Search This Blog

Tuesday, October 18, 2011

THOMAS VERMAELEN ASAINI MKATABA MPYA NA ARSENAL

Pamoja na kuandamwa na majeruhi kwa muda mrefu akiwa na Gunners, Beki wa katik kutoka Ubelgiji Thoms Varmaelen amefanikiwa kuongezewa mkataba wa kuitumikia klabu hiyo ya kaskazini mwa London.

Arsenal wamethibitisha kuwa mlinzi huyo amesaini

mkataba mpya wa miaka 4 kuendelea kuwa Emirates.

The Belgium international star amekuwa akiandamwa na majeruhi kwa kipindi kirefu baada ya kuwa msimu mzuri wa kwanza na kufanikiwa kuwemo katika PFA Premier League Team of the Season in 2009-10.

Varmaelen amecheza mechi 54 so far akiwa na Gunners baada kuwasili kutoka Ajax ya Uholanzi na meneja wake Arsenal wenger amefurahi kwa beki kuongeza mkataba.

Wenger aliuambia mtandao wa klabu hiyo: “Tumefurahi kabisa kwamba Varmaelen ameongeza mkataba wa muda mrefu.Mipango yetu siku zote imekuwa ni kusaini wachezaji wenye quality hivyo kitendo cha Varmaelen kuongeza mkataba kinaonyesha dhamira yetu.Thomas ni mchezaji mzuri na special, ambaye siku zote amekuwa akijituma sana uwanjani.”

RAGE: TUPO TAYARI KUVUNJA MKATABA NA YONDANI


Uongozi wa klabu ya Simba kupitia mwenyekiti wake Aden Rage umesema suala la mchezaji wao Kelvin Yondani ambaye anatuhumiwa kwa utovu wa nidhamu, na kupewa barua mbili na ambazo hakujibu hata moja, sasa uongozi wa Simba pamoja na kamati ya ufundi umemtaka aje azungumze nasi kama anataka kuvunja mkataba na wako tayari.

Alisema kuliko kitendo cha kuongea na vyombo vya habari ni bora aende kuzungumza na uongozi na wao watamruhusu kama atahitaji kuondoka, kuliko kukaa kimya bila ya sababu.

Aliongeza kuwa kutokana na kosa la Yondani, wangeamua kuchukua hatua kwa kufuata kanuni za FIFA na za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ingemwia vigumu mchezaji huyo, kwani mchezaji akiwa na kosa la utovu wa nidhamu, anastahili kufukuzwa na haruhusiwi kwenda kujiunga na klabu yoyote mpaka uongozi wa timu husika aliyokuwa anaichezea ukubaliane na hilo.

SIMBA NA PROJECT YA KUJENGA JENGO LA GHOROFA 12 MSIMBAZI




Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam iko katika mikakati ya kuimarisha vitega uchumi wake, ikiwamo kujenga jengo la ghorofa 12 makao yake makuu ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kuacha kutembeza bakuli.



Katika kuelekea mipango hiyo, tayari wamezungumza na benki mbili tofauti zenye nia ya kupanga kwenye jengo hilo ambapo wanatarajia kuziweka hadharani hapo baadaye.



Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, alisema klabu hiyo kwa sasa ina mikakati mingi ya kujiweka vizuri kiuchumi, ili kuondokana na ukata, pamoja na kuishi katika jengo ambalo haliendani na hadhi ya klabu hiyo kubwa hapa nchini.



“Katika kufanikisha maendeleo mbalimbali ya klabu, nimeamua kuunda kamati mbalimbali ili klabu kuwa na manufaa na mimi kupunguza majukumu, kwa kuwa sasa nitakuwa na majukumu mawili tu la uwanja pamoja na mikakati ya maendeleo ya klabu,” alisema Rage.



Alizitaja kamati hizo kuwa ni ya Fedha, Mashindano, Ufundi, Usajili pamoja na Kamati ya Nidhamu.



Aliwataja wanaounda Kamati ya Fedha ambayo inaongozwa na Geodfrey Nyange ‘Kaburu’, ni Adam Mgoi, Makamu Mwenyekiti; huku wajumbe wakiwa Saidi Pamba, Kifiri, Zitto Kabwe, Juma Pinto, Abdul Mteketa na Murtaza Mangungu; huku Kamati ya Mashindano ikiwa na Joseph Itang’are (Mwenyekiti), Azim Dewji (Makamu Mwenyekiti), Jerry Ambe, Swedy Mkwabi, Hassan Hassanol, Mohamed Nassoro, Amosi Makala, Richard Ndasa na Suleiman Zakazaka (Wajumbe).



Kamati ya Ufundi ni Ibrahim Masoud (Mwenyekiti), Evans Aveva (Makamu Mwenyekiti), Dan Manembe, Khalid Abeid, Musley Rwekha, Mulamu Ng’hambi, Saidi Tuli, Rodney Chidua na Patrick Rweyemamu (Wajumbe), wakati Kamati ya Usajili wako Zacharia Hans Poppe (Mwenyekiti), Kasimu Dewji (Makamu Mwenyekiti), Francis Waya, Crecensius Magori, Salim Abdallah, Collins Frisch na Gerald Lukumay (Wajumbe).



Rage aliitaja Kamati ya Nidhamu kuwa ni Mwenyekiti, Peter Swai, huku Makamu Mwenyekiti akiwa Jamal Rwambow na wajumbe wakiwa Charles Kenyera, Evody Mmanda na Chaulembo.

