Search This Blog

Tuesday, October 18, 2011

WEZI WA TIKETI ZA TFF KUFIKIKISHWA MAHAKAMI



Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, linatarajiwa kuwafikisha mahakamani wakati wowote kuanzia sasa watuhumiwa wawili wa wizi wa tiketi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).


Hivi karibuni, TFF iliwakamata Seleman Masoud na Salum Abdallah wakati wa mechi ya Ligi Kuu Tanzania kati ya Yanga na Azam FC iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Septemba 18, mwaka huu, baada ya baadhi ya vitabu vya tiketi kuibiwa katika mazingira ya kutatanisha na watuhumiwa kukutwa nazo.


Kauli hiyo, imekuja siku chache baada ya baadhi ya wadau wa michezo, kulishutumu Jeshi la Polisi Mkoa huo, kwa kushindwa kuwafikisha mahakamani kwa muda mrefu watuhumiwa hao, hatua ambayo ilikuwa ikitafsiriwa kuwa walikuwa wanawalinda watuhumiwa.


Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Missime, alisema upelelezi wa kesi hiyo ambayo watuhumiwa walikamatwa na tiketi 300 na kuhojiwa katika kituo cha polisi Chang’ombe, umefikia hatua za mwisho kabla ya kupandishwa kizimbani.


Alisema upelelezi wa kesi hiyo ulikuwa mgumu kutokana mkanganyiko uliokuwapo, lakini vijana wake wamefikia hatua nzuri ambayo itawezesha kuwafikisha mahakamani watuhumiwa hao.


Watuhumiwa hao walikamatwa Septemba 18 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kufunguliwa jalada namba CHA/IR/6257/2011 ambapo mmoja wa wauzaji tiketi za mchezo huo, Seleman Masoud, aliripoti kupotelewa kitabu kimoja, mara baada ya ugawaji wa vitabu hivyo kufanyika asubuhi ya siku ya mchezo na baada ya uchunguzi kufanyika, baadhi ya mashabiki waliokuwa wamenunua tiketi walimtaja Salum Abdallah ambaye naye alitiwa mbaroni.



No comments:

Post a Comment