Search This Blog

Wednesday, August 3, 2011

TP MAZEMBE YAZINDUA KITUO CHA AFYA.......( SIMBA NA YANGA MPOOOOOOO )




HII NI KADI YA MSHAMBULIAJI ALAIN DIOKO KALIOUTOUKA





HII NI YA GIVEN SINGULUMA











MTAALAMU WA KITUO AKITOA MAELEKEZO...






HILI NI JENGO LA KITUO HICHO LINAVYOONEKANA KWA NJE


































Muuza Maandazi aliyejaliwa kipaji cha soka Ulaya

ANAITWA Ambokile George, kijana wa Kitanzania anayejaribu bahati yake ya kucheza soka la kulipwa nchini Sweden, hapa chini ni anaelezea kuhusu historia yake.
Kwanza kabisa nilizaliwa Mbeya, wilayani Tukuyu kwenye kijiji cha Kagwina.
Mama yangu alipata shida sana kunilea wakati nilipokuwa mdogo, kwani niliumwa sana alafu alikuwa peke yake. Baadaye kidogo mama alihamia Dar es Salaam wakati nikiwa bado mtoto. Lengo hasa likiwa ni kutafuta maisha.
“HAKUNA KAMA MAMA YANGU, NAMPENDA SANA JINSI ALIVYOKUWA AKIJISHUGHULISHA ILI NIWEZE KUISHI, MUNGU AMBARIKI NA AMSAMEHE MAKOSA YAKE.”
Kwa hiyo baada ya kufika Dar es Salaam, tukawa tunaishi Keko Machungwa mtaa wa Bondeni, wakati nilikuwa napenda mpira wa miguu pamoja na umri wangu kuwa mdogo.

Tulikuwa na timu ndogo ya mtaani iliyokuwa ikiitwa Mkulundungu Maji ya Shingo, alafu tukahamia mtaa wa mwingine wa Keko Machungwa uitwao mtaa wa Tatu pia nikawa nacheza soka katika timu ya Bankasa Bankunyembe Toto Africa.

Kumbuka wakati wote huo, mimi nilikuwa nahodha wa timu hizo. Baada ya kuonekana nacheza vizuri mtaani hasa kutokana na chenga zangu, nakumbuka siku moja kuna timu ya watoto ilikuwa ina kocha mtaa wa Polisi ilitaka ‘kuninunua’ kwa Tsh 1,000.

Kwa wakati huo hiyo ilikuwa ni heshima kubwa na nilijiona kama mtu maalum mtaani kwa kutaka kununuliwa na timu nyingine kwa dau la Tsh. 1000.


Baadaye kidogo nilicheza michuano ya fulani iliyokuwa inachezwa mara kwa mara Keko Mwanga maeneo ya TAZAMA. Kulikuwa kuna timu inaitwa Warunguri Ganja Shishi, nilicheza katika klabu hii sambamba na Ramadhani Chombo ‘Redondo’ (sasa anacheza Simba) wakati huo tulikuwa tunamuita Double Suka (tulikuwa tukimaanisha Davor Ĺ uker- mshambuliaji wa zamani wa Croatia).
Mimi na Redondo tulikuwa tunaazimwa ‘ndondo’ kucheza katika timu hiyo, hii ilikuwa kama tabia yetu na imezoeleka sana katika mitaa mingi ya uswahilini.
Lakini kutokana na umbo na umri wangu kuwa mdogo nilikuwa naonewa kila wakati, katika uwanja kuna sehemu kulikuwa na dimbwi la maji ukichezwa rafu, una dumbukia, ilikuwa balaa, timu yetu ilikuwa ina mastaa watoto ambao waliweza kufanya vizuri katika michuano ya makombe mbalimbali kama ya Kuku, Jezi, Mchele na Njiwa. Aaahaa….aaahh, ilipendeza sana wakati huo.
Sasa nilipoanza kukua kidogo, nikaanza kumsaidia mama kuuza Chapati, Maandazi, kutembeza ndizi, mihogo, viazi, machungwa na vitu vingine vidogovidogo vya kula ili tupate fedha itakayotukidhi kupata mlo wa kila siku.
Punde kidogo tukasikia kuna timu inaanzishwa katika viwanja vya Chang´ombe TCC, mimi na Redondo tukaenda kufanya majaribio na kufanikiwa. Tulikuwa watoto tupatao 400, lakini tulichujwa na kubaki 250, katika michujo yote hiyo tukawa tunapita tu.

Baadaye nikaja kuifahamu timu hiyo kuwa inaitwa DYOC, ilikuwa ikinolewa na Siza Peter Mapunda na Ramadhani Aluko Simango. Aluko alikuwa kocha mzuri sana katika kukuza na kujaribu kuendeleza vipaji vya chipukizi.

Aluko alikuja na mbinu za kiulaya akatufanya kuwa tishio Tanzania nzima, kwani tulikuwa tuna piga Samba katikati hadi kuwapigia wapinzani Sambusa, walikuwa wakiangahika sana kupata mpira.

Muda kidogo tukapata mwaliko wa kushiriki Kombe la Zawadi lililoandaliwa na kituo cha kukuzia vipaji vya soka cha Rollingstone mjini Arusha, nikiwa kama nahodha wa timu, tukawa tunazunguka karibu maeneo mengi ya Dar es Salaam kutafuta nauli.

Tulikuwa tukiombaomba katika makampuni tofauti tofauti, baadaye tulipata nauli na kushiriki michuano hiyo ambayo tuliweza kutwaa ubingwa.

Mara baada ya michuano hiyo, nilifanikiwa kuchaguliwa katika kundi la vijana 150, tukawa wanne ambao ni mimi, Aboubakar Yahaya, Kasim Ibrahim na Alphonce Matogo, tuliungana na watoto wa shule za kimataifa za nchini kwenda Sweden na Denmark kushiriki baadhi ya michuano iliyoendeshwa huko.

Baadaye Aluko ambaye ni kocha wetu, alimuomba mama yangu ili aishi na na mimi nyumbani kwake pamoja na vijana wengine aliowachagua kutokana na uzuri wa uchezaji wetu. Kwa hiyo nikawa mimi, Kasim na wengine tuliokuwa tukiishi kwa Aluko.

Aluko alituchukua akihitaji tuwe pamoja na kutusaidia kimahitaji kupitia mfadhili, kwa hiyo aliniomba kwa mama yangu lakini hakusaini mkataba wowote na mama, sasa kutokana na nidhamu yangu, umahili wangu wa uchezaji, kujituma na kufunga mabao,
nikawa nakubalika hadi nikapewa unahodha wa timu.

Baadaye tukashiriki michuano ya Kombe la Coca Cola mwaka 2002, nikabahatika kuwa mchezaji bora wa michuano hiyo kisha nikasafiri na DYOC tena mwaka 2003 kwenda kucheza Kombe la Tivoli nchini Denmark na Gothia Cup lililofanyika Sweden.

Tulifanikiwa kutwaa makombe yote na kuweza kupata tuzo ya ‘Most Valuable Player Of The World Youth Gothia Cup Under 12’ na kupewa tuzo (naweza kusema hii ilikuja kwa sababu nilikuwa mtu wa maombi, namwomba sana Mungu nikiwaongoza wenzangu katika maombi na umahili wa upachikaji mabao na kutengeneza nafasi kwa wenzangu alafu nilikuwa ‘team fighter’)


Mwaka 2004 nilisafiri tena na timu yangu ya DYOC kushiriki Kombe la Tivoli huko Denmark, Kombe la Gothia na lile la Laxen yote nchini Sweden na Kombe la Norway huko Norway.

Tulifanikiwa kuchukua makombe yote na kuacha historia ya kuitwa ‘The Dream Team Never Happen’ kwa jinsi tulivyokuwa tunacheza, wengine walikuwa wakituita Samba, walifikiri sisi ni Wabrazili, kumbe tulikuwa tunatoka Tanzania.

Kwa bahati, nikawa tena ‘The Most Valuable Player Of The World Youth Gothia Cup Under 13’ nikapewa tuzo nyingine, ifahamike kwamba hii ni michuano mikubwa sana kwani timu karibu 60 zilikuwa zikishiriki.

Baadaye nikawa mchezaji bora wa michuano ya Kombe la Norway ambalo ni kubwa sana, kama kawaida nilipachika mabao mengi sana, nilijituma nikiongoza wenzangu kumwomba Mungu kabla na baada ya mechi katika michezo yote.

Namshukuru Mungu kwa kweli, si kwa uwezo wangu wala akili zangu, bali ni yeye aliyeniwezesha na kunichagua katika kundi la watoto wote wa duniani walioshiliki Kombe hilo nampa sifa na Utukufu Mungu kwa kazi yake katika kunisimamia maisha yangu.

Mwaka huo nilipata bahati ya kutakiwa na mwangalia vipaji wa Manchester United, na timu nyingine za Sweden na Denmark kwani vyombo vya habari na magazeti yalikuwa yananizungumzia sana,
lakini sijui ni kwa nini sikuweza kuuzwa.

Baadaye nikapata nafasi tena ya kwenda Hispania kati ya vijana watano, lakini ajabu nikashindwa kufanya hivyo, iliniuma sana lakini uzuri nilikuwa nimetambua kwamba Mungu ndiye mtetezi wangu na ni yeye anayeyapigania maisha yangu na wala si mwingine.

Nikawa naendelea kumwomba Mungu na kufanya yale anayotaka nifanye ikiwa ni pamoja na kusoma biblia, kusilikiza neno la Mungu kanisani na nyumbani kwa kweli nilimwomba Muumba sana ili aniepushe na kujiona nafahamu zaidi ya wenzangu.

Tamaa za ujana kama uvutaji bangi, madawa ya kulevya, uzinifu niliziepuka kwa kusoma biblia kila wakati na kuwa karibu katika mambo ya Mungu. Kwa hiyo nikawa naendelea kukubalika kwa wenzangu pamoja na makocha wote Siza Mapunda na Aluko.

Nilikuwa kati ya vijana wasikivu, mwenye nidhamu na akili darasani (sijisifu nasema ukweli nilikuwa na akili kweli darasani) pia na heshima niwapo ndani na nje ya uwanja.

Nje ya uwanja nilikuwa naiheshimu jamii mkubwa kwa mdogo ikanitengeza katika mazingira ya kukubalika kila nilipoingia watu walikuwa wananipenda na kunikubali jinsi nilivyo katika adabu na unyenyekevu, ikawa rahisi mimi kukubalika.


Pia tulikuwa tuna Kocha mzuri, Siza Mapunda alikuwa anajua kutufundisha na kutuweka kama timu, hongera yake pia namshukulu Mr Kipingu (Idd Kipingu), ni mzee mzuri sana anastahili pongezi alinipatia nafasi ya shule ingawa nilikuwa nalipiwa na sponsor wa Kijerumani kupitia Nehemia Foundation ni Shirika la Walokole, nilipo kuwa Makongo High School nilikuwa nacheza mpira na kusoma.
Nilikuwa sina dharau na kujiona najua zaidi ya wenzangu, bali nilikuwa nawapenda wote na kuwaheshimu, niliweza kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Copa Coca Cola nikiwa katika timu ya mkoa wa Temeke ilikuwa nzuri sana, tulielewana na kucheza mpira wa kutulia.
Nakumbuka nilicheza safi sana mechi ya ufunguzi nikitokea benchi hadi Micho (Kocha wa zamani wa Yanga Milutin Sredojevich) na Chamangwana (pia Kocha wa zamani wa Yanga, Jack Loyd) walinifurahia jinsi nilivyokuwa mhamasishaji wa timu si hao pekee bali wenzangu kama Yusuph Soka, Mau Mkami (Himid), Johannes Kajuna, Adam Asheli, Ben Jacob na wengine pamoja na makocha wangu Golo, Mfaume na viongozi wote wa TEFA (Chama cha Soka wilaya ya Temeke).
Lakini haikuwa bahati kwani walipochaguliwa vijana wa timu ya taifa kutoka Temeke sikuwamo, sikujua tatizo ni nini sema nilimwachia Mungu anayetujalia pumzi ya kuishi.
Baadaye kulikuwa na michuano ya shule nzima katika vidato vyote Makongo High School, nilicheza vizuri sana wakati huo nilipokuwa kidato cha pili, nikawa mchezaji bora wa michuano hiyo na kupewa zawadi na Kipingu.
Ikatokea wanahitajika watu wawili katika kampuni ya Models, kutoka kwenye kituo chetu tukachaguliwa mimi na mwenzangu aitwaye Stanley Sila kwa hiyo kampuni ya Models wakatupeleka kwenye kampuni ya Lowe Scanad (hii ni kampuni ya matangazo).
Tukafanyiwa majaribio baadaye nikachaguliwa kushiriki tangazo la la biashara la Twiga Cement, nikaenda India kutengeneza tangazo hilo, Mungu akanisaidia kuweza kulicheza vizuri.
Itaendelea...

TBL YAINGIA MKATABA MPYA WA MIAKA 5 WENYE THAMANI YA BILIONI 5 kuvidhamini vilabu vya SIMBA na YANGA.

Kampuni ya bia nchini ,TBL kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro Premium Lager imeongeza mikataba ya kuvidhamini vilabu kongwe chini Tanzania vya Simba na Yanga.
Mkataba wa awali na vilabu hivyo uliosainiwa mnamo mwaka 2008 uliokuwa wa miaka mitatu umemamlizika mwishoni mwa mwezi uliopita,
TBL imeingia Mkataba mpya wa miaka mitano na vilabu hivyo.
Maboresho ya mkataba mpya ni kama ifuatavyo.( kwa kila klabu )
A ) Sponsorship fee ya kila mwezi sasa itakuwa tsh 25,000,000 kutoka tsh 16,000,000 ,Pia kila mwaka kutakuwepo na ongezeko la 10% ya kiasi hichi cha pesa.
B) kila klabu itapata basi kubwa jipya lenye uwezo wa kubeba abilia 54,hapo awali kampuni hiyo ilivipatia vilabu hivyo mabasi mawili ya aina ya Hiace na Coaster.
C ) TBL pia itaghalamia mkutano mkuu wa wanachama kila mwaka.
D ) Kila mwaka vilabu hivyo vitapatiwa kiasi cha tsh 20,000,000 kwa ajili ya kufanya maandalizi ya matamasha yao.( Smba day na Yanga day- coming soon )
E) Vifaa vya michezo vyenye thamani kati ya milioni 60-70 kila mwaka .
F) Kiasi cha shilingi milioni 25 kwa timu itakayobeba uchampioni wa ligi kuu ya Vodacom na milioni 15 kwa timu itakayoshika nafasi ya pili.
Baada ya dili kukamilika..




