Search This Blog

Thursday, June 23, 2011

HAPPY BIRTHDAY ZINEDINE YAZID ZIDANE


Miaka 39 iliyopita siku kama ya leo kaskazini mwa jiji la Marseille- France familia ya Smail na Mallika Zidane walifanikiwa kupata mtoto wao wa tano Zinedine Zidane.

Zidane a.k.a Zizou ni moja ya wachezaji bora kabisa kuwahi kutokea katika historia ya mchezo wa soka duniani, takwimu zinadhihirisha juu ya uwezo wa Zidane.

Alianza kucheza la ushindani akiwa katika klabu ya Cannes kuanzia mwaka 1988-1992 akiwa na miaka 17, na alifanikiwa kucheza mechi 61 na kufunga magoli sita pamoja na kuiwezesha timu hiyo kupata nafasi ya 4 kwenye ligi na kwa mara ya kwanza AS Cannes walifanikiwa kucheza UEFA Cup.

Mwaka 1992-1996 alikuwa akiitumikia klabu ya Bordeaux ambapo aliichezea michezo 139 na kufunga mabao 28.Akiwa pamoja na Bixente Lizarazu na Chistopher Dougary ndani kikosi cha Bordeaux walifanikiwa kuipa timu hiyo ubingwa wa Intorto Cup in 1995 na pia kuwa washindi wa pili wa UEFA Cup.Mambo aliyoyafanya akiwa na timu hiyo yalimvutia kocha wa Blackburn Ray Harford kutaka kumsajili Zizou na Dugarry lakini mmiliki wa Blackburn Jack Walker alimwambia unamtak Zidane w NINI WAKATI TAYARI TUNAYE TIM SHERWOOD?

1996 Zizou alihamia Italy na kibibi kizee cha Turin-Juventus kw uhamisho wa paundi million 3.2.Alifnikiwa kushinda ubingwa wa Serie A 1996-1997, 1996 Intercontinental Cup lakini wakapoteza ubingwa wa ulaya baada ya kufungwa na Dortmund.Baada ya hapo alifanikiwa kushinda makombe mengine ya 1997–98 Serie A, ushindi wa pili wa 1998 UEFA champions league na 2000–01 Serie A.

Mwaka 2001 Real Madrid walimsajili kwa uhamisho wa rekodi ya dunia €75 million.Akiwa Madrid alifanikiwa kucheza michezo 155 na kufunga mabao 37.Pia alifanikiwa kushinda ubingwa wa ulaya mwaka 2001-2002, ubingwa wa La Liga 2003.Mwaka 2006 Zizou aliacha majonzi miongoni mwa wapenda soka baada ya kutangazakustaafu soka.

TAKWIMU ZA MICHEZO YA TIMU YA TAIFA

National TeamYearAppsGoalsAssists
France1994220
1995623
19961224
1997810
19981553
1999611
20001344
2001820
2002912
2003733
2004741
2005521
20061031
Total1083123

MAFANIKIO BINAFSI
ANGALIA MAVITU YA ZIDANE

No comments:

Post a Comment