Search This Blog

Thursday, November 22, 2012

MTANZANIA APEWA MKATABA EA SPORTS KWA AJILI YA GAME ZA FIFA.

Wednesday, November 21, 2012

DROGBA AOMBA KUSAJILIWA KWA MKOPO - KURUDI CHELSEA??

DIDIER DROGBA amefungua mlango wa kurudi kwenye premier league baada ya kuomba ruhusa ya kujiunga na klabu nyingine nje ya dirisha la usajili.

FIFA ilisema kwamba inafikiria ombi la mshambualiaji wa Shanghai Shenhua katika siku moja ambayo kocha wa zamani wa Chelsea Di Matteo alipofukuzwa.
  Taarifa ya FIFA ilisema: “Tunaweza kuthibitisha kwamba mchezaji Didier Drogba ametuma ombi la kuruhusiwa kusajiliwa nje ya dirisha la usajili na klabu kwa mkopo."


Drogba, ambaye aliondoka Chelsea baada ya kufunga penati ya ushindi katika fainali ya champions league, amekuwa akifikiria kurudi kufanya mazoezi na klabu yake ya zamani wakati ligi kuu ya China itakapokuwa imeisha - kitu ambacho Di Matteo alisema atakukaribisha vizuri kabla ya kutimuliwa leo asubuhi.
Kwa sheria zilizopo za FIFA haziruhusu Drogba kuhamia timu yoyote mpaka January 1.

BECKHAM ATANGAZA KUONDOKA L.A GALAXY BAADA YA MIAKA 6

Siku moja baada ya mabingwa watetezi L.A. Galaxy kuingia kwenye fainali ya pili mfululizo ya MLS, David Beckham ametangaza kwamba fainali hiyo itakuwa ya mwisho japokuwa amebakiwa na mwaka mmoja katika mkataba wake.
Beckham alisaini mkataba wa miaka miwili mwezi January baada ya kumaliza wa kwanza miaka 5 mwaka uliopita ambapo Galaxy walibeba ubingwa wao kwanza tangu alipojiunga na timu hiyo. Mwaka 2012, Beckham amekuwa na msimu mzuri katika ligi ya MLS akifunga mabao 7 na kutengeneza mengine matano katika mechi 28. Lakini wiki iliyopita, tetesi za kumhusu kiungo huyo wa miaka 37 kuondoka kwenda Australiakwenye A-LEAGUE zilianza kusambaa lakini kwa haraka zikakanushwa na msemaji wake.

Sasa akiwa anaondoka Galaxy, uhamisho wa kwenda A-League sasa unawezekana, lakini pia anaweza kwenda kwenye klabu nyingine ya MLS au mahala pengine popote duniani ambapo wanataka kuuza jezi za David Beckham.

Monday, November 19, 2012

EXCLUSIVE:MADUDU YA UCHAGUZI DRFA YAENDELEA


Mjumbe Mwarami Kobe Ally ( kushoto ),mwenyekiti,Juma Simba (kati ) na Katibu wa kamati bwana Peter Hella (kulia ) .

