Katibu wa Baraza la wazee wa klabu ya Young Africans Sports Club,
Mzee Ibrahim Akilimali ametoa ufafanuzi juu ya timu ya Yanga kutovaa
jezi zenye nembo nyekundu ya mdhamini wa ligi kuu Tanzaniza bara kampuni
ya simu ya Vodacom.
Akiongea na wandishi wa habari makao makuu ya klabu makutano ya mitaa
ya Twiga/Jangwani, Mzee Akilimali amesema kamwe hawatakubali matakwa ya
vodacom na TFF ya kuweka nembo yenye doa jekundu katika jezi za Yanga.
Ni
afadhali hao TFF watufute katika ligi yao kama wataendelea
kutulazimisha kuvaa jezi zenye nembo nyekundu, kwani tupo radhi kubaki
kucheza michezo isiyodhaminiwa na Vodacom kama bao, ngumi, na mingineyo
au hata kuhamia ligi ya visiwani Zanzibar ambako tutacheza bila vikwazo.
Labda
kwa wasiofahamhu historia, Yanga mwaka 1953 mbele ya aliyekua Gavana wa
Tanganyika, Sir Edward Twinning ilikataa kuvaa jezi zenye madoa ya
rangi nyekundu ilizoletewa na timu pinzani ya mabaharia kutoka
Uingereza, na kusema ni bora tucheze vifua wazi kuliko kuvaa jezi hizo
alisema 'Mzee Akilimali'.
Mzee Akilimali aliongeza pia kuwa hata
chama cha TANU kiliwahi kuiomba Yanga ibadilishe rangi zake za kijani na
njano, lakini Rais wa kwanza wa Tanzania, Baba wa Taifa Julius Nyerere
aliwambia wajumbe wa TANU kwamba waacheni Yanga na rangi zao, rangi hizo
wanazotumia zinawatambulisha wao, madini, na maliasili ya nchi hii.
Aidha
pia Mzee Akilimali alisema mnamo mwaka 1963, aliyekuwa mkuu wa mkoa Dar
es salaam mh Mustapha Songambele aliziita timu zote zilizokuwa na
majina ya kigeni kwamba zibadilsihe majina hayo na kujiita majina ya
kitanzania, timu zote zilibadilisha majina lakini Young Africans
ilipotafsiriwa ilileta maana ya Vijana wa Afrika hali iliypolekea Yanga
kuendelea kutumia jina lake, na timu zingine kubadilisha majina yao.
Kaimu
katibu mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako amesema wanashindwa kuelewa
kwa nini vodacom mwaka huu wanalazimisha Yanga ivae jezi zenye rangi
jekundu, ili hali mwaka jana walikubali kutoa jezi zenye rangi nyeusi ya
doa la vodacom.
Mkataba kati ya TFF na Vodacom sisi hatujauona,
sasa inakuwa vigumu kujua kipi kimeandikwa ndani ya huo mkataba na
kinapaswa kutekelezwa, ilipaswa vilabu tuepewe nakala ya mkataba tuusome
kabla ya kusainiwa, ili na sisi tupate nafasi ya kutoa hoja katika
mkataba huo, lakini wao wamefanya kinyume kisha wanatulazimisha tuvae
hiyo nembo, ikiwa hatujui maslahi ya mkataba wenyewe alisema
'Mwalusako'.
Yanga itashuka dimbani siku ya jumamosi kucheza na
timu ya Ruvu Shooting katika muendelezo wa michezo ya Ligi ya Kuu ya
Vodaco nchini raundi ya 8.
Naye Mzee Mwika aliongezea kwa kutoa
mfano kwamba "haiwezekani Mnyamwezi aje zake Pwani toka Tabora atukataze
wazaramo kucheza mdundiko au dogoli", alichokikuta anapaswa kukifuata
na kukiheshimu na sio kuja na kutaka kubadillisha tamaduni za watu,
Yanga ina rangi kuu tatu (3) Kijani, Njano na Nyeusi.
(Source: http://youngafricans.co.tz/news/)
Jana bin zubery aliwapiga picha timu ya yanga ya vijana imevaa jezi za vodacom zenye nembo nyekundu,akauliza swali nembo nyekundu ni kwa wakubwa 2,ila kwa vijana wanaruhusiwa?naamin kuna cku yanga itakataa mkataba wa mamilion ya shilingi kwa ujinga wao huu,kuna cku watu wa yanga watawakataa wale wadada wa huduma ya kwanza kwa msimamo wao huu,cos wale wa red cross wana nembo nyekundu sasa nachelea kusema tunaweza mpoteza mtu uwanjan kwa ujinga wa watu wachache
ReplyDeletemambo hayo ya kung'ang'ania rangi ya kizamani KISHENZI, sasa uliona wapi VODACOM Nyeusi
ReplyDeleteHuu ndo ukomavu unabidii uonekane mpka kwnye maendeleo ya timu ya Taifa c'o mnakaza huku halaf kwenye T-starz madudu 2....Everton hawatakuja kuvaa Rangi nyekundu....Kama unaona unahalibiwa biashara yaKo "OFF YOU GO" na TFF ic'we kama hajui taratibu za TIMU inazosimamia kila TIMU inautaratibu kama waliweza kusimama kidete kwenye issue ya AFRICAN LYON wasimamie na Masilahi ya TIMU na c'o Mdhamini pekee yk...Je, leo Adidas au Nike wakitaka Jezi za Timu ya T-stars ziwe Nyekundu watakubali mana kila nchi ina rangi yk kwenye Bendera yake huwezi kusikia Brazil imevaa rangi nyekundu hata siku moja.
ReplyDeletelAZIMA WATU WAHESHIMU UTAMADUNI NA KATIBA ZA TIMU KWA SABABU NI MSINGI WA MAISHA YA KLABU HUSIKA. HATA KESHO SIMBA WAKIAMBIWA WAVAE DOA LA NJANO AU KIJANI UTAUONA MOTO WAKE. LAZIMA KATIBA ZA TIMU FLANI ZIHESHIMIWE NA SHERIA ZINGINE ZA SOKA ZITAFUATWA LAKINI SI MATAKWA YA MDHAMINI NI SAWA VODA WASEME SISI TUTAIDHAMINI DINI ZOTE KWA SHARTI LA KWAMBA WAKRISTU WAINGIE KANISANI NA MSAFU AU QUORAN KITU KAMA NEMBO YA MDHAMINI HUU NI UPUUZI. YANGA ENDELEENI NA MSIMAMO HUU HADI KIELEWEKE KAMA VODA HAWATAKI WAVUNJE MKATABA NA WADHAMINI WENGINE WATAKUJA.
ReplyDeleteIn the Premier League, domestic broadcast revenue is divided on a 50:25:25 basis; 50% is divided equally between the clubs; 25% is awarded on a merit basis determined by a club’s final league position and the final 25% is distributed as a facilities fee for the number of matches shown on television involving the club.
ReplyDeleteThe income from overseas rights is divided equally between the 20 Premier League clubs.
Sasa clouds sports extra wanashangaa africa lyon na yanga kuulizia mapato ya mkataba wa TFF superspot!!! EPL mapato ya clubs ndogo kiasi kikubwa kinatoka kwenye TV rights!!!.