Search This Blog

Wednesday, May 9, 2012

WAZEE WA YANGA WATOBOA UKWELI KUHUSU 5-0 ZA SIMBA: DENI LA PAPIC NA WACHEZAJI ZAIDI YA MILIONI 75 NDIO CHANZO KIKUBWA CHA KIPIGO DHIDI YA SIMBA.

Takribani zaidi ya masaa 48 baada ya klabu bingwa ya Tanzania bara na mwakilishi pekee wa Afrika mashariki na kati katika michuano ya kimataifa - Simba Sports Club kuifanyia mauaji ya kutisha mahasimu wao wa jadi klabu bingwa ya Afrika mashariki na kati Dar Young African kwa kuitandika bao tano kwa nunge - leo hii wazee wa klabu ya Yanga chini ya uongozi wa Ibrahimu Akilimali umeamua kuweka wazi sababu kuu zilizochangia mno kupokea kipigo kutoka kwa mnyama. 

Akizungumza leo hii katika mkutano wa waandishi wa habari Mzee Akilimali kwanza kabisa alikana madai ya uongozi wa Mwanasheria Lloyd Nchunga kwamba wazee hao waliihujumu klabu hiyo katika mchezo, pia akimuonya Nchunga asithubutu kumfukuza mchezaji hata mmoja kwa madai ya kuhusika kuihujumu Yanga.

Mzee Akilimali pia amesema Nchunga na uongozi wake ndio watu wa kulaumiwa kwa klabu hiyo kupokea kipigo cha aibu kutoka kwa watani wao, huku akitoa sababu zifuatazo.

1: MAANDALIZI
Timu ya Yanga iliingia kambini siku tatu kabla ya mchezo dhidi ya Simba huku wachezaji wakiwa hawana morali yoyote kutokana na kuwa walikuwa wakidai malimbikizo ya mishahara na bonasi za mechi za msimu mzima.

2: KOCHA PAPIC NA MADAI YA MIL. 24
Kwa muda mrefu kocha mkuu wa Yanga amekuwa akiudai uongozi wa Yanga shilingi milioni 24 za malimbikizo ya mshahara wake, hali iliyopelekea Mserbia huyo kutokuweza kuishi vizuri nchini na kupelekea kutokuwa na maelewano mazuri ya uongozi hivyo mwishowe kukosa kabisa utulivu wa akili wa kuweza kuitumika klabu kuelekea katika crucial moment ya msimu-hasa katika mechi ya marejeano na watani wao jadi.

3: MADAI YA BONASI ZA  SHILINGI 70,000 KWA KILA MCHEZAJI KWA MECHI - MSIMU MZIMA. (JUMLA YA PESA ZA BONASI ZA MSIMU MZIMA NI 52,780,000)
Uongozi wa Yanga umejiwekea utaratibu wa kutoa bonasi ya shilingi 70,000 kwa kila mchezaji kila baada ya mechi. Lakini katika hali ya kushangaza ndani ya kipindi chote cha Ligi kuu ya Tanzania bara uongozi wa bwana Lloyd Nchunga haukuwalipa hata shilingi ya bonasi za mechi zote za msimu wachezaji kama walivyokubaliana. Na pale alipoulizwa alikuwa akitoa ahadi tu.Kutokana na deni hili na kushindwa kutimiza ahadi Lloyd hakuwa hata akienda kuangalia kambi inaendaje wala kuwatia hamasa wachezaji kuelekea mchezo dhidi ya mahasimu wao wa jadi. Kiukweli hali ya kambi ilikuwa mbaya kifedha na kuwafanya wachezaji wa Yanga kutokuwa katika hali nzuri ya kiakili kuweza kuvaana na wapinzani wao bila kuambulia matokeo ya namna ile. Ilifikia hatua mpaka wachezaji wakaamua kwamba kabla ya mechi walipwe pesa zao au hawatoenda uwanjani kucheza na Simba - kitu ambacho kama wangekifanya wangeweza kushushwa daraja kama adhabu. Lakini wale wale watu ambao Bwana Lloyd amekuwa akiwatuhumu kwamba wanawarubuni wachezaji na pesa zao chafu ndio waliokuja kuokoa jahazi na kutoa kiasi cha shilingi 300,000 kwa kila mchezaji, ja,bo ambalo liliwafanya wachezaji kuingia uwanjani kucheza japo kwa shingo upande.
Sasa mchezaji akiwa kwenye hali waliyokuwa nayo wachezaji hawa halikuwa jambo la ajabu kuona wakiwa katika morali ya chini na kucheza ovyo kwenye mechi dhidi ya Simba." -Alisema Mzee Akilimali.

MASWALI
Ikiwa tuhuma hizi zilizotolewa na wazee wa Yanga ni kweli. Je ni wapi zilipokuwa zinaenda fedha nyingi zinazotolewa na mdhamini wa klabu hiyo Bia ya Kilimanjaro kila mwezi kwa madhumuni ya kulipa mishahara ya wachezaji, kocha na staffs wengine? Papic anadai mshahara wake.

Yanga ina chanzo kikubwa cha kukusanya mapato ya mlangoni tofauti na timu nyingi kwenye ligi kuu. Je yale mapato yote waliyokuwa wakiyakusanya ama kuyapata kutokana na viingilio vya mashabiki yamekwenda wapi kiasi cha kufikia kushindwa kuwalipa bonasi wachezaji?

Kwa undani zaidi wa stori hii sikiliza taarifa kutoka kwa wazee wa Yanga.

2 comments:

  1. Nakumbuka yanga iliwahi fungwa moro na simba wachezaji nsajigwa na mapunda ivo walisimamishwa kwa tuhuma za hujuma,yanga imewahi fukuza karibu wachezaji wote baada ya kufungwa na simba 4-1,hatukuwahi sikia wazee wakizuia wasifungiwe,iweje leo watie mkwara,wazee wamehusika wakishirikiana na yanga maslahi kuhujuma na wachezaji wakaingia mtego wa pesa,leo wamemfanyia nchunga,kesho wanaweza mfanyia kifukwe,dawa ni kutiimua na kubaki na waadiilifu tu

    ReplyDelete
  2. tungekua hatujaona mpira ungetuambia huo upuuzi wa wazee wa Yanga,kiukweli Simba wako onfire na yanga kagongwa vizuri tu sasa hiz sababu zisizo za kimpira hazina nafasi hapa,walizidiwa tu technically hasa beki yao ilikua imepoteana na simba alichezesha viungo wengi so katikat yanga wakawa outnumbered,nyinyi watu wa media nashangaa kuwaentatain wazee ambao ndo chanzo cha migogoro,wanamchukia NchungA Kwakua hawapi pesa kama wengine
    chela wa dom

    ReplyDelete