Search This Blog
Monday, January 30, 2012
MAXIMO APATA TIMU.
EDO KUMWEMBE
KOCHA wa zamani wa Taifa Stars, Mbrazili Marcio Maximo, hatimaye amepata timu ya Ligi Kuu nchini mwake, baada ya kukabidhiwa kikosi cha E.C Democrata cheye maskani yake Jimbo la Minas Gerais.
Akizungumza na Mwanaspoti kutoka Rio de Janeiro anakoishi, Maximo alisema ameanza kazi ya kuifundisha timu hiyo tangu Novemba 2011 baada ya kumaliza kozi mbalimbali za mwendelezo za ukocha.
Ndiyo, klabu yangu mpya ni E.C Democrata inayoshiriki Ligi Kuu lakini katika Jimbo la Minas Gerais. Hapa Brazil kila jimbo lina ligi yake inayochezwa kwa miezi minne kabla ya kupata timu zinazokwenda kucheza Ligi Kuu ya ujumla, alisema Maximo aliyezaliwa jijini Rio de Jeneiro Aprili 29, 1962.
Niko hapa nafanya kazi na kila kitu kinakwenda safi. Nawatakia kila la kheri Watanzania na kamwe siwezi kuwasahau.
E.C Democrata ilianzishwa mwaka 1932 kufuatia ugomvi wa mashabiki wa klabu ya Flamengo ambapo baadhi yao walienda kuunda timu hiyo.
Inatumia uwanja wa nyumbani wa Mamudao ambao una uwezo wa kuchukua mashabiki 15,000.
Maximo aliteuliwa kuwa kocha wa Taifa Stars Juni 29, 2006 na akaondoka Juni 2010 baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kushindwa kumwongezea mkataba mwingine kutokana na mgawanyiko wa kihisia miongoni mwa mashabiki dhidi ya uwezo wa kocha huyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment