YAYA TOURE AKISUKUMA GOZI HUKU AKIWA PEKUPEKU NCHINI KWAO IVEORY COAST KATIKA KLABU YA ASEC MEMOSAC. |
Yaya Toure aliwasili Ubelgiji akiwa hana chochote bali kipaji chake. Hiyo ndio kumbukumbu waliyokuwa nayo juu ya Toure pale Beveren: hakuwa hata na pea za viatu vya kuchezea soka.
Nyingine ni kwamba hakuwa na tabia ya kuamka mapema asubuhi; alikuwa anakula kama farasi na kunywa kama samaki, soda ya fanta na sio pombe.
Yaya Toure alitua Beveren, mji mdogo uliopo magharibi mwa Antwerp, akiwa tu ndio anafikisha miaka 18, akiwa amelelewa kwa kuongea lugha ya kifaransa katika mitaa ya Abidjan, Ivory Coast. Alikuwa na pesa kidogo sana, pair moja ya viatu na nguo chache.
Lakini pale Flanders, wanasema hata akiwa mdogo, kijana ambaye ameshinda Champions league na Barcelona na ambaye msimu huu amekuwa moyo wa timu ya Manchester City alikuwa mtu ambaye anapenda kuwa yeye kitu ambacho kilimtofautisha na wenzake.
Leo hii Toure anaonekana na kung'ara - moja ya viungo bora kwenye soka, mwenye uzoefu na akiwa tayari kuiongoza Manchester City kushinda taji lake kwanza baada ya miaka 44 jumapili ijayo, ambayo itakuwa ndio siku yake ya kuzaliwa akitimiza miaka 29. Tangu zamani Yaya alionekana kuwa mtu ambaye atakuja kufanikiwa.
Nyingine ni kwamba hakuwa na tabia ya kuamka mapema asubuhi; alikuwa anakula kama farasi na kunywa kama samaki, soda ya fanta na sio pombe.
Yaya Toure alitua Beveren, mji mdogo uliopo magharibi mwa Antwerp, akiwa tu ndio anafikisha miaka 18, akiwa amelelewa kwa kuongea lugha ya kifaransa katika mitaa ya Abidjan, Ivory Coast. Alikuwa na pesa kidogo sana, pair moja ya viatu na nguo chache.
Lakini pale Flanders, wanasema hata akiwa mdogo, kijana ambaye ameshinda Champions league na Barcelona na ambaye msimu huu amekuwa moyo wa timu ya Manchester City alikuwa mtu ambaye anapenda kuwa yeye kitu ambacho kilimtofautisha na wenzake.
Leo hii Toure anaonekana na kung'ara - moja ya viungo bora kwenye soka, mwenye uzoefu na akiwa tayari kuiongoza Manchester City kushinda taji lake kwanza baada ya miaka 44 jumapili ijayo, ambayo itakuwa ndio siku yake ya kuzaliwa akitimiza miaka 29. Tangu zamani Yaya alionekana kuwa mtu ambaye atakuja kufanikiwa.
YAYA ALIYEZUNGUSHIWA KIDUARA ALIPOKUWA UBELGIJI PALE BEVEREN |
"Nilikuwa nawachukua kila siku, Yaya na rafiki zake wawili,' anasema Anour Bou-Sfia, ambaye alicheza na Toure pale Beveren. 'Yaya alikuwa na tabia fulanihivi - alikuwa anajua atakuja kufanikiwa na kuwa bora.
"Mahali walipoishi ndio ilikuwa njia yangu ya kwenda uwanjani na kulikuwa na siku nyingi tu ambazo ilibidi Yaya tuwe tunamuamsha kwenda mazoezini, lakini yeye alikuwa tofauti ukilinganisha na wengine - Yaya alikuwa na akili sana na aliyepevuka. Wengine wote walikuwa na mentallity za kijinga za vijana kutoak afrika ambao ghafla tu walijikuta wapo ulaya. Yaya hakuwa anapenda camera, magazeti, alikuwa na aibu sana. Alikuwa hapendi kutoka kama wenzake. Alikuwa muislamu kamili. Mimi ni mmoroco, ni muislam.
"Muda mwingine tukiwa uwanjani angeweza kufanya vitu ambavyo vilitushangaza wote. Nilicheza nae kwa misimu miwili na nusu lakini kwa muda wote huo nilikuwa bench. Hivyo nilikuwa namuangalia, niliwaleta rafiki zangu kuja tu kumuangalia alikuwa mchezaji mzuri sana.