Mgombea asiyeudhuria usaili apitishwa kugombea
WAKATI majina ya wagombea katika uchaguzi mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) yakiwekwa hadharani, majina ya wagombea Said Tully,Ally Mayay na Philemon Ntahilaja yamekatwa huku Isaac Mazwile akipitishwa bila hata ya kuwepo katika usaili.
 Awali Tully ambaye ni wakala anayetambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) aliwekewa pingamizi la kutokuwahi kufanya kazi katika klabu ya Ashanti United ya Ilala na hata alipowasilisha barua ya kuchaguliwa katika moja ya kamati za timu hizo, alitupwa nje.
 Mbali ya Mazwile kupitishwa kuwania nafasi ya mwakilishi wa mkutano mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na makamu mwenyekiti, mtu mwingine aliyepitishwa ni Muhsin Balbhou anayewania nafasi ya mwakilishi wa mkutano mkuu huku akiwa amewekewa pingamizi.
 Uteuzi wa Mwarami Ally Kobe kwa mara ya pili katika kamati ya uchaguzi
Kwa mujibu wa mmoja wa wagombea wa nafasi ya uwakilishi wa mkutano mkuu, Shaffih Dauda, mjumbe wa kamati hiyo Ally Kobe, hakustahili kuchaguliwa tena kuwamo ndani ya kamati hiyo kwani alishiriki madudu ya awali yaliyoifanya kamati iliyokuwa chini ya Mwenyekiti, Muhidin Ndolanga kuvunjwa na TFF.
 Hivi karibuni, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Deo Lyato alivunja kamati ya uchaguzi ya DRFA iliyokuwa chini ya Ndolanga kutokana kukiuka kanuni mbalimbali za uchaguzi huku kubwa likiwa kutia kasoro fomu za wagombea kadhaa.
 Kobe anadaiwa kuhusika kwa kiasi kikubwa katika madudu hayo, lakini Mwenyekiti wa DRFA anayemaliza muda wake, Said Bakhressa ambaye ameenguliwa na kamati ya Lyato kutetea nafasi yake, alihakikisha Kobe anabaki katika kamati ili tu kuhakikisha mtandao wake wa viongozi unapitishwa kuwania uongozi DRFA.
 Hivyo, Kobe aliachwa ili kuwalinda baadhi ya wagombea wanaodaiwa kuwa ama wafuasi au kupandikizwa na Bakhressa katika mchakato wa usaili hata mapingamizi wanayowekewa.
 Ili haki itendeke, ilitakiwa Kobe asiwepo tena katika kamati mpya ili kufanya mambo yaendelee katika mstari mnyoofu kwani lengo la Lyato lilikuwa kuhakikisha haki inapatikana katika mchakato wa uchaguzi huo. Hii ina maana si Ndolanga peke yake aliyekuwa na matatizo katika kamati hiyo.
 Inaweza hata mambo yaliyotokea wakati mwenyekiti akiwa Ndolanga, yalisababishwa na wajumbe kama kina Kobe. Kwa hali hii, hakuna jipya lililofanywa na Lyato, kwani madudu yameendelea. 
 Miongoni mwa mambo yaliyofanywa na kamati ya sasa ya uchaguzi ya DRFA iliyo chini ya Mwenyekiti, Juma Simba ‘Gaddafi’ ni kupitisha majina ya Mazwile na Balhabou huku wakiwa wamewekewa mapingamizi na wagombea wenzao.
 Gaddafi kutokuwepo katika kamati kwaruhusu madudu
Katika kikao cha kupitia mapingamizi yaliyowekwa kwa baadhi ya wagombea wa uchaguzi wa DRFA, mwenyekiti, Juma Simba hakuwepo kutokana na udhuru aliotoa ili kuhudhuria mambo ya siasa katika Chama cha Mapinduzi (CCM) ambako ana majukumu.
 Kwa kutumia mwanya huo, wajumbe Said Rubeya na Kobe walitumia kila njia kuhakikisha wanawabeba baadhi ya wagombea ambao ndani yake wapo Mazwile na Balhabou.
