Salum Mkemi
0715 847474
17/10/2012
Katibu Mkuu,
TFF,
D’Salaam.
Ndugu,
KUONDOLEWA KWA VIONGOZI WA DRFA IKIWA MUDA WA UONGOZI WAO UMEMALIZIKA.
Tafadhali rejea somo nililotaja hapo juu.
Naomba nichukue nafasi hii kukumbusha kuwa muda wa uongozi wa DRFA ulimalizika tarehe 12/10/2012. Siku hiyo ndio ambayo DRFA ilifanya uchaguzi mwaka 2008 mwezi wa kumi(10). Kulingana na katiba ya DRFA muda wa uongozi ulimalizika baada ya wao kumaliza muda wao wa kukaa madarakani kwa miaka minne (4).
Kulingana na katiba ya DRFA hakuna sehemu inayowapa hawa waliokuwa viongozi nafasi ya kujiongezea muda. Ibara ya 34 (Muda wa Madaraka) kifungu cha pili (2) na katiba ya mfano ya TFF inasema kuwa”The mandate of the members of the Executive Committee may be renewed. However the person who is 75 years and above shall not to be allowed to stand for presidency”
Kwa kifungu hiki hakuna mamlaka yoyote ya kisheria inayowafanya viongozi hao kuendelea kuwepo madarakani.
Hali hii inaonyesha kuwa viongozi waliomaliza muda wao wanavamia madaraka na inaonyesha TFF mnaafiki uvunjwaji huu wa katiba kwa haya yafuatayo;
1. Kuendelea kufanya nao kazi na mawasiliano ya kiofisi.
2. Kuwaachia kusimamia na kuendesha ligi mbalimbali.
3. Kuendelea kuwapatia fedha za mgao wa ligi mbalimbali.
Uchaguzi wa DRFA sio jambo la siri kuwa umeharibiwa na Kamati ya Uchaguzi ya DRFA. Kwa kuharibu kwao imefanya kuchelewesha kuingia madarakani kwa uongozi mpya kwa wakati. Lakini jambo hili halihalalishi kuwepo kwao madarakani mpaka muda huu.
Kanuni za uchaguzi za TFF ziko wazi na zinaelekeza ni kitu gani kifanyike iwapo hali kama hii ikitokea. Article namba 25 ya kanuni za Uchaguzi imetoa maelekezo ya kufanya katika kifungu namba 3 kinachosema”TFF may likewise suspend or invalidate the electoral processes and /or appoint a provisional administration for the association as the case may be”
Kwa kifungu hiki yafuatayo yanawezekana;
(A) Kuifuta au kuibatilisha Kamati ya Uchaguzi ya DRFA.
(B) Kuteua Uongozi wa DRFA kuelekea Uchaguzi.
Kwa maelezo hayo Uongozi uliomaliza muda wake ni batili na hautakiwi kushirikishwa katika shughuli zozote za DRFA.
Naomba TFF iangalie utekelezaji wake kutokana na kifungu hiki.
Michezoni.
Michezoni,
Salum B. Mkemi
Nakala; Rais TFF
Mwenyekiti Kamati ya Uchaguzi TFF
No comments:
Post a Comment