa Jupa Remix ambao Fally alishirikishwa na J Martin na ndipo alipomualika kuja kutumbuiza binafsi lakini Fally alipowasiliana na Drogba alimwambia kuwa wimbo ule ni wa J. Martin hivyo akitaka aupige ni lazima mwenye wimbo pia awepo ndipo mwanamuziki J. MArtin alipopewa mualiko rasmi.







WAGENI WAALIKWA WAKIELEKEA UKUMBINI..

Drogba na mpenzi wake walikutana awali mwaka 1999 huko Paris Ufaransa ambapo Drogba alikuwa katika harakati zake za mwanzo za soka, na tangu hapo wamekuwa wapenzi na walifanikiwa kupata watoto watatu lakini walikuwa bado hawajafunga ndoa.
Kwa mujibu wa gazeti la The Sun la Uingereza toleo la leo, Tofauti na watu wengine Drogba alikataa wazo la kufanya harusi ya kifahari na kusema kuwa anataka kitu cha kawaida kabisa.
“Anataka kufanya ndoa ya kawaida kabisa ikishuhudiwa na marafiki wa karibu pamoja na ndugu wa karibu tuu, anataka kumpa mpenzi wake Lala harusi ambayo aliiwaza kwani hawakuwa na uwezo wakati wanakutana” kilisema chanzo cha habari cha The Sun.
Weekend ya iliopita pia ilishuhudia mchezaji wa Manchester City Vincent Kompany na mwingine wa Luka Modric pia wakifunga ndoa.






Drogba na mkewe wakitoka kanisani baada ya kufunga pingu za maisha.



Drogba na MkeweLalla Diakite wanatoka dini tofauti huku mkewe akiwa Muislamu na Drogba ni Mkristu wa madhehebu ya Roman Katoliki lakini wote wanaheshimu dini zao.
Wachunguzi wa maisha ya Ma Star wanasema Drogba na Mkewe Lalla Diakite hawa ni version ya kiafrica mpya ya David and Victoria Bekham huku mitandao ikimsifia kuwa ni mtu aliyemheshimu sana mkewe na kutokuwa nakashfa za ngono kama wachezaji wengine.










Natamani makala hii imfikie Tenga na FIFA..

RAIS WA TFF-LEODEGAR TENGA

Napenda kutumia nafasi hii kufikisha mawazo na maoni kama sio malalamiko yangu juu ya ufanisi wa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF).

Lengo langu ni kuzungumzia jinsi TFF isivyo makini kuhusu waamuzi wa kandanda hapa nchini. Ikumbukwe kuwa moja ya vilio vya wapenzi wa soka nchini kwetu ni uamuzi mbovu unaofanywa na wataalamu hawa(marefa). Hivyo basi ili mwamuzi awe na kiwango kizuri ni lazima azijue vizuri sana sheria 17 zinazolinda mchezo wa soka, kwa vitendo, nadharia na awe na utimamu wa mwili kwa asilimia mia moja.

Mambo yote hayo yanapimwa kwa mitihani husika ya aina mbalimbali, yaani kuandika, kujieleza, vitendo na kupimwa utimamu wa mwili ikijumlisha na uwezo wa macho ya mwamuzi, iwapo mwamuzi atafeli moja ya majaribio hayo ni wazi basi mwamuzi husika hayupo fiti na hafai kwa michezo ya ndani wala ya kimataifa mana huko ataliahibisha Taifa husika.

Hivyo basi TFF na washirika wake FRAT (Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania) kwa pamoja waliendesha mitihani uliofanyika mwezi August mwaka jana kwa ajili ya kuwapata waamuzi wa kuchezesha mashindano mbalimbali ya msimu wa (2010/2011).

Pia mtihani huo ulitumika kupata waamuzi walioshiriki kozi ya FIFA kwa ajili ya kutafuta beji za FIFA kwa mwaka 2011 kwa waamuzi wa Tanzania. Katika kozi ya FIFA mambo yote ya msingi yalizingatiwa katika kutambua uwezo wa mwamuzi, kwani katika kozi ile ya takribani wiki moja waamuzi walijaribiwa juu ya ufahamu wao wa sheria za mchezo wa soka kwa nadharia, vitendo, kwa mahojiano na mwisho walipimwa utimamu wa mwili ( Physical Fitness Test).

Katika kozi ile ya FIFA kwa mujibu wa walihudhuria ni kwamba kuna baadhi ya waamuzi wakongwe waliohudhulia walichemsha vibaya sana, baadhi yao walipata alama sifuri katika mitihani yao ya kuandika na hata fwalipotakiwa kujieleza hali ilikuwa ngumu zadi kwani waamuzi wale kama Hamis Changwalu na wengineo mambo yaliwawia ugumu sana, kiasi cha kuwahudhi, kuwakasirisha na kuwakatisha tamaa wakufunzi wa FIFA hadi kufikia hatua ya kuuliza inakuwaje waamuzi kama hao wanafika hadi ngazi ya kimataifa lakini hawajui lolote?

Wakati hali ikiwa hivyo, baadhi ya waamuzi walifanya vizuri sana katika kozi ile hadi kufikia hatua ya wakufunzi kuwapa zawadi ili kuleta changamoto, kwani vijana walionesha kuiva na hamu kubwa ya kusonga mbele katika fani ya uamuzi wa soka.

kwa kuwa hali halisi ilishajionesha darasani ni wazi ikaonekana wazi kuwa sasa wakati umefika wa kuondokana na waamuzi wa kupendelewa,, hivyo basi ratiba ya ligi kuu ilipotoka waamuzi wale wakongwe hawakupangwa kabisa na inasemekana hawakupangwa kwa sababu walifeli mtihani ulioandaliwa na TFF mahususi kwa ajili ya kusaka waamuzi wa ligi kuu, hivyo kufeli kwao kulimaanisha hawafai kwa msimu wote wa 2010/2011.

Zaidi ya hapo waamuzi walewale waliofeli mtihani wakakumbana na kashfa ya kujihusisha na michezo isiyo tambuliwa na FIFA, hivyo kwa mantiki hiyo FIFA hakuwa inawahitaji tena katika jopo lake,achilia mbali kuwa wamefeli mitihani .
Lakini cha kushangaza ni kwamba tarehe 21/12/2010 TFF kupitia kaimu katibu wake mkuu bwana Sunday B. Kayuni, limetangaza majina ya waamuzi 14 ambao FIFA imewapatia beji baada ya TFF kuwa imewaombea kwa madai kuwa walifaulu vizuri mitihani ya FIFA! Haiingii akilini hata kidogo kuwa eti katika list hiyo wale waliofeli wamepatiwa beji then wale waliofaulu majina yao hayakutumwa au FIFA wameyanyima beji!!! Sijui TFF ilitumia kigezo gani kutuma majina huko FIFA, lazima kunamchezo mchafu hapa hususani wa RUSHWA na zaidi Kayuni anauelewa..asiwafanye Watanzania wote wanaopenda soka na zaidi fani ya uamuzi ni wajinga na yeye ndio mweerevu....TAKUKURU mpo wapi ...?