WEZI WA TIKETI ZA TFF KUFIKIKISHWA MAHAKAMI



Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, linatarajiwa kuwafikisha mahakamani wakati wowote kuanzia sasa watuhumiwa wawili wa wizi wa tiketi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).


Hivi karibuni, TFF iliwakamata Seleman Masoud na Salum Abdallah wakati wa mechi ya Ligi Kuu Tanzania kati ya Yanga na Azam FC iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Septemba 18, mwaka huu, baada ya baadhi ya vitabu vya tiketi kuibiwa katika mazingira ya kutatanisha na watuhumiwa kukutwa nazo.


Kauli hiyo, imekuja siku chache baada ya baadhi ya wadau wa michezo, kulishutumu Jeshi la Polisi Mkoa huo, kwa kushindwa kuwafikisha mahakamani kwa muda mrefu watuhumiwa hao, hatua ambayo ilikuwa ikitafsiriwa kuwa walikuwa wanawalinda watuhumiwa.


Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Missime, alisema upelelezi wa kesi hiyo ambayo watuhumiwa walikamatwa na tiketi 300 na kuhojiwa katika kituo cha polisi Chang’ombe, umefikia hatua za mwisho kabla ya kupandishwa kizimbani.


Alisema upelelezi wa kesi hiyo ulikuwa mgumu kutokana mkanganyiko uliokuwapo, lakini vijana wake wamefikia hatua nzuri ambayo itawezesha kuwafikisha mahakamani watuhumiwa hao.


Watuhumiwa hao walikamatwa Septemba 18 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kufunguliwa jalada namba CHA/IR/6257/2011 ambapo mmoja wa wauzaji tiketi za mchezo huo, Seleman Masoud, aliripoti kupotelewa kitabu kimoja, mara baada ya ugawaji wa vitabu hivyo kufanyika asubuhi ya siku ya mchezo na baada ya uchunguzi kufanyika, baadhi ya mashabiki waliokuwa wamenunua tiketi walimtaja Salum Abdallah ambaye naye alitiwa mbaroni.



SIPATI PICHA KWENYE KIUNGO YUPO GAGA,CHINA NA MASHA,MBELE YAO MOGELLA


KUTOKA KULIA : HUSSEIN AMAN MASHA, ATHUMAN CHINA,ZAMOYONI MOGELLA,HAMIS THOBIAS GAGA HUYO MWINGINE MSAADA JAMANI...


KWA KIKOSI HIKI SIDHANI KAMA KUNA TIMU BARANI AFRIKA KWA HIVI SASA INGEKISUMBUA.... ANAYEBISHA AKITAJE KIKOSI AMBACHO KINGEWASUMBUA HAWA WANAUME.......NATAMANI KULIA MIE....KWELI WAKATI NI UKUTA !










KAMPUNI YA SMART SPORTS YAIDAI TFF tsh 51,265,125



Habari kaka,

Sasa ni hivi,kampuni yangu ya Smart Sports inalidai shirikisho la
mpira wa miguu nchini jumla ya Tsh 51,265,125.00,pesa hizi zote
nilikuwa natoa huduma ya usafiri katika shirikisho hilo kwa muda wa
zaidi ya miezi mitano, deni ni kuanzia april 2010 mpaka august
2010,wakati huo katibu mkuu alikuwa ni Mwakalebela.na kuanzia august
2010 alikuwa anakaimu Sunday kayuni.

Kilichokwamishwa kulipwa kwa wakati ni pale mwezi june TRA ilizifunga
account zote za Tff ili wazifanyiwe ukaguzi kwa vile walikuwa
wanakwepa kulipa mapato tra,na nakumbuka ilichukua kama miezi mitatu
mpaka september ndipo tra walipozifungua ac zao baada ya
kujiridhisha,lakini zilipofunguliwa hizo ac hapo ndipo lilipotokea
tatizo la kutowalipa wote waliokuwa wanalidai shirikisho hilo.

Baada ya Sunday kayuni kukaimu ukatibu mkuu kwa kipindi cha miezi 6
kabla ya angetile kuwa katibu mkuu mpya, ndio aliyelikuta deni langu
na maelezo aliyekuwa ananipa kuwa madeni yote yanafanyiwa uhakiki ili
wajiridhishe ndipo walipe,hapo ndipo lilipoanzia tatizo la kugoma
kulipwa.

Maneno mengi sana nimeyasikia juu ya madeni yangu kuwa siwezi kulipwa
kwa vile yana utata na hawana ukweli wa hizi kazi kama kweli
zimefanyika.

Lakini cha kushangaza kuna kazi ambayo ilifanyika ya kuibeba timu ya
taifa U20 wakati wanajiandaa kwenda kucheza na U20 ya Ivory coast na
kazi hii ilifanyika wakati katibu ni yeye Kayuni,na hii pesa
ilishalipwa na kampuni ya serengeti katika hotel waliyokuwa U20 na
gharama ya usafiri kwa takribani siku kama 20,vilevile timu ya Ivory
coast U20 ilipokuwa hapa kucheza mchezo wa marudiano na U20 ya
Tanzania,mimi ndio niliotoa huduma hiyo,hiyo ni kazi moja ambayo
niliifanya chini ya katibu kayuni,sasa leo inakuwaje Kayuni huyohuyo
anasema hatambui hayo madeni.Mzazi nina ushahidi tosha wa kufanyika
kwa kazi hizi na mpaka watendaji wa hizi timu nikimaanisha mameneja,na
wajumbe wa kamati za utendaji walitumia gari hizi katika timu za
taifa,mashindano ya taifa cup 2010,nk.

