Search This Blog

Monday, June 13, 2011

SABABU ZILIZOSABABISHA SIMBA KUCHEZA HOVYO PAMOJA NA KUSHINDA BAO 1-0

Na Shaffih Dauda
KWA VIPINDI TOFAUTI TOFAUTI NIMEKUWA NIKIANGALIA MECHI ZA SIMBA,KWA MUDA SASA SIJAWAHI KUONA SIMBA INACHEZA MCHEZO MBOVU KAMA MCHEZO DHIDI TA DCMP.
NIMEKUWA NA MASWALI MENGI YA KUJIULIZA NINI HASA KIMESHUSHA KIWANGO CHA SIMBA GHAFLA NAMNA HIYO, NI KWELI WACHEZAJI TAYARI WALIKUA MAPUMZIKONI BAADA YA KUMALIZA MSIMU WA LIGI ,UKIPITIA KWENYE BLOG YANGU YA www.shaffih.blogspot UTAWEZA KUONA BAADHI YA WACHEZAJI WA VILABU VYA ULAYA WAKIWA MAPUMZIKONI WAKILA RAHA NA FAMILIA ZAO,IVI KAMA IKITOKEA DHARURA JOHN TERRY KWA JINSI UNAVYOMUONA ANAJIACHIA ANATAKIWA KUCHEZA MECHI YA KIUSHINDANI ATASHINDWA ETI ALIKUA MAPUMZIKONI ?
BINAFSI SITAKI KUAMINI JUU YA HILO, NAKUMBUKA KWENYE FAINALI ZA EURO 1992 TIMU YA TAIFA YA DENMARK ILIPATA NAFASI YA KUSHIRIKI MASHINDANO WIKI MBILI KABLA YA MASHINDANO BAADA YA KUPEWA NAFASI YA ILIYOKUA YUGOSLAVIA ILIYOTOLEWA MASHINDANO KUTOKANA NA VITA VYA YUGOSLAVIA, DENMARK PAMOJA NA KUPEWA TAARIFA YA KUSHIRIKI DAKIKA ZA MAJERUHI WALIFANIKIWA KUCHUKUA UBINGWA TENA KWA KUWAFUNGA WALIOKUWA MABINGWA WATETEZI UHOLANZI KWENYA NUSU FAINALI NA PIA UJERUMANI KWENYE MCHEZO WA FAINALI.
BAADA YA KUTAFAKALI NIMEONA HIZI SABABU ZIMEIGHALIMU SIMBA

1. KUKOSEKANA KWA AMRI SAID
ACHILIA MBALI KUKOSEKANA KWA PATRICK PHIRI, KWA MUDA MREFU KTK MCHEZO DHIDI DC MOTEMA PEMBE KOCHA MOSES BASENA NDIYE ALIKUA NA JUKUMU LA KUONGEA NA WACHEZAJI WAKATI MCHEZO UKIENDELEA, BINAFSI SIKUCHEZA SOKA KWA NGAZI YA JUU SANA,ILA MWAKA 2001 KWENYE LIGI DARAJA LA KWANZA NIKIWA NA COSMOPOLITAN,TULIKUA NA KOCHA RAIA WA CONGO DC KWASASA NI MAREHEMU,SELEMAN KIIZA,HAKUWA NA UWEZO WA KUWASILIANA NASISI MOJA KWA MOJA WAKATI MCHEZO UNAENDELA KUTOKANA NA KUTOWEZA KUONGEA LUGHA YA KISWAHILI KWA UFASAHA BADALA YAKE ALIKUA ANAMPA MAELEKEZO KOCHA WETU MSAIDIZI AMBAYE ALIKUA NI MZAWA NA SISI TUKAWA TUNAWASILIANA NAYE MOJA KWA MOJA, HATA KOCHA MSAIDIZI WA TIMU YA TAIFA YA ENGLAND STUART PEARCE NDIYE HUWA ANAWASILIANA MOJA KWA MOJA NA WACHEZAJI WAKATI MCHEZO UKIENDELEA HUKU FABIO CAPELLO AKIWA AMEKAA TU,NAKUMBUKA NDANI YA KIKOSI CHA SIMBA CHA PATRICK PHIRI JUKUMU HILI ALIKUA NALO AMRI SAID NA NDIVYO INAVYOTAKIWA KUWA POPOTE PALE AMBAPO KUNA KOCHA AMBAYE HAWEZI KUWA NA MAWAASILIANO YA MOJA KWA MOJA NA WACHEZAJI KUTOKANA NA MATATIZO YA LUGH A. NAAMINI KUNA MANENO AMBAYO BASENA ALIKUA ANAYAZUNGUMZA NA ANATAKA YAFANYIWE MABADILIKO HARAKA SANA HAYAKUFANYIWA SABABU YA KUTOKUZUNGUMZA LUGHA YA KISWAHILI KWA UFASAHA.

