Search This Blog

Thursday, February 2, 2012

MADEMU NA WAKE WA WANASOKA WENYE MVUTO DUNIANI

Hakuna ubishi Cristiano Ronaldo ni moto uwanjani na anatajwa kama mmoja ya   wachezaji bora wa dunia. Hivyo mchezaji bora wa dunia mtu ambaye ni nembo ya soka, hivyo anahitaji kuwa vitu bora kimojawapo ni mwanamke, huyu hapa mtot wa kirusi anaitwa Irina Shyk ni kweli kabisa anastahili kuwa demu wa mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo. Irina Shyk ndio anatufungia listi yetu ya wasichana ambao wana mvuto wamewahi ama wapo katika mahusiano na wanasoka.

Antonella Ruccozzo, binti wa kiaregentina ndiye aliuteka moyo wa mwanadamu ambaye inasemekana yupo tofauti na wacheza soka wote kwa uwezo wake wa kulisakata kabumbu. Huyu mtoto ni ndiye usingizi wa Lionel Messi - mchezaji bora wa dunia kwa sasa.


Anaitwa Aida Yespica, alikuwa galfriend wa mcheza soka Matteo Ferrari ambaye alizaa nae mtoto. Kwa sasa huu ni usiungizi wa moja ya viiungo bora duniani Mesut Ozil wa Real Madrid.


Ana mtoto mmoja na moja ya kiungo bora wa ulinzi kuwahi kutokea katika soka la karibuni Claude Makelele. Anaitwa Noemie Lenoir, unaambiwa si tu Makelel alikuwa anajua kuzuia mashambulizi ya uwanjani tu kwani huko Ufaransa mtoto anatingisha hatari lakini Makelele anawatuliza mapedeshee wote wanaomsumbua mama watoto wake.




Mke wa mchezaji wa Tottenham Hotspur Rafael Van Der Vaart ni hatari. Anaitwa Sylivie Van Der Vaart.

Moja kati wengi waliotekwa na mtoto wa Kireno Cristiano Ronaldo. Letizia Filippi moja ya washiriki wa Miss Italy mwaka 2007.

Anajulikana kama ex-wife wa Ashley Cole - Cherly Tweedy aka Cherly Cole. Muimbaji na mwandishi wa nyimbo wa kiingereza. 

Anaujua uwendazimu wote hata ambao kijana Wayne Rooney hatuoneshi uwanjani. Muite Coleen Rooney aka Mama Kai. Mwanamke wa kwanza katika maisha ya Rooney na ndio anayejua kumtuliza Rooney kuliko hata babu Fergie.


English actress amekuwa na mahusiano na wanasoka kadhaa. Alianza na Cristiano Ronaldo, na baadae akachumbiwa na Marcus Bent.

Iker Cassilas hajui tu kudaka mipira pia ana uwezo mkubwa wa kuwakamata watoto waziuri. Huyu Eva Gonzalez nae aliwahi kumpitia katika kipindi cha fainali za kombe la dunia mwaka 2006 nchini Ujerumani.

Alipigiwa kura kuwa"Mtangazaji mwenye mvuto kuliko wote na jarida la FHM, Carbonero anafahamika kwa tabia yake ya kupenda kumkiss in public boyfriend wake Iker Cassilas, katika kila mechi ya World Cup 2010. Pia katika fainali hizo alishutumiwa kwa kumkosesha umakini Cassilas katika mechi waliyofungwa na Uswiss. Mmmmh mtoto alivyo mzuri hivi mie hata simlaumu Cassilas.

Mwigizaji wa kike maarufu kwa TV Series maarufu duniani kwa sasa iitwayo NIKITA. Anaitwa Maggie Q demu wa zamani wa mchezaji bora wa Asia Hidetoshi Nakata.

Model huyu wa kibrazil pia yeye mwenyewe aliwahi kuwa mwanasoka. Yumo katika listi hii kwa sababu ya aliwahi kuolewa na mwanasoka bora wa dunia mara 3 Ronaldo De Lima na wana mtoto mmoja. Pia sasa ameolewa na mwanasoka wa kihispania David Aganz.


 Mwanamuziki maarufu kwa sasa ana date na Mhispania Gerard Pique, na ndio maana yupo katika listi hii. Mcolombia huyo anajulikana sana kwa kujua kucheza. Naamini atakuwa akimchezea Pique Pique kila usiku kabla hawajalala.

Model wa kibrazil Raica Oliveira ni binti mwingine aliyeingia katika mikono ya Ronaldo na kutumalizia kipaji cha El Phenomena wetu wa soka.

Demu wa zamani wa mchezaji wa Arsenal Freddie Ljunberg pia ni demu wa sasa wa mchezaji wa zamani wa Manchester United anayeichezea Sunderland Kieran Richardson. Ana miaka 20

Zamani alikuwa anajulikana kama Posh Spice aka Victoria Beckham, Mke wa David Beckham. Yeye na mumewe wanatajwa kama moja ya couples bora kabisa miongoni macelebs walio katika mahusiano. Ndoa yao ina watoto wanne mpaka sasa.

