Search This Blog

Wednesday, February 1, 2012

CHICHARITO NA BERBATOV WAWAPELEKA UNITED KILELENI SAWA NA CITY


MATOKEO YA ENGLISH PREMIER LEAGUE
Manchester United 2-0 Stoke City
Everton 1-0 Man City
Liverpool 3-0 Wolves


UPANGAJI MATOKEO WAWAPELEKA WACHEZAJI 67 WA ZIMBABWE JELA YA SOKA


Chama cha soka cha Zimbabwe (ZIFA) kimewasimamisha wachezaji 67, wakiwemo wengi wa timu ya taifa, kufuatia uchunguzi wa muda mrefu juu ya tuhuma za upangaji matokeo ya mechi.
Uchunguzi wa muda mrefu ulioanza mwaka jana  ulipelekea wachezaji wengi kukiri kupokea fedha kutoka kikundi cha kiasia ili kupoteza mechi walizoenda kucheza huko mashariki ya mbali kutokea mwaka 2007-09.
Ripoti ya ZIFA inasema pesa hizo zilikuwa zikitolewa na wakala ambaye ni raia wa Singapore Wilson Raj Perumai, ambaye kwa sasa yupo jela nchini Finland kwa makosa ya kupanga matokeo ya mechi nchini humo.
Katika taarifa iliyotolewa na CEO wa ZIFA Jonathan Mashingaidze alisema wachezaji waliokutwa na hatia wote hawatakiwi kuitwa timu ya taifa mpaka watakaposafishwa majina yao na kamati ya maadili.
Nahodha wa zamani wa Zimbabwe Method Mwanjali na wachezaji wengine wakubwa Daniel Vheremu, Benjamin Marere na Thomas Sweswe walitoa ushahidi wa kupokea pesa pamoja na mjumbe wa jopo la makocha, Joey Antipas.
Katika listi ya wachezaji waliofungiwa pia wapo wachezaji muhimu wa timu ya taifa kama Nyasha Mushekwi, Khama Billiat na Ovidy Karuru.

KALI YA LEO: HIVI ALIKOSAJE HILI GOLI?

Tuesday, January 31, 2012

SIKU YA MWISHO YA USAJILI: USAJILI ULIOKAMILIKA MPAKA SASA

Siku nzuri kwa Everton baada ya kumsaini Jelavic, kasha kuwafunga City sasa wamefanikiwa kumsaini Steven Pienaar kwa mkopo hadi mwisho wa msimu.

Sebastien Bassong wa Tottenham amejiunga na Wolves kwa mkopo hadi mwisho wa msimu. Pia Ryan Nelsen amejiunga na Tottenham akitokea Blackburn.

David Pizarro amejiunga na Manchester City akitokea AS Roma kwa mkopo mpaka mwisho mwa msimu.


Louis Saha anaelekea jijini London kujiunga na Tottenham Hotspur kwa mkopo wa miezi 6, baada ya Everton kumsaini Nikica Jelavic kutoka Rangers. Saha anaenda Spurs kama mbadala wa Pavlyuchenko aliyeenda Lokomotiv Moscow.

Manchester United wamemsaini kinda kutoka Manchester City Frederic Vessel.

Roman Pavlyuchenko amejiunga na Lokomotiv Moscow kutoka Tottenham Hotspur.

Bobby Zamora anafanyiwa vipimo  @ QPR lakini bado makubaliano baina ya mchezaji na QPR hayajamalizika.


Official, Arsenal wamemsaini Thomas Eisfeld kutoka Dortmund.

Mchezaji kinda wa Manchester United Ravel Morrison amejiunga na West Ham kwa ada ya uhamisho ya £650,000.



Sulley Muntari - Inter (Getty Images)
Klabu ya AC Milan imethibitisha imemsajili kwa mkopo Sulley Muntari kwa mkopo kutoka kwa mahasimu wao wakubwa Inter Milan mpaka mwishoni mwa msimu.


Paris Saint Germain wamekamilisha uhamisho wa Thiago Motta kutoka Inter Milan kwa ada ambayo haijatajwa.


  • Barcelona wamefikia makubalianao ya kumuachia kiungo wa zamani wa Arsenal Alexander Hleb kutoka katika mkatba aliokuwa nao na klabu hiyo. Hivyo kuanzia sasa Hleb ni mchezaji huru.




QPR wamekamilisha usajili wa mshambuliaji Djibril Cisse kutoka Lazio kwa ada ya uhamisho ambayo haijatajwa.



Bolton Wonderers wamekamilisha usajili wa mkopo wa kiungo wa kijapan Ryo Miyaichi kutoka Arsenal.

MAMA YAKE DROGBA MPISHI WA MASHABIKI IVORY COAST NCHINI GUINEA


Huku mwanae akiwa kiwanjani kutetea heshima ya nchi yake. Mama yake amekuwa yupo jikoni akiwaandalia chakula mashabiki wa nchi hiyo waliosafiri kwenda Equatorial Guinea katika michuano ya African Cup of Nations.
Clotilde Drogba ana majukumu ya kuwapikia kuku na samaki pamoja na wali mashabiki Ivory Coast, huku mwanae akiwa anakula katika hotel na wachezaji wengine.

Mrs.Drogba pia amewahi kuwaandalia mashabiki msosi katika fainali za kombe la dunia mwka 2006 nchini Ujerumani.
Drogba ni moja ya watu maarufu sana nchini Ivory Coast – mwaka jana alitangazwa kuwemo katika kamati ya usuluhishi ya mgogoro wa kisaisa uliotokea baada ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.
Kikundi cha washabiki zaidi ya 60 wamesafiri mpaka Equatorial Guinea, ambapo timu ya Ivory Coast ndipo ilipochezea mechi zao za ufunguzi – na kila siku kiukundi cha washabiki kinakula chakula cha asili kinachopikwa na mama yake Drogba.
“Kila mtu anacho kitu ambacho anapenda kufanya,” Mrs Drogba akiwa kavaa nguo ya rangi ya orange aliiambia AP baada ya kuandaa chakula cha mchana.
“Hii sio kwa ajili ya mwanangu, nafanya hivi kuisapoti nchi yangu.”
Mama yake Drogba pia aliwaaambia AP kwamba aliangalia mechi mbili za Ivory Coast katika TV-huku akiwa anakata vitunguu na nyanya kwa ajili kuwaandalia chakula mashabiki. Pia aliongeza ana imani ataweza kuangalia mechi za nusu fainali katika uwanja wa Bata – ikiwa Drogba na wenzake watafanikiwa kufika hatua hiyo.