Lawama nyingi juu ya hili wakuzibeba ni Kayuni na LESLIE LIUNDA kwani wao ndio wanaojua namna majina yalivyotumwa FIFA, Maana inasemekana kama huna wa kukubeba au huna pochi beji ya FIFA Tanzania uitaisikia kwenye radio tu,maana wakina Kayuni na Liunda na TFF kwa ujumla wamegeuza ulaji wao...na ndio maana waamuzi wa Tanzania WANAISHIA HAPA HAPA, NA SI KWAMBA HAWANA UWEZO BALI upendeleo umezidi; mwisho wa siku tunapeleka waamuzi wa hovyo na kuwacha wa kweli nyuma.

Tafadhali Tenga epukana na aibu hii kwa kuunda kamti UCHUNGUZE JINSI MAJINA YALIVYOTUMWA FIFA NA MWISHO WA SIKU WAHUSIKA WAWAJIBISHWE, LINDA HESHIMA ULIYOJIJENGEA MKUU.

Natamani makala hii imfikie Tenga na FIFA lakini siwezi mi sipo karibu na watu hawa, sina adress zao,


*Walaka huu umeandikwa na mmoja wa wadau kutoka ndani ya chama cha waamuzi Tanzania ( FRAT )


MAN UTD KWELI INABEBWA? USHAHIDI HUU HAPA!


mwamuzi Howard Webb ni kweli anaipendelea Man Utd?
Na Geofrey Lea
Ujumbe wa Twitter uliotumwa na Ryan Babel aliyekuwa mchezaji wa Liverpool kipindi hicho ambao ulikuwa umesindikizwa na picha ya kutengenezwa iliyokuwa inamuonyesha mwamuzi Howard Webb akiwa amevalia jezi ya Man United ni moja ya kelele zisizoisha dhidi ya Man United toka kwa wapinzani wake wanaodai kuwa klabu hii hubebwa na waamuzi pamoja na ukweli kuwa takwimu zinaonyesha kinyume cha yale ambayo wengi wanadhani .
Mashabiki wengi wa soka hasa wale wanaofuatilia kwa karibu ligi kuu ya England wamejenga imani kuwa Manchester United ni klabu inayopendelewa na waamuzi wanaochezesha mechi zao . Imani hii si kwa mashabiki tu bali imehamia hata kwa waandishi wa habari za michezo hususani soka na wachambuzi wa mechi za ligi kuu ya England ambapo utawasikia wakisema kwa lugha ya kiingereza kuwa ‘YOU DON’T GET THOSE AT OLD TRAFFORD ‘ yaani huwezi kupata hizo Old Trafford wakimaanisha kuwa timu pinzani hazipati penati Old Traford , wengine utawasikia wakisema kuwa ‘IF THAT WAS DOWN AT THE OTHER END IT WAS A PEN’ yaani ‘ kama hii ingetokea kwenye upande wa pili ingekuwa penati bila wasiwasi ‘ na wengine wakiubatiza ule muda wa nyongeza wa dakika za majeruhi kwa jina la ‘Fergie Time’ yaani muda wa fergie . Lakini swali la kujiuliza ni moja , je tuhuma hizi kwa waamuzi na kwa Man United zina ukweli wowote ndani yake ? Takwimu zinasema si kweli .
Msimu huu wakiwa wanaongoza ligi kwa tofauti ya pointi baada ya michezo 29 huku wakiwa wamefuzu kwa hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa na nusu fainali ya kombe la FA,Manchester United wamezawadiwa jumla ya penati tano katika michuano hii yote wanayoshiriki , wakiwa Old Traford dhidi ya Liverpool kwenye kombe la FA , Old Traford tena kwenye EPL dhidi ya Arsenal , na dhidi ya West ham pia kwenye EPL , na ugenini wamepata penati dhidi ya Fulham kwenye EPL na dhidi ya Rangers kwenye ligi ya mabingwa. Katika penati hizo zote zilizotajwa United wamefanikiwa kufunga penati tatu tu , hii ikimaanisha kuwa penati zimechangia kwa asilimia 3.8 % ya magoli yaliyofungwa na Manchester United msimu huu na katika penati hizi ni penati moja tu ambayo United walipewa dhidi ya Liverpool ambayo unaweza kusema walipendelewa .
Kwa wapinzani wa United ambao wengi ndio wanaongoza hizi nyimbo za kuwa marefa wengi ni wanazi wa Mashetani wekundu , Arsenal wamezawadiwa penati 14 msimu huu huku nyingi kati ya hizo zikiwa za utata hasa pale anapohusika Mmorocco Marouane Chamakh . Kati ya penati hizi arsenal wamefanikiwa kufunga kumi na hii inamaanisha asilimia 11.8% ya mabao yote ambayo Arsenal imefunga yamechangiwa na penati . Kwa upande mwingine Chelsea wamezawadiwa penati 10 ambazo wamefunga 8 na kukosa 2 na ikiletwa kwenye mahesabu ya asilimia utagundua asilimia 9.5 ya mabao yaliyofungwa na Chelsea yametokana na matuta . Matajiri wa Manchester City wamepata jumla ya penati 9 ambazo wamefunga 7 na kukosa mbili kwa asilimia ya 9.3 ya mabao yao yote . Liverpool nao wamepewa penati 8 ambazo wamefunga 6 huku wakiwa na asilimia 11.8 ya mabao ya penati .
Takwimu hizi zinawatia aibu wale wanaodai United inapendelewa hasa kwa kutumia kigezo cha penati wanazopata . Ukiwatazama Arsenal wamepewa penati ambazo ni zaidi ya mara tatu ya zile walizopata United huku timu zingine zilizotajwa hapo juu nazo zikiwa zimezidi United sana tu kwa penati ambazo waamuzi wanatoa , na hata ukitazama asilimia ya mabao ambayo timu inafunga kupitia penati utaona kuwa United ndio yenye asilimia chache kuliko wenzie , sasa kwa penati tu ni nani mwenye faida ya kupendelewa na marefa ? hiyo nawaachia wasomaji .
Tukiwa hapa hapa kwenye mjadala wa penati hebu turudi nyuma na kutazama idadi ya penati ambazo timu mbalimbali za EPL zimepewa tangu mwaka 2003 ambapo takwimu hizi zilianza kutunzwa .
Liverpool – 36
Arsenal – 35
Chelsea – 30
Aston Villa – 27
Fulham – 24
Tottenham – 23
Blackburn – 22
Man City- 22
Everton 21.