Popote utakapokutana na huyu mwanamke kama wewe ni mwanaume kamili ni lazima umtazame mara mbili. Anaitwa Yolanthe Cabau, mke wa kiungo wa Inter Milan Wesley Sneijder. 

Mrembo wa kiswidishi ameolewa na mmoja wanaosoka bora bora waliowahi kutokea katika historia ya soka, Luis Figo.

Usimuone Diego Forlan anapiga sana mashuti ya mbali ukajua yanakuja hivi hivi tu. Analelewa vizuri na mpenzi wake modo wa Kiargentina Zaira Nara.


Huyu Miss England 2004 na Miss Great Britain 2006, amekuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanasoka kama vile Teddy Sherigham, Marcus Bent na Jermain Defoe. Aliporwa taji lake la Miss Great Britain mara baada ya picha zake za uchi za jarida la Playboy kutoka, pia aligundulika alikuwa na mahusaino na moja ya majaji wa Miss Great Britain Teddy Sheringham.



Ogaaaaadrx9drdpysmv55h1ohaf6llpnld9iwmkwesohhwf2qjfhq1wik67z-izhou9jrf7-nte1wbdeut-bvjmwmxyam1t1uj_bmb_affd96orkwrppgdgda3dc_display_image
Demu wa high school wa Kaka, Carolina Celico ni mzuri hatari. Japokuwa ni vigumu kwa wanasoka au watu maarufu kudumu na mwanamke mmoja kwa muda mrefu lakini mlokole Kaka na utajiri pamoja na umaarufu wote alionao hapa ndio kafika. Wameshaona na wana mtoto mmoja.

Mke wa mwanasoka Joe Cole na vingi vya kui-offer camera. Uzuri wake ni hatari na ndio maana haishangazi kuona Cole akiwa kaamua kumueka ndani.







Anajulikana mno kwa mahusiano yake yaliyotingisha mno ndoa ya John Terry - pia Vanessa Perroncel ndiye aliyeleta ugomvi kati ya Wayne Bridge . Ni vigumu kumlaumu Terry kwa uzuri alionao huyu binti.

English model na mwandishi wa makala za urembo katika gazeti la Daily Mirror ndiye mwanamke aliyeuteka moyo wa The Fantastic Captain Steven Gerrard.



Mrembo huyu aliyezaliwa Spain ni moja kati ya wanawake wengi wanaomjua Cristiano Ronaldo akitoka kuamka anakuwa na sura gani. Nererida Gallardo pia amewahi kutekwa na Sergio Ramos.
Huyu ni mrembo ambaye alishawahi kushinda tuzo ya mwanamke mzuri kuliko wote nchini Nigeria, ameolewa na mchezaji wa Fenerbahce Joseph Yobo pia ni mtoto wa kufikia mchezaji John Fashanu.

Anajulikana kwa mahusiano yake yaliyowagonganisha wachezaji wa England Peter Crouch na Shaun Wright Philips. Lauren Pope ni mjasiliamari anayefanya kazi kama DJ katika moja ya kumbi huko jijini London.

Huyu ni mke wa kiungo wa timu ya taifa ya Argentina Martin Demichelis - anaitwa Evangelina Anderson.

Model huyu wa kibrazil anaipenda timu yake ya taifa.
Warner alikuwa na mahusiano na Ronaldo de lima mpaka 1999. Baadae akaolewa na golikipa wa taifa hilo Julio Ceaser na sasa wana watoto wawili.


Pamoja na umalya wake lakini huyu ndio mwanamke aliyeweza kumtuliza Kapteni John Terry. Tayari ndoa imeshajibu na ipo imara japokuwa imekuwa ikiandamwa naskendo za umalaya wa mumewe


Carlos Tevez anajulikana kwa kujua kulisakata soka, lakini muaregentina huyo pia ni hatari kwa warembo wakali. Natalia Fassi ni mrembo mwingine aliyeiletea kashikashi ndoa ya Carlitos.

Mrembo huyo Mariana Paesanialishea chumba kimoja na Carlos Tevez kipindi mke wa Carlitos akiwa anamlea mtoto wao mchanga.

USHAURI WA KISHERIA JUU YA MGONGANO WA VYOMBO VYA MAAMUZI VYA TFF.

FELIX SUNZU KUANZA MAZOEZI LEO!

Mshambuliaji Felix Sunzu anaanza rasmi mazoezi leo jioni kwenye uwanja wa Tanganyika Packers.
Sunzu ambaye ni raia wa Zambia aliumia mwishoni mwa mwaka jana,majeraha hayo yalimsababishia kuikosa michezo miwili iliyopita ya raundi ya pili.
wakati huo huo kocha wa Simba Milovan Cirkovic amesema ushindi wa jana dhidi ya JKT OLJORO wameu-dedicate kwa kiungo Haruna Moshi baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu.