YANGA NA ZAMALEK HAWACHEKANI!

zimesalia siku chache kabla ya Mabingwa wa soka kwa mujibu wa  Ligi kuu ya Tanzania Bara Dar Es Salaam Young Africans hawajatupa karata yao ya kwanza kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika safari hii wakivaana na Zamalek Sc ya nchini Misri.
Hadi kufikia tarehe 18 ambapo mchezo huu utakuwa unachezwa Yanga watakuwa wamepata michezo kadhaa ambayo kwa upande wake itakuwa majaribio muhimu ama sehemu ya maandalizi .
Rekodi haionyeshi matumaini kama Yanga wanaweza kweli kuitoa Zamalek lakini rekodi hizi hizi kwa kawaida huwa zinawekwa ili zivunjwe na mwamuzi wa mchezo ni dakika 90 na kwa hatua kama hii ni dakika 180 za michezo miwili yaani ule wa nyumbani na wa ugenini.
Bahati mbaya zaidi ni ukweli usiopingika ambao wote tunaufahamu juu ya maandalizi mabovu ya timu za Tanzania kuelekea michezo mikubwa kama hii. Zamalek ni moja ya timu 3 bora barani Afrika kwa kipindi cha karne iliyopita na wana historia ambayo inatosha kuzifanya timu nyingi ziogope hata kuwakaribia.
Lakini kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita rekodi hazizungumzi vizuri kuhusu Zamalek na hapa ndio watanzania wanaweza kutazama na kuona matumaini yalipo. Zamalek haijaonja mafanikio kwenye michuano ya kimataifa kwa zaidi ya miaka mitano na mara ya mwisho walitolewa kwenye raundi ya pili na Club Africain ya Tunisia.
Ukirudi kwenye ligi kuu nchini Misri Zamalek mwenendo wake umekuwa wa kusuasua kwa muda sasa na imepita miaka takribani saba Klabu hii haijaonja ladha ya mafanikio ya ubingwa wa ligi kuu na ahueni yake ya kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa imekuwa nafasiiliyo nayo nchi ya Misri kwenye viwango vya ubora vya CAF ambavyo vinaipa nchi hii fursa ya kutoa washiriki wawili kwenye michuano ya Klabu bingwa barani afrika.
Hata hivyo hayo hayatoshi kuwafanya Yanga waone wepesi wa kuitoa Zamalek kwani bila shaka kila mmoja anatambua kuwa Yanga ndio vibonde kwenye mchezo huu nab ado Zamalek wanabaki kuwa tishio kwa Yanga hivyo lazima kazi ifanyike ili Yanga ifanikiwe kuitoa klabu hii toka Misri.
Katika msimu huu wa ligi ya Misri , Zamalek hadi sasa wanashika nafasi ya Tatu nyuma ya Klabu za Al Ahly wanaoshika usukani wa Ligi hiyo na Haras El Hadoud wanaoshika nafasi ya pili . Cha ajabu ni kwamba Klabu hizi zilizoko mbele ya Zamalek zote zimeshawahi kucheza na klabu za Tanzania Yanga wakiwemo pamoja na Simba kwa nyakati tofauti . Zamalek hadi sasa zikiwa zimechezwa raundi 14 za michezo ya ligi kuu wamefaikiwa kushinda jumla ya michezo 10 huku wakipoteza miwili na kutoka sare miwili . Katika michezo hiyo Zamalek wamejikusanyia jumla ya pointi 32  ambapo wamefanikiwa kutikisa nyavu za wapinzani wake mbalimbali mara 27 na kwa upande wao wenyewe wameruhusu wavu wao kuguswa mara zisizopungua 11 . Katika kikosi hi jukumu la ufungaji limemwangukia kiungo Ahmed Hassan ambaye hadi sasa amefunga mabao 7 . Ahmed Hassan hayuko peke yake , Zamalek ina nyota wa kutosha ambao wana uwezo wa kuifanya timu yoyote ‘kitu mbaya ‘ pale itakapokutana nayo . Kuna watu kama Amr Zaki na Ahmed Hossam Mido ambao wamerudi nyumbani baada ya kuhangaika ulimwenguni kote wakicheza soka la kulipwa . Uwezo wa watu hawa unafahamika kwa watu wote na hakuna jipya ambalo halijawahi kuzungumzwa kuwahusu . Mido amekuwa akifunga mabao katika ngazi ya juu ya mchezo wa soka kwenye ligi mbalimbali barani ulaya hususani kwenye ligi kama za England ambako amewahi kuzichezea Tottenham Hotspurs na Middlesborough, Ligi ya Serie A , Ufaransa na sehemu nyingi tu . Zaki amewahi kuichezea Wigan Athletic ambako mabao yake 9 kwenye michezo kadhaa misimu miwili iliyopita yaliwafanya hata Liverpool wamzungumzie mchezaji huyu. Nyuma ya washambuliaji hawa yuko kiungo mahiri pengine kuliko wote kwenye soka la Misri kwa miaka ya hivi karibuni Mahmoud Abd El Razak maarufu kwa jina la Shikabala na wote hawa wako chini ya kocha mwenye historia ya kipekee barani Afrika Hassan Shehata ambaye amerejeshwa kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Hossam Hassan aliyeachia ngazi miezi michache iliyopita.
Rekodi za Yanga kwa msimu huu hazitofautiani sana na Zamalek hadi kufikia hatua hii . Juzi tu Yanga wamecheza mchezo wake wa 15 ambapo walifanikiwa kupata ushindi wa 3-1 dhidi ya JKT RUVU . Yanga imekusanya jumla ya pointi 31 huku wakiwa wameshinda michezo 9 , wametoka sare michezo minne na wamepoteza michezo miwili. Kwenye ufungaji bado Yanga haitofautiani sana na Zamalek wakiwa wamekusanya jumla ya mabao 25 huku wakiruhusu wavu wao kuguswa mara 12.  Mshambuliaji toka Ghana Kenetth Asamoah amekuwa kinara ambapo amefunga mabao 9 .
Takwimu zinafanana kwa kiasi Fulani lakini ukiangalia ligi za nyumbani ambazo timu hizi mbili zinashiriki hapo ndio unapoweza kuona tofauti kubwa baina ya timu hizi mbili ilipo.Wanadamu huamini kuwa hakuna jambo linaloshindikana chini ya jua na mashabiki , wapenzi , viongozi na wachezaji wa Yanga wataamini vivyo hivyo lakini kwa yale yanayowezekana baada ya dhana hii ya hakuna kinachoshindikana huwa wanafanya vitu Fulani ambavyo vinawafanya wawe na hali ya kustahili kufanya yale wanayotaka . Maana yake ni kwmaba Yanga wanapaswa kufanya maandalizi yatakayowafanya wastahili kupata ushindi na sio kuishia kutegemea bahati .
Endapo maandalizi ya ukweli na ya dhati yatafanyika kweli hakuna kinachoshindikana chini ya jua na hata kwenye uwanja wa mita mia moja kwa sitini za uwanja wa mpira ambao Yanga watacheza na Zamalek hiyo tarehe 18 na wiki mbili baada ya hapo kwenye mchezo wa marudiano.