Mwenyekiti wa Yanga Lloyd Nchunga akimwaga wino kwenye mkataba mpya.





Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, David Minja akiweka saini mikataba ya timu hizo.






Makamu Mwenyekiti wa Simba Godfrey Nyange Kaburu akiweka saini kwenye mkataba mpya.







Mtangazaji wa kipindi cha michezo cha Radio One,Maulid Kitenge akifanya mahojiano ya Mkurugenzi wa masoko wa TBL Mr David Minja.




Hapa Nchunga akiteta jambo na Kaburu





















TAARIFA ZA USAJILI BARANI ULAYA


FERGUSON: BERBATOV ANAWEZA KUONDOKA

Miaka ya kuhangaika kufanya vizuri ndani ya United kwa Dimitar Berbatov inaonekana kuelekea mwishoni baada ya jana usiku Sir Alex Ferguson kukiri kuwa mbulgaria huyo anaweza kujiunga na Paris Saint Germain.

Klabu mpya tajiri ya Ufaransa wamekuwa wakimtaka Berbatov kipindi hiki chote cha usajili na hatimaye wamefanya mawasiliano na Red Devils.

Akiulizwa kupitia French TV baada ya kikosi cha United XI kufungwa na Mersaile 8-2 mjini Monaco kama Dimitar anaweza kwenda Ufaransa, United Manager alisema: “Ndio, anaweza.Hilo linawezekana.”

TOTTENHAM WATOA £10 MILLION KWA SAMBA



Tottenham jana usiku walipeleka ofa ya £10million kwa Blackburn kwa ajili ya beki Christopher Samba.

Spurs pia pamoja na kutoa kiasi hicho watamtoa mchezaji mmoja ili kuongeza uzito katika dili hilo.

Arsenal na Everton wote wanamtaka Samba, anayetajwa kuwa na thamni ya £12million, lakini Spurs hawapo tayari kutoa pesa hizo(£12m) ila watatoa pesa walizo-offer pamoja na mchezaji mmojawapo kati ya Jermain Defoe, Robbie Kean, David Bentley or Sebastian Bassong.

DUUUUUH !!!

WAWAPO NJE YA UWANJA HUWA HIVIII...

WESLEY SNEIJDER NA FAMILIA YAKE....


RAFAEL & FABIO








ROBERT PIRES NA FAMILIA YAKE WAKINYOSHA NYOSHA
MIGUU.





RADAMEL FALCAO AKIMALIZIA MALIZIA MAPUMZIKO YAKE.



















Tuesday, August 2, 2011

Maisha baada ya Steven Gerard. Jinsi Liverpool walivyoweza kuishia baada ya kuondoka kwa nyota mbambali.

Maisha yatakuwaje Anfield baada ya kuondoka kwa Steven Gerard?
Hivi karibuni mashabiki wa Liverpool walipokea kwa mshtuko taarifa kuwa nahodha wao shujaa kama wanavyopenda kumuita “captain fantastic” atakosa mwanzo wa msimu wa ligi kuu ya England kwa majeraha ambayo kwa sasa yameanza kuwa sugu kwake huku yakitishia uchezaji wake wa muda mrefu.
Inawezekana umri umesogea sana au labda kucheza kwa muda mrefu bila kupumzika na wakati mwingine pia athari za muda mrefu za sindano za kuondoa maumivu pale alipokuwa akiumia siku za nyuma yoyote kati ya hayo ni sababu ila lililo dhahiri ni ukweli kuwa Steven Gerard hana muda mrefu wa kucheza kwenye kiwango cha juu na ni vyema Liverpool wakaanza kutafuta mbadala na ishara zote zinaonyesha kuwa Kenny Dalglish ameanza kufanya hivyo kwa kuwasajili kina Charlie Adam na Jordan Henderson na hata mwishoni mwa msimu uliopita chini ya Kenny Dalglish kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu Liverpool walionekana kucheza vyema bila Stevie G ambaye aliumia .
Historia inaonyesha kuwa Liverpool wameweza kufanikiwa kusonga mbele kwa mafanikio pale ambapo wachezaji tegemeo wanapokuwa wameondoka iwe ni kwa kustaafu au kuhama klabu na wafauatao ni baadhi ya watu ambao waliwahi kuwa tegemeo Liverpool na wakaondoka na Liverpool ikasonga mbele .
Billy Liddell


Kwa mashabiki wengi wa Liverpool ambao umri umesogea Billy Liddell ni mchezaji bora kuliko wote waliowahi kuchezea klabu hiyo . Liddell alicheza mechi takribani 534 ndani ya uzi wa Liverpool. Winga huyu toka Scotland alifunga mabao 228 katika kipindi cha miaka ya 1946 na 1960 . Katika kipindi cha miaka ya 1950 Billy Liddell alikuwa tegemeo la liverpool pale ambapo klabu hiyo iliyumba . Liddell alionyesha kuwa yeye ni Liverpool damu pale ambapo alibakia na klabu hiyo iliposhuka daraja mwaka 1954 baada ya kuwa wametwaa ubingwa mwaka 1947. Billy alikuwepo kwenye kipindi cha kocha mwenye mafanikio kuliko wote Liverpool Billy Shankly mwaka 1959 lakini hakukaa muda mrefu kwani alicheza mechi yake ya mwisho mwaka mmoja kabla mapinduzi ya Shankly hayajaanza.
Liverpool walichezaje baada ya Billy Liddell kuondoka? Kocha Bill Shankly alitambua kuwa Liverpool ni tegemezi kwa wajina wake Billy Liddell na aliona mbali kuwa wangepata tabu akikosekana hivyo alianza kujiandaa mapema na muda mfupi kabla Liddell hajaondoka rasmi Shankly alimpa nafasi chipukizi mwenye miaka 18Ian Callaghan kwenye kikosi cha kwanza . Callagan alianza taratibu lakini mwisho wa siku alikuja kuvunja rekodi ya mechi nyingi iliyowekwa na Billy Liddell mtu aliyekuwa akicheza kama mrithi wake ambapo Callagan alicheza mechi 857 akitwaa mataji mbalimbali England katika kipindi cha miaka 18.

