1:Alizaliwa tarehe 17, 1977 akiitwa Luis Andre Pina Cabral.Anaongea vizuri kabisa lugha ya kiingereza akiwa amefundishwa vizuri lugha hiyo na babu yake.
2: Ameoa na ana watoto wawili, pia Villas-Boas ametoka katika familia yenye historia ya utajiri.
3:Alianza kucheza soka kama kiungo lakini akagundua kuwa hakuwa na uwezo ulijitosheleza kuwa mchezaji wa kucheza mechi za ushindani, Villas-Boas akaamua kujiunga na uhandishi wa habari za michezo lakini akasitisha mpango huo na kuamua kujiunga na mafunzo ya ukocha kupitia Hayati Sir Bobby Robson, rafiki wa bibi yake.Anelezea: "Kipindi Mr.Robson alipokuja Porto kuwa kocha mwaka 1994 alihamia katika jengo letu.Nilikuwa mdogo lakini kwa sababu nilikuwa napenda soka nilienda kwake kumwelezea matamanio yangu.Alipenda jinsi nilivyokuwa na mapenzi na mchezo wa soka hivyo akanisaidia kuweza kuingia katika mafunzo ya ukocha ndani ya chuo cha Lilleshall.Kiukweli nisingeruhusiwa kujiunga pale kwa kuwa sheria zilikuwa haziruhusu vijana wadogo kujiunga na mafunzo.Nilikuwa kocha mdogo kuliko wote pale lakini nilikuwa na nia ya dhati ya kufanikiwa kuwa kocha mzuri."
4: Villas-Boas alikuwa na miaka 21 alipokuwa mkurugenzi wa ufundi wa visiwa vya Virgin nchini Uingereza mwaka 2000, lakini FA walikuwa hawajui.Anasimulia: "Nilikuwa mdogo, lakini hawakutambua.Niliwaambia ukweli kuhusu umri wangu siku ambayo nilikuwa naacha kazi."
5: Kocha Villas-Boas alikuja kuwa kocha msaidizi wa Porto chini ya Jose Mourinho mwaka 2002.Alikuwa ndiye kiongozi wa kitengo cha kuwasoma wapinzani, na baadae wote kwa pamoja na Mourinho wakaamia Chelsea. Mourinho alikuwa akiwaita wasaidizi wake "macho na masikio yake".Alipokuwa Chelsea alipewa jukumu la kuwapa wachezaji DVDs za kuonyesha mchezo wa wapinzani wao kwa kila mechi, akiewalezea wachezaji udhaifu na uimara wa wapinzani wao.
6: Villas-Boas anatajwa kuwa moja ya wasaidizi wa Mourinho waliohusika na ugomvi na Frank Rijkaard mwaka 2005.Andre anasema kuwa alimuona Rijkaard akiongea na refa Frisk kwa mara 3 kipindi cha mapumziko katika mchezo wa kwanza UEFA Champions League february 2005.Mourinho nae alirudia kutoa shutuma hizo za Rijkaard kumshawishi refa kuipendelea Barca hivyo kupelekea kufungiwa kwa Special One katika mechi ya pili dhidi ya Barcelona.
6: Villas-Boas anatajwa kuwa moja ya wasaidizi wa Mourinho waliohusika na ugomvi na Frank Rijkaard mwaka 2005.Andre anasema kuwa alimuona Rijkaard akiongea na refa Frisk kwa mara 3 kipindi cha mapumziko katika mchezo wa kwanza UEFA Champions League february 2005.Mourinho nae alirudia kutoa shutuma hizo za Rijkaard kumshawishi refa kuipendelea Barca hivyo kupelekea kufungiwa kwa Special One katika mechi ya pili dhidi ya Barcelona.
7:Villas-Boas pia alifanya kazi na Mourinho ndani ya Inter Milan, ingawa kwa sasa watu hawa wawili hawaongei kwa sababu ambazo Villas-Boas anazificha lakini anasema: "Tuna itikadi na maono tofauti kuhusu mchezo wa soka.Namuheshimu Mourinho lakini sitaki kufuata mitazamo yake.Nataka kuwa na uhuru wa kufanya kazi nitakavyo bila kujizuia wala kuwa wasiwasi kama anavyofikiria."
8:Villas-Boas aliacha kazi Inter mwezi wa 10, 2009 ili aweze kupata nafasi ya kuwa kocha mkuu kwenye timu ya Academia De Coimbra, iliyokuwa chini ya mkia wa msimamo wa ligi, ikiwa haijashinda mechi yoyote kati ya michezo saba lakini alifanikiwa kuifanya timu hiyo kushika nafasi ya 11 kati ya timu 16 na pia kuingoza kucheza nusu fainali ya kombe la Ureno.Mafanikio haya ndani ya miezi miwili yaliwavutia Sporting Lisbon na wakata kumpa nafasi ya kuwa kocha wao lakini Andre aliamua kurudi Porto.
9: Villas-Boas aliweka rekodi msimu uliopita akiwa Porto, baada ya kuwa ndiyo timu ya kwanza ya bara la ulaya kushinda mara mbili makombe matatu ya kombe la ligi kuu, kombe la FA, na kombe la UEFA cup.Ushindi wa kombe la UEFA cup umemfanya awe kocha umri wa mdogo kuweza kushinda kombe kubwa la barani ulaya.
10: Villas-Boas anapenda kutumia mchezo wa mashambulizi katika mfumo 4-3-3.
KARIBU STAMFORD BRIDGE SPECIAL ONE NO.2
KARIBU STAMFORD BRIDGE SPECIAL ONE NO.2
No comments:
Post a Comment