Raisi wa shirikisho la soka Senegal (FSF) Augustin Senghor amesema tukio la vurugu lilotokea siku ya jumamosi ilikuwa hujuma iliyopangwa kuharibu soka la nchi hiyo na kuliharibia sifa shirikisho hilo.
Boss wa FSF alisema ilitolewa oda ya tiketi kutoka mtu binafsi na tiketi zikagawawiwa kwa wahuni kwa dhumuni la kufanya vurugu katika mechi ya Senegal na Ivory Coast katika mechi ya marudiano ya kufuzu kushiriki AFCON 2013, mechi ambayo kwa bahati mbaya iliishia dakika ya 76 baada ya kuibuka kwa vurugu katika uwanja wa watu 60,000 uitwao Leopold Senghor jijini Dakar.
"Kuna mtu alitoa oda ya tiketi nyingi na akazigawa kwa wahuni waliofanya vurugu kwenye mechi. Wanataka kuharibu siafa ya ya soka la nchi yetu, ili waweze kutusema vibaya siku za mbele kwa mashabiki na taifa zima kwa ujumla," alisema.
Mapema Jumatatu, winga wa Leeds United El Hadji Diouf alisema wazi kwamba walizizuia tiketi 1,000 alizotoa oda kwa ajili ya kugawa kwa mashabiki, kutokana na shirikisho kuhisi kwamba mchezaji huyo alikuwa amewakusanya wahuni ili wakafanye vurugu uwanjani na kuitibua mechi.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kilicho karibu na shirikisho la FSF, Diouf alikuwa ndio mtu binafsi peke aliyenunua tikieti nyingi kwa ajili ya mchezo huo.
Japokuwa mchezaji huyo amesema hahusiki na chochote kuhusu vurugu za usiku wa Jumamosi, huku akiisisitiza serikali kuwaondoa viongozi wote wa shirikisho na kuliunda upya.
No comments:
Post a Comment