ROONEY AMTOA OUT GIBSON KWA KUWAFUNGA CITY

Baada ya mechi za usiku wa jumanne katika premier league, ni magoli 6 sasa yanawatofautisha City na United katika uongozi wa ligi kuu ya England.
Na kama kusema shukrani kwa mchezaji mwenzie wa zamani wa United, Mshambuliaji wa England na United Wayne Rooney aliamua kumtoa out mfungaji wa goli la Everton dhidi ya Darron Gibson.
Wawili hao wakiwa pamoja na mke wa, Coleen Rooney na girlfriend wa Gibson, walienda kuona onyesho la music @Palace Theatre Jumatano usiku – kabla hawajaenda katika mgahawa wa kichina.
Gibson alifunga goli @Goodison Park na kuwafanya City kuwa sawa na United kwa pointi.
Manager wa United Sir Alex Ferguson alitania kuhusu goli la Gibson ambaye aliuzwa siku chache nyuma akisema: “Hii ndio ilikuwa plan yetu.”
Rooney nae ndiye alikuwa wa kwanza kumpongeza Gibson baada ya mchezo akiandika kwenye Twitter: “Yesssssssssssssss gibbo. Nakupenda dogo.”


MATOKEO YA LIGI MBALI MBALI ULAYA NA AFRIKA!

Barclays Premier League

Aston Villa 2 - 2 Queens Park Rangers


12' 0 - 1 Djibril Cissé
28' 0 - 2 Stephen Warnock (og)
45' Darren Bent 1 - 2
79' Charles N'Zogbia 2 - 2


Blackburn Rovers 0 - 2 Newcastle United


11' 0 - 1 Scott Dann (og)
44' David Dunn (pen miss)
90' +2' 0 - 2 Gabriel Obertan


Bolton Wanderers 0 - 0 Arsenal


Fulham 1 - 1 West Bromwich Albion


68' Clint Dempsey 1 - 0
81' 1 - 1 Somen Tchoyi


Sunderland 3 - 0 Norwich City


21' Fraizer Campbell 1 - 0
27' Stephane Sessegnon 2 - 0
53' Daniel Ayala (og) 3 - 0

Italian Serie A


Atalanta P - P Genoa


Bologna P - P Fiorentina


Cagliari 4 - 2 AS Roma


5' Ribeiro Cardoso Thiago 1 - 0
13' 1 - 1 Juan
34' 1 - 2 Fabio Borini
40' Mauricio Ferreira Pinilla 2 - 2
48' Ribeiro Cardoso Thiago 3 - 2
90' +2' Albin Ekdal 4 - 2


Internazionale 4 - 4 Palermo


15' 0 - 1 Andrea Mantovani
21' Diego Milito 1 - 1
52' 1 - 2 Fabrizio Miccoli
55' Diego Milito (pen) 2 - 2
61' Diego Milito 3 - 2
66' 3 - 3 Fabrizio Miccoli
68' Diego Milito 4 - 3
85' 4 - 4 Fabrizio Miccoli


Lazio 2 - 0 AC Milan


75' Hernanes 1 - 0
84' Tommaso Rocchi 2 - 0


Napoli 0 - 0 Cesena


Siena P - P Catania


Udinese 2 - 1 Lecce


2' Michele Pazienza 1 - 0
26' 1 - 1 David Di Michele
35' Antonio Di Natale 2 - 1

Spanish Copa del Rey

Valencia 1 - 1 Barcelona


27' Jonas 1 - 0
35' 1 - 1 Carles Puyol

African Nations Cup

Group D

Botswana 1 - 2 Mali


49' Mogakolodi Ngele 1 - 0
55' 1 - 1 Garra Dembele
73' 1 - 2 Seydou Keita


Ghana 1 - 1 Guinea


28' Emmanuel Badu Agyemang 1 - 0
45' +2' 1 - 1 Abdoulaye Camara
70' Mamadou Bah

VURUGU KUPITIA SHADAKA TV!





VURUGU ZA MASHABIKI NCHINI MISRI KATIKA PICHA!








Vifo vya watu 74 uwanjani

     inahofiwa idadi ya waliokufa huenda ikaongezeka.

Watu 74 wamefariki kufuatia ghasia kati ya mashabiki wa timu mbili katika mji wa Port Said, nchini Misri.


Taarifa hizo ni kwa mujibu wa televisheni ya taifa.


Watu hao walikiufa baada ya mashabiki kuanza kuingia uwanjani, baada ya mechi kati ya vilabu viwili vikuu vinavyoongoza ligi nchini humo, Masry na Al-Ahly, siku ya Jumatano.


Inahofiwa kwamba idadi ya vifo huenda ikaongezeka, kwani zaidi ya watu 156 wamejeruhiwa.


Huu ndio msiba mkubwa zaidi nchini Misri kuwahi kutokea katika uwanja wa kandanda, alielezea naibu waziri wa afya nchini Misri.


“Huu ni msiba wa kusikitisha mno”, alisema Hesham Sheiha kupitia matangazo ya televisheni.


Kati ya waliokufa ni pamoja na maafisa wa usalama.


Mwandishi wa BBC anaelezea kwamba ukosefu wa usalama mkali ambao hudumishwa kwa kawaida huenda ikawa ni jambo ambalo lilichangia kutokea ghasia hizo.


Polisi nchini Misri wametulia mno tangu kufanyika maandamano yaliyomtoa Rais Hosni Mubarak madarakani.


