Haruna Moshi Boban akiwa ndani ya kandambili uwanja wa taifa jana. |
Kiungo mshambuliaji wa timu ya Simba, Haruna Moshi ‘Boban’ jana alikuwa kivutio kwa mashabiki, wasindikizaji na hata baadhi ya wasafiri waliomuona wakati wakiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, kuelekea Sudan.
Simba inakwenda Sudan katika mchezo wa marudiano dhidi ya Al Ahli Shendi utakaopigwa Jumapili, huku ikiwa na mtaji wa ushindi wa mabao 3-0, iliyoupata kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Uvaaji wa Boban, ndio uliowavutia watu kumtizama, kutokana na kuvaa kama mtu asiyesafiri.
Boban alikuwa amevaa fulana, suruali ya kimichezo ‘trakisuti’ na kandambili, hivyo kusababisha watu kuvutika kumuangalia, huku baadhi yao wakibaki kujiuliza kuhusu vituko vya nyota huyo ambaye mashabiki humuita Balotteli wa Bongo.
Mchezaji huyo anafananishwa na mshambuliaji mahiri wa Italia, anayekipiga klabu ya Manchester City ya England, ambako mara kwa mara amekuwa akibeba vichwa vya habari katika magazeti ya England na Ulaya kutokana na vituko vyake.
Ukiondoa vituko hivyo vya uvaaji wa Boban, msafara wa watu 25 wakiwamo viongozi watano na wachezaji 20 wa timu hiyo waliondoka chini ya uongozi wa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Hussein Mwamba, majira ya saa 8:00 mchana
Nothing strange on that. A plane is just another means of travelling from point A to B. How one dresses doesn't matter except to simple minds.
ReplyDeleteBoban knows the agony of airport security checks - it's so annoying when one is asked to remove shoes for security scanning before boarding a plane in some airports including JNIA (Dar). Some air companies even distribute socks and sandals aboard flights to give confort to their passengers.
Sofolks, this is normal and not a big deal!
Mkuu huo usumbufu wa security ni dar air port tu?tukiangalia wenzetu wa nchi nyingine hata kenya hapo wanavaa vizuri,angalia man u,arsenal wakishuka kwenye mabasi yao utapenda,mpira ni nidhamu,usafi pia.tunatakiwa kumfundisha sio kusifia tu.
DeleteWote tunajua hayo ya usumbufu airport....cha muhimu ni kuwa wachezaji wengi wa kitanzania na vilabu vyao hawana dress code, na kutojua umuhimu wa kuwa ROLE MODELS!! in short jamaa anazidi kutafsiliwa kuwa ni 'mhuni' tu. Naomba tusome alama za nyakati!!
ReplyDelete