Search This Blog

Friday, May 11, 2012

Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’-Nilifunga safari hadi Kinshasa, nikalala nje ya geti la Nonda,

Na Saleh Ally
*Baridi ilinipiga usiku kucha bado sikumpata
*Kabla, nilikamatwa na polisi kwa dawa za kulevya
MWAKA 2006 ndiyo Bakari Malima maarufu kama Jembe Ulaya aliamua kutundika daruga na kustaafu soka la ushindani, baada ya hapo yakaanza mambo mengine ya maisha.

Kabla ya hapo, Malima anajulikana kutokana na uwezo wake mkubwa wakati anaichezea timu ya Yanga na Vaal Professionals ya Afrika Kusini pamoja na timu ya taifa, Taifa Stars.
Sifa kubwa ya Malima, ilikuwa ni uwezo mkubwa katika ulinzi na kufunga mabao ya vichwa. Kila mshambuliaji aliyekabana na Malima alijua kazi aliyonayo, mwisho akabandikwa jina la Jembe Ulaya.
Baada ya kustaafu soka, pamoja na biashara ndogo ndogo, Malima aliamua kufanya kazi, aliajiriwa kuendesha mitambo na magari makubwa katika machimbo ya Barrick huko mkoani Shinyanga.
Maisha ya Malima, yamejaa misukosuko mingi nje ya uwanja na huenda akawa mmoja mchezaji mwenye simulizi za kusitikisha. Kupitia ukurasa huu wa Maisha Baada ya Soka, Malima anasimulia mambo yaliyowahi kumkuta.
Nonda Shaaban:
Nonda alikuwa alikuwa rafiki yangu mkubwa, wakati tukicheza wote Yanga alikuwa akiishi nyumbani kwangu kwa kipindi kirefu. Tuliishi vizuri sana na maisha yetu yalikuwa ni mazuri tu.
Wakati tulipokwenda Vaal Professionals kule Afrika Kusini, mwenzangu alifanikiwa kupata kibari cha kucheza soka na mimi nikakosa. Nitaelezea baadaye, labda nianze na mwishoni halafu nitarudi mambo yalivyokuwa mwanzo.
Maana nimewahi kukutana na misukosuko mingi sana, nakumbuka nikiwa nimebakiza mwaka mmoja kustaafu soka wakati huo nachezea timu ya Twiga, nilipata taarifa kuwa Nonda angerudi kwao Congo kwa ajili ya mechi ya kimataifa.
Wakati huo Nonda ambaye nilikula naye msoto Dar es Salaam na Afrika Kusini alikuwa amefanikiwa kimaisha. Alikuwa anaichezea Monaco ya Ufaransa na alishakuwa mshambuliaji tegemeo.
Nikaona itakuwa ni vizuri niende kumuona, maana baada ya kujaribu sana maisha tena kwa juhudi lakini mambo yalikuwa ni magumu na wakati huo soka lilikuwa linaenda ukingoni.
Unajua kuna wakati niliwahi kukamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam (DIA), kwa tuhuma za madawa ya kulevya. Nayo ikanirudisha nyuma sana, nitahadithia baadaye namna mambo yalivyokuwa.
Hivyo nilianza safari ya kumfuata Nonda, nilipofika Lubumbashi, hakukuwa na namna, ilikuwa ni lazima nipande ndege hadi Kinshasa ambako mechi ilikuwa inachezwa. Nakumbuka Congo walitoka sare katika mechi hiyo.
Baada ya hapo, nilianza kazi ya kuhakikisha nakutana na Nonda kwa kuwa kulikuwa kuna mambo mawili yalinitia hofu. Kwanza, sikuwa na fedha za kutosha, mfukoni nilikuwa na dola 50 tu.
Pili sikuwa na miadi na Nonda, halafu baada ya kufika Kinshasa nikagundua alikuwa ni staa mkubwa. Kila mtu aligombania kumuona na ulinzi wake ulikuwa mkali sana, hivyo kumuona ilikuwa ni mbinde.
Nilianza kutafuta alipokuwa anaishi, lakini ilikuwa ni kazi kubwa watu kukubali kunionyesha. Mtu mmoja alinielekeza hoteli aliyokuwa anaishi na nilipofika pale wakanieleza huwa analala nyumbani kwake.
Hivyo nilianza kutafuta watu wa kunielekeza wapi anakoishi, pia ilikuwa ni kazi kubwa wao kukubali. Niliwaeleza kuwa nilicheza naye soka Tanzania na baadaye Afrika Kusini, walikubali kunielekeza baada ya kuwaonyesha picha zangu na Nonda ambazo tulipiga pamoja.
Baada ya hapo, mmoja wao akanielekeza na kuniambia nisiseme kama yeye alinielekeza kwa kuwa hawakuruhusiwa kufanya hivyo. Basi nikaenda hadi sehemu niliyoelekezwa na nilipofika pale nikamkuta mlinzi.
Kukawa na tatizo kubwa limeibuka, yule mlinzi alikuwa hazungumzi Kiswahili wala Kingereza, alizungumza Kifaransa na Kilingala. Tukawa hatuelewani, ukazuka mzozo mkubwa kati yetu.
Mzozo huo ulisababisha majirani watoke, mmoja wao alisogea karibu na kutaka kujua kilichokuwa kinaendelea. Nikamueleza kuwa mimi ni Mtanzania na nilicheza soka na Nonda, shida yangu ilikuwa ni kukutana naye.
Basi akazungumza na yule mlinzi ambaye alizidi kuonyesha ni mkorofi, akasisitiza nikae pembeni. Yule jirani akaingia ndani na kutoka na kiti, geti lake lilikuwa karibu kabisa na pale kwa Nonda. Akaniambia nimsubiri pale.
Akaniambia kuna gari aina ya Range Rover Vogue ndiyo anatumia akiwa pale Kinshasa, hivyo niliona basi nijitambulishe. Lakini akasisitiza kama nitakuwa simjui Nonda, nitaingia matatizoni.
Nikakaa kwenye kiti pale nje, ilikuwa ni baridi kali sana, nilitetemeka usiku kucha hadi ilipofika muda kama saa tisa usiku, nikaona taa za gari. Nilipoangalia kweli ilikuwa ni Vogue inakuja. Nikaona nikizubaa tu, nitamkosa jamaa. Nikasimama katikati ya geti.
Yule mlinzi alikasirishwa na kitendo change, akataka kunitoa lakini taratibu vioo vya gari vikateremshwa na nikashituka baada ya kuona aliyekuwa kwenye gari ni mdogo wake na Nonda na si yeye mwenyewe.
Alihoji sababu ya mimi kusimama katikati ya geti, nilianza kumuelezea na nilishukuru alipoanza kuzungumza Kishwahili. Alionekana kunielewa, lakini akasisitiza kwa kuwa haniamini maana hanijui vizuri, nirudi na kulala tena pale nje hadi asubuhi.
Alisema akiamka, tutaongozana kwenda kwa Nonda ambaye alikuwa amelala hotelini na aliniambia ingekuwa vigumu kuruhusiwa kumuona bila ya kwenda naye.
Sikuwa na ujanja, nilirudi pale kwenye kiti nilichopewa na jirani. Dakika chache jirani akatoka na kuniuliza imekuwaje, nikamueleza mambo yalivyokwenda. Akaniambia niendelee kusubiri.
Nikalala pale hadi alfajiri, yule jirani wa Nonda aliyenipa kiti akatoka na kunishauri. Alinieleza kwamba huenda yule mdogo wake Nonda akalala hadi saa nne asubuhi, hivyo ingekuwa vizuri kama mwenyewe ningeondoka na kwenda hotelini kujaribu kumpata.
Niliona ni wazo zuri, nikarejesha kiti chake na kumshukuru, wakati huo nilikuwa sijala siku ya pili. Nikaanza safari ya kwenda kumtafuta Nonda. Nilipofika hotelini, bado hawakukubali nimuone, wala hawakutaka kumpigia simu.
Mhudumu mmoja akanishauri nizunguke nyuma ya hoteli kwa kuwa lazima angepitia huko. Niliamua kufunya hivyo na huko niliwakuta waandishi kibao wa habari ambao walikuwa wanasubiri kuzungumza na Nonda.
Hofu ya Malima ni kama kweli ataweza kumuona mshikaji wake, Nonda Shaaban Papii. Akimkosa, ataishi vipi au atarudi vipi Tanzania wakati amebaki na dola 50 pekee ambayo ugenini ni matumizi ya siku moja tu? MKASA ZAIDI, TUENDELEE KUWA PAMOJA!