WAMISRI KUICHEZESHA STARS FEB 29

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Misri kuchezesha mechi ya kwanza ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za 29 za Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Tanzania na Msumbiji. Waamuzi watakaochezesha mechi hiyo namba 25 itakayochezwa Februari 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni Farouk Mohamed atakayekuwa mwamuzi wa kati. Wasaidizi wake ni Ayman Degaish na B.T Abo El Sadat wakati mwamuzi wa akiba ni Ghead Grisha. Kamishna wa mechi hiyo ni Loed Mc Ian wa Afrika Kusini. Mchezo wa marudiano kwa ajili ya fainali hizo zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini utafanyika jijini Maputo baadaye mwaka huu.

NAHODHA TWIGA STARS KUCHEZA UTURUKI



Nahodha wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanawake (Twiga Stars), Sophia Mwasikili ameondoka jana alfajiri (Januari 30 mwaka huu) kwa ndege ya Turkish Airlines kwenda Uturuki kucheza mpira wa kulipwa. Mwasikili amekwenda kujiunga na Luleburgazgucu Spor Kulubu inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza ya Wanawake nchini humo. Beki huyo wa kati wa Twiga Stars aliyekuwa akichezea timu ya Sayari Women amejiunga na klabu yake hiyo mpya kwa mkataba wa miaka miwili. Awali Mwasikili alitakiwa kujiunga mapema na timu hiyo lakini alilazimika kusubiri kwanza mechi ya marudiano ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) kati ya Twiga Stars na Namibia (Brave Gladiators) iliyochezwa Januari 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

CLOUDS MEDIA GROUP YAIPATIA TWIGA STARS SHILINGI MILIONI MOJA.

HAPA NIKIMKABIDHI BWANA EDWINI HUNDI YENYE THAMANI YA TSH 1,000,000 KWA NIABA YA CLOUDS MEDIA GROUP.


Kampuni ya Clouds Media Group imemkabidhi hundi yenye thamani ya Tsh milioni moja ( 1,000,000) mkurugenzi mtendaji wa kampuni Edge Entertainment Ltd bwana Edwin Ngere.
Kampuni hiyo imepewa jukumu na TFF la kukusanya michango ya Twiga Stars.
Shaffih Dauda akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Clouds Media Group Bwana Joseph Kusaga amesema wameamua kutoka kiasi hicho cha pesa ili kiwe kianzio cha kufunguliwa Akaunti maalum ya Twiga Stars ili pesa zinazokusanywa na wadau mbali mbali ziingizwe kwenye iyo akaunti ya Twiga stars.

KALI YA LEO: GOLI LA KISIGINO LA MBALI KULIKO YOTE

ZIFAHAMU REKODI ZA FC BARCELONA


**Lionel Messi ndiye mchezaji pekee wa Barcelona kuwahi kushinda tuzo ya Uchezaji bora wa Dunia, Ballon d’Or, Pichichi na Kiatu cha dhahabu katika msimu mmoja. Alifanya hivyo katika msimu wa 2009/10.
***Na imetokea mara tu katika historia ya Barcelona kwa wachezaji watatu ambao wametokea katika timu ya vijana na kucheza pamoja katika timu ya wakubwa kuteuliwa kugombea tuzo ya Ballon d’Or: Messi, Xavi na Iniesta waligombea mwaka 2010.

***Pep Guardiola ndio kocha aliyeshinda mataji mengi kuliko katika historia ya klabu ya Barcelona. Ameshinda mataji 12 kati aya 15 aliyopaswa kushinda.

***Victor Valdes ndio golikipa aliyecheza kwa dakika nyingi bila kuruhusu wavu katika historia ya Barcelona. Akiwa amecheza dakika 877 katika msimu wa 2011/12.