Katika mechi hiyo ya Jumatano, timu ya Port Said, Masry, ilipata ushindi wa magoli 3-1.


Walioshuhudia walielezea kwamba kulikuwa na hali ya wasiwasi muda wote wa mechi hiyo, tangu shabiki mmoja wa Al-Ahly alipoinua bango ambalo inadaiwa lilikuwa linawatukana mashabiki wa timu ya nyumbani.


Katika mitandao ya jamii, licha ya kutokuwepo ushahidi, uvumi umekuwa ukienea kwamba maafisa wa usalama walikuwa wanapanga njama ya kupambana na mashabiki wa Al-Ahly.


Maafisa wachache wa polisi walijitahidi kuwapa ulinzi wachezaji, lakini hawakufanikiwa kabisa.


Sehemu moja ya uwanja ilichomwa moto.


Maafisa wanaohusika wameelezea kwamba vifo vingi vilitokana na watu kupata majeraha makubwa ya kichwa kwa kupigwa au kukatwa, na wengine kuzimia hadi kufa wakati wa mkanyagano.


Ndege za helikopta zilitumwa hadi Port Said kuwasafirisha hadi hospitali mashabiki waliojeruhiwa.


"Huu si mpira. Hivi ni vita na watu wanakufa mbele yetu", alisema mchezaji wa Al-Ahly, Mohamed Abo Treika.


Mbunge wa Port Said, Albadry Farghali, aliwalaumu maafisa wa usalama.


"Walikuwa wapi haya yote yakitokea?"


"Watu wa Mubarak bado wako uongozini. Kiongozi wa utawala ameng'atuliwa, lakini watu wake bado wapo madarakani", alielezea kupitia televisheni.


"Usalama uko wapi? Serikali iko wapi?"


Mjini Cairo, mwamuzi alisitisha mechi nyingine, alipoarifiwa juu ya ghasia za Port Said.


Jambo ambalo liliwafanya mashabiki kuchoma moto sehemu fulani za uwanja.


Mechi zote za ligi kuu zimefutiliwa mbali, na bunge jipya la Misri siku ya Alhamisi litakutana katika kikao cha dharura kuujadili msiba huu.

Source: bbcswahili.com

Wednesday, February 1, 2012

MSIKILIZE MBWIGA MBWIGUKE LEO!


MAONI YA MDAU JUU YA NAMNA YA YANGA KUJIKWAMUA KIUCHUMI!


Katika suala zima la kuchangia maendeleo ya michezo nchini na kwa Vilabu hasa vikongwe vya YANGA na SIMBA, wadau wa michezo tumekuwa walalamishi pasipo kutoa mwongozo au mwelekeo wa nini kifanyike katika kuzikwamua kiuchumi.

Hivyo kama mdau wa klabu ya YANGA napenda kushauri uongozi wa kubuni na kuweka mkakati endelevu wa kukusanya mtaji wa kutoka kwa wadau wa Klabu kwa maendeleo ya Klabu hasa kwa ujenzi wa Uwanja na Vitega Uchumi vyingine kama Majengo.

Hivyo uongozi wa klabu uandae utaratibu wa kuunda kamati ya Ujenzi na Akaunti yake, itakayosimamia kukusanya michango mbalimbali kutoka kwa wanachamana na wapenzi wapatao 710,345 wa klabu hii ya Yanga kulingana na nafsi zao kiuchumi.

 Hivyo kwa utaratibu huu klabu inaweza kujikusanyia fedha za kuanzisha ujenzi wa uwanja zipatazo Tshs. 12,140,000,000/= kwa kipindi cha Mwaka.
Nimejaribu kuunda makundi 15 ya wanachama kulinga na uwezo wa kiuchumi, na michezo angalau 25 inayohusisha klabu katika mikoa.
Mchanganuo huu wa makundi ni kama ifuatavyo:
Na Aina ya wadau Idadi ya wadau Kiwango (Tshs) Thamani Kisiwa (Tshs)

1 Wadhamini wa Klabu  10 @50,000,000 = 500,000,000

2 Yanga Family -A  10 @ 20,000,000 = 200,000,000

3 Yanga Family - B 10 @10,000,000 = 200,000,000

4 Yanga Family - C 80 @ 5,000,000 = 400,000,000

5 Viongozi(Klabu/Matawi) 100 @1,000,000 = 100,000,000

6 Wabunge 50 @ 3,000,000 = 150,000,000

7 Wanachama - kadi 100,000 @ 20,000 = 2,000,000,000

8 Wakereketwa wa klabu 200,000 @10,000 = 2,000,000,000

9 Wanachama-A 10,000 @ 500,000 = 5,000,000,000

10 Wanachama -B 200,000 @ 5,000 = 1,000,000,000

11 Wanachama - C 200,000 @ 1,000 = 200,000,000

12 Matawi ya Klabu 20 @ 1,000,000 = 20,000,000

13 Taasisi Rafiki wa Klabu 20 @ 1,000,000 = 20,000,000

14 Makampuni 15@ 5,000,000  = 75,000,000

15 Balozi- Nchi Rafiki 5 @ 5,000,000 = 25,000,000

16 Mechi za Timu 25 @ 10,000,000  = 250,000,000
               
 Jumla                                     12,140,000,000




Hivyo kwa mchanganuo huo na kwa kushirikiana na vyombo vya habari nchini; klabu itajikusanyia mtaji wa kutosha kwa maendeleo yake kiuchumi na kisoka.
Napendekeza pia wadau kutoa mawazo endelevu kwa viongozi na wanachama kwa kutumia vyombo mbali mbali vya mawasiliano mfano TV, emails, radio, internet, n.k. Kwa mijadala hii ya kimaendeleo kwa viongozi na wanachama inaweza kuwa mawazo chanya kwa maendeleo ya soka letu la Tanzania.