Thursday, May 10, 2012

BAADA YA MASAA MANNE BARABARANI SIMBA YAFIKA MJI WA SHANDY KWA TAABU: WENYEJI WAWAKIMBIA - HAWAJALA KITU CHOCHOTE KWA MASAA TAKRIBANI SITA SASA

Hatimaye baada ya masaa manne ya kusafiri kutoka Khartoom mpaka Shandy wawikilishi wa Tanzania katika michuano ya kimataifa ya soka Simba SC imefika mjini Shandy salama kabisa.

Lakini katika hali ya kushangaza wenyeji wao timu Al Ahly Shady wamepotea na kuwaacha wageni wao Simba katika hali tata - kwa mujibu wa mchezaji Emmanuel Okwi wamefikia sehemu mbaya na tangu wamefika takribani masaa sita yaliyopita hawajitia kitu chochote mdomoni. "Bwana huku tumefika lakini kwa shida sana, tunashukuru mungu tumefika salama ila tangu tumefika hapa hatujatia kitu chochote mdomoni na wenyeji wetu hawaonekani. Ila tunawaomba wanasimba na watanzania kwa ujumla waendele kutakia kheri na tunawahidi hizi hila za wasudani hazitowaepusha na kipigo siku ya mechi." - Emmanuel Okwi.

ON THIS DAY: NAPOLI WACHUKUA UBINGWA WAO KWANZA WA SERIE A WAKIWA NA JEMBE DIEGO ARMANDO MARADONA

Siku kama ya leo miaka 25 iliyopita, Napoli walisherehekea ubingwa wao wa kwanza kabisa nchini Italia. 
 Matokeo ya sare dhidi Fiorentina yaliwawezesha Napoli kuwa timu ya kwanza kutoka kusini mwa Italia kushinda kombe la Scudetto chini ya mwanaume Diego Maradona.

BRAZIL YATANGAZA SHERIA MPYA KWA AJILI YA KOMBE LA DUNIA 2014 - POMBE RUKSA VIWANJANI

Seneta ya Brazil hatimaye imeptisha sheria ya kombe la dunia na kutoa guarantii kwa FIFA waliyokuwa wakihitaji juu ya kuandaa kombe la dunia mwaka 2014.

Sheria hiyo imekuja siku moja baada ya serikali ya Brazil kukutana na maofisa wa FIFA nchini Switzerland kujadili maandalizi ya nchi hiyo na kusuluhisha tofauti zao.

Sio watu wote wamefurahishwa na sheria hiyo. Vilevi vimekatazwa katika viwanja vya soka nchini Brazil tangu mwaka 2003, na baadhi ya wabunge wameonekana kuwa na wasiwasi na usalama viwanjani baada ya mabadiliko mapya yaliyofanyika katiba sheria mpya.

Sheria mpya imeruhusu uuzwaji wa pombe ndani ya viwanja wakati wa kombe la dunia na michuano ya mabara.

Uuzwaji wa vilevi viwanjani ulikatazwa baada ya matukio vurugu kuzidi viwanjani nchini humo - hivyo kuna baadhi ya wabunge wa nchi hiyo wanahisi suala hilo linaweza likahatarisha usalama.

BREAKING NEWS: ADIDAS KUIDHAMINI TAIFA STARS

Habari za uhakika nilizozipata kutoka ndani ya shirikisho la soka Tanzania TFF ni kwamba kampuni ya utengenezaji wa mavazi ya Adidas imeingia mkataba wa kuidhamini Taifa Stars katika suala zima la jezi. Kwa taarifa zaidi endelea kutembea http://www.shaffihdauda.com/

PICHA: HAYA NDIO MAISHA ANAYOISHI DANNY MRWANDA





JULIO: HAKUNA KAMA MILOVAN NA KIM POULSEN

Kocha Jamhuri Kiwhelu akizungumza na EXCLUSIVELY na http://www.shaffihdauda.com/ amesema makocha Milovan Cirkovic wa Simba pamoja na Kim Poulsen wa timu ya Taifa ya vijana ndo makocha pekee wenye uwezo wa kufundisha soka miongoni mwa makocha wazungu waliofanikiwa kufanya kazi hapa nchini.
pamoja na kuwasifia makocha hao Jamhuri maarufu kwa jina la Julio hakusita kumpa sifa za kipekee kocha wa timu ya taifa ya vijana mdenish Kim Poulsen kuwa ndiye kocha bora mzungu miongoni mwa makocha wote wazungu waliowahi kufanya kazi hapa nchini. 
Pia Julio ameliomba shirikisho la soka nchni kumtumia Kim Poulsen kama kocha mkuu katika timu ya taifa ya wakubwa ili kuweza kuiwezesha timu ya taifa kupata mafanikio kwa kuwa ni kocha ambaye anaipenda kazi na kuiheshimu na uwezo mkubwa wa kufundisha soka.
 

KUTOKA KUCHEZA PEKUPEKU MPAKA KUJA KUWA MWANASOKA TAJIRI DUNIANI: FAHAMU NJIA ALIZOPITIA YAYA TOURE KUFIKA HAPA ALIPO.




YAYA TOURE AKISUKUMA GOZI HUKU AKIWA PEKUPEKU NCHINI KWAO IVEORY COAST KATIKA KLABU YA ASEC MEMOSAC.

Yaya Toure aliwasili Ubelgiji akiwa hana chochote bali kipaji chake. Hiyo ndio kumbukumbu waliyokuwa nayo juu ya Toure pale Beveren: hakuwa hata na pea za viatu vya kuchezea soka.

Nyingine ni kwamba hakuwa na tabia ya kuamka mapema asubuhi; alikuwa anakula kama farasi na kunywa kama samaki, soda ya fanta na sio pombe.

Yaya Toure alitua Beveren, mji mdogo uliopo magharibi mwa Antwerp, akiwa tu ndio anafikisha miaka 18, akiwa amelelewa kwa kuongea lugha ya kifaransa katika mitaa ya Abidjan, Ivory Coast. Alikuwa na pesa kidogo sana, pair moja ya viatu na nguo chache.

