Search This Blog
Wednesday, February 1, 2012
MAONI YA MDAU JUU YA NAMNA YA YANGA KUJIKWAMUA KIUCHUMI!
Katika suala zima la kuchangia maendeleo ya michezo nchini na kwa Vilabu hasa vikongwe vya YANGA na SIMBA, wadau wa michezo tumekuwa walalamishi pasipo kutoa mwongozo au mwelekeo wa nini kifanyike katika kuzikwamua kiuchumi.
Hivyo kama mdau wa klabu ya YANGA napenda kushauri uongozi wa kubuni na kuweka mkakati endelevu wa kukusanya mtaji wa kutoka kwa wadau wa Klabu kwa maendeleo ya Klabu hasa kwa ujenzi wa Uwanja na Vitega Uchumi vyingine kama Majengo.
Hivyo uongozi wa klabu uandae utaratibu wa kuunda kamati ya Ujenzi na Akaunti yake, itakayosimamia kukusanya michango mbalimbali kutoka kwa wanachamana na wapenzi wapatao 710,345 wa klabu hii ya Yanga kulingana na nafsi zao kiuchumi.
Hivyo kwa utaratibu huu klabu inaweza kujikusanyia fedha za kuanzisha ujenzi wa uwanja zipatazo Tshs. 12,140,000,000/= kwa kipindi cha Mwaka.
Nimejaribu kuunda makundi 15 ya wanachama kulinga na uwezo wa kiuchumi, na michezo angalau 25 inayohusisha klabu katika mikoa.
Mchanganuo huu wa makundi ni kama ifuatavyo:
Na Aina ya wadau Idadi ya wadau Kiwango (Tshs) Thamani Kisiwa (Tshs)
1 Wadhamini wa Klabu 10 @50,000,000 = 500,000,000
2 Yanga Family -A 10 @ 20,000,000 = 200,000,000
3 Yanga Family - B 10 @10,000,000 = 200,000,000
4 Yanga Family - C 80 @ 5,000,000 = 400,000,000
5 Viongozi(Klabu/Matawi) 100 @1,000,000 = 100,000,000
6 Wabunge 50 @ 3,000,000 = 150,000,000
7 Wanachama - kadi 100,000 @ 20,000 = 2,000,000,000
8 Wakereketwa wa klabu 200,000 @10,000 = 2,000,000,000
9 Wanachama-A 10,000 @ 500,000 = 5,000,000,000
10 Wanachama -B 200,000 @ 5,000 = 1,000,000,000
11 Wanachama - C 200,000 @ 1,000 = 200,000,000
12 Matawi ya Klabu 20 @ 1,000,000 = 20,000,000
13 Taasisi Rafiki wa Klabu 20 @ 1,000,000 = 20,000,000
14 Makampuni 15@ 5,000,000 = 75,000,000
15 Balozi- Nchi Rafiki 5 @ 5,000,000 = 25,000,000
16 Mechi za Timu 25 @ 10,000,000 = 250,000,000
Jumla 12,140,000,000
Hivyo kwa mchanganuo huo na kwa kushirikiana na vyombo vya habari nchini; klabu itajikusanyia mtaji wa kutosha kwa maendeleo yake kiuchumi na kisoka.
Napendekeza pia wadau kutoa mawazo endelevu kwa viongozi na wanachama kwa kutumia vyombo mbali mbali vya mawasiliano mfano TV, emails, radio, internet, n.k. Kwa mijadala hii ya kimaendeleo kwa viongozi na wanachama inaweza kuwa mawazo chanya kwa maendeleo ya soka letu la Tanzania.
Nawasilisha mjadala kwenu,
Emmanuel Rutatora
Mdau wa Soka – Rorya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Ni ngumu kutoa pesa kama msaada tu ivi ivi,cha msingi ni yanga iandae strategic plan document na policy ya kufanya mabadiliko ya kimuundo kutoka ilivyo na kua kampuni then watu wanunue hisa ambazo hisa hizo zitagawanywa katika categories za preferance shares na ordinary shares,na itengeneze commitment policy ya namna itakakavyosimia uwekezaji huu,hapo watu watatoa pesa lakin kwa muundo wa sasa ukitoa pesa ni kama umetoa pesa ya rambirambi coz hakuna mpango mkakati makini,hakuna policy ya kubadili muundo na hakuna comitment policy ya kusimamia na kutekeleza huo uwekezaji na hakuna usalama wa pesa hizo wakila nani atawadai? ni hayo tu
ReplyDeleteChela wa dom
Ungewasaidia na jinsi ya kuzila...
ReplyDelete