***Ronaldo De Lima na Lionel Messi ndio wachezaji pekee wa Barcelona ambao wamewahi kushinda tuzo ya kiatu cha dhahabu. Ronaldo katika msimu wa 1996/97 akifunga mabao 34, na Messi katika msimu wa 2009/10 akifunga mabao 34.
*********Rekodi nyingine za klabu hii bora kabisa ulimwenguni tutaendelea kuzitoa kila siku mpaka tutakapomaliza******************************

AZAM WAZIDI KUTESA LIGI KUU - WAIADHIBU MORO UNITED CHAMAZI


Goli pekee la mshambuliaji mahiri wa Azam FC, John Bocco limeipatia Azam FC pointi tatu muhimu katika mchezo waligi kuu baada ya kuifunga Moro United 1-0, mchezo uliochezwa leo uwanja wa Azam Chamazi jijini Dar es Salaam.
Azam FC walipata ushindi huo wa pili mfululizo katika mzunguko huu wa mwisho wa ligi kuu ya Vodacom, VPL msimuwa 2011/2012 na kufikisha jumla ya pointi 29 katika msimamo wa ligi hiyo.
Bocco amefunga goli hilo katika dakika ya 11 ya mchezo akitumia uzembe wa mabeki wa Moro na kupiga shutilililomshinda kipa wa Moro, Jackson Chove.
Kufuatia goli hilo, Bocco anaongoza wafungaji katika ligi kuu kwa kufikisha magoli 10 akiwa mbele ya KenethAsamoah wa Yanga mwenye magoli 9.
Azam walianza kutafuta goli mapema ndani ya dakika tano za kwanza walifanya mashambulizi matatu ambayohayakuzaa matunda.
Baada ya goli hilo Moro United walifanya mashambulizi wakitaka kusawazisha dakika ya 21 Kelvin Charles alipigampira wa adhabu ukaokolewa na kipa Mwadini wa Azam na kipindi cha pili Simon Msuva anayeichezea Moro Unitedkwa mkopo akitokea Azam FC, alifanya mashambulizi mawili dakika ya 60 na 86 lakini hakuweza kubadilishamatokeo hayo.
Azam walitengeneza nafasi nyingi walikosa kumalizia, Kipre Tchetche akiwa na kipa Chove alishindwa kufungakatika dakika ya 25 na Mrisho Ngassa alishindwa kufunga dakika ya 63.
Mabadiliko katika mchezo huo Azam waliwarejesha benchi dk 60, dk 75 Abdi Kassim ‘Babi’ na na Kipre Tchetchenafasi zao zikichukuliwa na Ibrahim Mwaipopo na Zahoro Pazi na baadaye dk 77 John Bocco akampisha GaudenceMwaikimba.
Kocha wa Azam FC, Stewart Hall amesema matokeo ya mchezo huo yanatoa nafasi ya kujiweka vyema katikakumalizia mzunguko huu, japokuwa timu yake haikufanya vizuri katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo.
Akizungumzia kukosekana ka Michael Kipre pacha wa Tchetche alisema bado hati yake ya kucheza ligi ya Tanzaniabara bado haijawasili kutoka nchini Ivory Coast. Stewart alisema pengo la Kipre ni kubwa sana
Mbali na mchezaji huyo beki Erasto Nyoni hakuweza kucheza kutokana na kufiwa na mama yake mzazi haliiliyopelekea wachezaji wa Azam FC kuvaa vitambaa vyeusi wakati wa mechi.
Kikosi Azam FC, Mwadini Ally, Aggre Moris, brahim Shikanda, Wazir Salum, Said Morad, Salum Aboubakar ‘Sure Boy’, Abdulhalim Humud, Abdi Kassim/Zahor Pazi, Mrisho Ngassa, Kipre Tchetche/Ibrahim Mwaipopo na JohnBocco/Gaudence Mwaikimba.
Moro Jackson Chove, Tumba Swed, Fred Mbuna, Salum Kanoni, Meshack Abel, Gideon Sepo, Godfrey Wambura,Hilali Bingwa, Kelvin Charle/Simon Msuva, Benedict Ngassa na Andrew Kas

SUDAN YAITOA KIMASOMASO CECAFA, YATINGA ROBO FAINALI MATAIFA HURU.

IVORY COAST YAIFUNGASHA VIRAGO ANGOLA

MCHEZAJI BORA WA DUNIA UPANDE WA WANAWAKE AENDA BARCELONA


Mchezaji bora wa dunia kwa upande wa wanawake, Mjapani Homare Sawa atakuwa Barcelona-Spain kwa muda wa takriban wiki moja akiwa anafanya mazoezi na klabu yake ya INAK Kobe Leonessa.
Siku ya alhamisi mabingwa hao wa Japan wakiongozwa na Homare watacheza na timu ya wanawake ya klabu ya FC Barcelona katika mechi ya kirafiki ambayo itaonyeshwa na Barca TV.

Monday, January 30, 2012

MICHEZO MITANO AMBAYO INAWEZA IKAAMUA HATMA YA MANCHESTER CITY MSIMU HUU


Pindi mwezi January utakapoisha hapo kesho, tutakuwa katika kipindi muhimu cha ligi kuu ya England, baada ya kupita kipindi cha Christmas na Mwaka Mpya.
Kwa timu kama Manchester City, muda huu ndio hatma yao ya msimu itakapoanza kujulikana kiukweli.
Manchester City imekuwa timu ya kuogopwa msimu huu, ndio timu ambayo imefunga mabao mengi zaidi na kuruhusu wavu wao kuguswa mara chache zaidi, huku wakiwa wanaongoza ligi kuu kwa muda mrefu sasa.
Pamoja na mafanikio yote haya lakini mambo yanaweza kuenda mlama kabisa na kuharibika. Kutokana na hilo leo blog hii inajaribu kuangalia michezo mitano ambayo matokeo yake yatakuwa na uamuzi mkubwa wa hatma ya msimu huu utakavyokuwa kwa Manchester City.