Pamoja na kuwa timu inayoshambulia zaidi kwenye ligi kuu ya England Manchester United imefunga mabao machache kupitia penati kutofautisha na wapinzani wake wakuu kwenye ile big four ambao ni Arsenal , Liverpool na Chelsea , United wamefunga mabao machache kwa penati kuliko hata Aston Villa , Fulham na Tottenham . Penati zimewapa United jumla ya asilimia 5.1 ya mabao yao kulinganisha na Liverpool , Arsenal na Chelsea ambao wamepata asilimia 9.1% , 7.5%, na 6.6% .
Tukiangalia upande wa pili wa penati ambazo zimepewa kwa timu ambazo zimecheza na United utagundua kuwa penati 13 zimegawiwa kwa wapinzani wa United huku wenzie kina Liverpool wakiwa wameshuhudia wapinzani wakipewa penati 15 , Arsenal 17, na Chelsea 12. Hii inamaanisha kuwa mabao ambayo United imefungwa kwa njia ya penati ni sawa na asilimia 7.2 % , huku Liverpool wakifungwa sawa na asilimia 7.4 ya mabao kupitia penati huku Arsenal na Chelsea wakiwa wamefungwa sawa na asilimia 8.1 ya mabao kupitia kwa mikwaju ya penati . Takwimu hizi kwa upande mmoja zinafanana .
Kama tukifananisha asilimia zote hizi za jumla ya mabao yote ambayo timu zimefunga na zimefungwa kupitia kwa penati ambapo United wamefunga asilimia 5.1 na wamefungwa 7.2 ukiongeza namba hizi utapata – 2.1 /% utagundua kuwa United wanaonekana kuwa na wastani mbaya kuliko wenzie ambao ni Liverpool ( wakiwa wamefunga 9.1% na wamefungwa 7.4% na ukuzidisha unapata wastani wa jumla wa +1.7% na Arsenal wao wamefunga 7.5% na wamefungwa 8.1% wanapata wastani wa kuzidisha ambao ni -0.6 na mwisho Chelsea ambao wamefunga 6.6% na wamefungwa -1.5% .
Kwa faida tu ya wale wanaopenda rekodi za takwimu hizi kati ya timu kubwa nne za England ( United , Chelsea , Liverpool na Arsenal ) ni Liverpool pekee ambao wameonekana kufaidika sana na maamuzi ya penati toka mwaka 2003 kuliko timu zingine , cha kuchekesha ni jinsi mashabiki hawa hawa wa Liverpool ambao wanaongoza kelele za kusema kuwa United inapendelewa na waamuzi . Takwimu zaidi zinaonyesha kuwa tangu mwaka 99 Liverpool wamezawadiwa jumla ya penati 53 tofauti na United ambao wamezawadiwa 46 . N takwimu zingine zinaonyesha kuwa tangu kuanzishwa kwa Premier league mwaka 92 hadi leo hii Manchester United wamezawadiwa jumla ya penati 88 ambazo ni sawa na wastani wa 4.7 kwa kila msimu na kati ya hizo wameweza kufunga 66 na kukosa zilizobaki na hii inamaanisha kuwa United wamefunga asilimia ndogo ya 4.7% ya mabao ya penati kati ya mabao yote waliyofunga tangu kipindi hicho . Kwa kukifananisha kiwango hiki cha muda wote na viwango vya msimu huu tu vya timu nyingine tunaweza kufikia muafaka kuwa United imepata faida ndogo sana ya penati toka kwa waamuzi kwa kulinganisha na wenzie tangu kuanzishwa kwa ligi kuu ya England .
Tuziache penati kando na tutazame maamuzi mengine ya uwanjani . Hapa ndio kwenye utata zaidi kwani ushahidi unajidhihirisha wenyewe kwa kuyatazama matukio mbalimbali yanayotokea ambayo ndio hasa kiini cha kelele za kuwa United wanafaidika na maamuzi ya upendeleo toka kwa marefa .
Wengi wanarejea kwenye matukio yaliyotokea kwenye michezo baina ya United na Stoke City na West Bromwich Albion ambapo wanadai kuwa United wana bahati kuongoza ligi kwani kwani Gary Neville alinusurika kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwenye michezo yote hii miwili kwa matukio tofauti yanayofanana huku West Brom wakinyimwa penati iliyoonekana dhahiri kabisa .
Wakati kukiwa na ukweli thabiti kabisa kwenye kesi ya West Brom kunyimwa penati kuna kitu kilichotokea kwenye mchezo huu ambacho wengi aidha wamekisahau , hawakukiona au wanakifumbia macho kwa unafiki wa kishabiki . Man United nao walinyimwa penati na mwamuzi huyu huyu aliyewanyima West Brom tena kwenye mchezo huu huu baada ya mchezaji wa West Brom kuunawa mpira kwenye eneo la hatari baada ya mpira uliopigwa na Fabio . Wakati wengi wanasema Neville ambaye kwa sasa amestaafu alinusurika kutolewa kwa kadi nyekundu wanasahu kuwa kadi ya njano ya kwanza iliyoonyeshwa kwa Neville haikuwa sahihi kwani hakucheza rafu bali aliucheza mpira . Pengine tunaweza kutofautiana kwa tafsiri ya kipi ni rafu na kipi si rafu lakini yaliyo wazi yanaonekana bila ubishi .
Tukio lingine ambalo ningependa kuukumbusha ulimwengu ni bao la kusawazisha alilofunga Lee Bowyer wakati United ilipomenyana na Birmingham City bao ambalo lilifungwa kwenye dakika ya mwisho ya mchezo . Bao hili kimsingi halikupaswa kukubaliwa kama bao halali kwani kulikuwa na matukio manne (4) tofauti yaliyotokea yanapelekea bao hili kutokuwa halali . Kulikuwa na nyakati mbili ambazo zilitokea haraka haraka ambapo mshambuliaji wa Birmingham Nikola Zigic aliwaparamia mabeki wa United mabegani kwa kutumia mikono yake , ukiacha hilo kulikuwa na tukio la mchezaji wa Birmingham kuunawa mpira na mfungaji Lee Bowyer alikuwa ameotea , haya yote yalitokea ndani ya sekunde zisizopungua 50 ambapo Birmingham walifunga bao la kusawazisha . Hakuna shabiki wa United , mchezaji , kocha wala kiongozi aliyesikika akilalamikia bao lile .
