Search This Blog

Wednesday, October 17, 2012

LIVE MATCH CENTRE: SIMBA SC 2 - 2 KAGERA SUGAR FULL TIME


Mpira unamalizika hapa uwanja wa taifa na kwa maoni yangu kwa kuangalia mpira ulivyochezwwa leo, naamini Kagera walistahili kupata pointi katika mchezo huu.

 DK 90: Simba 2 - 2 Kagera

DK 85: Simba 2 - 2 Kagera

DK 80: Simba wanaonekana kukosa mbinu za kuipita ngome ya Kagera katika dakika hizii, na wameendelea na tatizo lao la kutoweza kukaa na mpira kwa muda huku wakipoteza hovyo pasi.

 DK 75: Simba 2 - 2 Kagera 

 DK 68: Juma Nyoso anacheza rafu kwenye eneo la penati na mwamuzi anaamuru penati. Kagera wanapiga na kuandika bao la pili.

 DK 60: Hatimaye mfululizo wa mashambulizi ya Kagera yanazaa matunda na wanafanikiwa kupata goli moja. Simba 2 - 1 Kagera.

 DK 57: Emmanuel Okwi anaingia vizuri kutokea pembeni na kuwatoka mabeki wa Kagera anapiga shuti kali na kipa anaokoa kwa ustadi mkubwa.

DK 50 Mrisho Ngassa anaifungia Simba bao la pili.

Kipindi cha pili kinaanza hapa uwanja wa taifa.

HALF TIME

DK 45: Kagera Sugar wanaonekana kuwaelemea Simba ndani ya dakika za mwisho za kipindi cha kwanza, wanafanya shambulizi kali lakini Juma Kaseja anaifanya kazi yake vizuri ya kulinda lango la mnyama.

 DK 44: Simba 1 - 0 Kagera Sugar

 DK 37: Simba 1 - 0 Kagera Sugar

 DK 32: Haruna Moshi Boban anakosa bao la wazi baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Okwi.

DK 30: Timu zote zinashindana kumiliki mpira ingawa Kagera wanaonekana kuwazidi Simba kiasi, lakini Kagera wanakosa mipango mziru ya kuweza kupitisha mipira mbele ya Kaseja na kusawazisha goli.

 DK 22: Chollo anapiga krosi safi inayomfikia Sunzu anayepiga kichwa lakini anashindwa kulenga goli na mpira unatoka nje.

DK 20: Simba 1 - 0 Kagera Sugar

DK 13: Mpira sasa uanaanza kubadilika baada ya Simba kupata goli, Kagera nao wameamka na kuanza kujibu mashambulizi.

DK 8: Felix Sunzu anafunga bao safi la kichwa hapa uwanja wa taifa. Simba 1 - 0 Kagera Sugar.

 DK 5: Mchezo umeanza kwa kasi na Simba wanaonekana kulishambulia zaidi lango la Kagera wakifika mara kadhaa ndani ya sita ya Kagera lakini bado hawajatengeneza nafasi nzuri ya kufunga.

Kick off: Mpira unaanza hapa uwanja wa taifa 

Ukiwa umebakia muda mchache kabla ya kipenga cha kuashiria kipute cha kukata na shoka kati ya Simba na Kagera Sugar kuanza katika dimba la uwanja wa taifa. Simba wametangaza kikosi chao cha leo. 
Katika kikosi cha leo Simba itamkosa beki wake wa kutumainiwa Shomari Kapombe kutoka na kuumia, huku wakipata nguvu kutokana na kurudi kwa washambuliaji wao hatari Mrisho Ngassa na Emmanuel Okwi.

HIKI NDIO KIKOSI KINACHOANZA
Kaseja, Chollo, Maftah, Nyoso, Ochieng, Kazimoto, Ngassa, Kiemba, Sunzu, Boban, Okwi.

Sub;
Mweta, Ngalema, Hassan Hatibu, Jonas Mkude, Uhuru, Kinje na Edward Christopher

4 comments:

  1. Wee mnazi majina ya Kagera hukuyatafuta??????

    ReplyDelete
  2. Shaffie Sijakuelewa kama point si wamepata hiyo moja au ulikuwa una maanisha point ngapi? pia naomba nikuulize hivi kwa mtazamo wako Kagera Sugar walistahili kuwatungua Gogowazi?

    ReplyDelete
  3. Hii ligi inakuwa tamu sasa. Toto naye anaingojea Simba.. Patamu hapo!!

    ReplyDelete
  4. Aisee kumbe Simba=Gongo wazi.

    ReplyDelete