 Hata katibu wa kamati, Peter Hella alizidiwa nguvu na Rubeya na Kobe katika kuhakikisha haki inapatikana jambo lililomfanya achukue uamuzi wa kujiuzulu kwa kutokubaliana na kilichokuwa kikifanywa na wajumbe hao.
 Kuona hivyo, mwenyekiti Gaddafi alipopewa taarifa hizo na Hella, alimsihi katibu huyo asijiuzulu kwa ahadi ya kuzidi kuuchafua uchaguzi huo. Hella bado yupo mguu ndani mguu nje kuhusu nafasi yake kwenye kamati hiyo.
 Pingamizi la Mazwile lilivyozimwa.
Mgombea Mazwile aliwekewa pingamizi na Shaffih Dauda linalohusu kitendo chake cha kutokuwa mwadilifu katika kazi zake akiwa mtendaji wa Chama cha Soka Kinondoni (KIFA) kwa kumruhusu mtu asiye kiongozi kusaini kazi za chama hicho.
 Inadaiwa kuwa, Mazwile akiwa mtendaji wa KIFA alitakiwa kusaini fomu za wagombea mbalimbali waliokuwa wakitakiwa kuhalalishwa kugombea katika vyama mbalimbali vya soka ikiwemo DRFA ili kuthibitishwa uhalali wao.
 Akijua ni kinyume na taratibu, Mazwile akiwa safarini mkoani Dodoma aliruhusu mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Seif Ally Mailo 'Saddam' alisaini fomu na karatasi nyingine zilizopita KIFA kwa niaba yake, ikimbukwe Saddam hana madaraka yoyote KIFA.
 Katika pingamizi hilo, vithibitisho vilitolewa ikiwemo karatasi zilizosainiwa na Saddam kwa niaba ya Mazwile lakini kamati ya uchaguzi kupitia wajumbe wakina Rubeya na Kobe, walitupilia mbali pingamizi hilo. Hata katibu ambaye ni Hella alipowataka wajumbe wenzake kutazama kwa mara ya pili pingamizi hilo, alipingwa vikali. Hatimaye, pingamizi la Mazwile lilitupwa mbali.
 Pingamizi la Balhabou nalo utata mtupu  
Katika pingamizi lake kwa Balbhou, Shaffih Dauda alikuwa alipinga mgombea huyo kuwa na elimu ya kidato cha nne inayotakiwa kwa kila mgombea wa uongozi wa DRFA kwa sasa.
 Kamati ilitoa jibu la kuhakika vyeti vya Balbhou lakini ikimruhusu kuendelea na mchakato wa uchaguzi jabo ambalo ni kinyume na taratibu za uchaguzi huo. Hivyo pingamizi hilo nalo lilitupwa na kamati huku nguvu kubwa ikitoka kwa Rubeya na Kobe.
 Kwa kawaida taasisi inayotakiwa kuthibitisha elimu ya kidato cha nne nchini ni Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) na mchakato huo unaweza kuchukua siku saba hadi 14 tu.
 Mazwile hakuhudhuria usaili lakini kamati yampitisha
Madudu mengine yaliyofanywa na kamati ya uchaguzi ya DRFA ni kupitisha jina la Mazwile kuwania nafasi ya uwakilishi wa mkutano mkuu na makamu mwenyekiti bila ya kuhudhuria usaili wa wagombea wote uliofanyika katika ukumbi wa Uwanja wa Uhuru.
 Mmoja wa wagombea wa uchaguzi wa DRFA, Shaffih Dauda alikuwepo ukumbini tangu mwanzo hadi mwisho na hakumuona Mazwile kuhudhuria usaili huo, lakini jambo la ajabu jina la mgombea huyo limeorodheshwa katika majina ya wagombea waliopitishwa kuwania uongozi DRFA.
 Hayo ni baadhi tu madudu yaliyofanywa na kamati ya uchaguzi ya DRFA ambayo inasimamia uchaguzi unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
 ENDELEA KUWA NASI UPATE MADUDU MENGINE YA UCHAGUZI HUO

