Search This Blog

Monday, June 13, 2011

Mazembe sasa kukata rufaa Fifa kupinga kuondolewa mashindanoni.

Mabingwa watetezi wa kombe la klabu bingwa barani Afrika,TP Mazembe wamesema wanaenda kukata rufaa Fifa badala ya CAS baada ya kuondolewa kwenye michuano hiyo.
Caf iliiondosha TP Mazembe baada ya Simba kupinga uhalali wa mchezaji Janvier Besala Bokungu.
Mazembe iliifunga Simba jumla ya mabao 6-3 kwenye raundi ya pili lakini baadaye Simba ikakata rufaa dhidi ya Bokungu.
Timu hiyo toka nchini Congo imempata mwanasheria Luc Misson pamoja na mshirika wake Gregory Ernes kwa ajili ya kusimamia kesi hiyo.
Misson ndiye alikuwa mwanasheria aliyeisimamia kwa mafanikio kesi Jean-Marc Bossman mnamo mwaka 1995 aliyekua akipigania uhamisho huru mara tu baada ya mkataba ya wanasoka kumalizika.
Bokungu, mwenye umri wa miaka 22 mzaliwa wa jiji la Kinshasa alijiunga na Esperance mnamo mwaka 2007 akitokea Mazembe kabla ya kujiunga tena na klabu yake ya zamani.
Ripoti zinasema Bokungu aliuvunja mkataba na klabu hiyo ya Tunisia uliokua unadumu hadi mwezi wa june mwaka huu.
"TP Mazembe haitakiwi kulaumiwa kwa usajili wa Janvier Bessala Bokungu," walisikika hao mawakili wawili kupitia kwenye tovuti ya Mazembe.
"Bessala hakuwa mchezaji wa Esperance ya Tunisia tangu mwezi wa tatu mwaka 2010. Mkataba wake na klabu ya Tunisia ulisitishwa na chama cha soka cha nchi ya jamhuri ya Congo,ambacho kiliidhinisha uhamisho wake kujiunga na klabu ya Virunga, klabu ambayo baadaye ilimuuza kwa Mazembe.
"leo Esperance wanadai ni mchezaji wao wakati kwa kipindi chote hiki walikua hawamlipi msahara na wala hawakufanya jitihada zozote ili apate kibali cha kufanya kazi nchini Tunisia.
"kibaya zaidi kupitia tovuti yao walitoa taarifa mnamo mwezi machi mwaka 2010 ya kwamba wamemuacha na nafasi yake imechukuliwa na mchezaji mwingine."

No comments:

Post a Comment