Kevin Keegan



Kevin Keegan ni mmoja kati ya wachezaji wenye heshima kubwa Liverpool . Keegan alikuwa kwenye timu ya pili iliyotengenezwa na Billy Shankly ambapo alikuwa mmoja kati ya wachezaji maarufu duniani kwenye miaka ya sabini na ni yeye aliyeisaidia Liverpool kutwaa taji lao la kwanza la ulaya mwaka 1977 . Pamoja na taji hilo Keegan aliibeba liverpool kwenye ligi ya England ambapo Liverpool walikuwa mabingwa kwenye miaka ya 1973,76 na 77 sambamba na kombe la FA mwaka 1974, kombe la UEFA mwaka 1973 na mwaka 76 . Mashabiki wa Liverpool walipata presha waliposikia taarifa kuwa shujaa wao KK alikuwa mbioni kujiunga na Hamburg ya Ujerumani mwaka 1977.
Alipoondoka Keegan? Kocha wa Liverpool wakati Kevin Keegan anaondoka alikuwa Bob Paisley . Alichofanya Paisley kama hatua ya kuziba ufa ulioachwa na Kevin Keegan ni kulipa ada iliyokuwa rekodi kwa Liverpool ya paundi 440,000 kumsaini mshambuliaji Kenny Dalglish toka Glasgow Celtics . Dalglish alipewa jezi namba 7 aliyokuwa akiivaa Keegan . Huku namba 7 wa zamani wa Liverpool akifanya vitu vya hatari huko Ujerumani ambapo alitunukiwa tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya kwa miaka ya 1978 na 79 , Liverpool hawakumkosa nyota huyo kwani namba 7 mpya Kenny aliiwasahaulisha mashabiki wa Liverpool kuhusu Kevin Keegan . Dalglish alianza msimu wake wa kwanza Liverpool kwa mafanikio makubwa na bao lake ndio liliipa Liverpool ubingwa wa ulaya kwa msimu huo na aliendelea na moto huo huo na aliishia kuwa mchezaji bora wa Liverpool mpya kwa miaka iliyofuata .

Graeme Souness

Kiungo huyo mwenye kupiga “tackling” za nguvu aliing’aa kwenye midfield ya Liverpool kwa miaka 6 tangu mwaka 1978 hadi 84, katika kipindi hicho Souness alitwaa taji kila mwaka katika miaka yote hiyo aliyocheza na mara nyingi ilikuwa ni taji zaidi ya moja . Souness aliondoka Liverpool 1984 baada ya kuiongoza Liverpool kama nahodha wake kutwaa ubingwa wa ulaya , ubingwa wa ligi ya England na ubingwa wa kombe la Ligi .
Liverpool waliishi vipi baada ya Souness ?
Muda mfupi kabla Graeme Souness hajaondoka Anfield Liverpool ilimsajili kiungo John Wark na kwenye msimu wake wa kwanza Wark alifanikiwa kuwa mfungaji bora akiwa na mabao 27 kwenye mashindano yote . Kwenye msimu wake wa pili John Wark aliweza kutwaa mataji mawili lakini mchango wake ulikatishwa na majerha aliyoyapata msimu huo na ujio wa wachezaji wawili Jan Molby na Steve McMahon kama wapinzani wake kwenye midfield ya Liverpool . Hadi nusu ya kwanza ya ligi ya mwaka 1987/88 inaisha John Wark alikuwa njiani kurudi kwenye klabu yake ya zamani Ipswich Town. Na hapo Liverpool walikuwa wameziba nyufa mbili kwa wakati mmoja ufa wa Graeme Souness na wa John Wark .


Alan Hansen

Katika mechi 620 alizoichezea Liverpool kati ya miaka ya 1977 na 1991 Alan Hansen alileta ladha tofauti kwenye safu ya ulinzi ya Liverpool . Staili yake ya uchezaji ambayo ilikuwa tofauti na mabeki wa uingereza ambao hupenda ‘butua butua’ ilimpa Hansen Upekee. Jamaa alikuwa akiwapokonya washambuliaji mpira na kuundoa kwenye eneo la hatari kwa umakini wa hali ya juu na alikuwa mmoja wa watu walioipa Liverpool mafanikio makubwa katika kipinndi chake msimu hadi msimu kwa miaka yote 14 aliyoichezea Liverpool . Hansen alitwaa mataji 8,na alikuwa nahodha wa Liverpool wakati walipotwaa mataji mawili mwaka 1986 .
Liverpool waliziba vipi pengo la Hansen? Wakati Hansen alipostaafu mwaka 1991 kocha wa Liverpool Graeme Souness alitumia paundi milioni 2.2 kumsajili beki wa timu ya taifa ya England na Derby County Mark Wright kuziba pengo lake . MarimWright alikumbwa na balaa la majeruhi alipoojiunga na Liverpool. Ila Wright alitwaa kombe la FA kama nahodha wa Liverpool kwenye msimu wake wa kwanza . Wakati wa Souness kama kocha wa Liverpool uligubikwa na timu mbovu ambayo ilishindwa kufanya vyema kama Liverpool za miaka iliyopita ila pamoja na hayo Mark Wright alikuwa mchezaji wa kipekee . Hilo lilidhihirika pale aliposhutumiwa kuwa mchezaji mbovu na kocha wa zamani wa Liverpool Roy Evans , Wright alirejea kwenye kiwango chake katika kipindi ambapo Liverpool walionekana kufufuka na kurejea kwenye enzi zao katikati ya miaka ya 90. Jumla ya mechi 210 akiwa na jezi nyekundu za Liverpool zilimpa Mark Wright heshima aliyostahili kama gwiji wa Anfield lakini ukweli unabakia kuwa kwa mchezaji wa daraja na kiwango kama cha Mark Wright wakati wake na Liverpool ulikuwa mbaya sana kwake na kwa klabu ya Liverpool.

PASTORE: NAJIUNGA NA PSG


Mchezaji wa Kiargentina anayeichezea klabu ya Palermo Javier Pastore amezungumza na kuthibitisha kuwa atajiunga na klabu ya PSG mara tu atakapofaulu vipimo vya afya, na akisema anajiunga na klabu yenye historia kubwa.

Wiki iliyopita raisi wa Palermo Maurizio Zamparini alitoa taarifa ya kwamba amekubali kumuuza Pastore kwa £37.7million, na sasa mchezaji mwenyewe akiongea kupitia official website ya wakala wake, Dodici Corporation, Pastore alisema: “Unaweza kusema mimi tayari ni mchezaji rasmi wa Paris Saint – Germain , lakini nahitaji kufanya vipimo vya afya na kukamilisha taratibu nyingine.PSG ni klabu kubwa yenye historia kubwa.

“Nataka kushinda kila kitu nikiwa hapa, nataka kujitolea kucheza kwa asilimia zote kucheza vizuri katika kila mchezo na nina furaha sana kuona wmeniamini na kunipa nafasi hii.”-Pastore.

JE WAJUA ?




Mchezaji wa kwanza Tanzania kucheza SOKA akiwa amevaa viatu ni Hussein Mukadamu akiwa na Sunderland ( Simba ), ambaye baadaye alikuja kuwa wakili maarufu hapa nchini.




IPI LIGI BORA BARANI ULAYA ?

Wakati msimu mpya wa ligi mbali mbali barani ulaya ukitaraji kuanza ,Watu wengi hawawezi kuisahau mechi ya fainali ya Uefa Champions League ya msimu uliopita kati ya Man utd na Fc Barcelona. Ndiyo, ilichezwa katika kipindi cha majira ya joto barani Ulaya katika uwanja wa Wembley jijini London. Ni nani anaweza kusahau balaa la Barcelona dhidi ya Manchester United.

Mwisho wa siku, ilikuwa ni mechi iliyozikutanisha timu mbili bingwa kutoka Ligi mbili bora zaidi duniani kwa sasa, Ligi Kuu ya England ‘Premier league’ dhidi ya ligi kuu ya Hispania, Primera League.