Mimi nafikiri ilikuwa busara kwa Tff kuniita tukakaa meza moja kwabla
ya kwenda kuishitaki mahakani na kulitatua tatizo na kujua ukweli wa
jambo lenyewe,lakini ilishindikana pamoja na mwanasheria wangu kuwapa
demand notice mbili,mara ya kwanza ni october 2010,na ya pili ni
august 2011 lakini zote bila kujibiwa,vilevile na nilishawapa invoice
zote za kazi hizo,bila kujibiwa hapo ndipo nilipoona ni bora suala
hili nilipeleke mahakamani na kufunguliwa kesi namba 120 ya 2011katika
mahakama ya ilala na kusomwa kwa mara ya kwanza tarehe 29/9/2011 tena
kwa kiburi bila tff kuhudhuria wala sidhani kama wana taarifa kuwa
kuna kesi mahakamani ambayo katika historia ya michezo nchini ni mara
ya kwanza kwa tff kuburuzwa mahakamani tena bila sababu za msingi.eti
kudaiwa

Embu tujiulize hii kampuni ya Smart Sports ni kweli haina inachokidai
pale tff mpaka tff wapo tayari kupelekwa mahakamani?lakini hii kampuni
ya Smart Sports wanawezaje kwenda kufungua kesi mahakamani kama hawana
wanachokidai pale tff?hapa nakuwa na mashaka na tff kwa hiyo inatakiwa
wakae na kujiuliza mara mbilimbili kabla hii kesi aijaendelea na
kuwaweka pabaya tff,kwa wadau wa michezo,wadhamini,na wadau wanaotoa
huduma tofauti hapo tff.Sasa tunakuwa na mashaka inawezekana hizi pesa
zimeshalipwa na wadhamini wa timu za taifa,tbl lakini azikwenda kwa
mhusika,inawezekana zimekwapuliwa na wajanja pale tff,sasa wanashindwa
kuliweka wazi kwa mhusika kuhusu deni hili ndio maana kampuni ya
Smarts Sports ikaamuwa kuliburuza tff mahakamani ipate haki zake.Tff
ijiulize hathari gani watakaoipata pale itakapobainika huyu bwana
anadai kweli pale mahakamani,na adhabu yake itakuwa ninini,athari zake
zitakuwa ninini? Sasa napata picha inawezekana kweli huyu bwana
hajalipwa kama tff walikataa kuwalipa tra mapato yao mpaka wakafungiwa
ac zao ndipo walipokaa chini na kukubaliana watalipa hilo
deni,sintashangaa Smart Sports kutolipwa labda na yeye angekuwa na
nguvu ya kuzifunga ac zao.

Na Maico George Wakuganda



naomba Kaka uliangalie kwa makini suala hilo

















































DEO NJIKU AJIANDAA KUMKABILI JONAS SEGU WIKI IJAYO


Kocha wa Mchezo wa ngumi, Boma Kilangi (kushoto) akimsimamia mazoezi bondia Deo Njiku wa Morogoro wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa na mpambano wake wa ubingwa zidi ya Jonas Segu wa Dar es Salaam litakalofanyika Uwanja wa Jamuhuri Morogoro wiki ijao.(picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)







Bondia Deo Njiku akifanya mazoezi ya misuri ya tumbo kwa kutumia viaa vya kisasa kwa ajili ya kujiandaa na mpambano wake wa ubingwa zidi ya Jonas Segu wa Dar es Salaam litakalofanyika Uwanja wa Jamuhuri Morogoro wiki ijao.(picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)


















MAGEREZA waendeleza ubabe mpira wa magongo Moshi.

Na Dixon Busagaga,Moshi.

TIMU ya mchezo wa mpira wa magongo (HOCKEY) ya Magereza Tanzania
imeendelea kufanya vizuri katika mashindano ya Nyerere Cup yanayo
fanyika katika uwanja wa Hindul Mandal ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu
ya kifo cha Mwalimu Julius Nyerere.

Mashindano hayo ambayo yalianza ijumaa iliyopita yanashirikisha jumla
ya vilabu saba kutoka mikoa mbalimbali huku yakitaraji kufikia tamati
leo na mgeni rasmi anatazamiwa kuwa mkuu wa wilaya ya Moshi Musa
Samizi.

Katika mchezo wa kwanza timu ya Magereza Tanzania iliichapa timu ya
Moshi Casa B kwa jumla ya mabao 2 kwa 0 kabla ya kuishushia kichapo
timu ya Twiga ya Arusha kwa jumla ya mabao 4 kwa 2.

Katika mchezo mwingine timu ya Magereza iliadhibu bila huruma timu ya
Kili vijana ya mkoani Kilimanjaro kwa jumla ya mabao 6 kwa 0 na
kufanikiwa kucheza hatua ya nusu fainali.

Akizungumzia ushindi huo afisa msaidizi wa michezo wa Magereza Matilda
Mrawa alisema timu yake imejiandaa kuchukua ubingwa wa mahindano hayo
ambayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka.

Alisema timu ya Magereza imekuwa ikifanya mazoezi kwa muda mrefu huku
ikiongeza wachezaji wapya ambao watasaidia kuipatia ubingwa mwaka huu.

"Hivi sasa huu mchezo una kua ,kwa sababu kila mwaka tunaposhiriki
tunakutana na upinzania mkubwa kutokana na kwamba timu nyingi zimepata
vijana wengi ambao kwa sasa wameanza kuujua vizuri mchezo huu."alisema
Mrawa.

