WAKATI uongozi wa Yanga ukipuuza shinikizo zito la kutakiwa kujiuzulu toka baadhi ya wanachama wa klabu hiyo kwa madai ya kuwa kiini cha kipigo cha aibu toka Simba Jumapili iliyopita, wachezaji tisa timu hiyo wamekalia kuti kavu baada ya mikataba yao kufikia.
Wachezaji hao wako hatarini kutemwa kwa sababu kuna uwezekano mdogo, au usiwapo kabisa kusaini mikataba mipya, taarifa za ndani toka klabu hiyo ya Jangwani zimedai
Ni pamoja na Shamte Ally, Jerry Tegete, Chacha Marwa, Mohamed Mbegu, Abuu Ubwa, Zuberi Ubwa, Kigi Makasi, Shadrack Nsajigwa na Athuman Idd 'Chuji'.
Ni pamoja na Shamte Ally, Jerry Tegete, Chacha Marwa, Mohamed Mbegu, Abuu Ubwa, Zuberi Ubwa, Kigi Makasi, Shadrack Nsajigwa na Athuman Idd 'Chuji'.
Tegete anahusishwa kwenda Simba, wakati Nsajigwa anatuhumiwa kucheza chini ya kiwango katika mechi yao dhidi ya Simba, ambapo alisababisha penalti mbili kati ya tatu na kuwapa mahasimu wao ushindi wa mabao 5-0.
"Wachezaji wengi wamemaliza mikataba yao, wapo baadhi huenda wakaongezewa kama Chuji, lakini wengine watatemwa akiwamo Shamte ambaye hakuna ubishi hatarudi Jangwani msimu ujao," alisema mtoa habari.
Alisema wachezaji Nurdin Bakari, Hamis Kiiza, Kenneth Asamoah bado wana mkataba wa mwaka mmoja, wakati Yaw Berko na Davis Mwape mikataba yao itamalizika Novemba mwaka huu.
Alisema wachezaji Nurdin Bakari, Hamis Kiiza, Kenneth Asamoah bado wana mkataba wa mwaka mmoja, wakati Yaw Berko na Davis Mwape mikataba yao itamalizika Novemba mwaka huu.
"Uongozi umeshaanza kuzungumza na Berko kuangalia uwezekano wa kuongeza mkataba wake, lakini Mwape hatacheza Yanga msimu ujao mara baada ya mkataba wake kumalizika," alisema mpashaji huyo habari.
Jumamosi wiki hii Kamati ya Utendaji itakutana, na moja ya mambo watakayozungumza ni ushiriki wa Ligi Kuu, changamoto zilizokuwepo na kujadili wachezaji watakaochwa na wanaostahili kubaki.
Jumamosi wiki hii Kamati ya Utendaji itakutana, na moja ya mambo watakayozungumza ni ushiriki wa Ligi Kuu, changamoto zilizokuwepo na kujadili wachezaji watakaochwa na wanaostahili kubaki.
"Kikubwa kinachoangaliwa ni nidhamu wa wachezaji ndani na nje ya uwanja pamoja na kiwango, na pia kuna wachezaji wengine watahama kwenda timu nyingine haya yote yataangaliwa."
Alisema ajenda nyingine kwenye kikao hicho ni kupanga tarehe ya Mkutano Mkuu wa wanachama pamoja na vuguvugu la mgogoro lililopo ndani ya klabu hiyo.
Alisema ajenda nyingine kwenye kikao hicho ni kupanga tarehe ya Mkutano Mkuu wa wanachama pamoja na vuguvugu la mgogoro lililopo ndani ya klabu hiyo.
Mwenyekiti wa Yanga Llody Nchunga alisema masuala yote yanayohusu usajili wa wachezaji watawekwa wazi wiki ijayo mara baada ya kikao chao cha Kamati ya Utendaji.
Aidha, kuhusu wachezaji wanaodai, Nchunga alisema ni wale waliongezewa mikataba ambao ni Nurdin Bakari na Nadir Haroub.
