Search This Blog
Wednesday, February 1, 2012
SIMBA YAITANDIKA OLJORO MABAO 2:0
Nyota wa Kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi
amekihakikishia kikosi chake cha Simba, makazi ya
kudumu, kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara, baada
ya kufunga magoli mawili yaliyoipa ushindi wa 2-0,
dhidi ya JKT Oljoro.
Okwi raia wa Uganda, aliyeingia mwanzoni mwa
kipindi cha pili katika dakika ya 46, kuchukua nafasi
ya Kago Gervais.
Alifunga magoli hayo, la kwanza dakika ya 59,
kutokana na krosi ya Uhuru Suleiman, bao la pili,
alilifunga dakika 83 pasi ilitoka tena kwa Uhuru,
aliyepapokea pasi ya Patrick Mafisango.
Kuingia kwa Okwi ambaye hakuwa katika maandalizi ya pamoja na kikosi hicho kwa muda mferu kutokana na kupatwa matatizo nchini mwake ni baada ya
Haruna Moshi 'Boban' kuonyeshwa kadi nyekundu
dakika ya 44 na kuifanya safu ya ushambuliaji kupwaya.
Boban alipewa kadi hiyo ya moja kwa moja na
mwamuzi, Isihaka Shirikisho kutoka Tanga kwa kosa
la kumrudishia rafu beki wa Oljoro, Omary Mtaki
ambaye awali ndiye alianza kwa kumpiga kichwa.
Alifanya hivyo kutokana na kushindwa uvumilivu,
kutokana na rafu za mara kwa mara alizokuwa
akichezewa, awali alipigwa kichwa na Karage
Mgunda kabla ya hiyo ya pili.
Katika mchezo huo, ambao Oljoro inayosifika
kucheza safi, haikuonyesha kiwango cha juu na
kuwafanya Simba, watawale mchezo huo hasa
kipindi cha pili.
Bakari Kigodeko wa Oljoro itabidi ajutie nafasi za
wazi alizopoteza, dakika ya 62 na 70, aliingia ndani
ya 18 langoni mwa Simba, lakini akakosa maamuzi
na mipira yote kunyang'anywa na mabeki wa Simba.
Kocha mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic
ameuzungumzia mchezo huo ulikuwa mgumu, lakini
akasifu kiwango cha wachezaji wake.
Kutokana na kadi nyekundu ya Boban, Milovan
alisema; ''Boban hakustahili kadi nyekundu,
mwamuzi angeweza kumpa njano.''
Ally Kidi ambaye ni kocha wa JKT Oljoro aliwasifu
pia, nyota wake walicheza kiwango cha juu
kulingana na mazingira ya Uwanja wa Taifa.
''Wamejitahidi, kucheza katika Uwanja mkubwa
kama huu na mara ya kwanza ni kazi kwa vijana
wangu, kwani ni mara ya kwanza,''alisema Kidi.
Simba itaongoza ligi kwa pointi 34, Yanga ya pili ina 31 na Azam FC ni ya tatu ina 29, timu hizo zimecheza mechi 15 kila moja.
Simba
1 Juma Kaseja
2 Said Nassoro 'Cholo'
3 Amir Maftah
4 Shomari Kapombe
5 Kelvin Yondan
6 Jonas Mkude
7 Uhuru Suleiman / Ramadhan Singano dk 88
8 Mwinyi Kazimoto
9 Kago Gervais / Okwi dk 46
10 Haruna Moshi 'Boban'
11 Patrick Mafisango
JKT Oljoro
1 Said Lubawa
2 Omary Mtaki
3 Ally Omary
4 Omary Mtaki
5 Marcus Ndeheli
6 Ally Mkanga
7Karage Mgunda / Meshack Nyambele dk 65
8 Sunday Paul
9 Bakari Kigodeko
10 Amiry Omary
11Rashid Nassoro
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Hivi kweli huyu aliyeandika stori hii alikuwa uwanjani kweli? Yaani mimi nashindwa kuelewa iweje uandike stori na ushindwe kuweka picha ya kutoka kwenye tukio na sio picha kutoka maktaba? Hata caption hukuweka, na huu sio uwanja wa Taifa (Ben Mkapa) ni Chamazi uwanja wa Azam....jamani mtajifunza lini???
ReplyDelete