UEFA EUROPA LEAGUE DHIDI YA PORTO (HOME & AWAY)

Michuano ya Europa League ndio pekee iliyobaki ambayo City wanaweza kushinda ukiachana na premier league.
Lakini je wataichukulia kwa umakini? Mchezo dhidi ya Porto utatoa majibu yote.
The Portuguese giants ni timu nzuri na uwanja wao wa Estadio do Dragao ni sehemu ngumu sana kushinda. Timu pekee ya England iliyofanikiwa kushinda mahala pale ni Manchester United – shukrani ziliendee oli la umbali wa yard 40 la Cristiano Ronaldo.
Ikiwa Manchester City watachezesha kikosi dhaifu katika mchezo wowote kati ya miwili dhidi ya Porto, tutafahamu kwamba mioyo yao haipo katika kutaka kushinda kombe hilo. To be fair, kushinda kombe la English premier league ndio nia kubwa na malengo ya Roberto Mancini.


MCHEZO DHIDI YA BLACKUBURN (ETIHAD STADIUM)
Mchezo unaofuatia baada ya Porto, ni watoto wa Steve Keane – Blackburn katika uwanja wa nyumbani wa City.
Kama, ikiwa mpaka mwishoni mwa February , rekodi ya City ikiendelea kuwa nzuri then watakuwa na nafasi kubwa na nzuri ya kuuchukua ubingwa wa England.
Muhimu zaidi, City wanatakiwa kushinda kila mechi ndani ya kipindi hiki kama wanataka kushindana na kuwazidi United mbele ya harakati ya kuchukua ufalme wa England.
Kwa hali ilivyo, kuwafunga Blackburn ni kitu ambacho kinaweza kutabirika , lakini ugumu unakuja Blackburn watakuwa katika hali gani kipindi wanakutana na City, kama watakuwa bado wapo katika danger zone ya kushuka daraja mechi inaweza kuwa ngumu zaidi na kutoa matokeo ambayo yanaweza yasiinufaishe City.

DHIDI YA STOKE CITY (BRITTANIA STADIUM)
Uwanja wa Brittania stadium ni sehemu ngumu kushinda, Timu nyingi kubwa zimeshahaibika mahala pale kwa silaha za Tony Pulis.
Wikeiendi hiyo pia United watakuwa wanaikaribisha Fulham at Old Trafford. Nafahamu mpaka sasa umeshaona mechi gani itakuwa ngumu – kwa mtazamo tu.
Huku mbio za ubingwa zikiwa zimepamba moto, hii ndio wiki ambayo City wanaweza waka drop points na kufanya mbio za ubingwa kuwa ngumu kwao.
MECHI DHIDI YA MANCHESTER UNITED (ETIHAD STADIUM)
Trehe 28th April, Manchester City watawakaribisha mahasimu na majirani zao katika mchezo ambao wengi wanasema unaweza ukaamua mbio za ubingwa.
Huu ndio mchezo ambao unaweza ukaamua ni upande upi wa Manchester utakuwa unasherehekea mwisho mwa msimu.
Manchester United sasa hivi wana kikosi dhaifu kuliko City. Unakumbuka lini hali ilikuwa kama ilivyo leo? Hii derby ambayo City watataka kuonyesha hawajabahatisha kuwafunga United katika ngwe ya kwanza, na kama watafanikiwa kuwafunga then wanaweza wakaji-establish kama ndio timu bora kwa sasa katika jiji la Manchester.
Pia tusisahau United pamoja na udhaifu iliyonayo ni timu ambayo ina uzoefu mkubwa, na imekuwa na tenderness ya kushangaza katika hali kama hii, tena wakichagizwa na hasira za kutaka kulipiza kisasi cha kufungwa goli 6-1 katika uwanja wao wa nyumbani, hivyo mambo yanaweza yakawa magumu sana siku hiyo.

MECHI DHIDI YA QUEENS PARK RANGERS (ETIHAD STADIUM)
Mchezo wa mwisho wa msimu. Unaweza ukawa mkubwa sana.
Ikiwa mpaka siku ya mwisho vita ya ubingwa uikiwa haijaamuliwa, Manchester City watahitaji kuwa cool na kucheza vizuri dhidi ya QPR – kitu ambacho ni rahisi kusema kuliko kufanya.
Tumeshashuhudia namna inavyokuwa vigumu kuwa mtulivu na na kudeal vizuri na pressure hasa katika mchezo ambao unaamua hatma yako ya ubingwa.
Itakuwa vigumu zaidi kwa City ikizangatiwa QPR na wao nao wanapigania kubaki katika EPL. Ikiwa watendelea kuwepo katika danger zone.

The law of Noceribra


The law of Noceribra. Ibra and Nocerino have between them scored half of Milan's goals for is the best attack in Serie A with 10 more goals than Juventus in the league: 22 of 43 in total.

TAZAMA MAISHA WANAYOISHI WACHEZAJI WA AZAM FOOTBALL CLUB



Huyo ni mchezaji HIMID MAO, katika kila chumba wanakaa wawili wawili tu.


Kila chumba kina AC, choo na bafu,DSTV fulltime, kila mtu ana kitanda chake, kambi yao iko pembeni ya uwanja wao, Mbagala Chamazi.