BREAKING NEWS! ALLY MAYAY TEMBELE NAYE ACHINJWA DRFA!



Haya ndio majina yaliyopishwa na kamati
Mwenyekiti
Evance Aveva,  Ayoub Nyenzi, Brown Ernest, Almas Kasongo
Makamu Mwenyekiti.
Mede Ramadhan, Salum Mwaking`inda, Ngungulugwa Tambaza, Issck Mazwile
Katibu mkuu
Msanifu Kondo,  Hamisi Ambali

Mjumbe mkutano Mkuu
Shaffih Dauda, Muhsin Balabouh, Shufaa Jumanne, Issack Mazwile

Mwakilishi wa Vilabu mkutano mkuu
Ben Kisaka, Juma Pinto, Frank Mchaki

Wajumbe
Shaaban Mohamed, Siza Chenja, Sunday Mwanahewa, Hamisi Kisiwa, Frank Mchaki, Bakary Mtumwa.

Waliokatwa
Said Tully (Katibu Mkuu ) , Ally Mayay (Makamu Mwenyekiti ),  Philemon Ntahiraja ( Mwakilishi wa Vilabu mkutano mkuu ), Salum Mkemi ( Mwenyekiti ) 

COMING SOON!

BREAKING NEWS! SAID TULLY NA PHILEMONI NTAHILAJA WAKATWA RASMI UCHAGUZI WA DRFA,ISSACK MAZWILE APITISHWA PAMOJA NA KUTOKUEPO KWENYE USAILI.


Mwarami Kobe Ally ( shoto ),Juma Simba na Peter Hella.



Habari nilizozipata hivi punde kamati ya uchaguzi ya DRFA chini ya mwenyekiti Juma Simba imewakata wagombea Said Tully pamoja Bwana Philemon Ntahilaja  kutokana na kukosa sifa ya uzoefu wa kuongoza mpira, na kamati hiyo hiyo imewapitisha wagombea waliowekewa pingamizi la kutokua na elimu ya kidato cha nne kama ambavyo kanuni za uchaguzi zinavyoagiza,
Lakini cha kustajaabisha zaidi ni kupitishwa kwa Bwana Issack Mazwile ambaye hakutokea kwenye usahili.

Taarifa zaidi zitafuata hivi punde........

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Katika kikao chake cha tarehe 3 Novemba 2012, Kamati ya Utendaji ya TFF ilipokea taarifa ya mapendekezo ya marekebisho ya Katiba TFF kama ifuatavyo:
  1. Kuingiza kipengele kinachohusu “Club Lincencing” kama ilivyoagizwa na CAF katika waraka wake unaowataka wanachama wote wa CAF, ikiwemo TFF, kuhakikisha kuwa kipengele hicho kinaingizwa katika katiba zao.
  2. Kutokana na ushauri na maagizo ya FIFA, TFF inatakiwa kuunda wa Kamati ya Rufaa ya Uchanguzi (“Elections Appeals Committee”) na kuondokana na utaratibu tulionao hivi sasa ambao Kamati ya Rufaa (“Appeals Committee”) inajigeuza na kuwa Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi wakati wa mchakato wa uchaguzi wa TFF.
  3. Kuindoa nafasi ya Makamu wa Pili wa TFF pamoja na kutamka kuwa Wawakilishi wa klabu za Ligi Kuu katika Kamati ya Utendaji watachaguliwa moja kwa moja na klabu zenyewe. Hii inatokana na azimio la Mkutano Mkuu uliopita la kuruhusu uundwaji wa chombo huru cha kusimamia Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza pamoja na kupitishwa kwa Kanuni zinazokiongoza chombo hicho kama zilivyopendekezwa na klabu za Ligi Kuu na kupitishwa na Kamati ya Utendaji.
Baada ya kutafakari mapendekezo hayo, Kamati ya Utendaji ya TFF iliamua kuwa:
  1. Ipo haja ya kuifanyia marekebisho Katiba ya TFF kama iliyopendekezwa.
  2. Kwa vile mapendekezo mawili kati ya matatu ya ya marekebisho ya Katiba yana uhusiano na Uchaguzi Mkuu wa TFF, ipo haja ya marekebisho hayo kufanyika kabla ya kutangazwa kwa Mkutano Mkuu wa TFF na kuanza kwa mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa TFF.
  3. Aidha, kwa vile TFF haina uwezo wa kuitisha mikutano mikuu miwili – Mkutano Mkuu Maalum kwa ajili ya marekebisho ya Katiba ya TFF; na Mkutano Mkuu wa Uchaguzi – katika kipindi kifupi kijacho, marekebisho ya Katiba yafanywe kwa njia ya Waraka (“Circular Resolution”).



