Kiungo wa Chelsea Juan Mata amesema kuondoka kwa wingi wachezaji wenye vipaji kutoka kwenye ligi kuu ya taifa lake Spain kunampa mashaka juu ya mustakabari wa soka la nchi hiyo.
Mata aliondoka Valencia miezi 18 iliyopita na kujiunga na Chelsea.
"Nina wasiwasi kidogo kuona namna wachezaji wengi wakiwa wanaondoka La Liga. Ligi ina timu mbili tu zinazoshindania ubingwa. Timu inayoshika nafasi ya tatu na nne zinakuwa nyuma kwa pointi 30 mwishoni mwa msimu.
"Ikiwa huchezei katika vilabu vya Barcelona au Real Madrid, then huwezi kushinda ubingwa. Haiwezekani kwa klabu yangu ya zamani Valencia kuwa mabingwa.
"Hii kitu sio nzuri kwa soka la Hispania kwa sababu hakuna ushindani wa ukweli kwa vilabu vikubwa."
No comments:
Post a Comment