"Angalia goli la kwanza alilowafunga Newcastle jumapili, alilifanya lionekane rahisi. Angalia nmna alivyofunga. Alishinda Champions league pale Barcelona akicheza pembeni ya Gerard Pique katika safu ya ulinzi. Alilifanya suala lile lionekane rahisi.
"Nafikiri alikuwa kama anaboa muda mwingine alipokuwa akiichezea Barcelona. Ilikuwa rahisi sana. Hata Beveren alikuwa hivyo - kule ufaransa wanamuita nonchalance.
"Yaya hakuwa mtu anayependa kujionyesha. Nilikuwa mtafsiri lugha wao, kuwapeleka supermarket, kuwapeleka kwenda kununua viatu kwa sababu hawakuwa na viatu."
Career ya Yaya Toure ilipitita katika njia ngumu. Alienda Beveren mwaka 2001, ikiwa ni sehemu ya majaribio nchini Ubelgiji - wazo la mchezaji wa zamani wa Ufaransa Jean-Marc Guillou, mtu wa karibu sana na Arsene Wenger.
Guillou amejenga academy nchini Ivoery Coast - ambapo kaka yake Yaya, Kolo Toure ndio alitokea hapo na kwenda moja kwa moja mpaka Arsenal.
Pale KSK Beveren, Guillou aliipata timu ndogo iliyokuwa ikihitaji uwekezaji. Akainunua na msaada kutoka kutoka Arsenal.
Sheria nzuri za Ubelgiji zilikuwa na manufaa kwa Guilloi ambaye sasa kashayapatia maisha. Ada yoyote ya uhamisho kwa wachezaji watakaouzwa kutoka klabu hiyo - ilikuwa inagawanywa pasu kwa pasu. Guillou na Beveren.
YAYA TOURE NDANI YA UZI THE GUNNERS AMBAPO ALIFANYA MAJARIBIO. |
Mwaka 2003, kutokana na uhusiano uliopo kati ya Arsenal na Guillou pamoja Beveren Yaya Toure akapelekwa London kwa majaribio ya muda mfupi. Japokuwa sasa anafananishwa na Patrick Vieira - haikuwa hivyo mwanzoni.
Toure alicheza mechi ya pre-season dhidi ya Barnet lakini dimba la juu. Aidha Toure hakumshawishi au Wenger tayari alikuwa na mbadala wake, kijana kutoka Ivory Coast akarudi Ubelgiji. Wote wawili Wenger na Toure wameshasemakulikuwa na matatizo juu ya passport.
'Labda alikuwa bado hajakaa sawa,' alisema Martin Keown, ambaye bado alikuwa Arsenal kipindi hicho.
"Kulikuwa na attention kubwa sana juu yake kwa sababu alikuwa mdogo wake Kolo, lakini Yaya hakuwa na mwezi wa mazoezi wa pre-season kama wengine . Labda mwili wake bado haukuwa sawa.
"Lakini pamoja na yoteYaya aliacha gumzo. Yeye na kaka yake ni wakarimu na watu wazuri sana. Na wanapenda mpira - tumekuwa tukisikia kuhusu watoto wa mzee Neville walivyo, ndugu hawa wa Toure nao wapo hivyo hivyo."
Aliporudi Ubelgiji Toure hakukataa tamaa aliendeleza juhudi ya kujifunzana mazoezi na hata tabia zake hazikubadilika.
Ingawa katika mahojiano aliyoyafanya na Dailymail Toure anasema alifanya mambo mengi ya kijinga alipokuwa Beveren lakini hakuna mtu anakumbuka. lakini Danny Stuer mkufunzi wa mazoezi ya viungo anasema tofauti: "Yaya alikuwa mtu wa maadili, tofauti sana, muda wote mkimya na mtu anayependa kufanya kazi. Alikuwa anakuja gym na alikuwa proffessional tangu mwanzo - wengine wote hawakuwa hivyo - kwao gym ilikuwa mchezo mtu.
"Baada ya mechi Yaya hakuwa akitoka kwenda kunywa mabia kama wenzie. Alirudi nyumbani na kubaki kupumzika huku akiangalia TV, hasa soka na soka zaidi."
"Mwanzoni alikuwa akiishi na wenzie lakini wenzake walipokuwa wanatoka usiku na kurudi wamechelewahuanza kumsumbua. Hivyo mwishowe akaomba aishi peke yake, na klabu ikafanikisha hilo.