  1. Waraka huo (“Circular Resolution”) uwe umeshatayarishwa na Sekretariati ikishirikiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria ifikapo tarehe 15 Novemba 2012 na ukabidhiwe kwa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji wanaowakilisha Kanda za TFF ambao watahakikisha kuwa  kila Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Kanda husika anapata fursa ya kutoa ridhaa yake.
  2. Zoezi la kupata ridhaa ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu liwe limemalizika katika kipindi cha siku 21.
  3. Kikao kinachofuata cha Kamati ya Utendaji kitafanyika Jumamosi tarehe 15 Desemba 2012 kwa madhumuni ya kupokea taarifa ya zoezi hili na kufanya matayarisho ya Mkutano Mkuu. Katiba ya TFF inaelekeza kuwa taarifa ya Mkutano Mkuu itolewe kwa wanachama wake angalau siku 60 (“notice period”) kabla ya Mkutano. Hivyo Kamati ya utendaji inatarajia kuwa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi utafanyika Jumamosi na Jumapili ya tarehe 16 na 17 na Februari 2013.
Kamati ya Utendaji ya TFF inasisitiza kuwa utaratibu huu umeamuliwa kutokana na TFF kutokuwa na uwezo wa kifedha wa kutayarisha mikutano mikuu miwili katika kipindi kifupi kijacho. Kinyume chake ni kuchelewa zaidi kufanyika kwa Mkutano Mkuu, jambo ambalo hatuna budi kuliepuka.
Kamati ya Utendaji ya TFF inatarajia kupata ushirikiano wa karibu kutoka kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na wadau wa mpira wa miguu kwa jumla ili kufanikisha zoezi hili na hatimaye kufanikisha Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa TFF.
Wenu Katika michezo,