Manchester ilipotezwa uwanjani na wachezaji wake wakajikuta wakifukuza vivuli vya wachezaji wa Barcelona. Lakini je, ni kweli pambano moja linaweza kuamua ubishi uliotanda nchini kuhusu ligi bora duniani kati ya ile ya England dhidi ya Hispania?

Mashabiki wengi wa soka nchini wamekuwa wakibishana kuhusu ipi Ligi bora baina ya hizi mbili. Ukweli ni kwamba hakuna Ligi bora baina ya hizi mbili, inategemea tu shabiki anategemea aina gani ya soka.

Kuna wale wote ambao wanapenda zaidi staili ya soka la nguvu, kasi na hamasa iliyopindukia. Kwao watalipenda zaidi soka la Uingereza kuliko soka la Hispania.

Kuna wale ambao wanalipenda zaidi soka la kitabuni, soka lisilotumia matumizi makubwa ya nguvu wala kasi isiyo na sababu. Hawa watalipenda zaidi soka la Hispania kuliko soka la Uingereza. Na ndiyo maana mashabiki duniani wamegawanyika katika pande kuu mbili.

Kwa Uingereza, ushindi ni zaidi ya kucheza soka maridadi. Ni zaidi ya kupiga kanzu, tobo, chenga za maudhi na mbwembwe nyingine uwanjani. Wanachotaka ni ushindi tu na soka la kazi.

Kocha maarufu wa zamani wa Liverpool, Billy Shankly aliwahi kusema; “Kuna watu wanaosema soka ni mchezo wa maisha na kifo, mimi naona ni zaidi ya hapo”. Bill alikuwa anawakilisha falsafa ya soka la Kiingereza.

Kwa Hispania, soka si hivyo. Soka ni mchezo maridadi wa kuonyeshana ubora uwanjani na si vinginevyo. Kwao, bao maridadi linasakwa kwa mbinu maridadi na si zile za Kiingereza za kulazimisha zaidi.

Jaribu kutazama wakati timu ya Kiingereza inapojaribu kutafuta bao la kusawazisha. Soka litakalochezwa hapo ni la mipira mirefu, krosi, kona na kila mbinu ya ushindi wa haraka haraka. Kwa Hispania, soka litakalochezwa ni lile la kumiliki zaidi mipira na kutafuta mbinu za kupenyeza mipira ya chini katika misitu ya walinzi wa timu pinzani.

Na hapa ndipo linapoibuka jibu la kwa nini wachezaji wengi wa bara la Amerika Kusini wanapenda kucheza Ligi kuu ya Hispania kuliko ligi kuu ya England. Ligi kuu ya Hispania ni ndoto yao kwa sababu inafiti mfumo wao wa uchezaji kuliko Ligi kuu ya England.

Amerika Kusini, katika nchi kama Brazil, Argentina, Paraguay, Chile na nyinginezo, soka linachezwa katika staili ya kumiliki mpira zaidi na kuonyesha vipaji binafsi tofauti na Uingereza.

Kuanzia enzi za akina Diego Maradona, Romario, Careca, Rivaldo na wengineo, mpaka enzi hizi za akina Lionel Messi, Diego Forlan, Ronaldinho na wengineo, wachezaji wa Amerika Kusini wametamba zaidi Hispania na hata Italia, kuliko Uingereza.

Na wakati mwingine unaweza pia kupima namna ambavyo wachezaji wengi wa Hispania, au waliowahi kucheza Ligi ya Hispania namna walivyoshindwa kung’ara katika soka la Kiingereza.

Akina Josemi, Fernando Morientes, Asier del Horno, Maxi Rodriguez, Patrick Kluivert, Davor Suker na wengineo wengi kutoka Ligi Kuu ya Hispania walichemsha kucheza katika kiwango cha juu katika Ligi Kuu ya England.

Kasi na nguvu za soka la Uingereza ziliwashinda. Wakati wao wakifikiria zaidi kukaa na mipira na kucheza kwa uhuru, Ligi ya Kiingereza ilihitaji zaidi wachezaji wanaocheza kwa haraka na kuvamiana bila ya kuhitaji mipango sahihi ya soka.

Shukrani kwa Fernando Torres, Claude Makelele na Xabi Alonso ambao walimudu kwa kiasi kikubwa kasi ya ligi kuu ya England. Siwezi kumzungumzia Cesc Fabregas kwa sababu aliingia staili ya soka la Uingereza akiwa kinda na imempa wakati mzuri wa kuijulia kwa ufasaha.

Lakini rekodi zinaonyesha wachezaji wengi wanaotoka Ligi Kuu ya Uingereza kwenda Hispania, huwa hawapati mgumu wa kumudu soka la Kihispania. Sababu kubwa ni kwamba wanajikuta wakiwa katika nafasi nzuri ya matumizi ya nguvu kuliko wachezaji waliowakuta.

Wakati Michael Owen akionekana ameanza kusuasua katika Ligi Kuu ya Uingereza, Liverpool ilimtia sokoni. Lakini akaibuka na mabao 13 ya Ligi katika Ligi ya Hispania wakati rekodi yake ya ufungaji msimu mmoja kabla pale Uingereza ikionekana kuwa finyu.

David Beckham, Nicolas Anelka ‘Le Sulk’, Ruud Van Nisterlooy, Diego Forlan na wengineo wameonekana kuingia moja kwa moja katika mfumo wa uchezaji wa Hispania bila ya shida.

Msimu mmoja baada ya Sir Alex Ferguson kumuuza Diego Forlan, nyota huyo wa Amerika Kusini aliibuka kuwa mmoja kati ya wafungaji bora wa Ligi Kuu ya Hispania. Uingereza alionekana kama vile ni mshambuliaji wa kawaida.

Wengine wanapima ubora wa Ligi kutokana na mafanikio yao katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya. Lakini hata wale ambao wanaamini kuwa Ligi Kuu ya England ni bora kuliko ile ya Hispania kutokana na mafanikio ya sasa ya timu za England za England katika michuano ya Ulaya, nadhani wanakosea kwa sababu tayari timu za Hispania zilishafanya mambo makubwa siku za nyuma.

Ni kweli Waingereza wametesa zama hizi, ikiwemo fainali ya wenyewe kwa wenyewe kati ya Chelsea na Manchester United mwaka 2008 pale Moscow, Urusi. Lakini mwanzoni mwa miaka ya 2000 ni Hispania ndiyo ambayo ilitesa vilivyo katika soka la mabingwa wa Ulaya. Nao pia waliwahi kuingiza fainali ya timu mbili za Hispania kati ya Real Madrid na Valencia mwaka 2002.

Kwa kuhitimisha tu, nadhani ni wakati wa watu kuelewa kuwa linapokuja suala la timu ligi ipi ni bora kati ya England na ile ya Hispania, kigezo kinachoweza kutumiwa si mafanikio wala kingine zaidi ya mtazamo wa shabiki binafsi kuhusu staili ya soka analolipenda.

Kama utapenda soka la nguvu, kasi na vurugu za hapa na pale, nadhani soka la Uingereza litakaa moyoni mwako. Kama utapenda soka la akili zaidi, maarifa na ustaarabu wa kupeana nafasi katika kucheza soka, ni lazima utapenda soka la Hispania.

