Search This Blog

Monday, June 13, 2011

NASRI: NIPENI PAUNDI 160,000 AU NAONDOKA


SAMIR NASRI amewatuma wawakilishi wake Arsenal wampe mshahara wa kiasi cha £160,000 a week au aondoke.

Kutokana na kauli ya Nasri sasa inaonekana ni itakuwa ni vigumu kwa Arsenal kumshawishi mchezaji huyo asaini mkataba mwingine baada ya mkataba wake kuelekea kuisha.

Manchester United na sasa Bayern Munich wamekuwa wakihusishwa na kutaka huduma za mchezaji huyo tangu habari za mazungumzo ya Nasri na Arsenal yalipokwama.

Arsenal boss Arsene Wenger kwa sasa yupo katika hali ngumu, hataki kumpa Nasri mshahara mkubwa huku wachezaji wengine wakitaka kuondoka.

13 comments:

  1. uyu mtoto analana sana ka2ka 120 2 160 poa mwaache aende apishane namakombe

    ReplyDelete
  2. mpira pesa na mafanikio come nasri@man united.

    ReplyDelete
  3. Dogo kwa dau alilotaja ni wazi anataka kuondoka arsenal hivyo ni bora auzwe kwani hata akibaki hatacheza kwa kiwango kile kile kwa misimu ijayo.

    ReplyDelete
  4. Mchezaji mkubwa anapenda mafanikio, kwa hiyo huwezi kukaa timu ambayo inacheza misimu zaidi ya mi5, bila hata kombe la mbu, Nasri nenda kanyanyue vikomba Man U...........

    ReplyDelete
  5. vikombe siyo tatizo ila kucheza kwa moyo, upendo na ali ndiyo siri ya mafanikio, Nasri ameamua kuondoka acha aondoke bwana, hajui kwamba tunasuka kikosi bora, shauri yake atajuta.

    ReplyDelete
  6. hahahahahahahaha.... man u bana..... mnapenda kujipigia chapuoo.... by the way haondoki arsenal..

    ReplyDelete
  7. haendi kokote huyu Wenger anawajulia wafaransa wenzake

    ReplyDelete
  8. NASRI YOUR WELCOME MAN U, JAPO UVALISHWE NISHANI MWAKANI.

    ReplyDelete
  9. Dick mkali(The Gunners) KINACHO NISHANGAZA NI WEWE BWANA SHAFFIH SIJUI HIZI HABARI HUWA UNAZITOLEA WAPI NDUGU YANGU, UJUE KAMA HUWEZI MAMBO YA MPIRA BORA UKAE KIMYA KULIKO KUDANGANYA WATU, WE HUO MSHAHARA WA 160,000 KASEMA LINI HEBU ACHA KUTUNGA HABARI ZA UONGO AU KWA KUWA WEWE SHABIKI WA MAN U BASI UNAWAFARIJI MASHABIKI WENZIO. AU BORA UANDIKE MAMBO YA MAN U TU.

    ReplyDelete
  10. nasri nenda man ukalete utamu arsena hawataki vikombe

    ReplyDelete
  11. nasri! tumtoa machokolani na kwa taarifa yake mshahara wa paund 160,000 a week hapati na hauzwi na msimu mzima atakalia bench tuone kama hao wanao mtia wazimu na kumlingishia mipesa watamuona kwenye pitch, akikomaa sana tunamuuza Azam FC dolla 20,000 tu.

    ReplyDelete
  12. kwa mtazamu wangu arsenal hawawezi ktoa icho kiasi bola wamuachie aende man .

    ReplyDelete
  13. huyu dogo sasa sijui anataka nini hamna mfalme wa milele zaidi ya mungu tuu walikuwepo kina Henry na mashujaa wengine pale wako wapi sasa na yeye mwache aende tu kama aliletwa pale basi wataletwa na wengine na club itaendelea kuwepo ajue tuu yeye hatakuwa yupo siku zote .

    ReplyDelete