Alex Mgongolwa
Mwenyekiti
KAMATI YA SHERIA, MAADILI NA HADHI ZA WACHEZAJI

MASHABIKI WA ARSENAL WANAPOIOMBEA MAFANIKIO SPURS




Wakati Patrick Viera anapiga penalti ya mwisho pale kwenye uwanja wa Millenium katika jiji la Cardiff na kumfunga golikipa wa Manchester United wa wakati huo, Bw Roy Carroll kisha kusherehekea ubingwa wa kombe la FA wa mwaka 2005, hakuna aliyewaza kwamba Arsenal itakaa zaidi ya miaka 7 bila kushinda kombe lolote kubwa lakini leo hii kuna mashabiki wa Arsenal wanaoamini kwamba timu yao ya msimu huu inaweza isishinde kombe lolote msimu huu pia. Mimi naamini Arsenal msimu huu ina nafasi walau ya kufika fainali kama si kushinda kombe la ligi maarufu kama Capital One Cup.
Arsenal imeondoka kabisa kwenye vichwa vya watu wengi, wadau wa soka kwamba ni timu inayoweza kushinda ligi kuu ya Uingereza hasa kwa kipindi hiki. Hii haimaanishi kwamba Arsenal si timu bora au tishio Uingereza, hapana, kinachomaanishwa hapa ni kwamba Arsenal ya sasa haina nguvu ya kuhimili vishindo vya ligi kuu na mwisho wa msimu iibuke bingwa wa ligi kuu ya Uingereza kama ilivyoshinda mara ya mwisho katika msimu wa 2003/2004, kitu ambacho kwa kiasi fulani kinasanifu ukweli halisi wa mambo. Arsenal ya hivi sasa ni timu ambayo inajikita zaidi kwenye makombe mengine mbali na ligi kuu kutokana na mfumo wa hayo makombe ulivyo, mfumo wa mtoano. Pamoja na kujikita kwenye makombe hayo (FA, Ligi ya mabingwa ya Ulaya ie UEFA CL na Capital One Cup)  bado imekuwa haifanyi vizuri sana pia kwa sababu hata huko haijashinda hata moja kwa kipindi hiki cha miaka inayokaribia 8.
Sasa wakati wengi tukiona Arsenal haina nafasi ya kushinda ligi kuu ya Uingereza, kuna mashabiki baadhi wa Arsenal ambao hao dua zao za kuiombea timu yao ziko tofauti kabisa na matarajio ya wengi, wao wanaombea mafanikio mahasimu wao wakubwa zaidi, Tottenham Hotspur au Spurs. Unajua kwa nini wanaiombea mafanikio Spurs? Endelea kufuatana nami.
Hizi timu za Arsenal  na Tottenham, uhasama wao umekuwa ni wa muda mrefu sana, siku moja nitakuja hapa kuuelezea huu uhasama wao tu, chanzo na kwa nini unadumu hadi leo hii. Pamoja na uhasama huu kudumu kwa muda mrefu bado Arsenal imeendelea kuwa timu bora mbele ya Spurs kwa kipindi kirefu sasa.Tangu ligi ya Uingereza imekuwa ligi kuu, Tottenham Hotspur imewahi kumaliza juu ya Arsenal mara moja tu katika msimu wa 1994/95 wakati Spurs ilipokuwa ya saba na Arsenal ya 12. Hiki ndio kitu kinachowasukuma mashabiki hawa wa Arsenal waombee Spurs ishike nafasi ya pili kwenye ligi kuu ya Uingereza wakiamini timu hiyo haitakaa imalize juu yao tena na kama Spurs ikiwa ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya  Uingereza basi Arsenal itakuwa ya kwanza. Mtu mwingine unaweza kuona kama hawa mashabiki wa Arsenal aidha wanafanya mchezo wa kuigiza au labda haya ni maneno yao ya kuikashifu Spurs lakini kumbe wao wanamaanisha wanachokisema.
Pamoja na kuwa ligi kuu ya Uingereza bado ni ‘mbichi’ na bingwa hawezi kutajwa kipindi hiki, hili halinizuii kuwashauri mashabiki wa aina hii wa Arsenal kutokuwa na ndoto za kufikirika za aina hii badala yake washangilie kuwafunga Tottenham Hotspur goli 5 na Andre-Villas Boas goli 5 (wakati akiwa na Chelsea) wote kwa ujumla wao mara mbili mfululizo. Chakufanya, wamwambie kocha wa timu yao Bw Arsene Wenger ajikite zaidi katika kununua wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu na hasa wachezaji ambao tayari wameshaonekana kuwa bora (established players) kama Arteta, hapo kwa hakika watakuwa na timu bora ambayo haitangoja mpaka Spurs iwe ya pili ndipo yenyewe iwe ya kwanza.
Nakushukuru kwa kusoma makala hii mpaka hapa. Tuonane tena wakati mwingine.

Imeandaliwa na PodoBest
Twitter: @iPodoBest

SERENGETI BOYS YAWAPA MATUMINI WABONGO BAADA YA KUIFUNGA 1-0 KAGERA.

Wachezaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 ya Serengeti Boys wakishangilia bao lililofungwa na Mudathiri Yahaya Abbas wakati timu hiyo ilipopambana na Congo Brazzaville katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika kwa vijana wenye umri huo, zitakazofanyika  mwakani nchini Morocco. Serengeti Boys imeshinda 1-0. (Picha zote na Habari Mseto Blog)
 Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Jacob Michelsen na msaidizi wake Jamhuru Kihwelo  wakipongezana baada ya mchezo kumalizika. 
  Mshambuliaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 ya Serengeti Boys, Hussein Twaha akiwatoka mabeki wa timu ya Congo Brazzaville katika mchezo wa kufuzu kwa fainali za Afrika kwa vijana wenye umri huo zitakazofanyika  mwakani nchini Morocco. Mchezo huo ulifanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Serengeti Boys imeshinda 1-0. 
 Mshambuliaji wa timu ya Srengeti Boys, Faridi Mussa (katikati) akiwania mpira huku beki wa Cpngo Brazzaville, Tmouele Ngampio akijaribu kumzuia. Kulia ni Golipika wa Congo Brazzaville, Ombandza Mpea akijaribu kuokoa hatario langoni mwake. 
 Waamuzi wa mchezo huo wakitoka baada ya kwisha kwa pambano hilo
 Mshambuliaji wa Serengeti Boys, Tumain Baraka akichuana na beki wa Congo Brazzaville, Okombi Francis
 Heka heka katika lango la Congo Brazzaville
 Wachezaji wa Serengeti Boys, Hussein Twaha (shoto), Joseph Lubasha na Selemani Hamis Bofu wakibadilioshana mawazo wakati wakitoka mapumziko

UHURU SELEMANI AIGA RASMI SIMBA NA MASHABIKI WAKE KUJIUNGA NA AZAM


Sunday, November 18, 2012

SERENGETI BOYS YAITOA NISHAI CONGO BRAZZAVILLE KWA KUIFUNGA 1-0

Wachezaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 ya Serengeti Boys wakishangilia bao lililofungwa na Mudathiri Yahaya Abbas wakati timu hiyo ilipopambana na Congo Brazzaville katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika kwa vijana wenye umri huo, zitakazofanyika mwakani nchini Morocco. Serengeti Boys imeshinda 1-0. (Picha zote na Habari Mseto Blog)
Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Jacob Michelsen na msaidizi wake Jamhuru Kihwelo wakipongezana baada ya mchezo kumalizika.
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 ya Serengeti Boys, Hussein Twaha akiwatoka mabeki wa timu ya Congo Brazzaville katika mchezo wa kufuzu kwa fainali za Afrika kwa vijana wenye umri huo zitakazofanyika mwakani nchini Morocco. Mchezo huo ulifanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Serengeti Boys imeshinda 1-0.
Mshambuliaji wa timu ya Srengeti Boys, Faridi Mussa (katikati) akiwania mpira huku beki wa Cpngo Brazzaville, Tmouele Ngampio akijaribu kumzuia. Kulia ni Golipika wa Congo Brazzaville, Ombandza Mpea akijaribu kuokoa hatario langoni mwake.
Waamuzi wa mchezo huo wakitoka baada ya kwisha kwa pambano hilo
Mshambuliaji wa Serengeti Boys, Tumain Baraka akichuana na beki wa Congo Brazzaville, Okombi Francis
Heka heka katika lango la Congo Brazzaville
Wachezaji wa Serengeti Boys, Hussein Twaha (shoto), Joseph Lubasha na Selemani Hamis Bofu wakibadilioshana mawazo wakati wakitoka mapumziko
Selemani Hamis Bofu akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Congo Brazzaville, Tmouele Ngampio
 