Alisema timu yake ina historia nzuri ya mchezo huo ambapo mwaka jana
walifanikiwa kushika nafasi ya pili huku wakiibuka mabingwa katika
mashindano ya muungano yaliyofanyika mwezi januari mwaka huu jijini
Dar es salaam.

Kwa upande wake mwandaaji wa mashindano hayo Inderjeet Rehal alisema
mashindano hayo yameendelea kukua siku hadi siku na kwamba mategemeo
yake mwaka ujao mashindano hayo yashirikishe timu kutoka nje ya nchi.

Alisema mshindi wa kwanza katika mashindano hayo atajinyakulia zawadi
ya kikombe na kila mchezaji atapatiwa zawadi ambayo itakuwa kumbukumbu
huku mshindi wa pili akiondoka na kikombe pamoja na medali kwa kila
mchezaji.

Timu zinazoshiriki mashindano hayo ni pamoja na Magereza Tanzania na
TPDF kutoka jijini Dar es salaam,Hulks ya jijini Tanga,Moshi Casa
A,Moshi Casa B na Kili vijana za mkoani Kilimanjaro

UTATA MECHI YA SMALL KIDS

Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliketi Oktoba 16 mwaka huu pamoja na mambo mengine kutolea uamuzi utata uliojitokeza na kukwamisha mechi ya Ligi Daraja la Kwanza kati ya Polisi Iringa na Small Kids ya Mpanda, Rukwa iliyokuwa ichezwe Oktoba 15 mwaka huu Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora mjini Iringa. Utata huo ulisababishwa na uuzwaji wa timu ya Small Kids kwa mmiliki mwingine, huku Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Rukwa (RUREFA) kikipinga kuwa haukuwa halali. Hali hiyo ilisababisha ziwepo timu mbili za Small Kids kwenye mechi hiyo dhidi ya Polisi Iringa. Baada ya kupitia nyaraka zilizowasilishwa mbele yake zikiwemo za mauzo ya timu hiyo, pamoja na taarifa ya Msimamzi wa Kituo cha Iringa, Eliud Mvella uamuzi wa Kamati ya Mashindano ni kama ifuatavyo; Small Kids iliyouzwa ndiyo inayostahili kucheza ligi hiyo, kwa vile mwenye mamlaka ya kuuza klabu ni mmiliki mwenyewe na si chama cha mpira wa miguu cha mkoa husika au cha wilaya ambacho klabu ina makao yake. Isipokuwa uhamishaji wa umiliki unapofanyika vyama hivyo vinataakiwa kupewa taarifa. Vilevile Kamati ya Mashindano imekubali ombi la Small Kids kuhamisha kwa sasa mechi zake kutoka Mpanda baada ya kupokea vitisho kuwa ikienda kucheza huko itakiona cha mtema kuni. Hivyo Small Kids kwa sasa imeruhusiwa kuchezea mechi zake Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro. Pia mechi kati yake na Polisi Iringa ambayo haikufanyika sasa itachezwa Novemba 1 mwaka huu mjini Iringa. Katika uamuzi mwingine, Kamati ya Mashindano imeiagiza Sekretarieti ya TFF kuwasilisha kesi mbele ya Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi dhidi ya baadhi ya viongozi wa RUREFA waliosababisha mechi ya Iringa isichezwe na pia kutoa maneno ya vitisho kwa viongozi wa Small Kids.

MECHI YA STARS DHIDI YA CHAD

Taifa Stars inatarajia kuingia kambini Novemba 3 mwaka huu kujiandaa kwa mechi ya kwanza ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Chad itakayofanyika Novemba 11 mwaka huu jijini N’Djamena. Ili kutoa fursa kwa wachezaji watakaoitwa Stars kuripoti kambini ndani ya muda uliopangwa, mechi za mwisho kumaliza mzunguko wa kwanza Ligi Kuu ya Vodacom zimefanyiwa marekebisho. Mechi hizo sasa zitachezwa Novemba 2 mwaka huu badala ya tarehe ya awali ya Novemba 5 mwaka huu. Mechi hizo ni Oljoro vs Villa Squad (Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid), Moro United vs Simba (Uwanja wa Taifa), Polisi Dodoma vs Yanga (Uwanja wa Jamhuri), Toto Africans v Azam (Uwanja wa CCM Kirumba), Kagera Sugar vs Coastal Union (Uwanja wa Kaitaba), Mtibwa Sugar vs African Lyon (Uwanja wa Manungu) na Ruvu Shooting vs JKT Ruvu (Uwanja wa Mlandizi).

MAPATO YANGA vs KAGERA SUGAR

Mechi namba 58 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Kagera Sugar iliyochezwa Oktoba 14 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam iliingiza sh. 42,810,000. Watazamaji waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo walikuwa 11,559. Watazamaji 11,787 walikata tiketi kushuhudia mechi namba 62 ya ligi hiyo kati ya Simba na African Lyon iliyochezwa Oktoba 16 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mechi hiyo iliingiza sh. 41,800,000. Nayo mechi namba 60 kati ya JKT Ruvu na Azam iliyochezwa Oktoba 15 mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Chamazi iliingiza sh. 909,000 kutokana na watazamaji 303 waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo.