Tukio lingine wanalosahau wengi ni mechi mbili baina ya United na Chelsea pale Old Trafford mwishoni mwa msimu uliopita na kule Stamford Bridge mechi ambazo ukiangalia kiundani ziliigharimu United kuweka rekodi ya kutwaa taji la nne mfululizo la EPL . Mechi ya kwanza ambayo timu hizi zilicheza ilikuwa pale Stamford Bridge ambapo Chelsea walishinda kwa bao moja bila , bao lililowekwa wavuni na John Terry kwa kichwa . Bao hili la Terry halikuwa halali . Didier Drogba akiwa kwenye nafasi ya kuotea alimn’ga’ngania WesBrown na kumwangusha chini na kwa kufanya hivyo akamtengenezea Terry Mazingira ya kufunga . Tukirejea mechi iliyochezwa Old Traford ambapo matokeo yalikuwa ushindi wa mabao 2-1 kwa Chelsea utagundua kuwa bao la ushindi lililofungwa na Didier Drogba halikuwa sahihi kwani Didi alikuwa ameotea kwa takribani robo tatu nzima ya mita na hivyo hivyo Chelsea wakatwaa ubingwa wa EPL . Swali kwa wale wanaopiga kelele juu ya kupendelewa kwa United , ni lini United iliwahi kutwaa taji kwa kuwa na faida ya maamuzi ya refa kama walivyopoteza msimu uliopita .
Maamuzi ya marefa hayajaiuma United kwenye EPL pekee bali hata kwenye ligi ya mabingwa . Mashetani wekundu walikuwa njiani kuelekea kwenye ushindi dhidi ya Bayern Munich msimu uliopita mpaka pale beki Rafael alipoonyeshwa kadi mbili za njano na hivyo kutolewa nje kwa kadi nyekundu , sawa kabisa lakini mwamuzi hakuona faulo aliyochezewa Rafael sekunde mbili zilizopita kabla na pengine rafu ile ndio iliyomnkera Rafael na kumpelekea kucheza rafu iliyomtoa yeye huku aliyemchezea akibaki uwanjani . Mwaka 2003 , bao la Paul scholes kwenye mchezo dhidi ya Fc Porto lilikataliwa kwa madai kuwa aliotea wakati alikuwa kwenye eneo ambalo hakuwa ameotea tena wazi kabisa , bao hili lingeipa United faida ya bao moja zaidi na hata lile bao la Costinha lililoipa Porto faida na kuitoa United lisingekuwa na maana .
Kwenye kombe la Carling msimu uliopita wakati United inapambana na Manchester City kwenye hatua ya nusu fainali City walizawadiwa penati isiyo sahihi kwa rafu aliyochezewa Carlos Tevez nje ya eneo la hatari lakini United walienda na kushinda mchezo huo , hivyo wakati mashabiki wa Man City wakilalama juu ya muda wa ziada ulioongezwa juu ya ule wa majeruhi wa dakika nne ambapo Michael Owen alifunga bao la ushindi wanasahau kuhusu penati waliyopewa lakini kwa United issue ya penati aliyopewa Tevez imesahaulika kwa mashabiki wa United , kwanini? Kwa kuwa United hawakuruhusu suala lile liwadhuru walijinyanyua kama wanavyofanya siku zote na kuyendelea na kazi iliyokuwa mbele yao na wakaitimiza kwa kumfunga City mabao 3-1 kwenye mechi ya marudiano na wakaelekea kutwaa kombe hilo . Na ni sababu hii ambayo inafanya maamuzi ambayo yanaiuma United yasahulike haraka kwa kuwa ni timu ya washindi ambao mara nyingi hawaruhusu kunyimwa ushindi na masuala madogo kwani mara nyingi maamuzi hayawadhuru kwani huendelea na kazi na kushinda mwishowe na hivyo kuondoa maana ya maamuzi mabovu dhidi yao .
Moja ya vitu ambavyo mashabiki wengi hutaja kama ushahidi wa United kupendelewa ni ule muda unaoongezwa zaidi ya zile dakika 90 yaani Stoppage Time ambao kule England hivi sasa mashabiki wameupachika jina la Fergie Time wakidai kuwa mara nyingi United inapofungwa marefa huongeza dakika za kuwatosha United kufunga bao aidha la kusawazisha au hata la ushindi . Wengi hurejea matukio kama lile lililotokea mwaka 1993 kwenye mchezo kati ya Man United na Sheffield United ambapo dakika 7 za ziada ziliongezwa dakika ambazo United wakiwa nyuma waliweza kusawazisha na kufunga bao la ushindi na tukio la hivi karibuni ambapo United walifunga bao kwenye sekunde ya 88 baada ya dakika nne za nyongeza kuwa zimeisha . Wanachosahau watu wengi ni kuwa kwenye tukio la kwenye mechi ya United na Sheffield refa aliumia na hivyo alibadilishwa na hii ilikuwa baada ya kuwa amehudumiwa uwanjani kwa muda wa dakika tano ambazo ukiaongeza na zile za kufidia kuumia kwa wachezaji na mabadiliko utaona kuwa hata dakika 7 zilizoongezwa hazikuwa zinatosha bali ilibidi ziongezwe dakika zaidi . Tukija kwenye tukio la hivi karibuni tena Baada ya muda kuwa umeongezwa wa dakika 4 Manchester City walipata bao la kusawazisha ambapo walitumia dakika zisizopungua mbili kushangilia na kurejea uwanjani wakiamini kuwa wamepata walau sare , baada ya hapo Sir Alex Fergusson alifanya mabadiliko ambapo alimuingiza Michael Carrick hivyo utagundua kuwa dakika moja na sekunde 27 zilizoongezwa juu ya ule muda wa dakika 4 ni sahihi kabisa na wala hakuna upendeleo .
Kwa hali ya kawaida mafanikio hujenga hisia za chuki inayotokana na wivu walio nao wale ambao hawajafanikiwa . Kama zinavyoonyesha takwimu kelele zote ambazo United wanapigiwa juu ya kupendelewa sio sahihi . Sio kwa suala la Penati wala maamuzi ya kawaida tena ukiingia ndani zaidi utaona kuwa United ndio wanaopaswa kulalamika kwa sababu wanaonekana kugharimiwa na maamuzi mengi yasiyo sahihi yaliyoenda dhidi yao . Kokote pale uendako timu yenye mafanikio ndio inayochukiwa sana na wapinzani , ilikuwa hivyo Enzi za kina Kenny Dalglish na Kevin Keegan na Liverpool yao iliyokuwa inatesa England ,ilikuwa hivyo kwa Juventus italia miaka ya 90 , na hata Bayern Munich pia . Kikubwa ni kuwa United hairuhusu maamuzi kuwazuia na mara nyingi yale ambayo yameenda kwa upande wao ndio yanayoonekana kuliko yale yanayoenda dhidi yao kwani si mara nyingi huwa yanawadhuru

