Search This Blog
Wednesday, October 17, 2012
LIVE MATCH CENTRE: SIMBA SC 2 - 2 KAGERA SUGAR FULL TIME
Mpira unamalizika hapa uwanja wa taifa na kwa maoni yangu kwa kuangalia mpira ulivyochezwwa leo, naamini Kagera walistahili kupata pointi katika mchezo huu.
DK 90: Simba 2 - 2 Kagera
DK 85: Simba 2 - 2 Kagera
DK 80: Simba wanaonekana kukosa mbinu za kuipita ngome ya Kagera katika dakika hizii, na wameendelea na tatizo lao la kutoweza kukaa na mpira kwa muda huku wakipoteza hovyo pasi.
DK 75: Simba 2 - 2 Kagera
DK 68: Juma Nyoso anacheza rafu kwenye eneo la penati na mwamuzi anaamuru penati. Kagera wanapiga na kuandika bao la pili.
DK 60: Hatimaye mfululizo wa mashambulizi ya Kagera yanazaa matunda na wanafanikiwa kupata goli moja. Simba 2 - 1 Kagera.
DK 57: Emmanuel Okwi anaingia vizuri kutokea pembeni na kuwatoka mabeki wa Kagera anapiga shuti kali na kipa anaokoa kwa ustadi mkubwa.
DK 50 Mrisho Ngassa anaifungia Simba bao la pili.
Kipindi cha pili kinaanza hapa uwanja wa taifa.
HALF TIME
DK 45: Kagera Sugar wanaonekana kuwaelemea Simba ndani ya dakika za mwisho za kipindi cha kwanza, wanafanya shambulizi kali lakini Juma Kaseja anaifanya kazi yake vizuri ya kulinda lango la mnyama.
DK 44: Simba 1 - 0 Kagera Sugar
DK 37: Simba 1 - 0 Kagera Sugar
DK 32: Haruna Moshi Boban anakosa bao la wazi baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Okwi.
DK 30: Timu zote zinashindana kumiliki mpira ingawa Kagera wanaonekana kuwazidi Simba kiasi, lakini Kagera wanakosa mipango mziru ya kuweza kupitisha mipira mbele ya Kaseja na kusawazisha goli.
DK 22: Chollo anapiga krosi safi inayomfikia Sunzu anayepiga kichwa lakini anashindwa kulenga goli na mpira unatoka nje.
DK 20: Simba 1 - 0 Kagera Sugar
DK 13: Mpira sasa uanaanza kubadilika baada ya Simba kupata goli, Kagera nao wameamka na kuanza kujibu mashambulizi.
DK 8: Felix Sunzu anafunga bao safi la kichwa hapa uwanja wa taifa. Simba 1 - 0 Kagera Sugar.
DK 5: Mchezo umeanza kwa kasi na Simba wanaonekana kulishambulia zaidi lango la Kagera wakifika mara kadhaa ndani ya sita ya Kagera lakini bado hawajatengeneza nafasi nzuri ya kufunga.
Kick off: Mpira unaanza hapa uwanja wa taifa
Ukiwa umebakia muda mchache kabla ya kipenga cha kuashiria kipute cha kukata na shoka kati ya Simba na Kagera Sugar kuanza katika dimba la uwanja wa taifa. Simba wametangaza kikosi chao cha leo.
Katika kikosi cha leo Simba itamkosa beki wake wa kutumainiwa Shomari Kapombe kutoka na kuumia, huku wakipata nguvu kutokana na kurudi kwa washambuliaji wao hatari Mrisho Ngassa na Emmanuel Okwi.
HIKI NDIO KIKOSI KINACHOANZA
Kaseja, Chollo, Maftah, Nyoso, Ochieng, Kazimoto, Ngassa, Kiemba, Sunzu, Boban, Okwi.
Sub;
Mweta, Ngalema, Hassan Hatibu, Jonas Mkude, Uhuru, Kinje na Edward Christopher
SALUM MKEMI: MUDA WA DRFA MADARAKANI UMEKWISHA.
Salum Mkemi
0715 847474
17/10/2012
Katibu Mkuu,
TFF,
D’Salaam.
Ndugu,
KUONDOLEWA KWA VIONGOZI WA DRFA IKIWA MUDA WA UONGOZI WAO UMEMALIZIKA.
Tafadhali rejea somo nililotaja hapo juu.
Naomba nichukue nafasi hii kukumbusha kuwa muda wa uongozi wa DRFA ulimalizika tarehe 12/10/2012. Siku hiyo ndio ambayo DRFA ilifanya uchaguzi mwaka 2008 mwezi wa kumi(10). Kulingana na katiba ya DRFA muda wa uongozi ulimalizika baada ya wao kumaliza muda wao wa kukaa madarakani kwa miaka minne (4).
Kulingana na katiba ya DRFA hakuna sehemu inayowapa hawa waliokuwa viongozi nafasi ya kujiongezea muda. Ibara ya 34 (Muda wa Madaraka) kifungu cha pili (2) na katiba ya mfano ya TFF inasema kuwa”The mandate of the members of the Executive Committee may be renewed. However the person who is 75 years and above shall not to be allowed to stand for presidency”
Kwa kifungu hiki hakuna mamlaka yoyote ya kisheria inayowafanya viongozi hao kuendelea kuwepo madarakani.
Hali hii inaonyesha kuwa viongozi waliomaliza muda wao wanavamia madaraka na inaonyesha TFF mnaafiki uvunjwaji huu wa katiba kwa haya yafuatayo;
1. Kuendelea kufanya nao kazi na mawasiliano ya kiofisi.
2. Kuwaachia kusimamia na kuendesha ligi mbalimbali.
3. Kuendelea kuwapatia fedha za mgao wa ligi mbalimbali.