Nawasilisha mjadala kwenu,

Emmanuel Rutatora
Mdau wa Soka – Rorya.

SIMBA YAITANDIKA OLJORO MABAO 2:0


Nyota wa Kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi


amekihakikishia kikosi chake cha Simba, makazi ya


kudumu, kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara, baada


ya kufunga magoli mawili yaliyoipa ushindi wa 2-0,


dhidi ya JKT Oljoro.
Okwi raia wa Uganda, aliyeingia mwanzoni mwa


kipindi cha pili katika dakika ya 46, kuchukua nafasi


ya Kago Gervais.
Alifunga magoli hayo, la kwanza dakika ya 59,


kutokana na krosi ya Uhuru Suleiman, bao la pili,


alilifunga dakika 83 pasi ilitoka tena kwa Uhuru,


aliyepapokea pasi ya Patrick Mafisango.
Kuingia kwa Okwi ambaye hakuwa katika maandalizi ya pamoja na kikosi hicho kwa muda mferu kutokana na kupatwa matatizo nchini mwake ni baada ya


Haruna Moshi 'Boban' kuonyeshwa kadi nyekundu


dakika ya 44 na kuifanya safu ya ushambuliaji kupwaya.
Boban alipewa kadi hiyo ya moja kwa moja na


mwamuzi, Isihaka Shirikisho kutoka Tanga kwa kosa


la kumrudishia rafu beki wa Oljoro, Omary Mtaki


ambaye awali ndiye alianza kwa kumpiga kichwa.
Alifanya hivyo kutokana na kushindwa uvumilivu,


kutokana na rafu za mara kwa mara alizokuwa


akichezewa, awali alipigwa kichwa na Karage


Mgunda kabla ya hiyo ya pili.
Katika mchezo huo, ambao Oljoro inayosifika


kucheza safi, haikuonyesha kiwango cha juu na


kuwafanya Simba, watawale mchezo huo hasa


kipindi cha pili.
Bakari Kigodeko wa Oljoro itabidi ajutie nafasi za


wazi alizopoteza, dakika ya 62 na 70, aliingia ndani


ya 18 langoni mwa Simba, lakini akakosa maamuzi


na mipira yote kunyang'anywa na mabeki wa Simba.
Kocha mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic


ameuzungumzia mchezo huo ulikuwa mgumu, lakini


akasifu kiwango cha wachezaji wake.
Kutokana na kadi nyekundu ya Boban, Milovan


alisema; ''Boban hakustahili kadi nyekundu,


mwamuzi angeweza kumpa njano.''
Ally Kidi ambaye ni kocha wa JKT Oljoro aliwasifu


pia, nyota wake walicheza kiwango cha juu


kulingana na mazingira ya Uwanja wa Taifa.
''Wamejitahidi, kucheza katika Uwanja mkubwa


kama huu na mara ya kwanza ni kazi kwa vijana


wangu, kwani ni mara ya kwanza,''alisema Kidi.
Simba itaongoza ligi kwa pointi 34, Yanga ya pili ina 31 na Azam FC ni ya tatu ina 29, timu hizo zimecheza mechi 15 kila moja.




Simba
1 Juma Kaseja
2 Said Nassoro 'Cholo'
3 Amir Maftah
4 Shomari Kapombe
5 Kelvin Yondan
6 Jonas Mkude
7 Uhuru Suleiman / Ramadhan Singano dk 88
8 Mwinyi Kazimoto
9 Kago Gervais / Okwi dk 46
10 Haruna Moshi 'Boban'
11 Patrick Mafisango




JKT Oljoro
1 Said Lubawa
2 Omary Mtaki
3 Ally Omary
4 Omary Mtaki
5 Marcus Ndeheli
6 Ally Mkanga
7Karage Mgunda / Meshack Nyambele dk 65
8 Sunday Paul
9 Bakari Kigodeko
10 Amiry Omary
11Rashid Nassoro

UNAKUMBUKA? : YASIN NAPILI ALIPIGA MPIRA UKAPASUKIA HEWANI...

Mwaka 1988 ulikuwa ni mwaka wa wagosi kwa sababu mwaka huo timu zote mbili za Tanga zilizokuwa kwenye ligi kuu zilifanya vizuri.Coastal union walikuwa mabingwa wa bara na African sports walishika nafasi ya tatu nyuma ya yanga.