CAF YAWAPORA UENYEJI WA KOMBE LA MATAIFA YA AFRICA LIBYA


Shirikisho la soka barani Afrika CAF limefikia uamuzi wa kuyaondoa mashindano AFCON 2013 nchini LIBYA kutokana na nchi hiyo kugubikwa na vurugu za kisiasa.
Kwa mujibu wa CAF kwa sasa bado hawajaamua ni namna gani watatumia kupata mwenyeji mpya wa mashindano hayo yanayotarajia kufanyika mwakani.

Monday, June 13, 2011

KALI YA LEO

MARTIN PALERMO AASTAFU SOKA HUKU AKIMWAGA MACHOZI


Kuna vitu vingi vinanijia ndani ya kichwa changu muda huu.Nawashukuru wote kwa mapenzi mlionionyesha kwa miaka yote.Tumeshinda vitu vingi na tumehuzunika pamoja lakini siku zote tumekuwa tunatabasamu pamojal.” –ni maneno ya Martin Palermo mchezaji wa kimataifa wa Argentina na timu ya Boca Juniors akiwaaga mashabiki waliojazana katika uwanja wa Bombanera baada ya kuamua kustaafu huku akitokwa na machozi.

MAN U YATHIBITISHA USAJILI WA PHIL JONES

Manchester United leo wamethibitisha kumsajili beki/kiungo Phil Jones kutoka Blackburn kwa paundi 16.Jones amesaini mkataba wa kuichezea United kwa muda wa miaka mitano.

Mazembe sasa kukata rufaa Fifa kupinga kuondolewa mashindanoni.

Mabingwa watetezi wa kombe la klabu bingwa barani Afrika,TP Mazembe wamesema wanaenda kukata rufaa Fifa badala ya CAS baada ya kuondolewa kwenye michuano hiyo.
Caf iliiondosha TP Mazembe baada ya Simba kupinga uhalali wa mchezaji Janvier Besala Bokungu.
Mazembe iliifunga Simba jumla ya mabao 6-3 kwenye raundi ya pili lakini baadaye Simba ikakata rufaa dhidi ya Bokungu.
Timu hiyo toka nchini Congo imempata mwanasheria Luc Misson pamoja na mshirika wake Gregory Ernes kwa ajili ya kusimamia kesi hiyo.
Misson ndiye alikuwa mwanasheria aliyeisimamia kwa mafanikio kesi Jean-Marc Bossman mnamo mwaka 1995 aliyekua akipigania uhamisho huru mara tu baada ya mkataba ya wanasoka kumalizika.
Bokungu, mwenye umri wa miaka 22 mzaliwa wa jiji la Kinshasa alijiunga na Esperance mnamo mwaka 2007 akitokea Mazembe kabla ya kujiunga tena na klabu yake ya zamani.
Ripoti zinasema Bokungu aliuvunja mkataba na klabu hiyo ya Tunisia uliokua unadumu hadi mwezi wa june mwaka huu.
"TP Mazembe haitakiwi kulaumiwa kwa usajili wa Janvier Bessala Bokungu," walisikika hao mawakili wawili kupitia kwenye tovuti ya Mazembe.
"Bessala hakuwa mchezaji wa Esperance ya Tunisia tangu mwezi wa tatu mwaka 2010. Mkataba wake na klabu ya Tunisia ulisitishwa na chama cha soka cha nchi ya jamhuri ya Congo,ambacho kiliidhinisha uhamisho wake kujiunga na klabu ya Virunga, klabu ambayo baadaye ilimuuza kwa Mazembe.
"leo Esperance wanadai ni mchezaji wao wakati kwa kipindi chote hiki walikua hawamlipi msahara na wala hawakufanya jitihada zozote ili apate kibali cha kufanya kazi nchini Tunisia.
"kibaya zaidi kupitia tovuti yao walitoa taarifa mnamo mwezi machi mwaka 2010 ya kwamba wamemuacha na nafasi yake imechukuliwa na mchezaji mwingine."

NIKIONDOKA UNITED NATAKA NIFUNDISHWE NA MOURINHO- NANI


Manchester United winger Nani amekiri ana hamu ya kufundishwa na kocha Real Madrid Jose Mourinho.

Nani anasisitiza bado ana furaha ndani ya United lakini hatma yake imekuwa ikizua maswali mengi tangu Manchester United ilipoanza usajili msimu huu.

Antonio Valencia amekuwa akipangwa zaidi ya Nani, Ashley Young yupo njiani kuingia Old Trafford huku Kocha wa United Sir Alex Ferguson akiwa anawawania Wesley Sneijder, Samir Nasri na Alexis Sanchez.

Nani aliachwa katika kikosi kilichoanza katika Champions League final na amekuwa akizivutia timu za Real Madrid, Juventus na Inter Milan.


The 24-year-old Portugal international, ambaye aliwasili United kutoka Sporting Lisbon mwaka 2007, alisem: "Nipo vizuri hapa United, lakini ni vizuri kusikia kuna timu nyingine zinakutaka.Ningependa sana siku nikiondoka hapa nifundishwe na kocha Jose Mourinho.Niliachwa nikiwa na mawazo baada ya kutoswa katika kikosi cha champions league kwa kuwa nilikuwa na imani nitaanza ule mchezo, lakini ni juu ya maamuzi ya kocha.Msimu huliopita ulikuwa very positive kwa Manchester United na mimi binafsi."

Nani alifunga magoli 10 katika mashindano yote akiwa na United na alitoa pasi za magoli 18.

ARSENAL YAWAKATAA THIAGO ALCANTARA, BOJAN NA PAUNDI MILLIONI 30 KUTOKA BARCA KWA AJILI YA FABREGAS


Arsenal wamekataa ofa kutoka Barcelona kwa ajili ya kiungo Cesc Fabregas.

Gazeti la El Mundo Deportivo limesema Arsenal wamekataa ofa ya ya paundi millioni 30 pamoja na Thiago Alcantara na Bojan Krkic ili Fabregas ajiunge na mabingwa hao wapya wa Ulaya.The Gunners waliweka wazi mapema kuwa watafikiria kumuuza Cesc ikiwa timu inayomtaka itatoa fedha taslim wanayoitaka.

Arsenal wanataka £40 million ili kumwachia Cesc - kiasi ambacho Barca wamepanga kutumia kufanya usajili msimu huu.

Nafasi pekee kwa Barcelona ni pale ambapo Fabregas ataingilia kati na kuwaomba Arsenal wapunguze kiasi wanachotaka.

DALLAS WATWAA UBINGWA WA NBA

Dallas Mavericks wamefanikiwa kushinda taji lao la kwanza la NBA baada ya ushindi wa ponti 105-95 mbele ya Miami Heat na kushinda jumla ya michezo 4-2 kwenye fainali hizo za NBA msimu huu.
Guard Jason Terry alifunga pointi 27,mjerumani Dirk Nowitzki aliongeza pointi 21 kwa Mavericks, ambayo ilishinda michezo minne kati ya mitano iliyopita.
Ulikua ushindi mtamu kwa mashabiki wa Mavericks kwani walikua wanalipiza kisasi kwani Miami Heat nao walishinda taji lao la kwanza huko Dallas kwenye mchezo wa sita mwaka 2006.
Mshambuliaji wa Mavericks Nowitzki alitaja ' most valuable player (MVP)
.