Aidha, kuhusu wachezaji wanaodai, Nchunga alisema ni wale waliongezewa mikataba ambao ni Nurdin Bakari na Nadir Haroub.
"Wachezaji wanaodai fedha za usajili ni wachache tena waliongezewa mikataba kipindi cha uongozi uliopita na hata hivyo fedha hizo wanatakiwa walipwe msimu ujao kwa kuwa ndiyo watakaoanza kuutumikia," alisema Nchunga na kuwataja wachezaji hao kuwa ni Nurdin na Nadir.
"Nawashangaa wazee wetu wanavyosema wachezaji wanadai Sh127 milioni. Hivi hawa wazee ni wahasibu? Wamepata wapi hesabu hizi, napenda kuwaambia kuwa hatudaiwi kiasi hicho," alisema.
Kuhusu shinikizo la kutakiwa kujiuzulu, Nchunga alisema hawezi kufanya hivyo kwa shinikizo la watu wachache wakati Yanga ni timu ya wanachama.
Kuhusu shinikizo la kutakiwa kujiuzulu, Nchunga alisema hawezi kufanya hivyo kwa shinikizo la watu wachache wakati Yanga ni timu ya wanachama.
"Mimi nilichaguliwa na wananchana wa Yanga, wao ndiyo wanaweza kunitaka nijiuzulu tena kupitia Mkutano Mkuu wa Klabu. Tunaendeshwa na katiba na siyo kelele za vikundi vya watu. Hatima yangu itaamuliwa na Wanayanga, siyo kikundi.
"Kamati ya Utendaji itapanga tarehe ya Mkutano Mkuu, mimi nafuata katiba na wala sing'ang'anii madaraka Yanga. Wale wote wanaotaka mimi na uongozi wangu tujiuzulu, basi waje kwenye mkutano mkuu," alisema bosi huyo.
Alisema utamaduni wa kuondoa madarakani uongozi kwa njia za mkato umepitwa na wakati. "Mambo ya kupinduana yamepitwa na wakati, dhambi hii ya kupinduana haitaishia kwa Nchunga peke yake itawatafuta wengine. Ifike mahali tubadilike tufanye kazi kwa kufuata katiba na siyo mazoea."
Aliongeza: "Wanaona sifai wafuate taratibu na watoe sababu za msingi siyo kwa vile tumepokwa pointi tatu ndiypo wanishinikize nijiuzulu hayo ni makosa ya soka.
Naomba itoshe kusema hivi...wale wote wanaodhani nitajiuzulu nafasi yangu, ni wazi wamepitwa na wakati. Sijiuzulu kwa sababu ya kikundi cha watu wachache, wanachama ndiyo wataamua."
Kuhusu madai ya kocha wa Yanga Kostadin Papic, Nchunga alisema: "Papic tunamuandalia malipo yake ambayo ni mishahara ya miezi miwili na muda wowote atalipwa.
Alikiri uongozi wake kutokuwa na ushirikiano na Papic kwa sababu kocha mwenyewe amekuwa akionyesha dharau mbele ya uongozi kwa kushindwa kuheshimu maagizo anayopewa.
"Sikiliza nikuambie, Papic hatuwezi kuwa naye tena tunamuandalia chake aondoke, kwanza hata wachezaji hawamtaki. Tulishawahi kumuonya kuhusu kutoa mambo ya ndani ya klabu kwenye vyombo vya habari lakini hakuwahi kutekeleza agizo hilo.
"Mechi ya Toto kule Mwanza alichangia kwa kiasi kikubwa tukapoteza mchezo. Kwanza alikataa kwenda na timu, baadaye akataka atumiwe tiketi aende Mwanza akatumiwa kufika tu wachezaji wakakosa raha.