Nafasi ambayo iliwawezesha kushiliki ligi ya muungano.Walipokwenda kwenye muungano African Sports walikua mabingwa na Coastal walishika nafasi ya pili hivyo timu hizo za Tanga zikapata nafasi ya kuwakilisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa (klabu bingwa Africa na kombe la washindi wakati huo).


Kwenye ligi ya bara kulikua na msisimko wa hali ya juu kiasi kwamba ilikua ngumu kutabiri nani atakua bingwa,hadi mechi za mwisho ndipo bingwa alipofahamika.Uthibitisho wa hayo ni jinsi timu tatu za juu yaani Coastal,Yanga na A/sports kutofautiana magoli ya kufunga.Kwani zote zilikua na point 26.Coastal alikua na magoli ya kufunga 27,Yanga 24 na
” wanakimanumanu” A/Sports 23.

Hivyo bingwa alipatikana kwa kuangalia timu iliyokua na magoli mengi.Kabla ya mechi za mwisho za siku hiyo Coastal na Yanga zilizokua zikiongoza,zote zilikua tayari na point hizo 26 lakini zote zikapoteza mechi zao kwa kufungwa na mahasimu wao.Coastal alipigwa
2-0 na Africa Sports na na yanga alifungwa 2-1 na Simba(Simba akaokoka kushuka daraja).


*Kwenye mechi hiyo ya Tanga iliyotoa dira kwamba mwaka huu ni mwaka wa wagosi.Timu hizo mbili zilikutana tarehe 23/07 ndani ya uwanja wa mkwakwani.Hii ilikua siku ya jumamosi ,siku ambayo watani hao ambao wako jirani sana huko Tanga kuliko hata walivyokaribiana simba na yanga hapa Dar kwani wao wametofautishwa na majengo au nyumba zisizozidi 10 kwenye barabara ya 11 na 12.


*Hii ndio siku ambayo Coastal Union walitwaa ubingwa wa Tz bara kwa mara ya kwanza na ya mwisho licha ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa mahasimu wao “wanakimanumanu”,mechi hii ndio ambayo inadhaniwa kuingiza watazamaji wengi kuliko mechi nyingine yoyote ya kimashindano iliyochezwa ndani ya uwanja wa mkwakwani.Katika mechi hii A/sports iliwashangaza watazamaji kwa kuvaa jezi za njano tofauti na rangi ya jezi zake zilizozoeleka nyeupe na bluu.


*Licha ya siku hii kukumbukwa na wagosi kwa kuchukua ubingwa pia ndio siku ambayo wanaikumbuka kwa kucheka huku wakiwa wamenuna na pia kutokea kwa tukio la ajabu na la kushangaza.Tukio la kupasuka mpira ukiwa hewani,mpira ulipasuka hewani baada ya shuti kali la nahodha wa coastal Yassin Napili,shuti ambalo lilionekana kuwa lingezaa bao.
Hakuna mchezaji aliekuwa anamkaba Napili wakati akipiga shuti hilo,wengi waliamini kuwa ingeweza kuwa bao kama mpira huo ungefika langoni ukiwa na nguvu zake kwani baada ya kupasuka ukiwa angani ulidondoka chini na kuelekea moja kwa moja hadi kwa golikipa wa A/sports ambae aliuokota ukiwa hauna upepo.


*Ilikuwa ni katika dakika ya 25 mpira huo ulipopasuka bila kutarajiwa,wakati huo hakukua na timu iliyokua imepata bao.Beki namba 3 wa Coastal Douglas Muhani aliambaa na mpira upande wa kushoto akamuwekea pande Yassin Napili ambae alikuwa amepanda na move hiyo,akiwa katika nafasi nzuri Napili alijikunja na kujikunjua, kufumba na kufumbua kishindo kikubwa kikasikika uwanjani, mpira umepasuka, namna gani mpira huo ulipasuka hakuna alieweza kumuelezea mwenzake,ilibidi uletwe mpira mwingine.


Kipindi cha pili A/sports ambao walielemewa sana kwenye kipindi cha kwanza walianza kucheza vizuri na kufunga mabao mawili yaliofungwa na Juma Burhan”kakoko”kunako dakika ya 71 akiunganisha kwa shuti kali cross ya marehemu Abbas Mchemba na bao la pili lilifungwa dakika 87 na mfungaji bora wa mwaka huo (marehemu)Victor kefa mkanwa ambae alimzidi mbio beki Abdallah Tamimu “mdaula”.Baada ya bao hilo hali ndani ya uwanja wa mkwakwani ilikua ni vurugu tupu kwani muda huo huo kwenye uwanja wa Taifa simba nao walipata bao la pili (kupitia matangazo ya moja kwa moja ya Redio Tanzania)habari hiyo iliwapa nguvu mpya mashabiki wa Coastal waliokua tayari wameanza kununa na kupata nguvu mpya zilizo wawezesha kuimba Bingwa,Bingwa,Bingwa.