SABABU ZILIZOSABABISHA SIMBA KUCHEZA HOVYO PAMOJA NA KUSHINDA BAO 1-0

Na Shaffih Dauda
KWA VIPINDI TOFAUTI TOFAUTI NIMEKUWA NIKIANGALIA MECHI ZA SIMBA,KWA MUDA SASA SIJAWAHI KUONA SIMBA INACHEZA MCHEZO MBOVU KAMA MCHEZO DHIDI TA DCMP.
NIMEKUWA NA MASWALI MENGI YA KUJIULIZA NINI HASA KIMESHUSHA KIWANGO CHA SIMBA GHAFLA NAMNA HIYO, NI KWELI WACHEZAJI TAYARI WALIKUA MAPUMZIKONI BAADA YA KUMALIZA MSIMU WA LIGI ,UKIPITIA KWENYE BLOG YANGU YA www.shaffih.blogspot UTAWEZA KUONA BAADHI YA WACHEZAJI WA VILABU VYA ULAYA WAKIWA MAPUMZIKONI WAKILA RAHA NA FAMILIA ZAO,IVI KAMA IKITOKEA DHARURA JOHN TERRY KWA JINSI UNAVYOMUONA ANAJIACHIA ANATAKIWA KUCHEZA MECHI YA KIUSHINDANI ATASHINDWA ETI ALIKUA MAPUMZIKONI ?
BINAFSI SITAKI KUAMINI JUU YA HILO, NAKUMBUKA KWENYE FAINALI ZA EURO 1992 TIMU YA TAIFA YA DENMARK ILIPATA NAFASI YA KUSHIRIKI MASHINDANO WIKI MBILI KABLA YA MASHINDANO BAADA YA KUPEWA NAFASI YA ILIYOKUA YUGOSLAVIA ILIYOTOLEWA MASHINDANO KUTOKANA NA VITA VYA YUGOSLAVIA, DENMARK PAMOJA NA KUPEWA TAARIFA YA KUSHIRIKI DAKIKA ZA MAJERUHI WALIFANIKIWA KUCHUKUA UBINGWA TENA KWA KUWAFUNGA WALIOKUWA MABINGWA WATETEZI UHOLANZI KWENYA NUSU FAINALI NA PIA UJERUMANI KWENYE MCHEZO WA FAINALI.
BAADA YA KUTAFAKALI NIMEONA HIZI SABABU ZIMEIGHALIMU SIMBA

1. KUKOSEKANA KWA AMRI SAID
ACHILIA MBALI KUKOSEKANA KWA PATRICK PHIRI, KWA MUDA MREFU KTK MCHEZO DHIDI DC MOTEMA PEMBE KOCHA MOSES BASENA NDIYE ALIKUA NA JUKUMU LA KUONGEA NA WACHEZAJI WAKATI MCHEZO UKIENDELEA, BINAFSI SIKUCHEZA SOKA KWA NGAZI YA JUU SANA,ILA MWAKA 2001 KWENYE LIGI DARAJA LA KWANZA NIKIWA NA COSMOPOLITAN,TULIKUA NA KOCHA RAIA WA CONGO DC KWASASA NI MAREHEMU,SELEMAN KIIZA,HAKUWA NA UWEZO WA KUWASILIANA NASISI MOJA KWA MOJA WAKATI MCHEZO UNAENDELA KUTOKANA NA KUTOWEZA KUONGEA LUGHA YA KISWAHILI KWA UFASAHA BADALA YAKE ALIKUA ANAMPA MAELEKEZO KOCHA WETU MSAIDIZI AMBAYE ALIKUA NI MZAWA NA SISI TUKAWA TUNAWASILIANA NAYE MOJA KWA MOJA, HATA KOCHA MSAIDIZI WA TIMU YA TAIFA YA ENGLAND STUART PEARCE NDIYE HUWA ANAWASILIANA MOJA KWA MOJA NA WACHEZAJI WAKATI MCHEZO UKIENDELEA HUKU FABIO CAPELLO AKIWA AMEKAA TU,NAKUMBUKA NDANI YA KIKOSI CHA SIMBA CHA PATRICK PHIRI JUKUMU HILI ALIKUA NALO AMRI SAID NA NDIVYO INAVYOTAKIWA KUWA POPOTE PALE AMBAPO KUNA KOCHA AMBAYE HAWEZI KUWA NA MAWAASILIANO YA MOJA KWA MOJA NA WACHEZAJI KUTOKANA NA MATATIZO YA LUGH A. NAAMINI KUNA MANENO AMBAYO BASENA ALIKUA ANAYAZUNGUMZA NA ANATAKA YAFANYIWE MABADILIKO HARAKA SANA HAYAKUFANYIWA SABABU YA KUTOKUZUNGUMZA LUGHA YA KISWAHILI KWA UFASAHA.