LIGI DARAJA LA KWANZA

Ligi Daraja la Kwanza hatua ya makundi inayochezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini inaendelea tena kesho (Oktoba 19 mwaka huu) kwa mechi saba katika viwanja tofauti. Katika kundi A, Polisi Dar es Salaam itacheza na Burkina Faso ya Morogoro kwenye Uwanja wa Mlandizi mkoani Pwani wakati Transit Camp itakuwa mwenyeji wa Temeke United kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga. Nayo Mgambo Shooting itakuwa mgeni wa Morani katika mechi itakayochezwa mkoani Manyara. Kundi B itakuwa kati ya Small Kids na Tanzania Prisons zitakazocheza mjini Morogoro, Mbeya City itaumana na Mlale JKT kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine. Kundi C ni kati ya Manyoni FC na Polisi Morogoro itakayochezwa mjini Singida wakati Rhino FC itakuwa mwenyeji wa AFC kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora. Mechi kati ya Majimaji na Polisi Iringa ya kundi A yenyewe itachezwa Oktoba 20 mwaka huu Uwanja wa Majimaji mjini Songea kama itakavyokuwa kwa mechi ya kundi C kati ya 94KJ na Polisi Tabora itakayochezwa Uwanja wa Mlandizi mkoani Pwani.

VIINGILIO SIMBA v RUVU SHOOTING

Viingilio katika mechi namba 66 kati ya Simba na Ruvu Shooting itakayochezwa kesho (Oktoba 19 mwaka huu) Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam ni sh. 10,000 kwa VIP n ash. 5,000 kwa mzunguko. Tiketi za mechi hiyo zitauzwa uwanjani Chamazi katika magari maalumu kwa ajili ya shughuli hiyo. Boniface WamburaOfisa HabariShirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

: KAMANDA SULEIMAN KOVA KUWA MGENI RASMI KTK PAMBANO LA MATUMLA NA MIYEYUSHO DIAMOND JUBILEE


MKUU WA POLISI KANDA MAALUM YA JIJI LA DAR ES SALAAM AMBAYE PIA NI MLEZI WA MCHEZO WA NGUMI TANZANIA KAMANDA SULEYMAN KOVA ANATARAJIA KUWA MGENI RASMI KATIKA PAMBANO LA MASUMBWI LA UBINGWA WA MABARA WA UBO (UBO INTER-CONTINENTAL BANTAM WEIGHT CHAMPIONSHIP) KATI YA BINGWA MBWANA MATUMLA DHIDI YA FRANCIS MIYEYUSHO.
PAMBANO HILO LITAFANYIKA HIVI KARIBUNI SIKU YA JUMAPILI TAREHE 30 MWEZI HUU KATIKA UKUMBI WA DIAMOND JUBILEE.
AKIZUNGUMZIA HILO KAMANDA KOVA ALISEMA KUBWA ZAIDI LILILOMFANYA AKUBALI KUWA MGENI RASMI NI KATIKA KUUNYANYUA MCHEZO HUU AMBAO HUWAKUTANISHA VIJANA WA RIKA MBALIMBALI KTK KUJITAFUTIA KIPATO HALALI NA KUEPUKANA NA TABIA ZA UPORAJI,
UVUTAJI BANGI NA MADAWA YA KULEVYA.

PAMOJA NA KUWA KARIBU NA WANANCHI MBALIMBALI KATIKA KUTEKELEZA DHANA YETU YA POLISI JAMII.AKIZUNGUMZIA ZAIDI JUU YA PAMBANO HILO LITAKALOKUWA LA RAUNDI 12 MKURUGENZI WA KAMPUNI YA DARWORLD LINKS LTD AMBAO NDIO WAANDAAJI MOHAMED BAWAZIR ALISEMA MAANDALIZI YA PAMBANO HILO AMBALO LIMEANDALIWA KATIKA UTARATIBU MZURI WA KIMATAIFA YANAENDELEA VIZURI,
KUTAKUWA NA MAPAMBANO MENGINE MATANO MAKALI YA UTANGULIZI IKIWEMO LA UBINGWA WA PST KATI YA JUMA FUNDI NA FADHIL MAJIA NA PAMBANO LINGINE LITAKALOWAKUTANISHA KINA DADA ASHA NGEDERE NA SALMA KIOBWA WA MOROGORO " NAWAHAKIKISHIA WAPENZI WOTE WA MCHEZO HUU HASA KINA MAMA WAJE KWA WINGI KUSHUHUDIA PAMBANO HILI NA KUTAKUWA NA ULINZI NA USALAMA WA HALI YA JUU" MILANGO ITAKUA WAZI KUANZIA SAA 10 ALASIRI.KWA WALE WANAOHITAJI TICKET ZA KUKAA ENEO MAALUM LA PRIMIER KWA 20,000 TU WANAOMBWA KUWASILIANA NA MUANDAAJI KUANZIA SASA KWANI ZIMETENGWA NAFASI CHACHE TU,VIINGILIO VINGINE VITAKUWA 10,000 NA 5000 AMBAPO TICKET ZITAPATIKANA MLANGONI SIKU HIYO.

Monday, October 17, 2011

TP MAZEMBE WACHUKUA UBINGWA WA DRC

"Mshambuliaji Mbwana Samata kutoka Tzee ni mmoja ya wachezaji waliochangia kupatikana kwa ubingwa wa TP Mazembe msimu huu."

Klabu ya TP Mazembe imefanikiwa kuchukua ubingwa wa ligi ya DRC jana jumapili kufuatia ushindi wao wa 2-0 dhidi ya yenye mafanikio zaidi kisoka nchini humo, DC Motema Pembe.