Uchaguzi wa DRFA sio jambo la siri kuwa umeharibiwa na Kamati ya Uchaguzi ya DRFA. Kwa kuharibu kwao imefanya kuchelewesha kuingia madarakani kwa uongozi mpya kwa wakati. Lakini jambo hili halihalalishi kuwepo kwao madarakani mpaka muda huu.
Kanuni za uchaguzi za TFF ziko wazi na zinaelekeza ni kitu gani kifanyike iwapo hali kama hii ikitokea. Article namba 25 ya kanuni za Uchaguzi imetoa maelekezo ya kufanya katika kifungu namba 3 kinachosema”TFF may likewise suspend or invalidate the electoral processes and /or appoint a provisional administration for the association as the case may be”
Kwa kifungu hiki yafuatayo yanawezekana;
(A) Kuifuta au kuibatilisha Kamati ya Uchaguzi ya DRFA.
(B) Kuteua Uongozi wa DRFA kuelekea Uchaguzi.
Kwa maelezo hayo Uongozi uliomaliza muda wake ni batili na hautakiwi kushirikishwa katika shughuli zozote za DRFA.
Naomba TFF iangalie utekelezaji wake kutokana na kifungu hiki.
Michezoni.
Michezoni,
Salum B. Mkemi
Nakala; Rais TFF
Mwenyekiti Kamati ya Uchaguzi TFF
YANGA: KAMWE HATUTOKUBALI KUVAA NEMBO NYEKUNDU YA VODACOM KWENYE JEZI ZETU - BORA TFF WATUFUTE KWENYE LIGI
Katibu wa Baraza la wazee wa klabu ya Young Africans Sports Club,
Mzee Ibrahim Akilimali ametoa ufafanuzi juu ya timu ya Yanga kutovaa
jezi zenye nembo nyekundu ya mdhamini wa ligi kuu Tanzaniza bara kampuni
ya simu ya Vodacom.
Akiongea na wandishi wa habari makao makuu ya klabu makutano ya mitaa ya Twiga/Jangwani, Mzee Akilimali amesema kamwe hawatakubali matakwa ya vodacom na TFF ya kuweka nembo yenye doa jekundu katika jezi za Yanga.
Ni afadhali hao TFF watufute katika ligi yao kama wataendelea kutulazimisha kuvaa jezi zenye nembo nyekundu, kwani tupo radhi kubaki kucheza michezo isiyodhaminiwa na Vodacom kama bao, ngumi, na mingineyo au hata kuhamia ligi ya visiwani Zanzibar ambako tutacheza bila vikwazo.
Labda kwa wasiofahamhu historia, Yanga mwaka 1953 mbele ya aliyekua Gavana wa Tanganyika, Sir Edward Twinning ilikataa kuvaa jezi zenye madoa ya rangi nyekundu ilizoletewa na timu pinzani ya mabaharia kutoka Uingereza, na kusema ni bora tucheze vifua wazi kuliko kuvaa jezi hizo alisema 'Mzee Akilimali'.
Mzee Akilimali aliongeza pia kuwa hata chama cha TANU kiliwahi kuiomba Yanga ibadilishe rangi zake za kijani na njano, lakini Rais wa kwanza wa Tanzania, Baba wa Taifa Julius Nyerere aliwambia wajumbe wa TANU kwamba waacheni Yanga na rangi zao, rangi hizo wanazotumia zinawatambulisha wao, madini, na maliasili ya nchi hii.
Aidha pia Mzee Akilimali alisema mnamo mwaka 1963, aliyekuwa mkuu wa mkoa Dar es salaam mh Mustapha Songambele aliziita timu zote zilizokuwa na majina ya kigeni kwamba zibadilsihe majina hayo na kujiita majina ya kitanzania, timu zote zilibadilisha majina lakini Young Africans ilipotafsiriwa ilileta maana ya Vijana wa Afrika hali iliypolekea Yanga kuendelea kutumia jina lake, na timu zingine kubadilisha majina yao.
Kaimu katibu mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako amesema wanashindwa kuelewa kwa nini vodacom mwaka huu wanalazimisha Yanga ivae jezi zenye rangi jekundu, ili hali mwaka jana walikubali kutoa jezi zenye rangi nyeusi ya doa la vodacom.
Mkataba kati ya TFF na Vodacom sisi hatujauona, sasa inakuwa vigumu kujua kipi kimeandikwa ndani ya huo mkataba na kinapaswa kutekelezwa, ilipaswa vilabu tuepewe nakala ya mkataba tuusome kabla ya kusainiwa, ili na sisi tupate nafasi ya kutoa hoja katika mkataba huo, lakini wao wamefanya kinyume kisha wanatulazimisha tuvae hiyo nembo, ikiwa hatujui maslahi ya mkataba wenyewe alisema 'Mwalusako'.
Yanga itashuka dimbani siku ya jumamosi kucheza na timu ya Ruvu Shooting katika muendelezo wa michezo ya Ligi ya Kuu ya Vodaco nchini raundi ya 8.
Naye Mzee Mwika aliongezea kwa kutoa mfano kwamba "haiwezekani Mnyamwezi aje zake Pwani toka Tabora atukataze wazaramo kucheza mdundiko au dogoli", alichokikuta anapaswa kukifuata na kukiheshimu na sio kuja na kutaka kubadillisha tamaduni za watu, Yanga ina rangi kuu tatu (3) Kijani, Njano na Nyeusi.
(Source: http://youngafricans.co.tz/news/)