2. KUJIONDOA KIKOSINI KIUNGO HILLARY ECHESA
MKATABA WA ECHESA UNAMALIZIKA MWISHONI MWA MWEZI HUU WA SITA,KWAHIYO SIKU MOJA KABLA YA MCHEZO ECHESA ALIUAMBIA UONGOZI WA SIMBA UMPATIE MKATABA MPYA LA SIVYO HATACHEZA MCHEZO DHIDI YA DCMP,KWA UPANDE WAKE ALISHAONA KUNA LONGO LONGO JUU YA MUSTAKABALI WAKE WA BAADAE NDANI YA SIMBA,
MKATABA HAKUPEWA HIVYO AKATIMKA ZAKE,KIUTAALAM KUJIONDOA KWAKE GHAFLA KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE KULIATHILI SIMBA UKICHUKULIA YEYE NDIYE ALIKUA NA JUKUMU LA KUKIONGOZA KIKOSI HICHO KWENYE NAFASI YA KIUNGO. LAKINI PIA KWA MUDA ULE HATA WACHEZAJI WANAPOSIKIA MWENZAO AMEONDOKA KWASABABU KAMA HIZO KIDOGO ZINAWAPUNGUZIA UMAKINI KATIKA MAANDALIZI YAO.
3. KIKOSI FINYU
BAADA YA KIUNGO JERRY SANTO KUSIMAMISHWA KUTOKANA NA KUWA NA KADI ZA NJANO ,KIKOSI CHA SIMBA KILIBAKI NA WACHEZAJI 16 TU,KWA IDADI HII YA WACHEZA HATA PROGRAM ZA BENCHI LA UFUNDI HAZIWEZI KWENDA VIZURI.ACHILIA MBALI KINA HARUNA MOSHI,ULIMBOKA MWAKINGWE,ATHUMAN IDD NA OBADIA MUNGUSA AMBAO PIA WALIKUA SEHEMU YA KIKOSI LAKINI HAWANA RUHUSA YA KUCHEZA HAYA MASHINDANO.
4. MOHAMED BANKA NA NICO NYAGAWA KUCHEZA KWA WAKATI MMOJA.
LABDA SABABU YA TATU NDO IMESABABISHA HILI KUTOKEA, MCHEZO WA JANA SIMBA WALIZIDIWA SANA KWENYE SEHEMU YA KIUNGO KUTOKANA NA NAMNA AMBAVYO WALISHINDWA KUSHINDANA NA VIUNGO WA DCMP KUGOMBANIA MIPIRA KATIKA ENEO HILO, ANGALI YULE KIUNGO ALIYEKUA NA NYWELE NYEUPE ALIVYOKUA ANATEMBEA ,HIVI KARIBUNI KLABU YA AC MILAN YA NCHINI ITALIA ILIGUNDUA KUWATUMIA KWA PAMOJA VIUNGO ( GENARRO GATUSO,MASSIMO AMBROSINI, ANDREA PIRLO,GIANLUCA ZAMBROTTA,CLARENCE SEEDORF,MASSIMO ODDO LILIKUA KOSA LA JINAI,SI KWAMBA HAWAKUA NA UWEZO, LA ASHA,WAKATI ULIKUA NYUMA YAO KUTOKANA NA NAMNA MPIRA WA SIKU HIZI UNAVYOCHEZWA SPIDI NA NGUVU NI VITU VINAVYOTUMIKA SANA,KWA UMRI WA MIAKA ZAIDI YA 30 WALIOKUA NAO ISINGEWEZEKANA WOTE KWA PAMOJA KUCHEZA KWENYE TIMU MOJA,NDIYO MAANA MILAN ILILAZIMIKA KUWAJUMUISHA WACHEZAJI VIJANA KAMA MATHEAU FLAMINI, PRINCE BOATENG,IGNACIO ABATE,LUCA ANTONINI WAKAFANIKIWA KUCHUKUA UBINGWA WA SERIE A, PIA MSIMU HUU MAN UTD HAIKUWATUMIA KWENYE KIKOSI KIMOJA WAKONGWE PAUL SCHOLES NA RYAN GIGGS,KWAHIYO NADHANI KUWACHEZESHA KWA PAMOJA BANKA NA NYAGAWA AMBAO UMRI WAO NI ZAIDI YA MIAKA 30 KULIIPUNGUZIA SIMBA NGUVU KWENYE SEHEMU YA KIUNGO.
5. NYOSO NA YONDANI PATNERSHIP
SIKU HIZI MPIRA UMEBADILIKA SANA UKILINGANISHA NA ZAMANI ,SIKU H IZI MAJUKUMU YAMEBADILIKA SANA KIWANJANI UKILINGANISHA NA ZAMANI,ZAMANI WACHEZAJI WALIKUA WANAPANGWA KWA NAMBA SIKU IZI MIFUMO NDIYO INATENGENEZA VIKOSI,SASA BASI MAJUKUMU YA MABEKI WAWILI WA KATI KATI YAMEBADILIKA UKILINGANISHA NA WAKATI HUO WA NYUMA AMBAPO BEKI MMOJA WA KATI ALIKUA ANACHEZA HURU HUKU NAMBA SITA NA NAMBA NNE WAKIWA NA JUKUMU LA KUWAKABA WASHAMBULIAJI WA TIMU PINZANI,SIKU IZI BEKI MMOJA WA KATI LAZIMA AWE NA JUKUMU LA KUSAIDIA KUTENGENEZA MASHAMBULIZI NA PIA KWA WAKATI FURANI KUSOGEA KWENYE KIUNGO KUONGEZA IDADI,MFANO ANGALIA WANAVYOCHEZA GERALD PIQUE -BARCELONA ,RIO FERDINAND- MAN UTD,DANIEL AGGER –LIVERPOOL,ALEX AU DAVID LUIZ-CHELSEA,RIC CALVALHO-REAL MADRID,VINCENT KOMPANY-MAN CITY HAO NI WACHACHE TU PAMOJA NA KUWA NA JUKUMU LA KUOKOA NA KUZUIAMASHAMBULIZI PIA WAO NI WAANZILISHI WAZURI WA MASHAMBULI,SASA WAANGALIE YONDANI NA NYOSO KAZI WANAZOZIFANYA ZINA TOFAUTI ? HAKUNA HATA MMOJA ANAYESOGEA MPAKA KATIKATI ILI KUONGEZA IDADI YA WACHEZAJI KWENYE SEHEMU YA KIUNGO, KIBAYA ZAIDI WOTE WANABUTUA MIPIRA BAADA YA KUIANZISHA MATOKEO YAKE MABEKI WA TIMU PINZANI WANAPATA FAIDA YA KUANZISHA MASHAMBULIZI MARA NYINGI .
6. KOCHA MOSES BASENA
UKIANGALIA KWA UMAKINI WACHEZAJI WA SIMBA WALIKUA WAMECHOKA SANA ,NAJUA UTAKUA NA MASWALI MENGI, TATIZO KUBWA WACHEZAJI WALIPEWA MAZOEZI MAGUMU SANA YA KUWAJENGA .HIYO HAIKATAZWI LAKINI NAVYOFAHAMU KADRI SIKU ZA MECHI ZINAVYOKARIBIA NDIVYO MAZOEZI MAGUMU HUWA YANAPUNGUA,ILIKUA KINYUME KABISA KWA MOSES BASENA ,KUANZIA JUMATANO MPAKA IJUMAA TIMU ILIKUA INACHEZA UWANJA MZIMAMECHI YA WENYEWE KWA WENYEWE DAKIKA 70,TENA SIKU MBILI ZA MWISHO KWENYE UWANJA MPYA WA TAIFA,ASIKWAMBIE MTU KWA YEYOTE ALIYECHEZA SOKA ATAKUA ANAFAHAMU UKICHEZA MECHI TATU MFULULUIZO MWILI LAZIMA ‘UNOKI’
MAANA UNAKUA UMECHOKA KUPITA MAELEZO,KWA HILI BASENA ALIKOSEA KUWACHEZESHA MECHI SIKU TATU MFULULIZO SIKU NNE KABLA YA MECHI YA MASHINDANO.
NIMALIZIE KUWAPONGEZA SIMBA KWA NAMNA WALIVYOLIFUNGA GOLI LAO,

UTAJUTA - WENGER MWAMBIA NASRI


ARSENE WENGER amemuonya Samir Nasri kuwa hajamaliza mzunguko na kama anataka kukamilika kama mchezaji bora inambidi abaki Emirates.

Akiwa amebakisha mwaka mmoja katika wake Nasri sasa amekuwa ni hot cake katika dirisha la usajili barani ulaya, Manchester United, Inter Milan na Bayern Munich wakivutia na kiungo huyo wa Ufaransa.