Mabingwa watetezi AS V.Club, ambao walishikwa na ktoa sare ya tasa na CS Don Bosco, kwa sasa hawawezi tena kuwafikia TP katika msimamo wa ligi.TP Mazembe wanaongoza ligi hiyo kwa tofauti ya pointi 4 huku ukiwa umebakiwa mchezo mmoja kwa timu zote kumaliza mechi zao katika Super league.

GEORGE WEAH NA NDOTO ZA KUIONGOZA LIBERIA: APATA DIGRII YA KWANZA.


The living legend wa soka wa Liberia, George Opong Weah ambaye kwa sasa amejikita katika siasa na biashara, ametimiza kiu yake ya muda mrefu ya kuitwa msomi, baada ya hivi karibuni kutunukiwa Shahada ya Utawala wa Biashara.

Ametunukiwa Shahada hiyo katika Chuo Kikuu cha DeVry kilichopo Florida, Marekani
alikokuwa amejichimbia darasani kwa zaidi ya miaka miwili.

“Ilikuwa ndoto yangu kukaa darasani na kusoma. Namshukuru Mungu nimetimiza ndoto yangu nami kwa sasa ni miongoni mwa wasomi wa kweli,” alisema Weah, kijana mwenye umri wa miaka 45 ambaye kauli yake inatafsiriwa kuwa inajibu mapigo ya watu waliombeza wakati anawania urais wa Liberia kwa tiketi ya Congress for Democratic Change Party (CDC) mwaka 2005.

Wakati anawania urais mbele ya msomi aliyekuja kuibuka mshindi katika uchaguzi huo, Ellen Johnson-Sirleaf, wengi hasa wa vyama vya upinzani walimbeza, wakidai hawawezi kuongozwa na mtu asiye na upeo mpana, kwa maana ya msomi.

Mithili ya mwiba, maneno hayo yalimchoma Weah, ndiyo maana akaamua kujipanga upya na kurudi darasani. Hata hivyo anasisitiza kuwa, hakurudi kusoma kwa ajili ya kuusaka urais, bali kuonesha kuwa, hakushindwa kusoma kwa sababu ya kutokuwa na `kitu’ kichwani.

“Wote tunakuwa na ndoto za kusoma mpaka Chuo Kikuu. Baadhi wanaweza, wengine waliikosa kabisa hiyo nafasi na wengine walisubiri hadi wakati mwafaka.

Kwa upande wangu, nilisoma kwa njia ya masafa marefu, lakini haikusaidia sana, ndipo baada ya kustaafu nimekaa darasani na kufanikiwa kupata digrii ya kweli. Nashukuru imewafurahisha wazazi wangu, familia yangu na pia kuwaziba midomo walionibeza kwa kutokuwa na digrii,” anasema.

Anaongeza kuwa, ingawa kwa upande wake ametimiza ndoto ya kielimu, anasema hilo ni funzo kwa watu wengine kwamba, elimu haina umri na wala haina mwisho. Anawageukia wapinzani wake waliombeza kwa kutosoma akiwaambia kuwa, uongozi kamwe hauhitaji shahada za chuo kikuu, bali busara na uelewa wa mambo na pia kukubalika kwa wananchi.

“Kuna wengi walioongoza vizuri hata bila ya kuwa na digrii, bali kwa sababu
wameaminiwa na wao hufanya kazi usiku na mchana ili kutowaangusha waliomwamini. Na hata kwa Waliberia, ni zamu yao kuamua kama nafaa kuwaongoza au hapana, lakini elimu isiwe kigezo pekee.

“Ila ninajifahamu kuwa nina kipaji cha uongozi, ninachosubiri ni maamuzi ya Waliberia, lakini naamini ipo siku nitakuwa Rais wa nchi yangu,” anasema Weah amejiengua kuwania urais katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita na badala yake akimpisha Balozi Winston Tubman kuwania urais kwa tiketi ya CDC akichuana na Sirleaf, huku yeye akiwa mgombea mwenza wa Tubman.

Anasema Tubman ana uzoefu wa uongozi na ana nafasi kubwa ya kuwaunganisha Waliberia. Hata hivyo, watabiri wa mambo wanabashiri kuwa Tubman atakuwa na kibarua kigumu mbele ya mwanamama Sirleaf, msomi na mchumi wa miaka mingi ambaye wiki iliyopita nyota yake iling’ara kwa kuwa mmoja wa washindi watatu wa tuzo ya Nobel kwa mwaka 2011.

Kwa Sirleaf mwenye umri wa miaka 73, tuzo hiyo ina maana kubwa, kwani imemwongezea heshima na hivyo kuaminika huenda akashinda uchaguzi uliofanyika na matokeo ya mwisho kutarajiwa kutolewa kati ya sasa na Oktoba 26 mwaka huu na kama atashinda, ataendelea kuwa rekodi barani Afrika.

Anashikilia rekodi ya kuwa Rais wa Kwanza mwanamke kuwahi kuchaguliwa barani Afrika. Pamoja na rekodi hiyo na tuzo ya hivi karibuni, Weah anasema: “Sikugombea urais, lakini nimeshiriki kikamilifu katika kampeni kama mgombea mwenza.
Miongoni mwa vitu nilivyojifunza shule, katika darasa langu la watu 303 tuliosoma biashara, wakati mwingine unaweza kuwa na maamuzi, lakini nimeamua kutumia mbinu mbadala.