BREAKING NEWS! KAPOMBE KUWA NJE YA UWANJA KWA SIKU KUMI.

Beki Taarifa nilizozipata hivi punde beki Shomari Kapombe na kiungo Kiggi Makassy wamepata majeraha ambayo yatawaweka nje kwa takribani siku kumi.
Kapombe anasumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu ( ankle ) wakati Kiggi anasumbuliwa na goti.
Wachezaji wote wataukosa mchezo wa leo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Kagera Sugar.
CRISTIANO RONALDO MFALME WA FACEBOOK: AWAFUNIKA MESSI NA WANAMICHEZO WENGINE WOTE DUNIANI
Ronaldo is facebook king.
Linapokuja suala la nani ndio mchezaji bora wa dunia mjadala unaangukia kwa wachezaji wawili Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.
Kwa bahati mbaya kwa Ronaldo ni kwamba imeonekana majaji wengi waliopo kwenye kamati za FIFA na UEFA wapo upandewa Lionel Messi, pamoja na mreno huyo kuwa na rekodi nzuri kuanzia kwenye klabu yake ya zamani Manchester United mpaka sasa akiwa na Real Madrid.
Lakini linapokuja suala la mashabiki, hasa kwenye mitandao ya kijamii hakuna ushindani kabisa: Ronaldo ndio mfalme wao. Mshambuliaji huyo wa Real Madrid ambaye leo ametimiza mechi ya 100 tagnuaanze kuichezea Ureno, amekuwa mwanamichezo wa kwanza kufikisha idadi ya mashabiki 50 Million katika ukurasa wake wa mtandao wa Facebook - hiyo ni asilimia 5 ya watu wote waliopo kwenye mtandao huo.
Kwa maana hiyo Ronaldo amewafunika wanamichezo wote, akiwemo mpinzani wake mkuu Messi mwenye mashabiki millioni 38, huku wanasoka wengine kama Kaka, Beckham na Iniesta wakikamilisha Top 5.
2:
3:

4:

5:

Tuesday, October 16, 2012
SIKU KAMA YA LEO MIAKA 8 ILIYOPITA: MESSI ALIICHEZEA BARCELONA MECHI YAKE YA KWANZA
Siku kama ya leo miaka 8 iliyopita, October 16, 2004, Lionel Messi akiwa na miaka 17 na siku 114, alifanikiwa kucheza mechi ya kwanza ya mashindano akiwa na timu ya wakubwa ya Barcelona, katika mechi ya La Liga dhidi ya RCD Espanyol.
Kwa kucheza mechi hiyo Messi akawa mchezaji wa tatu mdogo kiumri kuwahi kuichezea Barcelona A na mchezaji mdogo zaidi wa klabu kuwahi kucheza La Liga, rekodi ambayo ilikuja kuvunjwa na Bojan Krkic mwezi September 2007.

EL HADJI DIOUF ATUHUMIWA KUHUSIKA NA VURUGU ZILITOKEA KWENYE MCHEZO WA SENAGAL NA IVORY COAST
Raisi wa shirikisho la soka Senegal (FSF) Augustin Senghor amesema tukio la vurugu lilotokea siku ya jumamosi ilikuwa hujuma iliyopangwa kuharibu soka la nchi hiyo na kuliharibia sifa shirikisho hilo.
Boss wa FSF alisema ilitolewa oda ya tiketi kutoka mtu binafsi na tiketi zikagawawiwa kwa wahuni kwa dhumuni la kufanya vurugu katika mechi ya Senegal na Ivory Coast katika mechi ya marudiano ya kufuzu kushiriki AFCON 2013, mechi ambayo kwa bahati mbaya iliishia dakika ya 76 baada ya kuibuka kwa vurugu katika uwanja wa watu 60,000 uitwao Leopold Senghor jijini Dakar.
"Kuna mtu alitoa oda ya tiketi nyingi na akazigawa kwa wahuni waliofanya vurugu kwenye mechi. Wanataka kuharibu siafa ya ya soka la nchi yetu, ili waweze kutusema vibaya siku za mbele kwa mashabiki na taifa zima kwa ujumla," alisema.
Mapema Jumatatu, winga wa Leeds United El Hadji Diouf alisema wazi kwamba walizizuia tiketi 1,000 alizotoa oda kwa ajili ya kugawa kwa mashabiki, kutokana na shirikisho kuhisi kwamba mchezaji huyo alikuwa amewakusanya wahuni ili wakafanye vurugu uwanjani na kuitibua mechi.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kilicho karibu na shirikisho la FSF, Diouf alikuwa ndio mtu binafsi peke aliyenunua tikieti nyingi kwa ajili ya mchezo huo.
Japokuwa mchezaji huyo amesema hahusiki na chochote kuhusu vurugu za usiku wa Jumamosi, huku akiisisitiza serikali kuwaondoa viongozi wote wa shirikisho na kuliunda upya.