************Hili ndio basi la wachezaji wa AZAM FC.

WOLPER: HUNIAMBII KITU KUHUSU ARSENAL NA YANGA


Jana jioni katika kiota kimoja cha kucheck soka, blog hii ilikutana na mwanadada na mwanamaigizo Jackline Wolper akiangalia mechi kati ya Arsenal na Aston Villa huku akiendeleana shughuli zake nyingine.
Blog hii ikataka kujua machache kuhusu mapenzi ya mwanandada huyu katika ulimwengu wa soka.
Shaffih: Wolper wewe ni shabiki wa timu gani ndani na nje ya Tanzania?
Wolper: Mimi ni Yanga damu kwa hapa bongo, naipenda yeboyebo tangu nikiwa mdogo na nitaendelea kuipenda maisha. Kwa nje ya Tanzania mimi ni die hard fan wa The Gunners – Arsenal, huniambii kitu kuhusu hii timu, Gunners Forever.
Shaffih: Mchezaji gani anayekuvutia kimapenzi?
Wolper: Daa kwa nje nampenda sana Theo Walcott, he’s so cute. Bongo kiukweli hakuna mwanasoka anayenivutia kimapenzi ila napenda sana uchezaji wa Juma Kaseja wa Simba.
Shaffih: Unadhani nini kifanyike ili Arsenal waweze kurudisha makali yao?
Wolper: Mimi nafikiri Wenger kama amechoka vile, labda abadilishwe kocha na ufanyike usajili wa maana wa wachezaji wenye hadhi na class ya kuwemo katika kikosi cha Arsenal then kila kitu kitaenda poa tutawakalisha ManSIX united mpaka Barcelona.
Shaffih: Timu gani ambayo huipendi sana Bongo na nje?
Wolper: Kiukweli bila kuficha mimi siipendi sana na Manchester United kwa nje na hapa bongo siipendi ile timu ya pale mtaa wa msimbazi. Kwanza kwasababu ndio wapinzani wangu wakubwa na wakibahatisha kutufunga tu basi ni kelele hatari mpaka tunakosa raha.

YANGA IJIFUNZE KUPITIA MCHEZO DHIDI YA ZAMALEK!


Wakati ilipotoka ratiba iliyoonyesha kuwa Yanga watacheza na Zamalek kwenye hatua za awali za michuano ya Ligi ya mabingwa barani afrika watu wengi kwa haraka waliamiani kuwa mwanzo wa mwisho wa yanga umewadia . Ukitazama historia ya timu za Tanzania dhidi ya timu za kaskazini mwa Afrika unapata sababu ya kwanza ya kuona jinsi Yanga walivyo na kazi kubwa ya kufanya lakini ukiangalia rekodi ya Yanga kama klabu katika michezo yao dhidi ya Klabu za Uarabuni hapo ndio kabisa unaona kiza mbele kwani katika mara chache ambazo klabu za Tanzania zimeonyesha kujitutumua mbele ya timu toka Uarabuni Simba ndio imekuwa ikifanya hivyo na si Yanga.
Hii haimaanishi kuwa Yanga wanapaswa kukata tama moja kwa moja kwani ndio hali halisi ya ushindani wa soka mahali kokote pale hata barani ulaya kwa mtu yoyote anayepangwa kucheza na Barcelona anaona kama UEFA imemuonea kwani asilimia 90 ya matarajio ni kipigo .
Kitu kimoja ambacho klabu za Tanzania zimekuwa zikizembea ni kuchukulia changamoto ya kufanya vibaya kama chachu ya kujipanga na kufanya vizuri siku za mbeleni kwa sababu pale unapofungwa haimaanishi kuwa mchezo wa soka ndio umefikia mwisho , mbele kuna michezo mingine ambayo kama kweli umejifunza kupitia makosa ya nyuma lazima utafanya vizuri .
Zamalek ni moja ya timu tano bora za miaka yote barani Afrika , hivi majuzi tu klabu hii imetimiza miaka mia moja na sehemu walikofika inaendana ama unaweza kusema inaakisi umri waliofikia katika miaka yote hiyo kwani klabu hii imewekeza kwenye soka na ndio maani imefika hapa ilikofika.
Kwa ufupi tu Historia ya Zamalek ilianzia mwaka 1911 ambapo mwanasheria raia wa Ubelgiji aliamua kuanzisha timu ya mpira wa miguu aliyoipa jina la Kasr El-Nile Club . Klabu hii wakati ilipoanzishwa ilikuwa na tofauti na klabu nyingine kwani yenyewe haikuwa na matabaka ambayo yangemzuia mtu kujiunga nayo , kwa kifupi ilikuwa klabu ya kila mtu.
Katika historia yake Zamalek imewahi kutwaa mataji 11 ya ubingwa wa Ligi ya Misri pamoja na mataji 11 ya Kombe la Misri au Egyptian Cup. Kwa upande wa mataji ya kimataifa Zamalek imetwaa ubingwa wa klabu bingwa ya Afrika mara tano pamoja na ubingwa wa kombe la washindi barani afrika mara moja huku wakiwa na mataji matatu ya Caf Super cup.
Hata hivyo hali haijawa nzuri sana kwa Zamalek kwenye miaka ya hivi karibuni kwani hawajatwaa ubingwa wa ligi ya Misri kwa miaka saba sasa huu wa 2012 ukiwa wa nane na mara ya mwisho walionja ladha ya ubingwa huo mwaka 2004. Mwezi uliopita tu bodi ya uongozi wa Zamalek ilisitisha kazi ya Hossam Hassan kama kocha baada ya miaka miwili isiyokuwa na mafanikio na nafasi yake ikachukuliwa na gwiji wa klabu hii pamoja na timu ya taifa ya Misri Hassan Shehata ambaye ndiye amepewa jukumu la kumaliza ukame wa Zamalek kwenye soka la nyumbani na la kimataifa.
Msimu huu ulioisha safari ya Zamalek kwenye klabu bingwa ya Afrika iliishia kwenye hatua za awali kabisa mikononi mwa Club Africain ya Tunisia .