“Mimi ni baba wa CDC, lakini cha msingi ni kwamba mwisho wa siku tunataka CDC ichukue nchi, hivyo si vibaya kumpa nafasi mtu mwenye uwezo, uzoefu na anayekubalika kote Liberia, na kwa wakati huu, nadhani Winston Tubman ndiye chaguo sahihi la Waliberia.”

Anaongeza kuwa, katika kuthibitisha kuwa hakubahatisha kupata Shahada ya kwanza, baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu anakusudia kuanza masomo ya Shahada ya Uzamili (digrii ya pili) kwa kusoma darasani, huku akitamba kuwa, atamaliza na kufaulu vizuri.

Je, Weah ni nani hasa? Huyu ni mwanasoka mahiri kuwahi kutokea katika Bara la Afrika, akiwa
na rekodi ya kipekee. Weah, aliyevuna utajiri mkubwa wa fedha katika soka, ndiye Mwafrika pekee kuwahi kutwaa Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia.

Aliiweka rekodi hiyo mwaka 1995, mwaka ambao aling’ara na kutwaa pia Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Ulaya na pia Mwanasoka Bora wa Afrika. Kisoka, nyota huyo aliyezaliwa Oktoba mosi mwaka 1966 katika kitongoji wanachoishi watu wenye maisha duni cha Clara, jijini Monrovia, alianzia katika klabu Invincible Eleven na baadaye Tonnerre Yaounde ya Cameroon.

Licha ya kucheza soka, alikuwa pia tayari mwajiriwa wa Shirika la Mawasiliano la Liberia
alikokuwa ameajiriwa kwa nafasi ya fundi wa simu.

Mambo yalimnyookea mwaka 1988 baada ya kujikuta akinyakuliwa na Monaco ya Ufaransa alikofanya mambo makubwa kabla ya kutua Paris Saint Germain (PSG), klabu nyingine ya Ufaransa aliyoichezea kati ya mwaka 1992 na 1995.

Makali yake uwanjani yalimpeleka AC Milan ya Italia mwaka 1995. Nako aling’ara hadi
mwaka 2000 alipotua England kuichezea Chelsea na baadaye Manchester City. Hata hivyo
mwaka 2001 alirejea Ufaransa kuichezea Marseille na kuamua kwenda kustaafia soka Falme za
Kiarabu katika klabu ya Al Jazira.

Ndipo baada ya kustaafu, alijikita katika shughuli za kijamii na kujikuta akiangukia katika
siasa, akiwania Urais wa Liberia mwaka 2005. Je, baada ya kuzidiwa kete na mwanamama wa shoka Ellen Johnson Sirleaf mwaka 2005, Weah ataweza kuingia Ikulu kwa mlango wa nyuma akitumia mgongo wa Tubman?

Kura ndiyo kwanza zimeanza kuhesabika na katika siasa lolote linawezekana, hata hivyo hilo ni
jambo la kusubiri. Huyo ndiye George Opong Weah ambaye kwa kiasi kikubwa amelelewa na bibi yake mzaa baba, Emma Klonjlaleh Brown, huku kwa zaidi ya miaka kumi mwanasoka huyo akiwa muumini wa dini ya Kiislamu, kabla ya baadaye kurejea katika Ukristo.

Ni baba wa watoto wanne aliozaa na mkewe mwenye asili ya Jamaica, Clar. Watoto wao ni
George Jr, Martha, Timothy George na Jessica. George Jr amefuata nyayo za baba yake, kwani kwa sasa anaichezea FC Baden ya Uswisi na timu ya vijana ya Taifa ya Marekani akiwa na swahiba wake Freddy Adu. Aliwahi kuichezea pia AC Milan ya Italia.

Source:HabariLeo

BARCLAYS PREMIER LEAGUE KIBOKO: INATIZAMWA NA WATU 1.46 BILLION.

Ligi kuu ya Uingereza imeendelea kuwa ndio ligi maarufu zaidi duniani baada ya kutajwa ndio ligi inayotizamwa na watu wengi zaidi ulimwenguni.

Katika repot iliyotolewa kampuni inayoongoza kwa research za kimichezo SPORT+MARKT, inaonyesha kwamba Barclays Premier league ligi hiyo inatizamwa na asilimi70 ya washabiki wa soka 2.08 billion duniani.

Kwa maana hiyo EPL inaangaliwa na watu billion 1.46, pia takwimu zimeonyesha kuwa kati ya watu hao karibu nusu ya watu hao ni wapenzi wa timu za Barclays Premier League.

EPL KWENYE NAMBA HUKU VAN PERSIE AKIVUNJA REKODI

0 – Norwich City bado hawajapata kuwa na clean sheet katika michezo 8 ya Barclays Premier league msimu huu.

1 – David Ngog alifunga bao lake la kwanza ugenini katika EPL, wakati alipofanikiwa kufungia Bolton Wenderers goili la pili katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Wigan Athletic @ DW stadium.

3 – Kiungo wa Chelsea Ramires sasa amefunga goli kwenye mechi zake 3 za mwisho za EPL.

3 – Goli la Steven Gerrard dhidi ya Manchester United, linaamnisha kuwa magoli yote matatu ya mwisho ya Liverpool dhidi ya United yametokana na Free kicks.

4 – Mabao manne kati ya nane ya Mario Balotelli katika Barclays premier league ameyafunga dhidi ya Aston Villa.

5 – Wolverhampton Wanderers and Wigan Athletic wote wamepoteza mechi 5 mfulululizo za Barclays Premier League.

6 – Bolton Wanderers wamemaliza mkosi wa kufungwa mechi 6 mfulululizo kwa kuwafunga Wigan Athletic 3-1.