Bahati mbaya, FIFA hawana utaratibu wa kuchagua Ligi bora kama wanavyochagua wachezaji bora. Nadhani wako sahihi. Kinachobakia ni mtazamo binafsi wa shabiki kuhusu staili ya soka wanalolipenda. Kama vile wachezaji wa Amerika Kusini wanavyochagua…

NUKUU YA LEO.

“Nilikuwa namdai fedha zangu Chang’walu na wala sikumkimbiza kwa ajili ya kumpiga”
-Kauli ya kiungo wa Yanga, Athuman Idd ‘Chuji’ alipohojiwa kwa madai ya kutaka kuwapiga waamuzi katika pambano la Yanga dhidi ya African Lyon.

RIPOTI: INTER WAKUBALI OFA YA UNITED KWA SNEIJDER


Wesley Sneijder atakuwa mchezaji mpya wa Manchester United wiki hii……….ikiwa atakubaliana na Red Devils kuhusu malipo ya mshahara, gazeti la daily mirror la UK limeandika.

Klabu ya Inter Milan wamekubali ofa ya £30million iliyotumwa na United weekend iliyopita.

Milan wapo tayari kutoa ruhusa kwa Sneijder kuongea na uongozi kutoka Old Trafford, na taarifa zinasema kuwa mazungumzo kati ya Sneijder na Red Devils yatafanyika ndani ya wiki hii.

Kizuizi pekee cha kukamilika kwa uhamisho huo unaotingisha ulimwengu wa soka ni kwamba mchezaji husika anahitaji mshahara mkubwa, kama anaoupata Inter kwa sasa.

Sneijder anataka mshahara wa £190,000 per week, fedha ambayo ipo nje ya mipaka ya ulipaji mishahara ndani ya mipango ya United, lakini baada ya mazungumzo kati Man United CEO David Gill na Sir Alex Ferguson wamekubaliana kutoa ofa ya mshahara mnono kwa Sneijder bila kuvunja mipaka ya matumizi ya klabu hiyo kwa msimu.

Wakala wa Sneijder anategemea kwenda U.K kabla ya weekend, na United wanategemea kuwa kiungo huyo wa kimataifa wa Uholanzi atafanya mazoezi na kikosi cha Reds kabla ya kuanza kwa Premier League JuMAMOSI.

Sneijder jana baada ya mechi ya fainali ya Doublin Cup dhidi ya Man City aliweka wazi kuwa uwezekano wa kuhama Inter upo a lolote linaweza kutokea.

JUVENTUS WAMSAJILI MIRKO VUCINIC


Juventus wamekamilisha usajili wa Mirko Vucinic kutoka AS Roma kwa mkataba wa miaka 4 kwa gharama ya 15million, Serie A club wametangaza leo Jumatatu kupitia official website yao.

Vucinic, 27, ambaye alikuwa akihusishwa na kujiunga na Tottenham, lakini Juventus walikuwa fasta na wamefanikiwa kukamilisha dili hilo baada ya general director wa Juve Giuseppe Marotta kuongea na mwanzake wa Roma Walter Sabatini ili ku-formalise uhamisho huo.

Taarifa rasmi kutoka Roma ilisema: “Juventus Football Club inatoa taarifa kuwa imefikia makubaliano na A.S Roma kwa uhamisho wa kudumu na haki za michezo za mchezaji Mirko Vucinic.Mkataba una thamani ya €15million na fedha hizo zitalipwa ndani ya misimu 3 ijayo.”

Monday, August 1, 2011

MTUKUTU JOEY BATON ATIMULIWA NEWCASTLE


Joey Borton amewekwa rasmi kwenye listi ya wachezaji wanaotakiwa kuondoka Newcastle katika kipindi hiki cha kiangazi.
Bad-boy Barton ameambiwa atafute klabu mpya baada ya kutangaza vita na viongozi wa klabu yake kwenye mtandao wa Twitter.
Kiungo huyo alitumia mtandao huo wa kijamii wiki hii kuwashambulia kwa maneno mabosi wake, ambao walimpiga faini Jose Enrique ambaye nae alifanya kitendo cha kuushambulia uongozi, pia Barton aliusema uongozi kwa kitendo cha kumuuza Kevin Nolan kwa West Ham.
Taarifa kutoka kwa uongozi wa Newcastle kupitia mtandao wa rasmi wa klabu ilisema: “Newcastle United inaweza kuthibitisha kuwa Joey Barton amewekwa katika listi ya wachezaji wanaotakiwa kuondoka.Mchezaji ameambiwa anaweza kuondoka kwa uhamisho wa bure kabisa.”
Barton, 28, alikuwa yupo katika mwaka wa mwisho wa mkataba na The Magpies na hakuwa amepewa ofa ya mkataba mwingine.

STAKELENBURG KUJIUNGA NA ROMA LEO


Golikipa wa Ajax Maarten Stakelenburg anatarajiwa kujiunga na AS Roma kwa mkataba wa miaka 4, mara baada ya kufanyiwa vipimo juzi Jumamosi.

“Nina furaha kwamba nitasaini mkataba wa miaka 4 na Roma.Kila kitu kuhusu klabu hii inahusu soka.Sijapata muda wa kutembelea uwanja bado, lakini nimefurahishwa na uwanja wa kufanyia mazoezi.” Alisema Stakelenburg katika mtandao wa Sport-Promotion unaomilikiwa na Wakala wake Rob Jansen.

“Pia nimeongea na kocha mkuu Luis Enriquekuhusu mipango yake na klabu, na yalikuwa ni mazungumzo mazuri sana.Pia ameniambia ana matumaini Ajax na Roma watafikia mwisho na kumalizana juu ya usajili wangu.”

Ajax walitangaza Ijumaa iliyopita kwamba wamekubaliana na Roma kwa kauli kuhusu uhamisho wa kipa huyo mwenye miaka 28.

Klabu hizi mbili zinategemea kumalizana ndani ya masaa 24 ya leo hii, huku Roma wakijipanga kumtambulisha Stakelenburg kwa waandishi leo jUMATATU.

MAARTEN STAKELENBURG TOP 10 SAVES

VALENCIA ASAINI MKATABA MPYA UNITED


Antonia Valencia amesaini mkataba wa miaka 4 ambao utamuweka Old Trafford mpaka mwisho wa msimu wa 2014/15.

The 25-year-old player ambaye alijiunga na mashatani wekundu kutoka Wigan Athletic katika kipindi cha kiangazi mwaka 2009 na ameshatumikia United kwenye mechi 69, akifunga mabao 10 huku akishinda kombe la Premier League na Carling Cup.