Timu zilipangwa kama ifuatavyo
Coastal Union


1. Mohamed Mwameja


2. Said Kolongo


3. Douglas Muhani


4. Abdallah Tamimu(mdaula)


5. Yasin Abbu Napili


6. Ally Maumba “white Horse”


7. Idrisa Ngulungu


8. Kassa Mussa


9. Juma Mgunda


10. Hussein Mwakuluzo


11. Razak Yusuf


Kocha: Zakaria Kinanda (marehemu)

A/SPORTS

1. Salim Waziri
2. Fransis Mandoza
3. Bakari Tutu(marehemu)
4. Hassan Banda
5. Mhando Mdeve (marehemu)
6. Raphael John
7. Juma Burhan “kakoko”
8. Abbas Mchemba(marehemu)
9. Victor kefa Mkanwa(marehemu)
10.Mchunga Bokari(marehemu)
11. Said Seif


Kocha: Sillersaid Mziray ( Marehemu )
TUZO ZILIZOTOLEWA BAADA YA MASHINDANO @ shs 10,000/= KWA WANAMICHEZO WAFUATAO


1. Kocha bora -‘’Arigo Sachi’’(marehemu)Zakaria Kinanda wa coastal
2. Mchezaji mwenye nidhamu na ambae pia alikua mchezaji bora - Yassin Napili wa coastal
3. Mfungaji bora – Victor Kefa Mkanwa wa African sports
4. Kipa bora - Joseph Katuba wa Sigara
5. Mchezaji mwenye umri mdogo aliengara - Athuman Abdallah ‘’China’’ wa Yanga
6. Mchezaji mwenye umri mkubwa – John Simkoko wa Reli morogoro

WACHEZAJI WA GHANA WAKIIMBA SIKU MOJA KABLA YA AFCON 2012 KUANZA.

HABARI NA MATUKIO YA MICHEZO YALIYOJIRI MKOANI MBEYA!



NA Junior MATUKUTA-Mbeya.

1.Ligi ya Mkoa wa Mbeya inaendelea hatua ya makundi na mechi kadhaa zimechezwa,

i)TZ Prisons Veteran(Chuma Chakavu) vs Mbalizi Rangers > 1-1

ii)Eleven Killers vs Scorpion> 3-0

iii)Mlowo United vs Kawetele> 1-1

iv) Boma United vs Chunya United> 3-0


2.Wachezaji wa Timu ya Mkoa wa Mbeya(Mapinduzi Stars) wameulalamikia Uongozi wa chama ya soka Mkoani hapa,Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya baada ya kushindwa kutimiza ahadi zao za kuwapatia Viwanja kwa ajili ya Ujenzi wa nyumba kama Zawadi baada ya Kutwaa ubingwa huo mwaka jana 2011 mkoani Arusha.
Nikiongea na wachezaji hao kwa nyakati Tofauti wamesema tayari wamashalipia kiasi cha Tsh 5000/= kama malipo ya usajili wa viwanja hivyo ktk ofisi za Ardhi,lakin mpaka leo hilo suala limebakia kuwa Danadana na ikizingatiwa Mkuu wa Mkoa aliyekuwepo kipindi hicho Mhe.John Mwakipesile tayari ameshastaafu na ndiye akilitoa agizo hilo la wachezaji hao kupewa Viwanja.

Wachezaji hao IDD AJIRO,DAVID MWANTIKA,LUGANO MWANGAMA na SAID MTUPA wameomba kupitia kipindi chenu cha Michezo cha SPORTS EXTRA kufikisha Ujumbe kwa wahusika hili watimize ahadi yao hiyo.


3.Pia Timu ya TZ Prisons inaendelea na Mazoezi yake ktk Uwanja wa Sokoine kwa ajili ya Mechi yake na Timu ya MBEYA CITY COUNCIL na Timu nyingine kwenye mzunguko wa pili wa ligi Daraja la kwanza Taifa,Timu hiyo ipo chini ya Kocha John Makatta na msaidizi wake Rungwe

HAPPY BITHDAY: GABRIEL BATISTUTA & MBWIGA MBWIGUKE

ANAYELISHWA KEKI NDIYE MBWIGA MBWIGUKE .


MCHUANO WA LIONEL MESSI NA CRISTIANO RONALDO MWEZI JANUARY


TAKWIMU ZA MWEZI JANUARY 
          

371MINUTES PLAYED374
5GOALS4
1PENALTIES2
2ASSISTS0
17 / 9 (52.9%)TOTAL SHOTS / ON GOAL25 / 6 (24%)
245 / 206 (84.1%)PASSES / COMPLETED174 / 142 (81.6%)
7.63
AVERAGE RATING
7.13
222011-12 LA LIGA GOALS24
34 (36)2011-12 COMPETITIVE GOALS (APPEARANCES)31 (31)

http://i1.goal.com/files/images/stats/goal/team-logos/1/451_48x48.jpg

CHELSEA NAO WATANGAZA KUPATA HASARA


Wiki kadhaa baada ya Manchester City kupata hasara kubwa iliyovunja rekodi, sasa ni zamu ya matajiri wa London Chelsea ambao wametangaza kupata hasara ya £68million.
The Blues  - ambao walimnunua Fernando Torres na David Luiz kwa gharama ya jumla ya £75million last January – leo hii wametoa taarifa ya hesabu za mwaka zilizoisha  June 2011. Hasara ya kipindi hiki imeshuka tofauti na £70.9m waliiyoipata mwaka juzi.
Mwenyekiti wa The Blues alisema: “Klabu sasa ina focuse katika kuweza kwenda sawa na mahitaji ya sheria ya matumizi ya fedha ya UEFA huku tukiwa tuna maintain uwezo wa kuweza kushindania makombe makubwa.”
Taarifa hizi zinakuja kama tatizo jingine kwa klabu hiyo ambayo kuna kipindi iliwahi kuwa na mtazamo wa kujitegemea yenyewe, kwa mujibu wa CEO wa zamani Peter Kenyon.
Chelsea wamemaliza dirisha la usajili kwa kutumia jumla ya £16m kwa Gary Cahil na Kevin de Bruyne.