SIMBA DHIDI YA KAGERA SUGAR - AZAM WAPO SHIMONI SOKOINE DHIDI WAJELAJELA PRISONS - VPL RAUNDI YA TANO
Ligi
Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaingia raundi nane
kesho (Oktoba 17 mwaka huu) kwa mechi tano huku vinara wa ligi hiyo
Simba wakiialika Kagera Sugar kutoka mkoani Kagera kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Mechi
hiyo namba 52 itachezeshwa na mwamuzi Ronald Swai kutoka Arusha wakati
waamuzi wasaidizi ni Julius Kasitu na Methusela Musebula, wote kutoka
Shinyanga. Mwamuzi wa akiba ni Ephrony Ndisa wa Dar es Salaam huku
mtathimini wa waamuzi akiwa Charles Mchau kutoka Moshi.
Uwanja
wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya
Tanzania Prisons inayofundishwa na Jumanne Chale na Azam iliyo chini ya
kocha Boris Bunjak kutoka Serbia. Nayo Polisi Morogoro iliyopanda msimu
huu itakuwa mwenyeji wa JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Jamhuri.
Mgambo
Shooting ambayo imepata ushindi mara mbili mfululizo itakuwa nyumbani
Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga ikiikaribisha Toto Africans katika
mechi itakayochezeshwa na Geofrey Tumaini wa Dar es Salaam. Oljoro JKT
inayonolewa na Mbwana Makata itakuwa nyumbani Uwanja wa Kumbukumbu ya
Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha dhidi ya African Lyon.
LIGI DARAJA LA KWANZA KUANZA OKTOBA 24
Michuano
ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ya Tanzania Bara inaanza rasmi Oktoba 24
mwaka huu kwa timu 18 kati ya 24 kujitupa kwenye viwanja tisa tofauti
katika ligi hiyo inayochezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.
Mechi
za raundi ya kwanza za kundi A zitakazochezwa Oktoba 24 mwaka huu ni
Burkina Faso dhidi ya Mbeya City (Jamhuri, Morogoro), Mlale JKT na Small
Kids (Majimaji, Songea) na Kurugenzi Mufindi dhidi ya Majimaji (Uwanja
wa Wambi, Mufindi mkoani Iringa).
Mkamba
Rangers na Polisi Iringa zitakamilisha raundi ya kwanza kwa kundi hilo
Oktoba 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Mechi
za raundi ya pili kwa kundi hilo zitachezwa Oktoba 27 mwaka huu kwa
Polisi Iringa vs Mbeya City (Samora, Iringa), Majimaji vs Small Kids
(Majimaji, Songea), Burkina Faso vs Mkamba Rangers (Jamhuri, Morogoro)
na Kurugenzi Mufindi vs Mlale JKT (Wambi, Mufindi).
Raundi
ya tatu ni Oktoba 31 mwaka huu kwa mechi kati ya Mbeya City vs Mlale
JKT (Sokoine, Mbeya), Small Kids vs Mkamba Rangers (Nelson Mandela,
Sumbawanga), Majimaji vs Burkina Faso (Majimaji, Songea) na Polisi
Iringa vs Kurugenzi Mufindi (Samora, Iringa).
Kundi
B Oktoba 24 mwaka huu ni Ndanda vs Transit Camp (Uwanja wa Nangwanda
Sijaona, Mtwara), Villa Squad vs Moro United (Mabatini, Pwani) wakati
Oktoba 25 mwaka huu ni Green Warriors vs Tessema (Mabatini, Pwani) na
Polisi Dar es Salaam vs Ashanti United (Chamazi, Dar es Salaam).
Raundi
ya pili kwa kundi hilo ni Oktoba 27 mwaka huu Ndanda vs Green Warriors
(Nangwanda Sijaona, Mtwara), Villa Squad vs Tessema (Mabatini, Pwani)
wakati Oktoba 28 mwaka huu ni Ashanti United vs Transit Camp (Mabatini,
Pwani) na Oktoba 29 mwaka huu ni Moro United vs Polisi Dar es Salaam
(Chamazi, Dar es Salaam).
Novemba
1 mwaka huu ni Green Warriors vs Ashanti United (Mabatini, Pwani),
Novemba 2 mwaka huu ni Polisi Dar es Salaam vs Villa Squad (Chamazi, Dar
es Salaam), Novemba 4 mwaka huu ni Tessema vs Ndanda (Chamazi, Dar es
Salaam) na Transit Camp vs Moro United (Mabatini, Pwani).
Kundi
C ni Oktoba 24 mwaka huu Kanembwa FC vs Polisi Dodoma (Lake Tanganyika,
Kigoma), Mwadui vs Morani (Kambarage, Shinyanga), Pamba vs Polisi Mara
(Kirumba, Mwanza) na Rhino Rangers vs Polisi Tabora (Ali Hassan Mwinyi,
Tabora).
Raundi
ya pili ni Oktoba 27 mwaka huu; Polisi Tabora vs Polisi Dodoma (Ali
Hassan Mwinyi, Tabora), Mwadui vs Polisi Mara (Kambarage, Shinyanga),
Kanembwa FC vs Morani (Lake Tanganyika, Kigoma) na Pamba vs Rhino
Rangers (Kirumba, Mwanza).
Oktoba
31 mwaka huu ni raundi ya tatu; Polisi Mara vs Rhino Rangers (Karume,
Musoma), Morani vs Polisi Tabora (Kiteto, Manyara), Polisi Dodoma vs
Pamba (Jamhuri, Dodoma) na Kanembwa FC vs Mwadui (Lake Tanganyika,
Kigoma).
MBAGA AZICHEZESHA KENYA, BAFANA BAFANA
Mwamuzi
Oden Mbaga wa Tanzania anayetambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la
Mpira wa Miguu (FIFA) ndiye anayechezesha mechi ya kirafiki kati ya
Kenya (Harambee Stars) na Afrika Kusini (Bafana Bafana).
Mechi
hiyo inachezwa leo Uwanja wa Kimataifa wa Moi Kasarani jijini Nairobi.
Mbaga anasaidiwa na waamuzi wasaidizi wa FIFA, John Kanyenye kutoka
Mbeya na Erasmo Jesse wa Morogoro.
TFF
