Search This Blog

Monday, January 30, 2012

Kocha Zamalek ajiuzulu ghafla

NA MICHAEL MOMBURI
KOCHA wa makipa wa Zamalek itakayocheza na Yanga Februari 18 kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Ahmed Soliman, amejiuzulu ghafla Jumatatu iliyopita, klabu yake imethibitisha na Yanga wameshtukia dili wakacheka wakidai ni danganya toto.

Soliman, ambaye ni swahiba wa kocha mkuu Hassan Shehata, imeripotiwa kwamba amejiuzulu kutokana na sababu binafsi ingawa kipa namba moja, Abdel Wahed El-Sayed, ameeleza kukerwa na jambo hilo.

Nafasi ya kocha huyo imezibwa na Ayman Taher ambaye ni mchezaji wa zamani wa Zamalek.

Habari zaidi zinasema Soliman ameachia ngazi kutokana na kutoelewana na bodi ya sasa kuhusiana na masilahi yake, lakini amekuwa mzito kuweka mambo hadharani kila anapoulizwa sababu za kuondoka.

Kocha msaidizi wa Yanga, Fred Minziro aliposikia habari za kujiuzulu kwa Soliman alionyesha kushangaa.

Sisi tunakomaa tu na mipango yetu ya ndani ya uwanja kuhakikisha mambo yanakaa sawa wala hatuhangaiki na hao jamaa, wana mbinu nyingi sana na safari hii tutawadhibiti tu, japokuwa najua kuna baadhi ya watu wana wasiwasi, sisi tunajua tunachokifanya ndiyo maana tunajiandaa na kwa kila hali.

Timu bado haijakaa sawa lakini tutapambana, muda uliobaki tukizidi kuwa makini unatosha. Tumewasisitiza wachezaji kwamba huu si wakati wa kufanya mzaha wala uzembe, haya ni maisha yao wafanye kazi na wasikilize kile wanachoambiwa na kukitekeleza.

Tatizo la baadhi ya wachezaji wetu ni wazembe na uwajibikaji ni mdogo ndiyo maana unasikia malalamiko ya hapa na pale na hata timu inapoteza mchezo kutokana na uzembe.

Hivi sasa hatukitaki mambo hayo na sisi makocha tutakuwa wakali. Wachezaji wengine wanajitolea kwa nguvu zote lakini wengine wanaona kawaida tu.

Hakuna mambo mapya na makubwa kiasi hicho kama yanavyokuzwa, hizo fomesheni ni matamshi tu lakini timu inabadilisha staili ya uchezaji kila dakika kutokana na aina ya timu tunayocheza nayo na tunataka nini.

Mambo mengine hayahitaji kocha, yanahitaji akili za kawaida tu na juhudi za mchezaji husika. Ndani ya wiki chache mambo yatakaa vizuri.

Yanga inacheza na JKT Ruvu leo Jumamosi saa 12.00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa.

Katika hatua nyingine, kocha msaidizi wa Zamalek, Ismail Youssef, amemlaumu beki Hazem Emam kwa kujibizana na mashabiki waliokuwa wakimzomea mazoezini juzi Alhamisi jioni

No comments:

Post a Comment