Chama cha soka cha Zimbabwe (ZIFA) kimewasimamisha wachezaji 67, wakiwemo wengi wa timu ya taifa, kufuatia uchunguzi wa muda mrefu juu ya tuhuma za upangaji matokeo ya mechi.
Uchunguzi wa muda mrefu ulioanza mwaka jana ulipelekea wachezaji wengi kukiri kupokea fedha kutoka kikundi cha kiasia ili kupoteza mechi walizoenda kucheza huko mashariki ya mbali kutokea mwaka 2007-09.
Ripoti ya ZIFA inasema pesa hizo zilikuwa zikitolewa na wakala ambaye ni raia wa Singapore Wilson Raj Perumai, ambaye kwa sasa yupo jela nchini Finland kwa makosa ya kupanga matokeo ya mechi nchini humo.
Katika taarifa iliyotolewa na CEO wa ZIFA Jonathan Mashingaidze alisema wachezaji waliokutwa na hatia wote hawatakiwi kuitwa timu ya taifa mpaka watakaposafishwa majina yao na kamati ya maadili.
Nahodha wa zamani wa Zimbabwe Method Mwanjali na wachezaji wengine wakubwa Daniel Vheremu, Benjamin Marere na Thomas Sweswe walitoa ushahidi wa kupokea pesa pamoja na mjumbe wa jopo la makocha, Joey Antipas.
Katika listi ya wachezaji waliofungiwa pia wapo wachezaji muhimu wa timu ya taifa kama Nyasha Mushekwi, Khama Billiat na Ovidy Karuru.
No comments:
Post a Comment