2. KUJIONDOA KIKOSINI KIUNGO HILLARY ECHESA
MKATABA WA ECHESA UNAMALIZIKA MWISHONI MWA MWEZI HUU WA SITA,KWAHIYO SIKU MOJA KABLA YA MCHEZO ECHESA ALIUAMBIA UONGOZI WA SIMBA UMPATIE MKATABA MPYA LA SIVYO HATACHEZA MCHEZO DHIDI YA DCMP,KWA UPANDE WAKE ALISHAONA KUNA LONGO LONGO JUU YA MUSTAKABALI WAKE WA BAADAE NDANI YA SIMBA,
MKATABA HAKUPEWA HIVYO AKATIMKA ZAKE,KIUTAALAM KUJIONDOA KWAKE GHAFLA KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE KULIATHILI SIMBA UKICHUKULIA YEYE NDIYE ALIKUA NA JUKUMU LA KUKIONGOZA KIKOSI HICHO KWENYE NAFASI YA KIUNGO. LAKINI PIA KWA MUDA ULE HATA WACHEZAJI WANAPOSIKIA MWENZAO AMEONDOKA KWASABABU KAMA HIZO KIDOGO ZINAWAPUNGUZIA UMAKINI KATIKA MAANDALIZI YAO.
3. KIKOSI FINYU
BAADA YA KIUNGO JERRY SANTO KUSIMAMISHWA KUTOKANA NA KUWA NA KADI ZA NJANO ,KIKOSI CHA SIMBA KILIBAKI NA WACHEZAJI 16 TU,KWA IDADI HII YA WACHEZA HATA PROGRAM ZA BENCHI LA UFUNDI HAZIWEZI KWENDA VIZURI.ACHILIA MBALI KINA HARUNA MOSHI,ULIMBOKA MWAKINGWE,ATHUMAN IDD NA OBADIA MUNGUSA AMBAO PIA WALIKUA SEHEMU YA KIKOSI LAKINI HAWANA RUHUSA YA KUCHEZA HAYA MASHINDANO.
4. MOHAMED BANKA NA NICO NYAGAWA KUCHEZA KWA WAKATI MMOJA.
LABDA SABABU YA TATU NDO IMESABABISHA HILI KUTOKEA, MCHEZO WA JANA SIMBA WALIZIDIWA SANA KWENYE SEHEMU YA KIUNGO KUTOKANA NA NAMNA AMBAVYO WALISHINDWA KUSHINDANA NA VIUNGO WA DCMP KUGOMBANIA MIPIRA KATIKA ENEO HILO, ANGALI YULE KIUNGO ALIYEKUA NA NYWELE NYEUPE ALIVYOKUA ANATEMBEA ,HIVI KARIBUNI KLABU YA AC MILAN YA NCHINI ITALIA ILIGUNDUA KUWATUMIA KWA PAMOJA VIUNGO ( GENARRO GATUSO,MASSIMO AMBROSINI, ANDREA PIRLO,GIANLUCA ZAMBROTTA,CLARENCE SEEDORF,MASSIMO ODDO LILIKUA KOSA LA JINAI,SI KWAMBA HAWAKUA NA UWEZO, LA ASHA,WAKATI ULIKUA NYUMA YAO KUTOKANA NA NAMNA MPIRA WA SIKU HIZI UNAVYOCHEZWA SPIDI NA NGUVU NI VITU VINAVYOTUMIKA SANA,KWA UMRI WA MIAKA ZAIDI YA 30 WALIOKUA NAO ISINGEWEZEKANA WOTE KWA PAMOJA KUCHEZA KWENYE TIMU MOJA,NDIYO MAANA MILAN ILILAZIMIKA KUWAJUMUISHA WACHEZAJI VIJANA KAMA MATHEAU FLAMINI, PRINCE BOATENG,IGNACIO ABATE,LUCA ANTONINI WAKAFANIKIWA KUCHUKUA UBINGWA WA SERIE A, PIA MSIMU HUU MAN UTD HAIKUWATUMIA KWENYE KIKOSI KIMOJA WAKONGWE PAUL SCHOLES NA RYAN GIGGS,KWAHIYO NADHANI KUWACHEZESHA KWA PAMOJA BANKA NA NYAGAWA AMBAO UMRI WAO NI ZAIDI YA MIAKA 30 KULIIPUNGUZIA SIMBA NGUVU KWENYE SEHEMU YA KIUNGO.
5. NYOSO NA YONDANI PATNERSHIP
SIKU HIZI MPIRA UMEBADILIKA SANA UKILINGANISHA NA ZAMANI ,SIKU H IZI MAJUKUMU YAMEBADILIKA SANA KIWANJANI UKILINGANISHA NA ZAMANI,ZAMANI WACHEZAJI WALIKUA WANAPANGWA KWA NAMBA SIKU IZI MIFUMO NDIYO INATENGENEZA VIKOSI,SASA BASI MAJUKUMU YA MABEKI WAWILI WA KATI KATI YAMEBADILIKA UKILINGANISHA NA WAKATI HUO WA NYUMA AMBAPO BEKI MMOJA WA KATI ALIKUA ANACHEZA HURU HUKU NAMBA SITA NA NAMBA NNE WAKIWA NA JUKUMU LA KUWAKABA WASHAMBULIAJI WA TIMU PINZANI,SIKU IZI BEKI MMOJA WA KATI LAZIMA AWE NA JUKUMU LA KUSAIDIA KUTENGENEZA MASHAMBULIZI NA PIA KWA WAKATI FURANI KUSOGEA KWENYE KIUNGO KUONGEZA IDADI,MFANO ANGALIA WANAVYOCHEZA GERALD PIQUE -BARCELONA ,RIO FERDINAND- MAN UTD,DANIEL AGGER –LIVERPOOL,ALEX AU DAVID LUIZ-CHELSEA,RIC CALVALHO-REAL MADRID,VINCENT KOMPANY-MAN CITY HAO NI WACHACHE TU PAMOJA NA KUWA NA JUKUMU LA KUOKOA NA KUZUIAMASHAMBULIZI PIA WAO NI WAANZILISHI WAZURI WA MASHAMBULI,SASA WAANGALIE YONDANI NA NYOSO KAZI WANAZOZIFANYA ZINA TOFAUTI ? HAKUNA HATA MMOJA ANAYESOGEA MPAKA KATIKATI ILI KUONGEZA IDADI YA WACHEZAJI KWENYE SEHEMU YA KIUNGO, KIBAYA ZAIDI WOTE WANABUTUA MIPIRA BAADA YA KUIANZISHA MATOKEO YAKE MABEKI WA TIMU PINZANI WANAPATA FAIDA YA KUANZISHA MASHAMBULIZI MARA NYINGI .
6. KOCHA MOSES BASENA
UKIANGALIA KWA UMAKINI WACHEZAJI WA SIMBA WALIKUA WAMECHOKA SANA ,NAJUA UTAKUA NA MASWALI MENGI, TATIZO KUBWA WACHEZAJI WALIPEWA MAZOEZI MAGUMU SANA YA KUWAJENGA .HIYO HAIKATAZWI LAKINI NAVYOFAHAMU KADRI SIKU ZA MECHI ZINAVYOKARIBIA NDIVYO MAZOEZI MAGUMU HUWA YANAPUNGUA,ILIKUA KINYUME KABISA KWA MOSES BASENA ,KUANZIA JUMATANO MPAKA IJUMAA TIMU ILIKUA INACHEZA UWANJA MZIMAMECHI YA WENYEWE KWA WENYEWE DAKIKA 70,TENA SIKU MBILI ZA MWISHO KWENYE UWANJA MPYA WA TAIFA,ASIKWAMBIE MTU KWA YEYOTE ALIYECHEZA SOKA ATAKUA ANAFAHAMU UKICHEZA MECHI TATU MFULULUIZO MWILI LAZIMA ‘UNOKI’
MAANA UNAKUA UMECHOKA KUPITA MAELEZO,KWA HILI BASENA ALIKOSEA KUWACHEZESHA MECHI SIKU TATU MFULULIZO SIKU NNE KABLA YA MECHI YA MASHINDANO.
NIMALIZIE KUWAPONGEZA SIMBA KWA NAMNA WALIVYOLIFUNGA GOLI LAO,

