Search This Blog

Wednesday, February 1, 2012

HABARI NA MATUKIO YA MICHEZO YALIYOJIRI MKOANI MBEYA!



NA Junior MATUKUTA-Mbeya.

1.Ligi ya Mkoa wa Mbeya inaendelea hatua ya makundi na mechi kadhaa zimechezwa,

i)TZ Prisons Veteran(Chuma Chakavu) vs Mbalizi Rangers > 1-1

ii)Eleven Killers vs Scorpion> 3-0

iii)Mlowo United vs Kawetele> 1-1

iv) Boma United vs Chunya United> 3-0


2.Wachezaji wa Timu ya Mkoa wa Mbeya(Mapinduzi Stars) wameulalamikia Uongozi wa chama ya soka Mkoani hapa,Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya baada ya kushindwa kutimiza ahadi zao za kuwapatia Viwanja kwa ajili ya Ujenzi wa nyumba kama Zawadi baada ya Kutwaa ubingwa huo mwaka jana 2011 mkoani Arusha.
Nikiongea na wachezaji hao kwa nyakati Tofauti wamesema tayari wamashalipia kiasi cha Tsh 5000/= kama malipo ya usajili wa viwanja hivyo ktk ofisi za Ardhi,lakin mpaka leo hilo suala limebakia kuwa Danadana na ikizingatiwa Mkuu wa Mkoa aliyekuwepo kipindi hicho Mhe.John Mwakipesile tayari ameshastaafu na ndiye akilitoa agizo hilo la wachezaji hao kupewa Viwanja.

Wachezaji hao IDD AJIRO,DAVID MWANTIKA,LUGANO MWANGAMA na SAID MTUPA wameomba kupitia kipindi chenu cha Michezo cha SPORTS EXTRA kufikisha Ujumbe kwa wahusika hili watimize ahadi yao hiyo.


3.Pia Timu ya TZ Prisons inaendelea na Mazoezi yake ktk Uwanja wa Sokoine kwa ajili ya Mechi yake na Timu ya MBEYA CITY COUNCIL na Timu nyingine kwenye mzunguko wa pili wa ligi Daraja la kwanza Taifa,Timu hiyo ipo chini ya Kocha John Makatta na msaidizi wake Rungwe

No comments:

Post a Comment