FRANCIS CHEKA MADA MAUGO KUGOMBEA UBINGWA WA IBF RAUNDI 12 APRIL 28 PTA SABASABA


Makamu mwenyekiti wa Oganaizesheni ya ngumi za Kulipwa Nchini, Madaraka Nyerer (Kushoto) akiwaelekeza mabondia Fransc Cheka kulia na Mada Maugo jinsi ya kusaini mkataba wa makubaliano wa kupigania ubingwa IBF raundi 12 litakarofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba Aprilo 28.(picha na http://www.superdboxingcoach.blogspot.com/)

Bondia Mada Maugo akiongea na waandishi wa habari wakati wa kusaini mkataba uho leokupigania ubingwa IBF raundi 12 litakarofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba Aprilo 28.(picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)



Bondia Fransic Cheka akizungumza na waandishi wa habari leo kupigania ubingwa IBF raundi 12 litakarofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba Aprilo 28.(picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

BREAKING NEWS: WILSHARE KUUKOSA MSIMU MZIMA


Kiungo wa Arsenal Jack Wilshare ana asilimia kubwa za kukaa nje msimu mzima baada ya vipimo kuonyesha kuwa maumivu mapya aliyoyapata ni makubwa kuliko ilivyofikiriwa.
The 20-year old midfielder pia sasa ana wasiwasi wa kukosa michuano ya EURO 2012 kwa kuwa atakosa kucheza msimu mzima.
Wilshare alikuwa anatarajiwa kurejea uwanjani mwezi huu lakini wiki iliyopita alipata majeruhi wiki iliyopita ambayo yameongeza tatizo zaidi.

RATIBA YA UCHAGUZI NA NAFASI ZA UONGOZI BIAFRA SPORTS CLUB

RATIBA YA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU WA KWANZA WA VIONGOZI WA KLABU YA MICHEZO YA BIAFRA UTAKAOFANYIKA TAREHE 11 MACHI, 2012.

Mara baada ya kupata usajili rasmi toka serikalini klabu ya michezo ya Biafra imejipanga kufanya uchaguzi mkuu wa kwanza wa viongozi ambao unatarajiwa kufanyika mnamo tarehe 11 Machi, 2011. Kwa mujibu wa mwenyekiti wa klabu hiyo Bw. Abdul Mollel, ratiba hiyo ya uchaguzi inafuatiwa na uchukuaji wa fomu za uanachama kwa mujibu wa ratiba inayoonekana hapa chini: -Ratiba ya uchukuaji na urudishaji fomu mbalimbali
1. Fomu za maombi ya uanachama zimeanza kuuzwa tarehe 28 Januari, 2012
2. Tarehe ya mwisho ya kurudisha fomu za uanachama ni 15 Februari, 2012
3. Fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi zitaanza kutolewa tarehe 19 - 22 Februari, 2012
4. Mwisho wa kurejesha fomu za kugombea nafasi za uongozi ni tarehe 25 Februari, 2012
5. Uchaguzi mkuu wa viongozi utafanyika tarehe 11 Machi, 2012


Nafasi za uongozi zitakazogombewa katika uchaguzi huo ni kama ifuatavyo: -
1. Mwenyekiti
2. Makamu mwenyekiti
3. Katibu Mkuu
4. Katibu Mkuu Msaidizi
5. Mweka Hazina
6. Wajumbe watano (5) watakaoingia kwenye kamati ya utendaji
7. Wajumbe nane (8) wa kamati ya uchumi na mipango
8. Wajumbe saba (7) wa kamati ya ufundi
9. Wajumbe saba (7) wa kamati ya nidhamu na rufaa
Kwa maelezo, maoni na maswali wasiliana na katibu wa klabu kwa anuani ifuatayo: -
BIAFRA SPORTS CLUB,
SIMU: +255 715 253 653
EMAIL: biafra.jsclub@gmail.com
HQ: MTAA WA ISELE, 90 DEGREES PUB, KINONDONI
DAR ES SALAAM

HUYU NDIYE ANAYEJUA KUUTULIZA MZUKA WA MTUKUTU MARIO BALOTELLI



Raffaella Fico mwanamitindo wa kiitaliano ambaye ndiye mpenzi wa Mtukutu Mario Balotelli - unaambiwa Baloteli na ukorofi wake wote hapindui wala hageuzi kwa mtoto huyu.



CHEMSHA BONGO! UWANJA HUU UNAPATIKANA NCHI GANI ?