Search This Blog

Tuesday, June 14, 2011

Natamani makala hii imfikie Tenga na FIFA..

RAIS WA TFF-LEODEGAR TENGA

Napenda kutumia nafasi hii kufikisha mawazo na maoni kama sio malalamiko yangu juu ya ufanisi wa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF).

Lengo langu ni kuzungumzia jinsi TFF isivyo makini kuhusu waamuzi wa kandanda hapa nchini. Ikumbukwe kuwa moja ya vilio vya wapenzi wa soka nchini kwetu ni uamuzi mbovu unaofanywa na wataalamu hawa(marefa). Hivyo basi ili mwamuzi awe na kiwango kizuri ni lazima azijue vizuri sana sheria 17 zinazolinda mchezo wa soka, kwa vitendo, nadharia na awe na utimamu wa mwili kwa asilimia mia moja.

Mambo yote hayo yanapimwa kwa mitihani husika ya aina mbalimbali, yaani kuandika, kujieleza, vitendo na kupimwa utimamu wa mwili ikijumlisha na uwezo wa macho ya mwamuzi, iwapo mwamuzi atafeli moja ya majaribio hayo ni wazi basi mwamuzi husika hayupo fiti na hafai kwa michezo ya ndani wala ya kimataifa mana huko ataliahibisha Taifa husika.

Hivyo basi TFF na washirika wake FRAT (Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania) kwa pamoja waliendesha mitihani uliofanyika mwezi August mwaka jana kwa ajili ya kuwapata waamuzi wa kuchezesha mashindano mbalimbali ya msimu wa (2010/2011).

Pia mtihani huo ulitumika kupata waamuzi walioshiriki kozi ya FIFA kwa ajili ya kutafuta beji za FIFA kwa mwaka 2011 kwa waamuzi wa Tanzania. Katika kozi ya FIFA mambo yote ya msingi yalizingatiwa katika kutambua uwezo wa mwamuzi, kwani katika kozi ile ya takribani wiki moja waamuzi walijaribiwa juu ya ufahamu wao wa sheria za mchezo wa soka kwa nadharia, vitendo, kwa mahojiano na mwisho walipimwa utimamu wa mwili ( Physical Fitness Test).

Katika kozi ile ya FIFA kwa mujibu wa walihudhuria ni kwamba kuna baadhi ya waamuzi wakongwe waliohudhulia walichemsha vibaya sana, baadhi yao walipata alama sifuri katika mitihani yao ya kuandika na hata fwalipotakiwa kujieleza hali ilikuwa ngumu zadi kwani waamuzi wale kama Hamis Changwalu na wengineo mambo yaliwawia ugumu sana, kiasi cha kuwahudhi, kuwakasirisha na kuwakatisha tamaa wakufunzi wa FIFA hadi kufikia hatua ya kuuliza inakuwaje waamuzi kama hao wanafika hadi ngazi ya kimataifa lakini hawajui lolote?

Wakati hali ikiwa hivyo, baadhi ya waamuzi walifanya vizuri sana katika kozi ile hadi kufikia hatua ya wakufunzi kuwapa zawadi ili kuleta changamoto, kwani vijana walionesha kuiva na hamu kubwa ya kusonga mbele katika fani ya uamuzi wa soka.

kwa kuwa hali halisi ilishajionesha darasani ni wazi ikaonekana wazi kuwa sasa wakati umefika wa kuondokana na waamuzi wa kupendelewa,, hivyo basi ratiba ya ligi kuu ilipotoka waamuzi wale wakongwe hawakupangwa kabisa na inasemekana hawakupangwa kwa sababu walifeli mtihani ulioandaliwa na TFF mahususi kwa ajili ya kusaka waamuzi wa ligi kuu, hivyo kufeli kwao kulimaanisha hawafai kwa msimu wote wa 2010/2011.

Zaidi ya hapo waamuzi walewale waliofeli mtihani wakakumbana na kashfa ya kujihusisha na michezo isiyo tambuliwa na FIFA, hivyo kwa mantiki hiyo FIFA hakuwa inawahitaji tena katika jopo lake,achilia mbali kuwa wamefeli mitihani .
Lakini cha kushangaza ni kwamba tarehe 21/12/2010 TFF kupitia kaimu katibu wake mkuu bwana Sunday B. Kayuni, limetangaza majina ya waamuzi 14 ambao FIFA imewapatia beji baada ya TFF kuwa imewaombea kwa madai kuwa walifaulu vizuri mitihani ya FIFA! Haiingii akilini hata kidogo kuwa eti katika list hiyo wale waliofeli wamepatiwa beji then wale waliofaulu majina yao hayakutumwa au FIFA wameyanyima beji!!! Sijui TFF ilitumia kigezo gani kutuma majina huko FIFA, lazima kunamchezo mchafu hapa hususani wa RUSHWA na zaidi Kayuni anauelewa..asiwafanye Watanzania wote wanaopenda soka na zaidi fani ya uamuzi ni wajinga na yeye ndio mweerevu....TAKUKURU mpo wapi ...?

Lawama nyingi juu ya hili wakuzibeba ni Kayuni na LESLIE LIUNDA kwani wao ndio wanaojua namna majina yalivyotumwa FIFA, Maana inasemekana kama huna wa kukubeba au huna pochi beji ya FIFA Tanzania uitaisikia kwenye radio tu,maana wakina Kayuni na Liunda na TFF kwa ujumla wamegeuza ulaji wao...na ndio maana waamuzi wa Tanzania WANAISHIA HAPA HAPA, NA SI KWAMBA HAWANA UWEZO BALI upendeleo umezidi; mwisho wa siku tunapeleka waamuzi wa hovyo na kuwacha wa kweli nyuma.

Tafadhali Tenga epukana na aibu hii kwa kuunda kamti UCHUNGUZE JINSI MAJINA YALIVYOTUMWA FIFA NA MWISHO WA SIKU WAHUSIKA WAWAJIBISHWE, LINDA HESHIMA ULIYOJIJENGEA MKUU.

Natamani makala hii imfikie Tenga na FIFA lakini siwezi mi sipo karibu na watu hawa, sina adress zao,


*Walaka huu umeandikwa na mmoja wa wadau kutoka ndani ya chama cha waamuzi Tanzania ( FRAT )


No comments:

Post a Comment