11 – Christopher Samba ameifungia Blackburn Rovers magoli 15 katika EPL na 11 kati ya hao ameyafunga kwa vichwa, alifunga goli la za kusawazisha dhidi ya QPR.

29 – Robin Van Persie aliipa uongozi Arsenal dhidi ya Sunderland sekunde 29 baada ya kick off, hili ndilo goli la haraka zaidi katika EPL msimu huu na pia lilikuwa goli la haraka zaidi katika historia ya EPL kwa Arsenal.

29 – Ushindi wa 2-0 wa West Bromwich Albion dhidi ya Wolves ulikuwa wa kwanza katika michuano ya ngazi ya juu dhidi majirani zao ndani ya kipindi cha miaka 29.

50 – Goli la Steven Gerrard kwa Liverpool dhidi ya United lilikuwa la 50 katika premier league katika uwanja wa Anfield.

286 - Heidar Helguson alikuwa ndio mchezaji wa kwanza wa QPR kufunga goli katika uwanja wa Loftus Road msimu huu, alipoiweka timu yake mbele dhdi ya Blackburn Rovers katika mechi yao nne @ home.

Sunday, October 16, 2011

MUSSA HASSAN MGOSI ACHEZA MECHI DHIDI YA DC MOTEMA MAPEMBE VS TP MAZEMBE


“Mgosi wa mwisho katika mstari akiisubiri kusalimiana na Mmiliki wa TP Mazembe.”

“Mussa Mgosi nyuma wa kocha wa TP Mazembe aliyevaa viatu vya njano”

Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Simba Mussa Hassan Mgosi ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya DC Motema Pembe, leo alikuwa mmoja ya wachezaji waliotumika katika mechi ya ligi kuu ya kongo dhidi ya TP Mazembe.Mchezo huo uliisha kwa TP kuibuka na ushindi wa bao 2-0.

PHOTOS: SIMBA VS AFRICAN LYON - KIOJA CHA JEZI YA KASEJA.



HIVI NI JEZI YA JUMA KASEJA NI YA SIMBA AU AFRICAN LYON?WADAU TUSADIANE KATIKA HILI.





GOLIKIPA WA AFRICAN LYON SIMBA JUMA KASEJA AKIZUNGUMZA NA WACHEZAJI WENZAKE KATIKA MCHEZO WA LEO ULIOISHA KWA SIMBA KUSHINDA 4-0.






MFUNGAJI WA MABAO MAWILI KWA UPANDE WA SIMBA, EMMANUEL OKWI AKIELEKEA LANGONI MWA AFRICAN LYON.




MTANANGE MKALI UKIENDELEA KATI JUMA JABU WA SIMBA AKIPAMBANA NA WACHEZAJI WA AFRICAN LYON.


LIVE MATCH CENTRE: SIMBA 4-0 AFRICAN LYON


WAFUNGAJI WA MABAO NI FELIX UNZU ALIYEFUNGA BAO LA KWANZA, NA MENGINEYO YAMEFUNGWA NA EMMANUEL OKWI LA 2 NA 3, KAPOMBE AMEFUNGA LA NNE. MPIRA NI KIPINDI CHA PILI DK.60.

PHOTOS: YANGA WAMRUDISHA MANJI JANGWANI KWA MAANDAMANO



NGASSA AFUNGA BAO LA KWANZA , AZAM WAKIISHUSHA YANGA IN VPL


USHINDI wa mabao 2-0 iliyoupata jana timu ya soka ya Azam dhidi JKT Ruvu, umewashusha nafasi moja mabingwa wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara, Yanga kutoka nafasi ya tatu hadi ya nne.

Mechi hiyo iliyokuwa na ushindani mkubwa ilipigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo iliwachukua sekunde 36 Azam kujiandikia bao la kwanza lililowekwa kimiani na mshambuliaji wake, Mrisho Ngasa, baada ya kumlamba chenga kipa wa JKT Ruvu, Shaaban Dihile.

Bao hilo liliwachanganya zaidi JTK ambao walianza kucheza kwa tahadhari sana, huku wachezaji wa timu hizo wakikosa mabao ya wazi baada ya kucheza fyongo.

Timu hizo zilikwenda mapumziko kwa Azam kuwa mbele kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa JKT kucheza bora liende, kwani hawakuonyesha jitihada yoyote ya kutaka kusawazisha.

Hata hivyo, mshambuliaji wa Azam, John Bocco ‘Adebayor’ aliifungia timu yake bao la pili katika dakika za nyongeza za mchezo huo.

Kwa ushindi huo, Azam iliyokuwa ikishika nafasi ya nne kwenye ligi hiyo imepanda hadi nafasi ya tatu baada ya kufikisha pointi 18, wakati nafasi ya kwanza inashikililiwa na JKT Oljoro yenye pointi 19, Simba inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 18 huku Yanga yenye pointi 15 ikishika nafasi ya nne na JKT Ruvu inashika nafasi ya tano kutokana na pointi 15 ilizonazo.

TP MAZEMBE WAZINDUA SHIRIKA LAO LA NDEGE - MAZEMBE AIRWAYS

MOJA YA TIKETI ZA SHIRIKA LA NDEGE LA TP MAZEMBE AIRWAYS LINALOMILIKIWA NA KLABU YA TP MAZEMBE YA NCHINI KONGO.





ABIRIA WAKIWA NDANI YA NDEGE YA SHIRIKA LA MAZEMBE AIRWAYS WAKATI WA UZINDUZI.