imeteua waamuzi hao baada ya kupata maombi kutoka kwa Shirikisho la
Mpira wa Miguu la Kenya (FKF) ambao ndiyo waandaaji wa mechi hiyo ambayo
ni moja ya vipimo kwa kocha mpya wa Harambee Stars, Henry Michel kutoka
Ufaransa.
TAFCA YAONGEZA MUDA WA KUCHUKUA FOMU
Kamati
ya Uchaguzi ya Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA)
imeongeza muda kwa wagombea kuchukua fomu kwa ajili ya uchaguzi wa chama
hicho ambao sasa utafanyika Novemba 25 mwaka huu.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA, Ramadhan
Mambosasa, jana ndiyo ilikuwa mwisho wa kuchukua fomu lakini mwitikio wa
wagombea bado umekuwa mdogo ambapo ni watano tu waliojitokeza.
Hivyo,
amesema wameongeza muda wa kuchukua na kurudisha fomu ambapo mwisho
itakuwa ni Oktoba 19 mwaka huu saa 10 kamili alasiri. Fomu zinapatikana
ofisi za TAFCA ambazo ziko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es
Salaam.
KUTOKA KUCHEZA BEKI WA KATI MPAKA KUWA MSHAMBULIAJI BORA - MECHI 100 ZA CRISTIANO RONALDO KWENYE JEZI YA URENO
![]() |
| Cristiano Ronaldo katika mechi yake ya kwanza kuichezea Ureno dhidi ya Kazakhstan |
"Ilikuwa mwezi August, 20, 2003, dhidi ya Kazakhstan, nilivaa jezi ya timu ya taifa kwa mara ya kwanza. Ilikuwa ni moja tukio kubwa la kukumbukwa katika maisha yangu na kitu ambacho najisikia fahari sana," Ronaldo aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Aliingia uwanjani badala ya Luis Figo, kitu ambacho leo kinaonekana ishara ya kupokezana kijiti kutoka kwa shujaa mmoja kwenda kwa mwingine.
Ronaldo, mchezaji bora wa dunia wa mwaka 2008, aliichukua Ureno mikononi mwa mchezaji bora wa mwaka 2001, Lusi Figo, na kuipeleka mpaka kushika nafasi ya tatu kwa ubora duniani kwa viwango vya FIFA.
Akiwa na miaka 27, atakuwa mchezaji mwenye umri mdogo barani ulaya kufikisha idadi ya mechi 100 nyuma ya Mjerumani Lukas Podolski na mchezaji wa Estonia Kristen Viikmae.
Ni mchezaji anayeshika nafasi ya tatu kwa kuichezea Ureno mechi nyingi nyuma ya Figo aliyecheza mechi 127, beki Fernando Couto aliyecheza 110.
"Jumanne hii nitafikisha mechi yangu ya 100 na jezi ya timu yangu ya taifa nikiwa uwanja wa nyumbani na nikiwa na fikra za ushindi tu kichwani. Ningependa kuwashukuru wote walionisaidia kufika hapa katika hatua hii," Aliandika Ronaldo kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Kiukweli ana wengi wa kuwashukuru, akianzia na mwalimu wake wa soka katika shule ya msingi ya Madeira, Francsico Afonso.
"Alikuwa akijituma na siku zote alikuwa na jitihada na moyo wa kutaka kuendelea mbele zaidi," Afonso alikaririwa akisema kwenye gazeti la kila siku la Ureno O Jogo. "Kwa kuanzia alianza kucheza kama sentahafu , lakini kwa sababu alikuwa akitaka kupanga kila kitu kwa mtazamo wake, hatimaye akaamua kwenda mbele na kucheza kama mshambuliaji."
Rekodi za Ronaldo akiwa na vilabu vya Manchester United na Real Madrid zinaongea zenyewe. Ameshinda La liga msimu uliopita na Copa del Rey wakati akiwa England, alishinda makombe matatu ya Ligi, Champions league na FA Cup.
![]() |
| Ronaldo akiwa na gwiji wa soka wa Ureno Eusebio |
"BORA KULIKO EUSEBIO"
Kocha wa zamani wa Sporting Laszlo Boloni, ambaye alimtambulisha Ronaldo katika dunia halisi ya soka kwa kumpa mechi kadhaa za kucheza akiwa na umri mdogo akiwa na Sporting Lisbon, anampanga Ronaldo kama mchezaji bora wa muda wote wa Ureno mbele ya wakongwe waliopita.
"Niliulizwa kwanini nilisema Ronaldo atakuwa bora kumliko Eusebio baada ya kucheza mechi tano tu. Nikajibu kwamba Cristiano alikuwa tofauti, na bora kuliko Eusebio," aliliambia gazeti la O Jogo.
Ronaldo sasa anatambulika dunia nzima kwa uwezo wake na jinsi anavyojiamini, wengine wanasema ni kiburi, lakini walio karibu nae wanamsema Ronaldo kama ni mtu mwenye huruma, adabu na mpenda kujituma katika kila anachokifanya.
"Nakumbuka alikuwa ni mtu mwenye aibu sana siku ya kwanza nilipomuona katika mazoezi ya timu ya taifa ya wakubwa," ansema mkurugenzi wa Ureno Carlos Godinho.
"Alikuwa mdogo sana, miaka 18, na aliweza kujitengenezea nafasi yake vizuri ndani ya timu ya taifa. Alikuwa anataka kuonyesha kila kitu alichonacho, hakuacha kufanya hivyo. Alijituma kiasi cha wachezaji wakongwe kwenye kikosi wakawa wanamshauri ajaribu kuwa anapumzika, mwishowe akawa anajikuta nachoka sana kutokana na kufanya sana mazoezi bila kupumzika."
Kwenye Euro 2004, Ronaldo alikaribia kushinda ubingwa huo lakini Ugiriki wakaushangaza ulimwengukatika finali dhidi yao. Kinda Ronaldo aliachwa akiwa analia lakini Figo, nahodha wa kipindi hicho matukio ya namna ile ndio yamemkomaza Ronaldo.