Lakini pale Flanders, wanasema hata akiwa mdogo, kijana ambaye ameshinda Champions league na Barcelona na ambaye msimu huu amekuwa moyo wa timu ya Manchester City alikuwa mtu ambaye anapenda kuwa yeye kitu ambacho kilimtofautisha na wenzake.

Leo hii Toure anaonekana na kung'ara - moja ya viungo bora kwenye soka, mwenye uzoefu na akiwa tayari kuiongoza Manchester City kushinda taji lake kwanza baada ya miaka 44 jumapili ijayo, ambayo itakuwa ndio siku yake ya kuzaliwa akitimiza miaka 29. Tangu zamani Yaya alionekana kuwa mtu ambaye atakuja kufanikiwa.


YAYA ALIYEZUNGUSHIWA KIDUARA ALIPOKUWA UBELGIJI PALE BEVEREN

"Nilikuwa nawachukua kila siku, Yaya na rafiki zake wawili,' anasema Anour Bou-Sfia, ambaye alicheza na Toure pale Beveren. 'Yaya alikuwa na tabia fulanihivi - alikuwa anajua atakuja kufanikiwa na kuwa bora.

"Mahali walipoishi ndio ilikuwa njia yangu ya kwenda uwanjani na kulikuwa na siku nyingi tu ambazo ilibidi Yaya tuwe tunamuamsha kwenda mazoezini, lakini yeye alikuwa tofauti ukilinganisha na wengine - Yaya alikuwa na akili sana na aliyepevuka. Wengine wote walikuwa na mentallity za kijinga za vijana kutoak afrika ambao ghafla tu walijikuta wapo ulaya. Yaya hakuwa anapenda camera, magazeti, alikuwa na aibu sana. Alikuwa hapendi kutoka kama wenzake. Alikuwa muislamu kamili. Mimi ni mmoroco, ni muislam.

"Muda mwingine tukiwa uwanjani angeweza kufanya vitu ambavyo vilitushangaza wote. Nilicheza nae kwa misimu miwili na nusu lakini kwa muda wote huo nilikuwa bench. Hivyo nilikuwa namuangalia, niliwaleta rafiki zangu kuja tu kumuangalia alikuwa mchezaji mzuri sana.

"Angalia goli la kwanza alilowafunga Newcastle jumapili, alilifanya lionekane rahisi. Angalia nmna alivyofunga. Alishinda Champions league pale Barcelona akicheza pembeni ya Gerard Pique katika safu ya ulinzi. Alilifanya suala lile lionekane rahisi.

"Nafikiri alikuwa kama anaboa muda mwingine alipokuwa akiichezea Barcelona. Ilikuwa rahisi sana. Hata Beveren alikuwa hivyo - kule ufaransa wanamuita nonchalance.

"Yaya hakuwa mtu anayependa kujionyesha. Nilikuwa mtafsiri lugha wao, kuwapeleka supermarket, kuwapeleka kwenda kununua viatu kwa sababu hawakuwa na viatu."

Career ya Yaya Toure ilipitita katika njia ngumu. Alienda Beveren mwaka 2001,  ikiwa ni sehemu ya majaribio nchini Ubelgiji  - wazo la mchezaji wa zamani wa Ufaransa Jean-Marc Guillou, mtu wa karibu sana na Arsene Wenger.

Guillou amejenga academy nchini Ivoery Coast - ambapo kaka yake Yaya, Kolo Toure ndio alitokea hapo na kwenda moja kwa moja mpaka Arsenal.

Pale KSK Beveren, Guillou aliipata timu ndogo iliyokuwa ikihitaji uwekezaji. Akainunua na msaada kutoka kutoka Arsenal.

Sheria nzuri za Ubelgiji zilikuwa na manufaa kwa Guilloi ambaye sasa kashayapatia maisha. Ada yoyote ya uhamisho kwa wachezaji watakaouzwa kutoka klabu hiyo - ilikuwa inagawanywa pasu kwa pasu. Guillou na Beveren.
YAYA TOURE NDANI YA UZI THE GUNNERS AMBAPO ALIFANYA MAJARIBIO.

Mwaka 2003, kutokana na uhusiano uliopo kati ya Arsenal na Guillou pamoja Beveren Yaya Toure akapelekwa London kwa majaribio ya muda mfupi. Japokuwa sasa anafananishwa na Patrick Vieira - haikuwa hivyo mwanzoni.

Toure alicheza mechi ya pre-season dhidi ya Barnet lakini dimba la juu. Aidha Toure hakumshawishi au Wenger tayari alikuwa na mbadala wake, kijana kutoka Ivory Coast akarudi Ubelgiji. Wote wawili Wenger na Toure wameshasemakulikuwa na matatizo juu ya passport.

'Labda alikuwa bado hajakaa sawa,' alisema Martin Keown, ambaye bado alikuwa Arsenal kipindi hicho.

"Kulikuwa na attention kubwa sana juu yake kwa sababu alikuwa mdogo wake Kolo, lakini Yaya hakuwa na mwezi wa mazoezi wa pre-season kama wengine . Labda mwili wake bado haukuwa sawa.

"Lakini pamoja na yoteYaya aliacha gumzo. Yeye na kaka yake ni wakarimu na watu wazuri sana. Na wanapenda mpira - tumekuwa tukisikia kuhusu watoto wa mzee Neville walivyo, ndugu hawa wa Toure nao wapo hivyo hivyo."

Aliporudi Ubelgiji Toure hakukataa tamaa aliendeleza juhudi ya kujifunzana mazoezi na hata tabia zake hazikubadilika.
Ingawa katika mahojiano aliyoyafanya na Dailymail Toure anasema alifanya mambo mengi ya kijinga  alipokuwa Beveren lakini hakuna mtu anakumbuka. lakini Danny Stuer mkufunzi wa mazoezi ya viungo anasema tofauti: "Yaya alikuwa mtu wa maadili, tofauti sana, muda wote mkimya na mtu anayependa kufanya kazi. Alikuwa anakuja gym na alikuwa proffessional tangu mwanzo - wengine wote hawakuwa hivyo - kwao gym ilikuwa mchezo mtu.

"Baada ya mechi Yaya hakuwa akitoka kwenda kunywa mabia kama wenzie. Alirudi nyumbani na kubaki kupumzika huku akiangalia TV, hasa soka na soka zaidi."

"Mwanzoni alikuwa akiishi na wenzie lakini wenzake walipokuwa wanatoka usiku na kurudi wamechelewahuanza kumsumbua. Hivyo mwishowe akaomba aishi peke yake, na klabu ikafanikisha hilo.

"Labda alienda kwenye party nyuma ya mgongo wangu kama wengine- lakini kwa kile ninachojua Yaya alikuwa tofauti"

Pale Beveren walikuwa wanajua wachezaji wa  kiafrika walikuwa wakienda Liege au Brussels kwa ajili ya kupati.

Baada ya misimu miwili na nusu na mechi 70 akiwa na Beveren, Toure aliuzwa kwa fedha ya ubelgiji millioni 2.