MAGOLI NANE YALIYOFUNGWA KATIKA MECHI ZISIZO ZA MASHINDANO

ZIDANE


CHRIS EAGLES vs Shenzhen


THIERRY HENRY vs SC Wiez


DIDIER DROGBA vs AC Milan


FILIPPO INZAGHI vs Barcelona


JOHN ARNE RIISE vs Celtic


YOSSI BENAYOUN vs Wycombe Wanderers


MICHAEL OWEN vs Hangzhou Greentown

SERENGETI FIESTA 10 YAITINGISHA DAR

"HAINA MAJOTROOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO" UMATI WA WATU WAKISHEREKEA MSIMU WA DHAHABU NA SERENGETI.FID Q NA IZZO B WAKIWAZOMEA TANESCOOOO KWENYE MSIMU WA DHAHABU WA FIESTA 10
PRIME TIME PROMOTION WALITISHA SANA CHECK OUT THE STAGE, ITS AMAZING
"I'VE GOT HO**S, IN A DIFFERENT AREA CODES" LUDACRISS ALITISHA SANA-SERENGETI FIESTA 10-HAINA MAJOTROOOOOOOOOOOOOOOO
KIROBOTO AKA JUMA NATURE AKIPOKEA TUZO YA HESHIMA KUTOKA KWA GODZILLAH KATIKA FIESTA 10.MNYAMWEZI MWENYEWE LUDACRIS AKIWAIMBISHA WANA DSM KATIKA SERENGETI FIESTA 10
"CHA ARUSHA TIME" JOH MAKINI AKIWAKILISHA KWA NIKKI WA 2 PAMOJA NA N2N SOLDIERS.
MKURUGENZI MTENDAJI WA SBL, RICHARD WELLS AKIWA NA MKURUGENZI WA MAWASILIANO TEDDY MAPUNDA WAKIFURAHIA SHOW YA FIESTA

Sunday, July 31, 2011

KWELI MTOTO WA NYOKA NI NYOKA..




HUYU NI MTOTO WA MSHAMBULIAJI JUAB PABLO ANDEL..





HUYU NDIYE JUAN PABLO ANGEL

Chimbuko la utawala wa wahindi katika soka la Tanzania

UKIANZA kuelezea historia ya soka Tanzania, bila shaka utaelezea miaka ya kuanzia 1970 kwenda mbele na si kurudi nyuma kutokana na uhalisia.

Nchi yoyote duniani lazima iwe na mfumo wake wa soka ili kutimiza malengo yake katika mpira wa miguu. Unaweza kuona jinsi Afrika Magharibi ilivyo na shule nyingi za soka.

Hapa chini, kuna maelezo kidogo yanayoeleza jinsi Tanzania ilivyoweza kutoa wachezaji wake katika miaka ya nyuma.

Mwaka 1970- 1976
Kwa Tanzania wakati wa miaka ya 1970, wachezaji waliojiunga na klabu zilizokuwa zikishiriki ligi walikuwa wakipatikana kwa njia ya kuibua vipaji kutoka mitaani na katika timu zilizokuwa zikishiriki michuano ya katika vijiji na majiji.

Wachezaji kama Adam Sabu, Kitwana Manara, Abdallah Kibaden, Jumanne Hassan ‘Masimenti’, Gibson Sembuli waliweza kufanya vizuri na kuweza kuwa kwenye chati kwa muda mrefu.

Chimbuko lao kiuchezaji, ndilo lililopelekea waweze kucheza kwa muda mrefu tofauti na sasa, mpango huu unaelezwa kwamba uliweza kutoa wachezaji wengi wenye vipaji na moyo wa kucheza soka kuliko sasa.

Ndani ya kipindi hiki, jamii iliendelea kumiliki timu na kuwekeana upinzani kuanzia ngazi ya mtaa hadi mkoa.

Mwaka 1976-1982
Hiki ni kipindi ambacho wachezaji wengi walikuwa wakitokea shuleni na vyuoni na kipindi kinachoelezwa kuwa kilitoa wachezaji wengi waliokuwa wanaona mbali katika soka na maisha.

Wachezaji kama Mohamed Salim, Thuwen Ally, Peter Tino, Omar Hussein, Adolph Richard, Leodegar Tenga, Mtemi Ramadhan, George Kulagwa waliweza kung’ara lakini miongoni mwao wako waliokuwa wakitumikia vitu viwili; shule na soka.

Watu kama Tenga, Mtemi na Laurence Mwalusako wanaweza kuwa mfano wa jambo hili hadi leo hii.

Ni kipindi hiki ambacho wachezaji wake waliweza kucheza kwa moyo wote na kufanikisha ushiriki wa Tanzania katika michuano ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 1980.

Ndani ya kipindi hiki timu za makampuni zilianza kuchomoza, lakini bado zilitegemea wachezaji kutoka shuleni na vyuoni ili kujiimarisha.

Mwaka 1982-1988
Ingawaje timu za makampuni na mashirika ya umma zilianza kushamiri tangu mwaka 1975, lakini kipindi hiki kinaelezwa kuwa kilikuwa cha timu hizo kutamba.

Timu kama Pamba, CDA, Bandari, Bima, Tegry Plastics, Tumbaku Moro, RTC Kagera na nyinginezo ziliweza kung’ara na kutishia uhai wa timu nyingine kama Simba, Yanga, Coastal Union, African Sports na nyinginezo.

Hapa wachezaji walikuwa wakicheza soka kama ajira kwao, kwani waliajiriwa katika kampuni hizo kama ilivyo kwa waajiriwa wengine, lakini wao wakiwa na jukumu la kucheza soka pekee.

Mchezaji Rashid Idd anaweza kukumbukwa jinsi alivyoingia katika kikosi cha timu ya taifa mwaka 1978 akitokea katika michuano ya mashirika na makampuni ya umma (Shimuta).

Idd, aliweza kung’ara katika michuano hiyo ambayo wakati huo ilikuwa na taswira kubwa tofauti na sasa, kiasi cha Kocha wa timu ya taifa kuishuhudia ili kuweza kupata wa watakaofaa kwa timu yake.

Licha ya timu za mashirika ya umma kutamba, pia klabu nyingine ziliweza kuteka soka la Tanzania na kuzima utawala wa Simba na Yanga.

Pamoja na hali hiyo, bado timu za kijamii ziliweza kung’ara. Kwa mfano mwaka 1988 Coastal Union na African Sports za Tanga ziliweza kuwekeana ushindani mkubwa katika ligi na kupokezana kukalia kiti cha uongozi kwa muda mrefu.


1988 – hadi sasa
Baada ya hali ya timu za kijamii kama Simba na Yanga kuwa siyo nzuri wafanyabiashara walianza kujitokeza ili kuzifadhili.

Mohamed Virani ‘Babu’, anaweza kuwa miongoni mwa ‘wahindi’ wa kwanza kujitokeza kudhamini soka.

Hali ilizidi kushamiri mwaka 1990 pindi Abbas Gulamali(sasa marehemu), Azim Dewji na Shiraz Sheriff walipojitokeza moja kwa moja kuzifadhili Simba, Yanga na Pan African F.C ya Dar es Salaam.

Wakati Gulamali akiwa na Yanga, Dewji ambaye kwa sasa yupo na Moro United alikuwa akiisaidia Simba kuweza kurudi katika hali yake. Shiraz yeye alikuwa ndiyo mfadhili mkuu na meneja wa timu ya Pan African.

Wafadhili hawa waliweza kuwanunua wachezaji kutoka katika makampuni na mashirika ili kuimarisha timu zao.

Hussein Masha, Gerorge Masatu, wanaweza kuwa miongoni mwa wachezaji walioihama Pamba na kujiunga na Simba kutokana na ahadi za Dewji, pindi walipohama waliweza kuidhohofisha timu hiyo huku wakiipandisha chati Simba.

Hivyo hivyo kwa Yanga, ambao waliweza kumnyakua Edibily Lunyamila kutoka Biashara ya Shinyanga na Mohamed Hussein ‘Mmachinga’ kutoka Bandari Mtwara na kuimarisha kikosi chao.