"Mechi 100 ni namba, ambayo nyuma yake kuna kujitoa sana, furaha na huzuni na pia tamaa ya kila kutaka kufanikiwa na kwenda mbele zaidi," anasema Figo.
Ronaldo ataiongoza Ureno wakiwa nyumbani kucheza dhidi ya Ireland ya Kaskazini leo Jumanne wakiwa wanatafuta na kurudi katika mstari wa kupata matokeo mazuri baada ya kufungwa 1-0 Ijumaa iliyopita na Russia katika mechi ya kundi F.
Ureno wanashika nafasi ya pili katika kundi hilo nyuma ya Warusi.
Monday, October 15, 2012
JUA MAANA YA NEMBO YA MNYAMA SIMBA KWENYE MIKANDA YA UBINGWA WA ECAPBA
EAST & CENTRAL AFRICA PROFESSIONAL BOXING ASSOCIATION
Technology House 35-38 Ghalla Road, P.O BOX 8307 Moshi, Tanzania
Tel / Fax: 255-54743 E-mail: ECAPBA@YAHOO.COM
TAARIFA MAALUM
13 OCTOBA, 2012
JUA MAANA YA NEMBO YA MNYAMA SIMBA KWENYE MIKANDA YA UBINGWA WA ECAPBA
Nembo ya mnyama Simba hapo juu kwenye ubingwa wa Afrika ya Mashariki na Kati ina maana ya ushupavu, uvumilivu, ukali, na hatari ya mnyama simba mwenyewe alivyo.
Nembo hii ilikubaliwa iwe ni alama ya kielelezo cha ubingwa wa ECAPBA ili iweze kuonyesha kuwa mabingwa wote wa ECAPBA wana viwango vinavyokubalika. Kesho ubingwa wa kati (Middleweight) katia ya bondia Mtanzania Thomas Mashali na Sebyala Med wa Uganda utafanyika katika ukumbi wa Friends Corner jijini Dar-Es-Salaam.
Nchi wanachama wa ECAPBA ni pamoja na Tanzania, Uganda, Kenya, Mawali, Rwanda, Burundi, Sudan, Ethiopia, Zambia na DRC Congo.
THOMAS MASHALI AMTWANGA MGANDA MEDY SEBYALA MANZESE
| Wachezaji wa Simba, Juma Nyosso kulia akiwa na kushoto Haruna Moshi, beki wa Yanga Godfrey Taita bwakiwa na Profesa Jay, wakimuombea dua bondia Thomas Mashali kabla ya pambano lake jana. |
| Bondia Thomas Mashali akiwa na mikanda yake ya ubingwa wa Tanzania pamoja na wa Afrika Mashariki na Kati alioupata jana |
| Rais wa TPBO, Yasini Abdallah 'Ustadh' akisalimiana na Profesa Jay kwenye kona ya Mashali |
| Boban, Nyosso, Taita, Profesa wakiwa kwenye kona ya Mashali wakati wa kupigwa wimbo wa taifa |
| Baadhi ya Viongozi pamoja na mgeni rasmi wakisimama kwa ajili ya wimbo wa tafa kabla ya mpambano |
| Bondia Medy Sebyala akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na bondia Thomas Mashali wakati wa mpambano wao wa kugombea ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati Mashali alishinda kwa pointi |
| BONDIA THOMAS MASHALI kushoto akioneshana uwezo wa kutupiana masumbwi na MEDY SEBYALA wa Uganda |
| Bondia Medy Sebyala akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na bondia Thomas Mashali wakati wa mpambano wao wa kugombea ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati Mashali alishinda kwa pointi |
| Bondia Thomasi Mashali akiwa na mkanda wake wa ubingwa wa Afrika Mashaliki katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali |
| Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azzan akiwa katika picha na Bondia Thomas Mashali baada ya kuvishwa ubingwa wa Afrika Mashariki |
| Bondia Medy Sebyala akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na bondia Thomas Mashali wakati wa mpambano wao wa kugombea ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati Mashali alishinda kwa pointi. Picha zote na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
SHAABAN MINTANGA ASHINDA KESI YA KUKAMATAWA NA MADAWA YA KULEVYA
Alhaji Shaaban Mintanga akiwa chini ya ulinzi mkali wakati wa kesi yake.
Rais wa zamani wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), Alhaji Shaaban Mintanga, leo ameachiwa huru baada ya kushinda kesi yake ya kukamtwa na madawa ya kulevya. Mintanga ameachiwa huru baada ya kusota rumande tangu April 4 mwaka 2008. (Picha kwa hisani ya GPL)