Mahasimuwawili wa Ubelgiji, Anderlecht na Club Bruges, wote walikuwa wakimtaka Toure, lakini sio kwa bei hiyo. Hivyo akiwa na miaka 20, akahamia Ukraine kwenye timu ya daraja ya pili ya Donetsk, Metalurh. Haikuwa sehemu nzuri kwa mtu ambaye alikuwa na ndoto ya kuwa star wa dunia, lakini Toure anasema uhamisho huo ulikuwa mzuri kwake. "Soka ni kazi; nilijifunza hivyo Ukraine."

Baada ya muda kidogo -akahamia Ugiriki na kujiunga na Olympiakos. Club Bruges inaweza kuwa ilikataa kulipa €2m lakini manager wao, mnorway Trond Sollied, ambaye alijiunga na Olympiakos akamsaini Toure na kushinda kombe la Ugiriki. "Niliona almasi, kitu fulani special kwake, alipokuwa pale Beveren," anasema Sollied. "Hakuwa na nguvu alizonazo sasa, au kufunga magoli mengi lakini alikuwa na kitu extra ndani ya timu.

"Kumpata na kumleta Ugiriki ilikuwa ni vizuri. Kimwili alikuwa amepevuka, alikuwa yupo vizuri kuliko alivyokuwa Ukraine. Tulijua hatutoweza kukaa nae sana. Alikuwa na uhakika sana kuhusu alivyo. Nafikiri kaka yake alimsaidia. Walikuwa wakibadilishana uzoefu."

Baada ya kombe la dunia la mwaka 2006, AS Monaco, timu ya zamani ya Wenger, ilimnunua Toure kwa ada ya £4million, ingawakulikuwa na kutokuelewana kidogo kule Donetsk kuhusu mkataba wake.
YAYA TOURE ALIPOKUWA BARCELONA.

Lakini baada ya msimu mmoja tu nchini Ufaransa, Barcelona wakamsaini. Yaya Toure akaenda Catalunya ambako alipata majina mengi kamavile "Colossus - yaaani sanamu kubwa sana la mtu", wengine wakamuita "Treni " lakini Pep Guardiola alimuelezea Yaya kama "Diesel Player" - inachukua muda muda mrefu kwenda anapopataka lakini hasimami.


Huyu ndio Yaya Toure ambaye ama kwa hakika ndio kiungo bora kabisa katika msimu huu wa Premier League ambayo inaisha Jumapili huku mwenyewe akitimiza miaka 29 siku hiyo.

ZIMBABWE YAFURAHIA KUJIPIMA KWA TWIGA STARS

Timu ya Taifa ya mpira wa miguu kwa wanawake ya Zimbabwe imefurahia kucheza mechi ya kirafiki na Tanzania (Twiga Stars) itakayofanyika Jumamosi (Mei 12 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kocha Mkuu wa Zimbabwe, Rosemary Mugadza amesema wamefurahi kupata mechi hiyo kwa vile wanaamini Twiga Stars ni kipimo kizuri kwao kabla ya kucheza mechi yao ya mashindano ya Afrika dhidi ya Nigeria.
Amesema anaijua vizuri Twiga Stars, kwani mwaka jana alicheza nayo mara mbili. Mara ya kwanza ilikuwa kwenye nusu fainali ya Kombe la COSAFA ambapo katika mechi hiyo iliyochezwa Julai 5 jijini Harare, Zimbabwe ilishinda kwa penalti 4-2. Mechi ya pili ilikuwa kwenye michezo ya All Africa Games (AAG) iliyofanyika Maputo, Msumbiji ambapo katika mechi yao iliyochezwa Septemba 11 timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2. Mabao ya Twiga Stars yalifungwa na Asha Rashid na Mwanahamisi Shuruwa. Mugadza amesema sababu nyingine iliyowafanya watake kucheza na Twiga Stars ni kwa vile ilishacheza na Nigeria kwenye fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) zilizofanyika Afrika Kusini mwaka 2010.

Twiga Stars ilifungwa na Nigeria mabao 2-1. Kocha huyo amesema hiyo itakuwa mechi ya pili kujipima nguvu kabla ya kuivaa Nigeria. Mwishoni mwa wili iliyopita Zimbabwe ilicheza mechi ya kirafiki jijini Harare dhidi ya Zambia na kushinda mabao 2-1. Zimbabwe ambayo iliwasili jana (Mei 9 mwaka huu) saa 1.30 usiku kwa ndege ya South African Airways (SAA) ina msafara wa watu 28 ambapo kati ya hao 20 ni wachezaji wakati waliobaki ni benchi la ufundi na viongozi wa timu hiyo.Viingilio katika mechi hiyo kati ya Twiga Stars na Zimbabwe itakayochezwa kuanzia saa 10.30 jioni ni sh. 1,000 tu kwa sehemu zote isipokuwa VIP A ambayo ni sh. 10,000 na VIP B ambayo kiingilio chake ni sh. 5,000.

Twiga Stars ilikuwa katika ziara ya mechi za kirafiki katika mikoa ya Dodoma na Mwanza na inatarajia kurejea kesho (Mei 11 mwaka huu) tayari kwa mechi hiyo itakayochezwa na mwamuzi wa kimataifa Judith Gamba. Boniface WamburaOfisa HabariShirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

WACHEZAJI WA MAN UNITED WAGAWA ZAWADI NCHINI KENYA: GARI LILOBEBA MIPIRA 200 LAENDESHWA KUTOKA UINGEREZA MPAKA KENYA



Man United star Nani amezoea kuingiza mipira kwenye nyavu za uwanjani, lakini sasa ameamua kuitumibikiza kwa gari aina ya Van.

Andy Cole na Fortune wakigawa mipira 200 iliyotoka Uingereza na kuletwa nchini Kenya kwa gari.



Mreno huyo akiwa wachezaji wenzie Jonny Evans, Chris Smalling na Park Ji Sung waliweza kuingiza mipira mia mbili kwenye gari la DHL katika uwanja wa wa mazoezi wa United - Carrington.


Watoto nchini Kenya wakiwa na zawadi ya mipira kutoka kwa wachezaji wa Man United

Gari hilo liliendeshwa kwa maili 4,395 mpaka kwenye World Hope Community Project nchini Kenya  na Dan Magness ambaye ni mchezea mipira wa ustadi.

AIRTEL RISING STARS YAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM.


Mashindano ya kuvumbua vipaji maarufu kama Airtel Rising Stars yamezinduliwa rasmi hii leo jijini Dar Es Salaam na Wazir wa Mawasiliano Sayansi na Teknojoria Profesa Makame Mbarawa,
Kwenye uzinduzi huo pia alikuepo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Bwana Sam Elangalloor. Mwakilishi wa TFF kwenye uzinduzi huo alikua ni mkurugenzi wa Mashindano Bwana Saad Kawemba.


 Kiungo wa zamani wa Manchester Utd Quinton Fortune akionyesha ujuzi wake wa kuuchezea mpira.