Mafanikio ya Yanga na ufadhili wa Gulamali yaliweza kuonekana mwaka 1994 pale ilipotwaa Kombe la Afrika Mashariki na Kati huku Simba ikifanikiwa kufika fainali ya Kombe la CAF mwaka 1993 na kufungwa na Stella Abidjan.

TIMU ZILIPO SASA;
Ukitoa timu za makampuni binafsi na taasisi za serikali kama Mtibwa Sugar, Kagera Sugar, Azam FC, African Lyon, Prisons, klabu nyingine za Ligi Kuu zilizobaki hazina chanzo cha uhakika cha fedha.

Nyingi zinaendelea kuwa imara kutokana na uhisani wa watu mbalimbali wenye mapenzi nazo, wengi wao hawana mikataba maalum ya kusaidia au kufadhili, jambo linalohatarisha uhai wake.

Moro United iliweza kutetereka baada ya kujiengua kwa waliokuwa viongozi wake, kama ilivyokuwa kwa Pallsons ya Arusha iliyokuwa chini ya uongozi Askofu Mollel.

MANCHESTER UTD YAIFUNGA BARCELONA 2-1

WHITE CAPS YA NIZAR KHALFAN YAPIGWA 4-0 NA GALAXY YA BECKHAM.




MIPANGO KABLA YA MCHEZO ILIKUWA HIVI...









MAKUNDI YA KUFUZU FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA 2014

Upangaji makundi ya mechi za mchujo kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil ulifanywa jana (Julai 30 mwaka huu) karibu na ufukwe wa Copacabana jijini Rio de Janeiro nchini Brazil ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) Jerome Valcke.

Tanzania (Taifa Stars) imepangwa kundi C Kanda ya Afrika ambalo lina timu za Cote d’Ivoire, Morocco na Gambia. Lakini kabla ya kuingia katika kundi hilo Stars italazimika kucheza raundi ya kwanza ya mchujo dhidi ya Chad.

Stars ikifanikiwa kuitoa Chad baada ya mechi mbili za nyumbani na ugenini zitakazochezwa kati ya Novemba 11-15 mwaka huu ndiyo itaingia katika kundi hilo la C. Pia mshindi wa kundi C ndiye atakayeingia katika raundi inayofuata kabla ya kupata tiketi ya kwenda Brazil.

Stars ni miongoni mwa timu 29 ambazo kwenye viwango vya ubora vya FIFA vya Julai mwaka huu katika Afrika ziko chini ya timu 24 bora, hivyo kulazimika kuanzia hatua hiyo ya kuchujana zenyewe kabla ya kuingia hatua ya makundi ambayo itachezwa kuanzia Juni 1, 2012 hadi Septemba 10, 2013.

Kwa mujibu wa viwango vya FIFA vya Julai mwaka huu, Tanzania iko katika nafasi ya 127 wakati Chad ni namba 158. Kwa upande wa Afrika, Tanzania ni namba 33 na Chad 43. Nchi 52 kati ya 53 za Afrika zimeingia katika michuano hiyo ya Kombe la Dunia. Ni Mauritania pekee ambayo haikuthibitisha ushiriki wake.

Timu 10 za juu kwa ubora barani Afrika ambazo zimeongoza makundi 10 ya Afrika katika upangaji ratiba ni Afrika Kusini, Tunisia, Cote d’Ivoire, Ghana, Burkina Faso, Nigeria, Misri, Algeria, Cameroon na Senegal.

Afrika ina nafasi tano kwenye fainali za Kombe la Dunia, huku Ulaya ikiongoza kwa kuwa nazo 13











CAF FIRST ROUND
Somalia v Ethiopia
Equatorial Guinea v Madagascar
Chad v Tanzania
Lesotho v Burundi
Sao Tome e Principe v Congo
Seychelles v Kenya
Djibouti v Namibia
Comoros v Mozambique
Eritrea v Rwanda
Guinea-Bissau v Togo
Swaziland v DR Congo
Mauritius v Liberia

GROUP A
South Africa
Botswana
Central African Republic
Somalia/Ethiopia






GROUP B




Tunisia
Cape Verde Islands
Sierra Leone
Equatorial Guinea/Madagascar
GROUP C
Ivory Coast
Morocco
Gambia
Chad/Tanzania
GROUP D
Ghana
Zambia
Sudan
Lesotho/Burundi
GROUP E
Burkina Faso
Gabon
Niger
Sao Tome e Principe/Congo
GROUP F




Nigeria
Malawi
Seychelles/Kenya
Djibouti/Namibia
GROUP G
Egypt
Guinea
Zimbabwe
Comoros/Mozambique
GROUP H
Algeria
Mali
Benin
Eritrea/Rwanda
GROUP I
Cameroon
Libya
Guinea-Bissau/Togo
Swaziland/DR Congo
GROUP J
Senegal
Uganda
Angola
Mauritius/Liberia




Concacaf

The teams ranked 7-25 in the region will be joined by the five play-off winning teams from round one to comprise six groups of four teams in the second round of qualification.

The group winners will then be drawn alongside the six best-ranked teams in the region in the third round of the qualification process before the fourth round, the Hexagon, commences.

SECOND ROUND:
GROUP A
El Salvador
Surinam
Cayman Islands
Dominican Republic
GROUP B
Trinidad & Tobago
Guyana
Barbados
Bermuda
GROUP C




Panama




Dominica
Nicaragua
Bahamas

GROUP D
Canada
St.Kitts & Nevis
Puerto Rico
St Lucia

GROUP E
Grenada
Guatemala
St Vincent & the Grenadines
Belize

GROUP F
Haiti
Antigua & Barbuda
Curacao
US Virgin Islands


THIRD ROUND:
GROUP A
USA
Jamaica
Winner E
Winner F

GROUP B
Mexico
Costa Rica
Winner A
Winner B

GROUP C
Honduras
Cuba
Winner D
Winner C
Conmebol

Brazil, as hosts, qualify automatically. Each of the other nine member teams will play against each other home and away in order to determine the final finishing order of qualified sides. The top four will play at the 2014 Fifa World Cup while the fifth placed team will face an intercontinental play-off with a Concacaf nation.

CONMEBOL TABLE
Argentina
Bolivia
Chile
Colombia
Ecuador
Paraguay
Peru
Uruguay
Venezuela





The winners of each group will qualify directly for the 2014 Fifa World Cup. The eight best runners-up will be drawn against each other in a two-legged play-off to determine the other four qualifiers.

GROUP A
Croatia
Serbia
Belgium
Scotland
FYR Macedonia




Wales




GROUP B
Italy
Denmark
Czech Republic
Bulgaria
Armenia
Malta

GROUP C
Germany
Sweden
Ireland
Austria
Faroe Islands
Kazakhstan




GROUP D
Netherlands
Turkey
Hungary
Romania
Estonia
Andorra

GROUP E
Norway
Slovenia
Switzerland
Albania
Cyprus
Iceland




GROUP F
Portugal
Russia
Israel
Northern Ireland
Azerbaijan
Luxembourg

GROUP G
Greece
Slovakia
Bosnia-Herzegovina
Lithuania
Latvia
Liechtenstein
GROUP H
England
Montenegro
Ukraine
Poland
Moldova
San Marino


GROUP I
Spain
France
Belarus
Georgia
Finland