JUAN MATA: SOKA LA HISPANIA HALINA USHINDANI - USIPOCHEZEA MADRID AU BARCA HUWEZI KUSHINDA UBINGWA.
Kiungo wa Chelsea Juan Mata amesema kuondoka kwa wingi wachezaji wenye vipaji kutoka kwenye ligi kuu ya taifa lake Spain kunampa mashaka juu ya mustakabari wa soka la nchi hiyo.
Mata aliondoka Valencia miezi 18 iliyopita na kujiunga na Chelsea.
"Nina wasiwasi kidogo kuona namna wachezaji wengi wakiwa wanaondoka La Liga. Ligi ina timu mbili tu zinazoshindania ubingwa. Timu inayoshika nafasi ya tatu na nne zinakuwa nyuma kwa pointi 30 mwishoni mwa msimu.
"Ikiwa huchezei katika vilabu vya Barcelona au Real Madrid, then huwezi kushinda ubingwa. Haiwezekani kwa klabu yangu ya zamani Valencia kuwa mabingwa.
"Hii kitu sio nzuri kwa soka la Hispania kwa sababu hakuna ushindani wa ukweli kwa vilabu vikubwa."

MOURINHO: FALCAO NI TUNDA ZURI NISILORUHUSIWA KULA
Kocha wa Real Madrid Jose Mourinho amesema hatoweza kujaribu kutaka kumsaini Radamel Falcao kutoka Atletico Madrid kwa sababu kuna hali ya kutokuelewana baina ya vilabu viwili vya mji mkuu wa Hispania.
Kocha huyo wa zamani wa Inter na Chelsea kuna makubaliano ya mdomo baina ya mahasimu hao wa jiji la Madrid yanafanya uhamisho huo wa kumsaini Falcao kutoka Los Rojiblancos usiwezekane.
"Falcao ni mchezaji mzuri kwa mahasimu wetu, kama ilivyokuwa kwa Kun Aguero. Kuna makubaliano kati ya Real Madrid na Atletico hivyo Falcao ni tunda zuri lenye katazo la kutoliwa," Mourinho aliiambia A Bola.
"Mchezaji mzuri sana, na ninahisi ni mtu mzuri sana, na nina furaha sana kumuona akifanya vizuri pale Atletico."