KALI YA LEO: BOBAN ASAFIRI KWENDA SUDAN AKIVAA KANDAMBILI

Haruna Moshi Boban akiwa ndani ya kandambili uwanja wa taifa jana.
Kiungo mshambuliaji wa timu ya Simba, Haruna Moshi ‘Boban’ jana alikuwa kivutio kwa mashabiki, wasindikizaji na hata baadhi ya wasafiri waliomuona wakati wakiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, kuelekea Sudan. 
     Simba inakwenda Sudan katika mchezo wa marudiano dhidi ya Al Ahli Shendi utakaopigwa Jumapili, huku ikiwa na mtaji wa ushindi wa mabao 3-0, iliyoupata kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Uvaaji wa Boban, ndio uliowavutia watu kumtizama, kutokana na kuvaa kama mtu asiyesafiri. 
   Boban alikuwa amevaa fulana, suruali ya kimichezo ‘trakisuti’ na kandambili, hivyo kusababisha watu kuvutika kumuangalia, huku baadhi yao wakibaki kujiuliza kuhusu vituko vya nyota huyo ambaye mashabiki humuita Balotteli wa Bongo.
 Mchezaji huyo anafananishwa na mshambuliaji mahiri wa Italia, anayekipiga klabu ya Manchester City ya England, ambako mara kwa mara amekuwa akibeba vichwa vya habari katika magazeti ya England na Ulaya kutokana na vituko vyake. 
Ukiondoa vituko hivyo vya uvaaji wa Boban, msafara wa watu 25 wakiwamo viongozi watano na wachezaji 20 wa timu hiyo waliondoka chini ya uongozi wa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Hussein Mwamba, majira ya saa 8:00 mchana

RADEMEL FALCAO NI HATARI: AIONGOZA ATLETICO MADRID KUTWAA NDOO YA EUROPA KWA KUWATANDIKA WABABE WA MAN UNITED 3-0


Atletico Madrid 3-0 Athletic Bilbao by fasthighlights-2012

SIMBA YAFIKA SALAMA SUDAN

  Majira ya saa 6 usiku nilifanikiwa kufanya mawasiliano na mchezaji wa Simba Emmanuel Okwi na ameniambia kwamba timu nzima imefika Salama huko Sudan. Kwa taarifa zaidi endelea kutembelea hapa

SIMBA ILIPOONDOKA KWENDA SUDAN LEO MCHANA

Makamu mwenyekiti wa timu ya Simba Bw. Godifrey Nyange ''Kaburu''akionyesha ishara ya vidole vitanona mchezaji nyota wa timu hiyo Emmanueli Okwi, kwa kuonyesha  alama hii huenda walikuwa wakimaanisha ushindi wa magoli 5 walioupata baada ya kuwafunga  watani wao timu ya Yanga .hii ilikuwa katika uwanja wa ndege wa mwalimu juliasi Nyerere jijini Dar es salaam wakati timu hiyo ikijianda kuondoka kwenda Sudani kwenye mchezo wao wa marudio na Al Hilal Shandy jumapili ijayo.
Kapteni wa timu ya Simba Juma Kaseja akihojiwa na waandishi wa habari kuhusiana na maandalizi ya timu hiyo.
Makamu mwenyekiti wa timu ya simba Bw;Godifrey Nyange ''Kaburu akiteta jambo na wachezaji wa timu ya Simba.
Wachezaji wa timu ya Simba wakiingia kwenye chumba maalumu tayari kwa kuondoka.

LLOYD NCHUNGA AJIBU MAPIGO: SITOJIUZULU YANGA, PAPIC ATAONDOKA, UONGOZI HAUDAIWI. FAGIO LA CHUMA KUPITA YANGA TISA KUONDOKA. MWAPE NA SHAMTE ALLY KUTOVAA JEZI ZA NJANO NA KIJANI MSIMU UJAO

WAKATI uongozi wa Yanga ukipuuza shinikizo zito la kutakiwa kujiuzulu toka baadhi ya wanachama wa klabu hiyo kwa madai ya kuwa kiini cha kipigo cha aibu toka Simba Jumapili iliyopita, wachezaji tisa timu hiyo wamekalia kuti kavu baada ya mikataba yao kufikia.
Wachezaji hao wako hatarini kutemwa kwa sababu kuna uwezekano mdogo, au usiwapo kabisa kusaini mikataba mipya, taarifa za ndani toka klabu hiyo ya Jangwani zimedai
Ni pamoja na Shamte Ally, Jerry Tegete, Chacha Marwa, Mohamed Mbegu, Abuu Ubwa, Zuberi Ubwa,  Kigi Makasi, Shadrack Nsajigwa na Athuman Idd 'Chuji'.
Tegete anahusishwa kwenda Simba, wakati Nsajigwa anatuhumiwa kucheza chini ya kiwango katika mechi yao dhidi ya Simba, ambapo alisababisha penalti mbili kati ya tatu na kuwapa mahasimu wao ushindi wa mabao 5-0.
"Wachezaji wengi wamemaliza mikataba yao, wapo baadhi huenda wakaongezewa kama Chuji, lakini wengine watatemwa akiwamo Shamte ambaye hakuna ubishi hatarudi Jangwani msimu ujao," alisema mtoa habari.
Alisema wachezaji Nurdin Bakari, Hamis Kiiza, Kenneth Asamoah bado wana mkataba wa mwaka mmoja, wakati Yaw Berko na Davis Mwape mikataba yao itamalizika Novemba mwaka huu.
"Uongozi umeshaanza kuzungumza na Berko kuangalia uwezekano wa kuongeza mkataba wake, lakini Mwape hatacheza Yanga msimu ujao mara baada ya mkataba wake kumalizika," alisema mpashaji huyo habari.
Jumamosi wiki hii Kamati ya Utendaji itakutana, na moja ya mambo watakayozungumza ni ushiriki wa Ligi Kuu, changamoto zilizokuwepo na kujadili wachezaji watakaochwa na wanaostahili kubaki.
"Kikubwa kinachoangaliwa ni nidhamu wa wachezaji ndani na nje ya uwanja pamoja na kiwango, na pia kuna wachezaji wengine watahama kwenda timu nyingine haya yote yataangaliwa."
Alisema ajenda nyingine kwenye kikao hicho ni kupanga tarehe ya Mkutano Mkuu wa wanachama pamoja na vuguvugu la mgogoro lililopo ndani ya klabu hiyo.
Mwenyekiti wa Yanga Llody Nchunga alisema masuala yote yanayohusu usajili wa wachezaji watawekwa wazi wiki ijayo mara baada ya kikao chao cha Kamati ya Utendaji.
Aidha, kuhusu wachezaji wanaodai, Nchunga alisema ni wale waliongezewa mikataba ambao ni Nurdin Bakari na Nadir Haroub.
"Wachezaji wanaodai fedha za usajili ni wachache tena waliongezewa mikataba kipindi cha uongozi uliopita na hata hivyo fedha hizo wanatakiwa walipwe msimu ujao kwa kuwa ndiyo watakaoanza kuutumikia," alisema Nchunga na kuwataja wachezaji hao kuwa ni Nurdin na Nadir.
"Nawashangaa wazee wetu wanavyosema wachezaji wanadai Sh127 milioni. Hivi hawa wazee ni wahasibu? Wamepata wapi hesabu hizi, napenda kuwaambia kuwa hatudaiwi kiasi hicho," alisema.
Kuhusu shinikizo la kutakiwa kujiuzulu, Nchunga alisema hawezi kufanya hivyo kwa shinikizo la watu wachache wakati Yanga ni timu ya wanachama.
"Mimi nilichaguliwa na wananchana wa Yanga, wao ndiyo wanaweza kunitaka nijiuzulu tena kupitia Mkutano Mkuu wa Klabu. Tunaendeshwa na katiba na siyo kelele za vikundi vya watu. Hatima yangu itaamuliwa na Wanayanga, siyo kikundi.
"Kamati ya Utendaji itapanga tarehe ya Mkutano Mkuu, mimi nafuata katiba na wala sing'ang'anii madaraka Yanga. Wale wote wanaotaka mimi na uongozi wangu tujiuzulu, basi waje kwenye mkutano mkuu," alisema bosi huyo.
Alisema utamaduni wa kuondoa madarakani uongozi kwa njia za mkato umepitwa na wakati. "Mambo ya kupinduana yamepitwa na wakati, dhambi hii ya kupinduana haitaishia kwa Nchunga peke yake itawatafuta wengine. Ifike mahali tubadilike tufanye kazi kwa kufuata katiba na siyo mazoea."
Aliongeza: "Wanaona sifai wafuate taratibu na watoe sababu za msingi siyo kwa vile tumepokwa pointi tatu ndiypo wanishinikize nijiuzulu hayo ni makosa ya soka.
Naomba itoshe kusema hivi...wale wote wanaodhani nitajiuzulu nafasi yangu, ni wazi wamepitwa na wakati. Sijiuzulu kwa sababu ya kikundi cha watu wachache, wanachama ndiyo wataamua."
Kuhusu madai ya kocha wa Yanga Kostadin Papic, Nchunga alisema: "Papic tunamuandalia malipo yake ambayo ni mishahara ya miezi miwili na muda wowote atalipwa.
Alikiri uongozi wake kutokuwa na ushirikiano na Papic kwa sababu kocha mwenyewe amekuwa akionyesha dharau mbele ya uongozi kwa kushindwa kuheshimu maagizo anayopewa.
"Sikiliza nikuambie, Papic hatuwezi kuwa naye tena tunamuandalia chake aondoke, kwanza hata wachezaji hawamtaki. Tulishawahi kumuonya kuhusu kutoa mambo ya ndani ya klabu kwenye vyombo vya habari lakini hakuwahi kutekeleza agizo hilo.
"Mechi ya Toto kule Mwanza alichangia kwa kiasi kikubwa tukapoteza mchezo. Kwanza alikataa kwenda na timu, baadaye akataka atumiwe tiketi aende Mwanza akatumiwa kufika tu wachezaji wakakosa raha.
Hata hivyo Nchunga hakutaka kuweka wazi mbadala wa Papic kwa madai kuwa Kamati ya Utendaji ndiyo itakayoamua hatima yake. Hata hivyo kuna taarifa klabu hiyo ipo kwenye mchakato wa kupitia vielelezo vya makocha kutoka Romania na Scotland.