"Labda alienda kwenye party nyuma ya mgongo wangu kama wengine- lakini kwa kile ninachojua Yaya alikuwa tofauti"
Pale Beveren walikuwa wanajua wachezaji wa kiafrika walikuwa wakienda Liege au Brussels kwa ajili ya kupati.
Baada ya misimu miwili na nusu na mechi 70 akiwa na Beveren, Toure aliuzwa kwa fedha ya ubelgiji millioni 2.
Mahasimuwawili wa Ubelgiji, Anderlecht na Club Bruges, wote walikuwa wakimtaka Toure, lakini sio kwa bei hiyo. Hivyo akiwa na miaka 20, akahamia Ukraine kwenye timu ya daraja ya pili ya Donetsk, Metalurh. Haikuwa sehemu nzuri kwa mtu ambaye alikuwa na ndoto ya kuwa star wa dunia, lakini Toure anasema uhamisho huo ulikuwa mzuri kwake. "Soka ni kazi; nilijifunza hivyo Ukraine."
Baada ya muda kidogo -akahamia Ugiriki na kujiunga na Olympiakos. Club Bruges inaweza kuwa ilikataa kulipa €2m lakini manager wao, mnorway Trond Sollied, ambaye alijiunga na Olympiakos akamsaini Toure na kushinda kombe la Ugiriki. "Niliona almasi, kitu fulani special kwake, alipokuwa pale Beveren," anasema Sollied. "Hakuwa na nguvu alizonazo sasa, au kufunga magoli mengi lakini alikuwa na kitu extra ndani ya timu.
"Kumpata na kumleta Ugiriki ilikuwa ni vizuri. Kimwili alikuwa amepevuka, alikuwa yupo vizuri kuliko alivyokuwa Ukraine. Tulijua hatutoweza kukaa nae sana. Alikuwa na uhakika sana kuhusu alivyo. Nafikiri kaka yake alimsaidia. Walikuwa wakibadilishana uzoefu."
Baada ya kombe la dunia la mwaka 2006, AS Monaco, timu ya zamani ya Wenger, ilimnunua Toure kwa ada ya £4million, ingawakulikuwa na kutokuelewana kidogo kule Donetsk kuhusu mkataba wake.
YAYA TOURE ALIPOKUWA BARCELONA. |
Lakini baada ya msimu mmoja tu nchini Ufaransa, Barcelona wakamsaini. Yaya Toure akaenda Catalunya ambako alipata majina mengi kamavile "Colossus - yaaani sanamu kubwa sana la mtu", wengine wakamuita "Treni " lakini Pep Guardiola alimuelezea Yaya kama "Diesel Player" - inachukua muda muda mrefu kwenda anapopataka lakini hasimami.
Huyu ndio Yaya Toure ambaye ama kwa hakika ndio kiungo bora kabisa katika msimu huu wa Premier League ambayo inaisha Jumapili huku mwenyewe akitimiza miaka 29 siku hiyo.
Asante kwa kutupa historia yake
ReplyDeletehivi ndivyo vitu ambayo tunahitaji kaka kutuinspire kuweza kufikia malengo, tunaomba uwe unatuekea story kama hizi mara kwa mara
ReplyDeletepia tunaomba utuekee ile speech ya legend wa zambia mzee wa ponga liwewe
ReplyDeletehapo ndipo wachezaji wa bongo wajifunze sio m2 anaenda sweden mwaka 1 anarud mara kodi kubwa wakati unasain mkataba ukusoma masuala ya kodi yatakuaje
ReplyDeleteje tanzania tunaweza kuwa na watu kama hawa kama mchezaji anapata nafasi na kuipuuzamfano haruna moshi bobani heti ndo wanajiita profesheno wakati wanachezea vilabu vinavyoshikwa na wanafiki kama watanzania wasio na uzalendo hata kidogo yaani mara kumi bora kocha wa twiga star mi binafsi nimempenda maana ameonesha hata timu ya taifa ya wanaume anaiweza je ndo ksema kwa sababu anawafundisha wanawake wanampa mambo ya paziani ukweli ni kwamba tusipobadilika tutaishia kushiriki ligi ya vodacom ambayo hata ITV,STAR TV,TBC na televisheni nyingine hazioneshi mechi yeyote tuko nyuma ya soka.wazalendo wapewe nafasi kuisaidi tanzania.
ReplyDeletehapa umefanya kazi ndugu yangu unastahili kupongezwa hongera sana taarifa imesimama.
ReplyDelete