CLOUDS MEDIA GROUP NA PRIMETIME PROMOTIN YATOA SHUKRANI KW WADHAMINI WAKE WA SERENGETI FIESTA 2012
Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga akitoa shukurani kwa Wadhamini wakuu waliofanikisha Serengeti Fiesta 2012 kufanyika na kumalizika kwa amani kwa mikoa takribani 12 nchini Tanzania ilhali tamasha hilo likiacha alama ya maendeleo na chembe za changamoto ya ukuzaji uchumi kwa wananchi wa mikoa iliyo kuwa kwenye ratiba.
Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga akitoa Cheti cha Ushiriki Bora kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bia ya (Serengeti SBL),Steve Gannon ambao ndio waliokuwa wadhamini wakuu wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012 kupitia bia yake maridhawa kabisa ya Serengeti Premium Lager pichani kati anaeshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi wa masoko wa kampuni hiyo ya SBL,Ephraim Mafuru.Hafla hiyo imefanyika mwishoni mwa wiki kwenye kiota cha maraha cha Escape Two,Mbezi beach jijini Dar.
Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga akitoa Cheti cha Ushiriki bora kwa wadhamini wa mafuta vyombo vya barabarani GAPCO walioshiriki vyema Tamasha la Serengeti Fiesta 2012,kwa Mkuu wa Masoko wa GAPCO, Ben Temu
Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya SBL,Ephraim Mafuru akitoa shukurani za dhati kwa wadau mbalimbali waliofanikisha tamasha la Serengeti Fiesta 2012 kwa namna moja ama nyingine.
Msanii mkongwe wa muziki wa kizaz kipya a.k.a Bongofleva Sir Juma Nature akimwimbia mmoja wa watangazaji wa Clouds FM kupitia kipindi cha Jahazi,Wasiwasi Mwabulambo. Katika hafla hiyo iliyokuwa ya aina yake iliwajumuisha watu mbalimbali wakiwemo wasani (Picha kwa hisani ya gsengo.blogspot.com)
UTATA - BALOTELLI AIDAI MALIPO KAMPUNI YA UMBRO KWA KUTENGENEZA FULANA ZENYE MANENO YA "WHY ALWAYS ME"
Toto tundu Mario Balotelli ameambia kampuni ya vifaa vya michezo imlipe baada ya kampuni hiyo kuuza Tshirt zenye msemo wake maarufu wa "Why Always Me."
Mshambuliaji huyo wa Manchester City alivaa T-shirt yenye maneno hayo siku ambayo walicheza na mahasimu wao Manchester msimu uliopita.
Alivua jezi yake halisi kuwaonyesha mashabiki baada ya kufunga bao la kwanza katika ushindi wa 6-1 City dhidi ya United - lakini Mario amekasirishwa baada ya kujua kwamba Umbro wanauza kopi ya T-shirt zake zenye maneno ya "Why Always Me".
Kutokana na hilo Balotelli akamwambia mtunza vifaa wa City Les Chapman aulizie malipo kutoka Umbro akiamini ana haki ya maneno yaliyotumika kwenye T-Shirts.
Leo alisema: "Mario alinifuata na kuniambia nini avae kwa ndani kabla ya mechi na United, nikamwambia hawezi kuvaa fulana yoyote itakayohusu kitendo cha kuchezea milipuko haswa katika dimba la United. Baada ya hapo dakika 10 mbele akaja kuniambia "Why Always Me"? Nikwambia safisana hiyo, na baada ya mechi tukaggundua kwamba Umbro walikuwa wanauza fulana kama zile zenye maneno yale yale.
"Mario akanituma niwapigie simu na kuulizia kuhusu malipo yetu lakini hakuna anayemiliki maneno." Pamoja na kutoswa kulipwa na Umbro, mshambuliaji huyo baadae alikaa chini na kutengeneza dili la kupromoti T-Shirts za mwanamuziki Tinchy Stryder na faida ya mauzo ya fulana hizo ilienda kwenye kusaidia jamii..

Sunday, October 14, 2012
CAMEROON KUTOCHEZA MATAIFA YA AFRIKA MARA MBILI MFULULIZO
Licha ya Samuel Eto'o kurejea katika kikosi cha Cameroon. Simba wasioshindika kwa mara ya pili mfululizo watakosekana katika michuano ya AFCON hapo mwakani nchi Afrika ya Kusini baada kutolewa kwa jumla ya mabao 3-2 na Cape Verde. Katika mchezo wa leo, Cameroon imeshinda mabao 2-1, lakini awali walifungwa mabao 2-0.
MATOKEO YOTE YA AFCON 2013 LEO
Result: Ethiopia 2-0 Sudan - Addis Ababa
MATOKEO YOTE YA AFCON 2013 LEO
Result: Ethiopia 2-0 Sudan - Addis Ababa
Aggregate: Sudan 5-5 Ethiopia
Ethiopia win on away goals
Result: Cameroon 2-1 Cape Verde Islands -Yaounde
Aggregate: Cape Verde 3-2 Cameroon
Result:Angola 2-0 Zimbabwe - Luanda
Aggregate Zimbabwe 3-3 Angola
Angola win on away goals
Result:Niger 2-0 Guinea - Niamey
Aggregate: Guinea 1-2 Niger
Result Togo 2-1 Gabon - Lome
Aggregate Gabon 2-3 Togo
Result: Equatorial Guinea 2-1 Congo DR - Malabo
Aggregate: Congo DR 5-2 Equatorial Guinea

HIVI NDIVYO AKINA DROGBA, YAYA TOURE NA WENZAO WALIVYONUSURIKA KUPIGWA NA MASHABIKI WA SENEGAL
![]() |
| Mawe, vyupa na silaha nyngine zilikuwa zimetawala katika uwanja |
![]() |
| Mashabiki wa Senegal wakiwa wameisha moto jukwaani |
![]() |
| Kolo Toure akijikinga nyuma ya polisi akisindikizwa kutoka nje ya uwanja |
![]() |
| Didier Drogba nae akijikinga nyuma ya polisi baada ya mashabiki kuingia uwanjani. |
DIDIER DRGOBA KIBOKO YA AKINA DEMBA BA - APIGA MBILI MECHI YAVUNJIKA
ANGALIA MECHI YOTE HAPA ILIVYOKUWA KATI YA SENEGAL VS IVORY COAST.
MATOKEO YA MECHI ZA KUFUZU AFCON 2013
Morocco 4 - 0 Mozambique
*Senegal 0 - 2 Ivory Coast
Tunisia 0 - 0 Sierra Leone
Nigeria 6 - 1 Liberia
Botswana 1 - 4 Mali
*Uganda (8) 1 - 0 (9) Zambia
Malawi 0 - 1 Ghana
Morocco 4-0 Mozambique
*Zambia v Uganda iliamuliwa kwa mikwaju ya penati.
*Senegal v Ivory Coast mechi haikumalizika kutokana na vurugu za mashabiki.

Subscribe to:
Posts (Atom)

.jpg)