source:mwananchi.co.tz

Wednesday, May 9, 2012

BREAKING NEWS! TBL YAINGIA MKATABA WA MIAKA 5 NA TFF


Tenga na Mgongolwa wakifurahia

Tenga na Mgongolwa

Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah kushoto, katikati mama Juliana Yassoda na kulia Robin

Wadau wa soka, Msafiri Mgoyi Mjumbe wa TFF, beki wa zamani Taifa Stars na Meneja wa timu hiyo, Leopold Mukebezi, Fred na kocha Joseph Kanakamfumu

Mwandishi wa Nipashe Somoe Ng'itu na kocha Jamhuri Kihwelo

Makamu wa kwanza wa rais wa TFF, Athumani Nyamlani na Mdau Salim


MUDA MCHACHE ULIOPITA KAMPUNI YA BIA NCHINI TANZANIA,TBL IMEINGIA MKATABA NA SHIRIKISHO LA MPIRA NCHINI TANZANIA TFF MKATABA WA MIAKA 5 WENYE THAMANI YA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI KUMI.

CHEMSHA BONGO! KITAJE HIKI KIKOSI NA ILIKUA MWAKA GANI ?

CHEMSHA BONGO! KITAJE HIKI KIKOSI NA KILIKUA CHA MWAKA GANI?

TANZANIA YAICHAPA LESOTHO 57-13 MICHUANO YA AFRIKA YA NETIBOLI

Kikosi cha timu ya Taifa ya Lesotho.Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete akisalimiana na wachezaji wa timu ya Taifa ya Netiboli ya Tanzania 'Taifa Queens'wakati ufunguzi wa mashindano ya Afrika yaliyoanza leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambapo Tanzania imeichapa Lesotho kwa 57-13. (Na Mpiga Picha wa Habari Mseto Blog.
Mashabiki wakifuatilia mchezo wa ufunguzi.Wanamuziki wa Bendi ya Mwenge Jazz wakitumbuiza wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Afrika ya Netiboli. Kikosi cha Taifa Queen'sMlinzi wa timu ya taifa ya Netiboli Tanzania, ‘Taifa Queens’, Lilian Sylidion (kushoto), akiwania mpira mbele ya wachezaji wa timu ya Lesotho katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Afrika uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Taifa Queen's imeshinda 57-13.
 

PAPISS DEMBA CISSE: NDOTO YANGU NI KUICHEZEA REAL MADRID - NAIPENDA TANGU UTOTONI

Papiss Demba Cisse amekiri kwamba ndoto yake ni kuichezea Real Madrid.

Straika huyo wa Newcastle na Senegal amefunga mabao 13 katika mechi 13 tangu alipokamilisha usajili wa £10million kutoka Freiburg mwezi January mwaka huu.

Lakini mshambuliaji huyo mwenye miaka 26 ameamua kukiri kwamba angependa kujiunga na mabingwa wapya wa La liga ikitokea nafasi ya kufanya hivyo siku moja.

Cisse alisema: "Ndoto yangu ya muda mrefu ni kuichezea klabu kubwa duniani na kushinda ubingwa wa ulaya. Nimekuwa naipenda Real Madrid tangu nilipokuwa mdogo.
Lakini nina furaha kwa sasa nipo Newcastle. Ni klabu kubwa - hata kama sio kama zilizvyo Manchester United au City."

BAADA YA KIPIGO KUTOKA MTANI: YANGA SASA YAANZA KUJENGA TIMU - OWEN KASULE WA UGANDA NJIANI KUTUA JANGWANI

Kiungo wa timu ya Taifa ya Uganda ‘The Cranes’, Owen Kasule ametua Dar es Salaam kufanya mazungumzo ya usajili na uongozi wa timu ya Yanga ya Dar es Salaam.

Kasule alifika Dar es Salaam juzi, ambapo jana alifanya mazungumzo ya muda mrefu na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga inayoongozwa na Salum Rupia kuhusiana na

kusajiliwa na timu hiyo kwa ajili ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.

Habari zilizopatikana ndani ya Yanga jana na kuthibitishwa na Rupia pamoja na Kasule zilieleza kuwa mazungumzo hayo yalikuwa mazuri, lakini kuna mambo ya kimsingi ambayo yaliwakwamisha kufikia mwafaka.


Rupia alikiri kuzungumza na Kasule jana, lakini alisema hawakusaini naye mkataba kwani amewaambia anaenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika timu ya Al Ahly ya Misri na kwamba kama atakwama huko atakuja kusaini Yanga.


Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Usajili alisema, Kasule amewaeleza kuwa ni rafiki wa karibu wa mshambuliaji Hamisi Kiiza wa Yanga na Emmanuel Okwi wa Simba ambao amesoma nao shule Uganda, hivyo wanapomjulisha habari za soka la Tanzania anatamani sana kuja kucheza.


“Ametwambia ana mapenzi sana na Yanga, hivyo naamini atakuja,” alisema Rupia. Okwi na Kiiza ni miongoni mwa wachezaji wa nje waliong’ara kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara iliyomalizika Jumapili.


Kwa upande wake Kasule akizungumza jana akiwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere kabla ya kurejea kwao, alikiri kuzungumza na Yanga, lakini akisema kuna mambo hawajafikia mwafaka.


“Mazungumzo yetu hayajaisha, nitakujulisha kwa kirefu zaidi, lakini kwa sasa hapana, elewa kwamba tumezungumza na Yanga,” alisema.


 

TAARIFA KUTOKA TFF!


VITUO LIGI YA TAIFA VYAPANGWA
Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imepanga vituo vitatu vya Ligi ya Taifa inayoshirikisha mabingwa wa mikoa kwa ajili ya ligi hiyo itakayoanza Mei 26 mwaka huu.

Kundi A lenye mabingwa wa mikoa ya Iringa (Kurugenzi Mufindi), Lindi (Lindi SC), Mbeya (Tenende FC), Morogoro (Mkamba Rangers), Mtwara (Ndanda SC), Pwani (Super Star), Rukwa (Mpanda Stars) na Ruvuma (Mighty Elephant) zitacheza mechi zake mjini Mtwara.

Mji wa Kigoma utakuwa mwenyeji wa mabingwa wa mikoa ya Dodoma (CDA), Kagera (Bandari FC), Kigoma (JKT Kanembwa), Mwanza (Pamba SC), Shinyanga (Mwadui SC), Singida (Aston Villa) na Tabora (Majimaji).

Kundi C lenye mabingwa wa mikoa ya Arusha (Flamingo SC), Dar es Salaam (Ashanti United ya Ilala, Red Coast ya Kinondoni na Tessema FC ya Temeke), Kilimanjaro (Forest FC), Manyara (Nangwa VTC), Mara (Polisi Mara) na Tanga (Korogwe United) watachezea mechi zao mkoani Mara.

Mwisho wa kuwasilisha fomu za usajili ni Mei 15 mwaka huu wakati kipindi cha pingamizi ni kuanzia Mei 16 hadi 22 mwaka huu. Mei 23 mwaka huu Kamati ya Mashindano ya TFF itakutana kupitia usajili huo. Wachezaji wanaosajiliwa ni wale wale waliochezea timu hizo katika ligi ya mkoa.

Mei 14 mwaka huu ni mwisho kwa mikoa yenye pingamizi kwa mabingwa wao kuwa wameshashughulikia rufani husika. Kamati ya Mashindano imeagiza kuwa kwa mikoa itakayoshindwa kufanya hivyo mpaka baada ya tarehe hiyo mabingwa wao hawatashiriki ligi hiyo.

Timu tano zitapanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao. Mshindi wa kwanza kutoka kila kundi na washindwa wawili bora (best losers) kutoka kundi A na C ambayo yana timu nane kila moja.

LIUNDA KUSIMAMIA MECHI LESOTHO
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limemteua Leslie Liunda wa Tanzania kuwa Kamishna wa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia 2014 Kanda ya Afrika kati ya Lesotho na Sudan itakayochezwa jijini Maseru.

Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili itachezwa kati ya Juni 1 na 3 mwaka huu. Lesotho na Sudan ziko kundi D pamoja na Ghana na Zambia.

Naye Hafidhi Ally ameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuwa Kamishna wa mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Dynamos FC ya Zimbabwe na Esperance Sportive ya Tunisia.

Mechi hiyo ya marudiano hatua ya 16 bora itachezwa Mei 13 mwaka huu kwenye Uwanja wa Rufaro jijini Harare. Esperance Sportive ilishinda mechi ya kwanza kwa mabao 6-0.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)


Powered by Sorecson : Creation de site internet


LIVERPOOL WAZIDI KUICHIMBIA KABURI LA CHELSEA KATIKA MICHUANO YA KIMATAIFA: WAITANDIKA 4-1


Liverpool 4-1 Chelsea All Goals & Highlights... by kofiswag

WAZEE WA YANGA WATOBOA UKWELI KUHUSU 5-0 ZA SIMBA: DENI LA PAPIC NA WACHEZAJI ZAIDI YA MILIONI 75 NDIO CHANZO KIKUBWA CHA KIPIGO DHIDI YA SIMBA.

Takribani zaidi ya masaa 48 baada ya klabu bingwa ya Tanzania bara na mwakilishi pekee wa Afrika mashariki na kati katika michuano ya kimataifa - Simba Sports Club kuifanyia mauaji ya kutisha mahasimu wao wa jadi klabu bingwa ya Afrika mashariki na kati Dar Young African kwa kuitandika bao tano kwa nunge - leo hii wazee wa klabu ya Yanga chini ya uongozi wa Ibrahimu Akilimali umeamua kuweka wazi sababu kuu zilizochangia mno kupokea kipigo kutoka kwa mnyama. 

Akizungumza leo hii katika mkutano wa waandishi wa habari Mzee Akilimali kwanza kabisa alikana madai ya uongozi wa Mwanasheria Lloyd Nchunga kwamba wazee hao waliihujumu klabu hiyo katika mchezo, pia akimuonya Nchunga asithubutu kumfukuza mchezaji hata mmoja kwa madai ya kuhusika kuihujumu Yanga.

Mzee Akilimali pia amesema Nchunga na uongozi wake ndio watu wa kulaumiwa kwa klabu hiyo kupokea kipigo cha aibu kutoka kwa watani wao, huku akitoa sababu zifuatazo.

1: MAANDALIZI
Timu ya Yanga iliingia kambini siku tatu kabla ya mchezo dhidi ya Simba huku wachezaji wakiwa hawana morali yoyote kutokana na kuwa walikuwa wakidai malimbikizo ya mishahara na bonasi za mechi za msimu mzima.

2: KOCHA PAPIC NA MADAI YA MIL. 24
Kwa muda mrefu kocha mkuu wa Yanga amekuwa akiudai uongozi wa Yanga shilingi milioni 24 za malimbikizo ya mshahara wake, hali iliyopelekea Mserbia huyo kutokuweza kuishi vizuri nchini na kupelekea kutokuwa na maelewano mazuri ya uongozi hivyo mwishowe kukosa kabisa utulivu wa akili wa kuweza kuitumika klabu kuelekea katika crucial moment ya msimu-hasa katika mechi ya marejeano na watani wao jadi.