Wenger ambaye kwa sasa yupo vitani katika kuhakikisha anawabakisha Nasri na Cesc Fabregas alisema "Tutafanya kila kitu kinachowezekana kumbakisha Nasri aendelee kuwa nasi.Kama ataangalia nyuma ataona ametoka mbali na sisi na nafikiri bado kuna kidogo vya kufanya.Ni klabu ndio inayomtengeneza mchezaji.

Akimuongelea Fabregas Wenger alisema, "Nitakuwa muwazi zaidi kwa suala hili, kwangu mimi Fabregas yupo na Arsenal na ataendelea kuwa hapa.Muda mwingine tetesi huwa zinatokea kipindi cha usajili.Msimu ujao tutaona utambulisho wa financial fair play system, ambayo itaweka udhibiti wa viwango kwenye uhamisho mkubwa, nafikiri huu ndio mwaka wa mwisho ambao kipindi cha usajili kitakuwa vurugu."


NASRI: NIPENI PAUNDI 160,000 AU NAONDOKA


SAMIR NASRI amewatuma wawakilishi wake Arsenal wampe mshahara wa kiasi cha £160,000 a week au aondoke.

Kutokana na kauli ya Nasri sasa inaonekana ni itakuwa ni vigumu kwa Arsenal kumshawishi mchezaji huyo asaini mkataba mwingine baada ya mkataba wake kuelekea kuisha.

Manchester United na sasa Bayern Munich wamekuwa wakihusishwa na kutaka huduma za mchezaji huyo tangu habari za mazungumzo ya Nasri na Arsenal yalipokwama.

Arsenal boss Arsene Wenger kwa sasa yupo katika hali ngumu, hataki kumpa Nasri mshahara mkubwa huku wachezaji wengine wakitaka kuondoka.

REDKNAPP: LAZIMA TUMBAKISHE MODRIC


Harry Redknapp amesema ni lazima ahakikishe kuwa Luka Modric abaki Spurs msimu ujao ili aweze kuwasaidia kupata nafasi ya kushiriki in Champions League.

Hatima ya Modric imekuwa na kitendawili baada ya baada ya Manchester United na Chelsea kuweka wazi kuwa wanahitaji huduma za mcroatia huyo.

"Kwa hakika tunaweza kumbakisha Luka, ni mchezaji muhimu hivyo inabidi tumbakishe hapa msimu ujao.Kama tukimuuza basi ni sawa na kuuza klabu hii"

"Manchester United hawawezi .Wayne Rooney, Chelsea hawawezi kumuuza Lampard wala Terry na hauwezi kuwasikia watu wakiongea wao kuuzwa, kwahiyo kwanini na sisi tumuuze Luka Modric kama tunataka tuifanye Spurs kuwa klabu kubwa". Harry aliambia Sky News.


Sunday, June 12, 2011

WAINGEREZA WAKIENDELEA KULA, NA WAHOLANZI NAO HAWAPO NYUMA

HUNTELAAR AKIWA DISCO BAADA YA MCHEZO KIRAFIKI DHIDI YA BRAZIL

CAPTAIN JOHN TERRY NA MKEWE WAKIENDELEA KULA BATA ABU DHABI

HEITINGA AKIKAMATA KIUNO CHA DEMU WAKE

"YOU'LL NEVER DANCE ALONE) DIRK KUYT AKIWA NA DEMU AMBAYE SIO MKEWE DISCO( COLEEN ROONEY AKIWA NA MWANAE KAI WAYNE ROONEY

BECKS NA FAMILIA YAKE WAKIZUNGUKA MITAANI LOS ANGELES
BABA KAI NA MAMA KAI WAKIENDELEA KUTUMIA HUKO BARBADOS

CAPTAIN TERRY NA FAMILIA YAKE WAKIWA WAMEPANDA NGAMIA HUKO ABU DHABI
BABA AKICHEZA NA WANAE SOKA

KAMA MOVIE VILE, CAPTAIN NA MKEWE

McLEISH AACHIA NGAZI BIRMIGHAM CITY


Alex McLeish ameachia ngazi ya kuifundisha Birmigham City na sasa anatajwa kama ni kocha anayekuja kuchukua nafasi ya Gerrard Houllier ndani ya Villa Park.

McLeish ameamua kuachana na Birmigham baada ya timu hiyo kushuka daraja siku ya mwisho ya ligi ya kuu ya England msimu huu.

McLeish alikuwa kocha wa timu ya taifa ya Scotland kabla ya kuamua kujiunga na Birmigham mwaka 2007.

Aliiongoza timu hiyo yenye maskani ndani ya ST.Andrews kuchukua ubingwa wa kombe la Carling Cup baada ya kuifunga Arsenal hivyo kufanikiwa kupata tiketi ya kucheza Europa League msimu ujao.

McLeish sasa yupo tayari kukatiza mji na kuchukua majukumu ya kuwqfundisha mahasimu wa Birmigham Aston Villa.

Villa kwa sasa wamekuwa wakatafuta mbadala wa Gerard Houllier ambaye aliachanan na klabu hiyo baada ya ligi kuu kuisha.


SIMBA VS DC MOTEMA MAPEMBE PHOTOS

Mfungaji wa goli Mussa Mgosi na Shija Mkina wakichuana na wachezaji DCMP
DC MOTEMA MAPEMBE WAKIFARIJIANA BAADA YA KIPIGO
KUTOKANA NA PUBLICITY MBOVU MECHI HII HAIKUPATA MAPOKEO MAKUBWA KWA WASHABIKI NA KUPELEKEA UWANJA KUWA MAPENGO.UONGOZI WA SIMBA UJIFUNZE
Mwanamuziki wa Acudo Impact Tatis Masela akiwa uwanjani kuisapoti timu ya DCMP YA NCHINI KWAO CONGO
Sports Extra Crew wakimuhoji Makamu Mwenyekiti wa Simba
Mashabiki wa Simba wakishangalia ushindi wa timu yao
Kiungo huyu wa DCMP aliwasumbua sana Simba

MATCH CENTER: FULL TIME SIMBA 1 - 0 DCMP


Msimbazi leo ni furaha tupu baada ya kufanikiwa kuwafunga DC Motema Mapembe katika uwanja wa taifa jijini Dar Es Salaam jioni hii katika mechi ya raundi kwanza ya Kombe la shirikisho.
Kwa ushindi huu Simba sasa wameingiza mguu mmoja katika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika.
Mechi ya marudiano itafanyika wiki mbili baadae jijini Kinshasha Congo.

MATCH CENTER: SIMBA 1 -0 DCMP HALF TIME


Simba inaongoza kwa goli moja dhidi ya DC Moteme Mapembe, goli limefungwa katika kipindi cha kwanza na mshambuliaji Mussa Hassan Mgosi.