Lunyamila amekuja , yupo kikosini? Hayo ndiyo yalikua maswali toka kwa Waganda pindi timu yoyote iwe ya Taifa au klabu toka Tanzania ilipokua ikienda nchini humo kwenye miaka ya tisini.
Edibily Lunyamila ni mmoja wa wachezaji magwiji wa mashindano haya ya ngazi ya vilabu kwenye ukanda huu wa CECAFA.
yanga waliwacharaza bila huruma SC Villa goli 2-1 katika uwanja wa nakivubo kwenye mechi ya fainali ya kombe lililokuwa na msisimko kipindi hicho la klabu bingwa afrika mashariki na kati na kupelekea serikali ya tanzania kutuma ndege mpaka katika uwanja wa ndege wa entebe kwenda kuwachukua waheshimiwa waliolitoa taifa kimasomaso.
hivyo kuweka adabu kwa waganda ambao hawawezi kuisahau yanga maishani mwao.
Lunyamila akiwa na swahiba wake Mohamed Hussein 'Chinga'
katika mechi hiyo mnamo dakika ya 81 beki mahili wa villa na timu ya taifa ya uganda marehemu Paul Hasule alivua jezi na kutoka nje kwa kile ambacho mwenyewe alikiri kuwa ameshindwa kumkaba winga wa yanga edibily lunyamila, lakini alilazimishwa na kocha wake kumaliza mechi kutokana na aibu iliyokuwa inawakabili.
kutokea hapo waganda walitekwa akili kutokana na kabumbu safi lililoonyeshwa na yanga na kupelekea daladala nyingi nchini humo kuandikwa majina kama "lunyamila trans" "kizota trans" au hata wengine walifuta majina ya salon zao na kuandika "gagarino hair salon" na mpaka leo hii waganda wakisikia timu kutoka tanzania inakwenda huko wanauliza "je ni yanga?".
‘’ Makali yangu kwa Waganda hasa yalianzia Kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya Express ambapo nilimbuluza sana beki George Ssemogerere na tukafanikiwa kuwafunga mabao 3-1,yaliyofungwa na ‘Chinga’ mawili na ‘ kizota’ baada ya hapo waganda hawakuamini kama nilikua na uwezo wa kumtia njaa kiasi kile Ssemogerere,kwenye mechi ya fainali dhidi ya Villa nahodha wao Paul Hasule ( Marehemu ) alikua na jukumu la kuzuia makali yangu lakini naye alishindwa kwani nilimtesa sana mapaka kuna wakati chenga yangu ilimfanya kukaa chini baada ya kukatika nyonga na huo ndio ulikua mwisho wake wa kucheza soka,tulifanikiwa kuwafunga Villa mabao 2-1 mimi nikifunga bao la pili na la ushindi’’- LUNYAMILA.

yanga katika mechi hiyo iliwakilishwa na:
1) Steven Nemes/Rifat Said ( Marehemu )
2) Mwanamtwa Kihwelu
3) Keneth Mkapa
4) Willy Mtendamema
5) Issa Athuman ( Marehemu )
6) Method Mogella ( Marehemu )
7) Zamoyoni Mogella
8) Steven Mussa/Hamis Thobias ‘gagarino’ (wote ni Marehemu )
9) Said Mwamba ‘kizota’ ( Marehemu )
10) Mohamed Husein ’Chinga’
11) Edibily Jonas Lunyamila
pia yanga walikuwa na bunduki nje kwenye benchi kama willy martin, rifat said, aboubakar salum "sure boy" david mwakalebela "MP" na wengine wengi ambao walikuwa ni miiba kwa waganda.

No comments:
Post a Comment