Tangu Shehata aingie kwenye benchi la Zamalek hali inaonekana kubadilika na wachezaji wanacheza kwa furaha tofauti na kipindi cha Hossam ambapo klabu hii ilikuwa inaoenekana kukosa muelekeo . Kwenye ligi Zamalek wana rekodi ya kushinda michezo minne kati ya mitano iliyopita wa mwisho ukiwa Alhamis iliyopita ambapo vijana wa Shehata waliifunga El Dakley 2-1.
Shehata amewarudisha washambuliaji mahiri wa timu ya taifa ya Misri ambao kwa muda waliwahi kucheza Zamalek Amr Zaki pamoja na Ahmed Hossam Mido ambao walikuwa barani ulaya kwa vipindi tofauti .Ukiwaacha hao , Zamalek pia inao wakali kama Razak Omotoyosi ambaye anatoka Benin pamoja na mtu ambaye wengi wanamtazama kama mchezaji bora wa misri katika miaka mitano iliyopita lakini hajawahi kupewa nafasi kwenye timu ya taifa Mahmoud El Razak Shikabala .
Hakuna anayeweza kusema kuwa Yanga watafungwa kirahisi na Zamalek kwani huenda rekodi ya mwaka 2003 ikajirudia na Zamalek ikatolewa na timu toka Tanzania lakini kinachobaki kama ukweli kwa Yanga ni kimoja tu kuichukulia michezo miwili dhidi ya Zamalek kama kozi muhimu ya mafunzo ya jinsi ya kuendesha soka kisasa na kuachana na mambo ya kizamani ambayo yanarudisha soka nyuma.

MAXIMO APATA TIMU.


EDO KUMWEMBE
KOCHA wa zamani wa Taifa Stars, Mbrazili Marcio Maximo, hatimaye amepata timu ya Ligi Kuu nchini mwake, baada ya kukabidhiwa kikosi cha E.C Democrata cheye maskani yake Jimbo la Minas Gerais.

Akizungumza na Mwanaspoti kutoka Rio de Janeiro anakoishi, Maximo alisema ameanza kazi ya kuifundisha timu hiyo tangu Novemba 2011 baada ya kumaliza kozi mbalimbali za mwendelezo za ukocha.

Ndiyo, klabu yangu mpya ni E.C Democrata inayoshiriki Ligi Kuu lakini katika Jimbo la Minas Gerais. Hapa Brazil kila jimbo lina ligi yake inayochezwa kwa miezi minne kabla ya kupata timu zinazokwenda kucheza Ligi Kuu ya ujumla, alisema Maximo aliyezaliwa jijini Rio de Jeneiro Aprili 29, 1962.

Niko hapa nafanya kazi na kila kitu kinakwenda safi. Nawatakia kila la kheri Watanzania na kamwe siwezi kuwasahau.

E.C Democrata ilianzishwa mwaka 1932 kufuatia ugomvi wa mashabiki wa klabu ya Flamengo ambapo baadhi yao walienda kuunda timu hiyo.

Inatumia uwanja wa nyumbani wa Mamudao ambao una uwezo wa kuchukua mashabiki 15,000.

Maximo aliteuliwa kuwa kocha wa Taifa Stars Juni 29, 2006 na akaondoka Juni 2010 baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kushindwa kumwongezea mkataba mwingine kutokana na mgawanyiko wa kihisia miongoni mwa mashabiki dhidi ya uwezo wa kocha huyo.

Kocha Zamalek ajiuzulu ghafla

NA MICHAEL MOMBURI
KOCHA wa makipa wa Zamalek itakayocheza na Yanga Februari 18 kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Ahmed Soliman, amejiuzulu ghafla Jumatatu iliyopita, klabu yake imethibitisha na Yanga wameshtukia dili wakacheka wakidai ni danganya toto.

Soliman, ambaye ni swahiba wa kocha mkuu Hassan Shehata, imeripotiwa kwamba amejiuzulu kutokana na sababu binafsi ingawa kipa namba moja, Abdel Wahed El-Sayed, ameeleza kukerwa na jambo hilo.

Nafasi ya kocha huyo imezibwa na Ayman Taher ambaye ni mchezaji wa zamani wa Zamalek.

Habari zaidi zinasema Soliman ameachia ngazi kutokana na kutoelewana na bodi ya sasa kuhusiana na masilahi yake, lakini amekuwa mzito kuweka mambo hadharani kila anapoulizwa sababu za kuondoka.

Kocha msaidizi wa Yanga, Fred Minziro aliposikia habari za kujiuzulu kwa Soliman alionyesha kushangaa.

Sisi tunakomaa tu na mipango yetu ya ndani ya uwanja kuhakikisha mambo yanakaa sawa wala hatuhangaiki na hao jamaa, wana mbinu nyingi sana na safari hii tutawadhibiti tu, japokuwa najua kuna baadhi ya watu wana wasiwasi, sisi tunajua tunachokifanya ndiyo maana tunajiandaa na kwa kila hali.

Timu bado haijakaa sawa lakini tutapambana, muda uliobaki tukizidi kuwa makini unatosha. Tumewasisitiza wachezaji kwamba huu si wakati wa kufanya mzaha wala uzembe, haya ni maisha yao wafanye kazi na wasikilize kile wanachoambiwa na kukitekeleza.

Tatizo la baadhi ya wachezaji wetu ni wazembe na uwajibikaji ni mdogo ndiyo maana unasikia malalamiko ya hapa na pale na hata timu inapoteza mchezo kutokana na uzembe.

Hivi sasa hatukitaki mambo hayo na sisi makocha tutakuwa wakali. Wachezaji wengine wanajitolea kwa nguvu zote lakini wengine wanaona kawaida tu.

Hakuna mambo mapya na makubwa kiasi hicho kama yanavyokuzwa, hizo fomesheni ni matamshi tu lakini timu inabadilisha staili ya uchezaji kila dakika kutokana na aina ya timu tunayocheza nayo na tunataka nini.

Mambo mengine hayahitaji kocha, yanahitaji akili za kawaida tu na juhudi za mchezaji husika. Ndani ya wiki chache mambo yatakaa vizuri.

Yanga inacheza na JKT Ruvu leo Jumamosi saa 12.00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa.

Katika hatua nyingine, kocha msaidizi wa Zamalek, Ismail Youssef, amemlaumu beki Hazem Emam kwa kujibizana na mashabiki waliokuwa wakimzomea mazoezini juzi Alhamisi jioni

Mnamkumbuka kocha huyu aliyeleta Raha Simba miaka ya 1990? Hapa yupo na 'Jembe' Mtwa Kihwelu



UNAMKUMBUKA HUYU ?


