Miaka 25 iliyopita siku kama ya leo katika robo fainali ya kombe la dunia 1986 kati ya England vs Argentina, Diego Armando Maradona alifunga bao mkono na mwenyewe alipoulizwa akadai lilikuwa ni bao la mkono wa mungu.Waingereza wakatolewa katika fainali hizo na mpaka leo wananung'unika kuhusu bao la mkono la Diego.
Lakini mwaka jana katika fainali za kombe la dunia lililofanyika Afrika ya Kusini siku kama ya leo ikiwa imepita miaka 24 tangu afunge bao la mkono Diego Maradona alikuwa kwenye benchi la timu ya taifa akiongoza timu ya taifa ya Argentina kuizamisha Greece kwa mabao 2-0.
No comments:
Post a Comment