3: MADAI YA BONASI ZA  SHILINGI 70,000 KWA KILA MCHEZAJI KWA MECHI - MSIMU MZIMA. (JUMLA YA PESA ZA BONASI ZA MSIMU MZIMA NI 52,780,000)
Uongozi wa Yanga umejiwekea utaratibu wa kutoa bonasi ya shilingi 70,000 kwa kila mchezaji kila baada ya mechi. Lakini katika hali ya kushangaza ndani ya kipindi chote cha Ligi kuu ya Tanzania bara uongozi wa bwana Lloyd Nchunga haukuwalipa hata shilingi ya bonasi za mechi zote za msimu wachezaji kama walivyokubaliana. Na pale alipoulizwa alikuwa akitoa ahadi tu.Kutokana na deni hili na kushindwa kutimiza ahadi Lloyd hakuwa hata akienda kuangalia kambi inaendaje wala kuwatia hamasa wachezaji kuelekea mchezo dhidi ya mahasimu wao wa jadi. Kiukweli hali ya kambi ilikuwa mbaya kifedha na kuwafanya wachezaji wa Yanga kutokuwa katika hali nzuri ya kiakili kuweza kuvaana na wapinzani wao bila kuambulia matokeo ya namna ile. Ilifikia hatua mpaka wachezaji wakaamua kwamba kabla ya mechi walipwe pesa zao au hawatoenda uwanjani kucheza na Simba - kitu ambacho kama wangekifanya wangeweza kushushwa daraja kama adhabu. Lakini wale wale watu ambao Bwana Lloyd amekuwa akiwatuhumu kwamba wanawarubuni wachezaji na pesa zao chafu ndio waliokuja kuokoa jahazi na kutoa kiasi cha shilingi 300,000 kwa kila mchezaji, ja,bo ambalo liliwafanya wachezaji kuingia uwanjani kucheza japo kwa shingo upande.
Sasa mchezaji akiwa kwenye hali waliyokuwa nayo wachezaji hawa halikuwa jambo la ajabu kuona wakiwa katika morali ya chini na kucheza ovyo kwenye mechi dhidi ya Simba." -Alisema Mzee Akilimali.

MASWALI
Ikiwa tuhuma hizi zilizotolewa na wazee wa Yanga ni kweli. Je ni wapi zilipokuwa zinaenda fedha nyingi zinazotolewa na mdhamini wa klabu hiyo Bia ya Kilimanjaro kila mwezi kwa madhumuni ya kulipa mishahara ya wachezaji, kocha na staffs wengine? Papic anadai mshahara wake.

Yanga ina chanzo kikubwa cha kukusanya mapato ya mlangoni tofauti na timu nyingi kwenye ligi kuu. Je yale mapato yote waliyokuwa wakiyakusanya ama kuyapata kutokana na viingilio vya mashabiki yamekwenda wapi kiasi cha kufikia kushindwa kuwalipa bonasi wachezaji?

Kwa undani zaidi wa stori hii sikiliza taarifa kutoka kwa wazee wa Yanga.

Tuesday, May 8, 2012

SIMBA KWENDA SUDAN NA NDEGE YA KUKODI

BAADA ya kumaliza Ligi Kuu bara kwa kishindo, Simba sasa inajipanga kwa safari ya kwenda Sudan kwa ajili ya mechi ya michuano ya kimataifa, na imepanga kuondoka kesho kwa ndege ya kukodi.

Simba iliifunga Yanga mabao 5-0 juzi katika mechi ya mwisho ya Ligi hiyo na hivyo kunogesha furaha za kutwaa ubingwa ilioutwaa tangu Ijumaa iliyopita.


Akizungumza Dar es Salaam jana, makamu mwenyekiti wa Simba Godfrey Nyange ‘Kaburu’
alisema kuwa timu yao itaondoka kesho kwa ndege ya kukodi kuelekea Sudan kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Kombe la shirikisho dhidi ya Al Ahly Shandy ya huko.

Katika mechi ya kwanza ya raundi ya tatu ya michuano hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa takriban wiki moja iliyopita, Simba ilishinda kwa mabao 3-0 na hivyo kuhitaji sare ama ushindi wa aina yoyote kwenye mechi hiyo ili kufuzu kwa hatua inayofuata.


Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage amesema kuwa mafanikio ya

timu yao msimu huu yanatokana na ushirikiano mzuri kati ya uongozi wa sasa, uongozi uliopita na marafiki wa klabu hiyo ‘Friends of Simba’.

Rage akizungumza baada ya ushindi wa juzi dhidi ya Yanga, alisema kuwa mshikamano

uliokuwepo ndani ya klabu hiyo kwa sasa ndio siri ya mafanikio ya timu yao.

Alisema kuwa siku zote panapokosekana mshikamano madhubuti miongoni mwa wanachama wa klabu hiyo lazima timu yao inakuwa haifanyi vizuri, lakini kwa sasa kwa kuwa wako pamoja ndio maana mafanikio yanaonekana

ANGALIA NAMNA DIDIER ZAKORA ALIVYOMLIPIZIA MCHEZAJI ALIYEMTOLEA MATUSI YA KIBAGUZI

Kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast anayeichezea klabu ya Trabzonspor Didier Zakora amefanya kitendo ambacho kimetafsiriwa kama kulipiza kisasi - kwa mchezaji kiungo wa Fenerbahce Emre Belozoglu - ambaye alimtuhumu kumtolea maneno ya kibaguzi Zakora mwanzoni mwa msimu.


Kutokea kipindi hicho kumekuwepo hakuna dalili yoyote ya kupatana kwa wawili hao kwa upande wa Zakora - ambaye nae juzi aliamua kulipa kisasi kwa namna ile ile lakini kwa ubaya zaidi.


Hii hapa ni video inayomuonyesha Zakora akikataa kushikana mikono na Emre, huku wachezaji wenzie wa Trabzonspor wakimchezea kindava zaidi Emre wakisaidiana na Didier mwenyewe.


Haki imetendeka? Nani anajua. Inaonekana kwamba Zakora alipata kadi ya njano tu kwa undava aliokuwa akimchezea Emre; labda tu-assume kwamba refa ameamua kuangalia matukio ya kabla ya mchezo baina ya wachezaji hao.

WAZEE WA YANGA WAANIKA SABABU ZA TIMU KUFANYA VIBAYA!

BONYEZA HAPA CHINI UWASIKILIZE.

SD TV: JE HUU NI UZALENDO ?

JERRY TEGETE AVALISHWA JEZI NA MASHABIKI WA SIMBA.




Mshambuliaji wa Yanga Jerry Tegete alivishwa jezi na mashabiki kwenye uwanja wa Taifa mara tu baada ya mchezo dhidi ya Yanga na Simba kumalizika.


JE HII INAASHIRIA NINI ?

SD TV : MABAO YOTE 5 YA SIMBA DHIDI YA YANGA

EURO 2012 COUNTDOWN: CARLES PUYOL KUIKOSA MICHUANO YA EURO

Kocha wa timu ya taifa ya Hispania Vicente Del Bosque amepokea taarifa mbaya kwamba katika kuelekea kwenye michuano ya EURO 2012 hatoweza kupata huduma za nahodha wake Carles Puyol kutokana na beki huyo kupata majeraha ya goti.

Puyol, 34, alicheza dakika zote 90 katika mechi kati ya Barcelona na Espanyol - lakini akapata maumivu makubwa ya goti baada ya mchezo.

Alifanya vipimo leo asubuhi ili kuweza kujua undani ya maumivu na majeraha yake - na Barcelona wametangaza kupitia website yao kwamba Puyol atafanyiwa upasuaji.

Puyol atapitiwa na visu jumamosi ijayo, na atakuwa nje ya dimba kwa takribani wiki sita.