3 comments:

  1. I agree with u Shaffii well done,mimi ni mshabiki wa kufa wa Simba na nilisafiri kutoka Dodoma kuja kucheki hiyo game bt to my suprise ningekua ni mtaani ningeomba nirudishiwe chenji yangu,very poor display,totally outplayed in The Midfield and it reached a time hawakua na game plan kivitendo,Yondani na nyoso wana mipira ya kizamani basi tu washabiki wanawajaza ujinga.Katika mabeki wa kati waliokua na uwezo wa kuanzisha mashambulizi Hiero wa Madrid ya ukweli is my Number one kaka.big up we komaaa unafanya kazi nzuri usichoshwe na maraia wanaochonga eti mnakopi,ofcoz hata mimi nasoma sana magazeti ya Daily mirror football,the sunfootball na Daily mail football but tangu uanzishe blog yako sijawahi kuacha kuitembelea,hawajui kwamba analyst wa bongo ana maneno yake yakuinogesha story ukaifurahia japokua ulishaisoma net na huo ndo utandawazi so mnachokifanya nikushare informations and not copying kama haters wanavyosema.Ujue kuna watu hawajawahi kua appreciate mtu kwa kitu chochote tangu wamezaliwa kaka wao ni fitina tu.

    ReplyDelete
  2. kiasi naungana nawe MAESTRO lakini wasiwasi wungu mkubwa kwa wachezaji wa kitanzania ni football intelligence yao. mara nyingi wanashindwa kujua majukumu yao kwa wakati husika. hata kadi nyekundu tuliyopata ni tatizo la Iq ya mchezaji. professionalism iko chini mno.

    mie nadhani tuendelee kupiga kelele kuwapo kwa academy nyingi hapa nchini, hizi ndio zitatibu matatizo yetu

    ReplyDelete
  3. umenena ila phiri pengo kubwa Msimbazi. Bora wangempigia magoti yule Mbulgeria, wa Jamhuri Kiwelo akarudi-namaanisha Benzisky!

    ReplyDelete