Wengi walimfahamu kama Arigo Sacch, ila huwezi kutaja mafanikio ya soka la Tanzania bila ya kumtaja kocha huyu ambaye kwa sasa ni marehemu, Zakaria Kinanda, hapa alikuwa na Ismail Aden Rage (mwenyekiti wa sasa wa Simba)

UNAKIKUMBUKA KIKOSI HIKI...kama ndio ebu KITAJE nikuone we MKAREEEE!

BARCELONA WAZIDI KUPOTEZA POINTI LA LIGA: WATOKA SARE NA VILLAREAL

REAL MADRID YAIZIDI BARCA KWA POINTI 7 SASA. WAIFUNGA ZARAGOZA 3-1

INTER MILAN HALI MBAYA : WAFUNGZWA NA LECCE

JUVENTUS WAIFUNGA 2-1 UDINESE

PENALTI 2 ZA VAN PERSIE ZAIVUSHA ARSENAL

AC MILAN WAZIDI KUTAMBA SERIE A

SHIBOLI APELEKA MSIBA MANUNGU, AITUNGUA MTIBWA SUGAR.


Timu ya wakata miwa wa Manungu Turiani – Mtibwa Sugar wamendelea kufanya vibaya katika hatua ya pili ya ligi kuu Tanzania bara baada ya kuchapwa na Coastal Union ya Tanga.


Mtibwa Sugar wamepoteza mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Manungu ukiwa ni mchezo wa pili kwa Mtibwa Sugar kupoteza katika uwanja huo wa Manungu.

Goli hilo la Coastal Union lilifungwa na Mshambuliaji wa Simba aliyopo Coastal kwa mkopo akitokea Kagera Sugar Ahmed Shiboli.

MSIMAMO WA VPL.
Kwenye Mabano Idadi ya Mechi Zilizochezwa.
1. Simba SC (14) 31
2. Yanga (15) 31
3. JKT Oljoro (14) 26
4. Azam FC (14) 26
5. Mtibwa Sugar (15) 22
6. Kagera Sugar (15) 20
7. JKT Ruvu (15) 17
8. Ruvu Shooting (15) 17
9. Moro United (14) 15
10. African Lyon (14) 14
11. Coastal Union (15) 14
12. Toto Africa (15) 13
13. Polisi Dodoma (14) 12
14. Villa Squad
(15) 10

ZAMBIA YAWAFUNGA GUINEA YATINGA ROBO FAINALI

SENEGAL WAFUNGWA TENA NA WALIBYA

Sunday, January 29, 2012

TWIGA STARS YAITANDIKA NAMIBIA MABAO 5-1

Timu ya Taifa ya Wanawake ya Soka Twiga Stars wamewasambaratisha Namibia kwa jumla ya magoli 7 kwa 2 na sasa wanawangoja kati ya Misri ama Ethiopia ambapo mchezo wa kwanza Misri walishinda goli 4-2.

Katika mchezo wa leo ambapo Twiga Stars wameibuka na ushindi wa goli 5-2 katika uwanja wa Taifa huku wa Namibia wakienda huku wakimkumbuka mshambuliaji alivaa jezi namba 8 Mwanahamisi Omary, kwanamna alivyokuwa wanawaenyesha mabeki wa timu hiyo.

Twiga Stars walianza kuandika goli la kwanza katika dakika ya 22 kupitia kwa Mshambuliaji Hatari na mwenye kasi Mwanahamisi Omar.

Goli hilo halikukaa sana kwani katika dakika ya 30 Albert Dakisi aliisawazishia goli hilo kwa mpira wa kona na yeye kuiunga kwa kichwa na mpira kutinga moja kwa moja nyavuni. Na kupelekea timu kwenda mapumziko wakiwa sare ya goli 1-1.

Katika kipindi Cha pili Mwanahamisi Omari aliyekuwa ana ama kila upande alimpa pasi murua Asha Rashidi katika dakika ya 47, ambapo Asha akufanya ajizi na kuundumbukiza mpira wavuni.

Baada ya goli hilo Namibia walikuja juu huku ukuta wa Twiga ukifanya makosa ya hapa na pale lakini Namibia walishindwa kuyatumia mpaka katika dakika 72, ambapo mpira ulidundishwa chini na mwamunzi ndani ya eneo la hatari ya Twiga stars baada ya Mwanahamisi Omary kuwa chini, wakati Twiga wakitegemea Namibia wangecheza fair play kwa kutoa mpira nnje mambo yalikuwa tofauti, kwani alitoa pasi ya goli huyo mchezaji wa Namibia na kuipatia goli la 2 Namibia.

Mwanahamisi Omari aliendeleza usumbufu wake safari hii akitokea kushoto, upande uliokuwa dhaifu kwa Namibia hii leo, kwa kuwalamba chenga mabeki wa Namibia na Kipa wake lakini mpira wake ulizuiwa na mlinzi na kumkuta Eto'o Mlenzi na kuifungia Twiga goli la 3 katika dakika ya 84.

Goli hilo liliwafanya Twiga kucheza soka safi na dakika ya 88 Asha Rashidi aliipatia Twiga Stars goli la 4 na la 5 likifungwa na Mwanahamisi Omari katika dakika 90 na mchezo kumalizika kwa Twiga kushinda goli 5-2.

Kwa ushindi huo Twiga Stars imeitoa Namibia kwa jumla ya goli 7-2 hivyo wanangoja mshindi kati ya Misri na Ethiopia. Na endapo wakishinda mchezo huo utakao chezwa mei watakuwa wamefuzu kwa mara ya pili mfululizo katika michuano ya 8 ya mataifa ya Africa itakayo fanyika Equaterial Guinea hapo november mwaka huu.

FRANCIS CHEKA AMDUNDA KALAMA NYILAWILA KWA POINT