
Klabu ya ligi kuu ya Uingereza Manchester United leo wamethibitisha kumsajili winga Ahley Young kutoka Aston Villa kwa mkataba wa miaka mitano, baada ya kufaulu vipimo vya afya jana jioni.

| National Team | Year | Apps | Goals | Assists |
|---|---|---|---|---|
| France | 1994 | 2 | 2 | 0 |
| 1995 | 6 | 2 | 3 | |
| 1996 | 12 | 2 | 4 | |
| 1997 | 8 | 1 | 0 | |
| 1998 | 15 | 5 | 3 | |
| 1999 | 6 | 1 | 1 | |
| 2000 | 13 | 4 | 4 | |
| 2001 | 8 | 2 | 0 | |
| 2002 | 9 | 1 | 2 | |
| 2003 | 7 | 3 | 3 | |
| 2004 | 7 | 4 | 1 | |
| 2005 | 5 | 2 | 1 | |
| 2006 | 10 | 3 | 1 | |
| Total | 108 | 31 | 23 | |
haaaa! haaaaa! hiyo mipira ni idadi ya magoli waliyojifunga.
Alexis Sanchez ameipiga chini Manchester City baada ya kukataa kupanda ndege kwenda kufanya mazungumzo ya kujiunga na Matajiri wa Premier League kwa dili lenye thamani ya £30 million.
Superstar huyo kutoka Chile ambaye kwa sasa yupo katika kambi ya timu ya taifa inayojiandaa na michuano ya Copa America alipewa ruhusa na klabu yake ya Udinese kwenda jijini Manchester kufanya mazungumzo na City baada ya timu hiyo inayomilikiwa na matajiri wa kiarabu kuwashinda Man United na Barcelona.
Lakini Sanchez baada ya kuambiwa na klabu yake aliwaambia City sio chaguo lake hivyo ajiunge na United au aongee na Barca kujua mipango yao.
Tukio la Sanchez kuikataa City lilitokea katika uwanja wa ndege wa Santiago ambapo waandishi wa habari walikuwa wamekusanyika kuangalia Sanchez akipanda ndege kuelekea England, lakini walikuja kugundua mchezaji amekataa kwenda uwanja wa ndege kuelekea Eastlands.
Sanchez alidhani kuwa anakwenda kuzungumza na mabingwa wa ulaya Barcelona, lakini ofa ya Barca ambayo ilihusishwa kutolewa kwa mchezaji Jeffren ilikataliwa na Udinese ambao waliamua kuichangamkia ofa nzuri ya City.
Kwa sasa usajili wa winga huyo ambaye ameamua kuingilia suala la usajili wake, upo wazi zaidi kwa vilabu vya United na Barca kupigania saini ya mchezaji huyo.
Inasemekana kuwa Barca walikuwa wanataka kutoa £22 million na kutoa mchezaji mmoja kati ya Bjoan Krkicc, Thiago Alcantara na Jeffren ambao wote walikataa kujiunga na Udinese.
Man United ambao wenyewe walitoa ofa ya £27 million cash, sasa wanapewa nafasi kubwa ya kushinda vita ya kumsaini winga huyo kutoka Chile.


Wakala wa kiungo raia wa Kenya Victor Wanyama amethibitisha kuwa klabu ya Celtic ya Uskochi wamekubali kumsajili mchezaji huyo.
Wanyama ambaye ni mdogo wake kiungo wa Inter Milan MacDonald Mariga amekuwa akizivutiwa klabu kadhaa za ulaya, lakini Celtic wanasemekana kuwa karibu na kukamilisha usajili wa mchezaji huyo.
Wanyama mwenye umri miaka 19 kwa sasa anacheza katika klabu ya Ubelgiji Germinal Beerschot, amekuwa akizivutia klabu nyingi kutokana na uwezo mzuri aliouonyesha katika klabu yake. na sasa wakala Ivan Modia amethibitisha kuwa mchezaji huyo anataka kuhamia Scotland.
Wanyama amecheza michezo 11 katika timu ya taifa, na sasa ameshajitengenezea nafasi ya kudumu ndani ya kikosi cha klabu yake, akicheza michezo 30 na akifunga magoli mawili.

'MSITARAJIE MAMBO YOTE TOKA KWA MTU MMOJA , TEGEMEENI MAFANIKIO TOKA KWA KUNDI LA WATU WATAKAOFANYA KAZI KWA PAMOJA , WATU WOTE KUWA PAMOJA , MASHABIKI KUWA PAMOJA NA TIMU, WATU KUFURAHI KUTOKANA NA KUWA NA USHIRIKIANO WA PAMOJA NA MAWASILIANO MAPYA NA UONGOZI MPYA ULIOPO. NA HILI NDILO LA MAANA NA LA MSINGI , SIO UJIO WANGU AMBAO UNAJALISHA.
KINACHOJALISHA NI MAFANIKO YA MUENDELEZO YA TIMU HII NA TUJATIBU KUYAREJEA YALE MAZURI AMBAYO TUMEYAFIKIA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA SITA NA YALE TUNAYOWEZA KUYAFIKIA PIA KATIKA MIAKA SITA IJAYO, HAKUNA UBISHI KUWA CHANGAMOTO NILIYO NAYO NI KUENDELEZA USHINDI , NIMEKUWA AINA YA MTU AMBAYE ANA NJAA YA USHINDI NA HILO NITALIENDELEZA HAPA CHELSEA.' -Andre Villas Boas

ANDRE VILLAS BOAS-KOCHA MPYA WA CHELSEA
Kitu ambacho Chelsea ya Roman Abramovich imeona kama kosa la jinai ambalo limemgharimu Ancelotti ajira yake ni kutotwaa taji la Ligi ya mabingwa barani Ulaya ambalo Roman Abramovich analitaka kwa udi na uvumba .Swali la kujiuliza ni moja , kwanini Chelsea imeukosa Ufalme wa ulaya ??? Kunaweza kukawa na majibu mengi kutoka kwa watu wenye mitazamo tofauti lakini nadhani jibu ambalo wote tutakubaliana nalo ni ukweli kwamba Chelsea walipokutana na Manchester United walizidiwa na timu ambayo ilikuwa bora zaidi yao.
Edibily Lunyamila akichanja mbuga
Lunyamila akiwa na swahiba wake Mohamed Hussein 'Chinga'
WAKATI timu zinazotarajia kushiriki katika michuano ya Klabu Bingwa afrika Mashariki na Kati zinatarajiwa kuwasili leo, Shirikisho la Kandanda Nchini, TFF bado halijalipa deni la hoteli za Tansoma na Tanso la sh. Milioni 35.