Hata hivyo Nchunga hakutaka kuweka wazi mbadala wa Papic kwa madai kuwa Kamati ya Utendaji ndiyo itakayoamua hatima yake. Hata hivyo kuna taarifa klabu hiyo ipo kwenye mchakato wa kupitia vielelezo vya makocha kutoka Romania na Scotland.
source:mwananchi.co.tz
Najua kwa hali hii watu wengi sana watanishangaa ila kwa moyo mmoja niko pamoja na bwana Lloyd lazima watanzania tujifunze kwa sababu huu ujinga wa kila siku kuna watu wanakaa nje ya timu chaguzi zikifanyika wao hawataki kugombea wanasubiri wengine waingie wao waanzishe vurugu,kuna timu zimeshafungwa na kupata matokeo mabovu zaidi ya Yanga kwa mfano Liverpool,Chelsea,Gor Mahia,Kaizer Chiefs,Marseille lakini maisha yanaendelea na wanajipanga upya kwani hizo timu hawana wazee?hawa wazee wa Yanga ni wahuni na wanatumiwa na watu ambao wako nyuma yao,viongozi wa Yanga lazima waonyeshe ujasiri sio kuyumbishwa na wajinga wachache'
ReplyDeleteU're right my friend.
ReplyDeleteNiliandika juzi na leo narudia kuwa, kilichofanywa na kikundi cha wazee hao (wanaojifanya wazee wa Yanga) ni kiini macho cha mbinu ovu za kujipatia fedha wagange njaa zao. Tunawafahamu wazee hao. Wengi ni retirees, ama kwa kuondoka katika ajira rasmi au kwa vile wameishiwa nguvu za kufanya kazi zilizokuwa zinawaingizia kipato.
Walichofanya ni kubuni mbinu ya kwenda kwa matajiri (hasa wale wenye lengo la kuingia klabuni kwa faida zao) wakawalilia kwa ahadi kuwa wakikabidhiwa timu wangepatiwa fedha za maandalizi (maandalizi feki) ya kuifunga Simba.
Huo ni upuuzi. Kama kweli genge hili la wazee wahuni lingekuwa na nia njema na Yanga wangeisaidia timu kwa kuwahamasisha wachezaji, kisha mashauriano yaje baada ya hapo, lakini kuihujumu timu ifungwe eti ili kuwachukiza wana-Yanga wautimue uongozi halali ni mbinu iliyozeeka kuliko hao wazee wenyewe.
Ndugu zanguni lazima waTZ hasa wapenda michezo tubadilike. Tunahitaji viongozi wenye kuona mbali wenye weledi, msukumo, mikakati na nguvu za kuiendesha klabu kwa mbinu za kisasa zaidi kama wafanyavyo Rage na wenzake pale Simba.
Namshukuru sana Shaffih na timu ya Sports Xtra pale Clouds FM kwa kutoelemea upande wowote katika zogo hili klabuni Yanga na wao kupigania kutoa elimu zaidi kwa wapenda michezo wote. Lakini kuna timu ya watangazaji katika Redio One, ikiongozwa na Maulid Kitenge, na Katanga nawashauri wabadilike na kuacha unafiki wa kujifanya wanataka Yanga iongozwe kwa utulivu huku kila siku wakitumia zaidi ya dk.20 za kipindi cha Spoti Leo kuendeleza uchochezi kwa kuwananga Nchunga na Uongozi wote wa Yanga. Kitenge na Katanga badilikeni, mbinu zenu na propaganda zenu haziui Yanga tu bali mchezo wote wa soka nchini.
Swalle gfs - Kilombero
ukituliza akili yako,ukautumikisha ubongo wako,ukaacha kupepesa macho,kung'ata maneno wala kutikisa masikio yako-utagundua spoti leo ya radio one haina mlengo wowote unaoegemea,kauli mbiu yetu ni moja tu-TUNATAKA KUONA MPIRA UNACHEZWA NA SIO MIGOGORO,sasa kama kuna kiongozi,mtu,watu au kikundi kinaonekana kutaka kuvuruga hii kauli mbiu yet,TUNAMNYOA NYWELE BILA KUPEPESA.
ReplyDeletehahahahahahaaaaaaaaaa,hide iz one of way 2 fear something,mambo yawe hadharani ndio mpango mzima!!!!!!!!!!!!!!!
ReplyDelete