Jana jioni katika kiota kimoja cha kucheck soka, blog hii ilikutana na mwanadada na mwanamaigizo Jackline Wolper akiangalia mechi kati ya Arsenal na Aston Villa huku akiendeleana shughuli zake nyingine.
Blog hii ikataka kujua machache kuhusu mapenzi ya mwanandada huyu katika ulimwengu wa soka.
Shaffih: Wolper wewe ni shabiki wa timu gani ndani na nje ya Tanzania?
Wolper: Mimi ni Yanga damu kwa hapa bongo, naipenda yeboyebo tangu nikiwa mdogo na nitaendelea kuipenda maisha. Kwa nje ya Tanzania mimi ni die hard fan wa The Gunners – Arsenal, huniambii kitu kuhusu hii timu, Gunners Forever.
Shaffih: Mchezaji gani anayekuvutia kimapenzi?
Wolper: Daa kwa nje nampenda sana Theo Walcott, he’s so cute. Bongo kiukweli hakuna mwanasoka anayenivutia kimapenzi ila napenda sana uchezaji wa Juma Kaseja wa Simba.
Shaffih: Unadhani nini kifanyike ili Arsenal waweze kurudisha makali yao?
Wolper: Mimi nafikiri Wenger kama amechoka vile, labda abadilishwe kocha na ufanyike usajili wa maana wa wachezaji wenye hadhi na class ya kuwemo katika kikosi cha Arsenal then kila kitu kitaenda poa tutawakalisha ManSIX united mpaka Barcelona.
Shaffih: Timu gani ambayo huipendi sana Bongo na nje?
Wolper: Kiukweli bila kuficha mimi siipendi sana na Manchester United kwa nje na hapa bongo siipendi ile timu ya pale mtaa wa msimbazi. Kwanza kwasababu ndio wapinzani wangu wakubwa na wakibahatisha kutufunga tu basi ni kelele hatari mpaka tunakosa raha.
we are on the same truck Jacqueline Wolper
ReplyDeleteUmepotea kozi Wolper unazozipenda zote rusha roho hazina uhakika na unuzozichukia mdio zenye uhakika pole sana kwa ugonjwa wa moyo,au presha yako unaitibu kwa kitunguu Swaumu?
ReplyDeleteWe together jack on ARSENAL FOR LONG N LONG lakn kwa yebo yebo nipo nje kdogo mi nawakubal watoto wa AZAM
ReplyDeleteHuyu Wolper bwana.
ReplyDeleteSi aseme kama alivyovutiwa na Theo Walcot iwe sawa na kwa Kaseja,eti anazuga tu kwa kuwa JK ni mbongo!
Anazingua tu,huyo Walcot utamtamani milele na humpati ng'o! Bora J.K coz yuko karibu na he deserve!
She has every reason to be a fan of all the good clubs like Arsenal and Yanga.... Keep up Jack...
ReplyDeleteSafi sana wolper Yanga poa sana na arsenal usiwasikilze simba hao hawajui soka wanajua kuongea!
ReplyDelete