Picha zote kwa hisani ya :www.francisdande.blogspot.com
 

NORWICH YAMPA MAN UNITED DOZI DOZI ILE WALIYOMPA ARSENAL



N1-0M www.fasthighlights.com by fasthighlights-2013

OLIVIER GIROUD KIWANGO, ARSENAL WAKIISAMBARATISHA SPURS KWA MIKWAJU MITANO KWA MBILI



A5-2T www.fasthighlights.com by fasthighlights-2013

WEST BROM WAIPA SOMO CHELSEA - WAITANDIKA 2-1


West Brom vs Chelsea 2:1 GOALS HIGHLIGHTS by UCL2410

LUIS SUAREZ AENDELEZA MAKALI YAKE - AIONGOZA LIVER KUIPA THALATHA KWA MTUNGI WIGAN



Liverpool 3 -0 Wigan All Goals & Highlights (17... by kofiswag

MAN CITY YAMTANDIKA ASTON VILLA 5 BILA NA KUKAA KILELENI EPL



Manchester City 5 0 Aston Villa hoofoot... by hoofoot

LIONEL MESSI AONGEZA MAWILI BAADA YA KUMPITA PELE - BARCA IKICHINJA 3-1



FC.Barcelona 3 1 Real ZARAGOZA hoofoot... by hoofoot

REAL MADRID YAZIDI KUWACHIMBIA KABURI AKINA LLORENT - WAWAPIGA KIGANJA



Real Madrid 5-1 Athletic Bilbao by goalsarena2012

Saturday, November 17, 2012

MCHEZAJI WA UJERUMANI AAMKA KUTOKA KWENYE COMA BAADA YA MWEZI 1

Klabu ya Bundesliga Hoffenheim imesema kiungo wake Boris Vukcevic ameamka kutoka kwenye coma, mwezi mmoja baada ya kujeruhiwa na ajali ya gari.

Vukcevic aliwekwa kwenye coma baada ya kufanyiwa upasuaji kufuatia ajali ya gari aliyopata tarehe 28 mwezi wa September, gari yake ilipongana na gari lingine kubwa.

Hoffenheim inasema kwamba kiungo huyo mwenye miaka 22, raia wa Ujerumani alipata fahamu masaa yaliyopita na kuweza kuzungumza na ndugu zake, lakini klabu hiy imesema kwa muonekano wa jeraha lake kichwani alilopata kwenye ajali ni vigumu kutoa utabii wowote juu ya upataji nafuu yake na kupona kabisa.

KILIMANJARO MARATHONI 2013 YAZINDULIWA

Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Bi. Kushilla Thomas akishirikiana na Mkurugenzi Msaidizi wa Michezo wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo Bi. Juliana Yassoda kukata utepe kuzindua rasmi mbio za Kilimanjaro Marathon 2013 zinazotarajiwa kufanyika Moshi mwezi Machi mwaka 2013. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki. (Picha: Executive Solutions)

Wash United kuungana na Taifa Stars kuweka mazingira na Usafi ‘salama’



Mpira wa miguu unaweza kufanya nini kuhusu mazingira na usafi?
Zaidi ya watu bilioni 2.6 duniani wanaishi bila ya kuwa na vyoo. Barani Afrika, magonjwa ya kuhara yanayosabishwa na ukosefu wa vyoo na usafi ni hatari zaidi na ndio yanayosababisha vifo kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano, hii ni zaidi ya magonjwa kama Ukimwi, Malaria na surua ikifuatia. Takwimu kutoka mashirika ya UNICEF na WHO zinaonyesha kuwa nchini Tanzania zaidi ya asilimia 90 ya watanzania wanaishi katika mazingira machafu, na asilimia 12 hawana vyoo wala maji. Matokeo yake zaidi ya watoto 24,000 nchini Tanzania hufariki dunia kila mwaka. Tabia ya kunawa mikono kwa kutumia sabuni ni njia rahisi na haina gharama kubwa katika kuzuia magonjwa ya kuhara ambayo haitumiki sana hapa nchini hasa kwa watoto. Tatizo kubwa ni kwamba usafi wa mazingira na afya haupewi kipaumbele katika mawazo ya watu wengi katika vyombo vya habari na jamii kwa ujumla.
Taasisi isiyo ya kiserikali ya Wash United inafanya kazi kuweka sawa mambo ya mazingira na usafi katika ngazi zote mahala popote na kuhamasisha watu kunawa mikono kwa sabuni kila mara. Wash United ni mpango mpya wa kwanza kutumia nguvu ya mpira wa miguu na mastaa wake katika kuhamasisha unywaji wa maji safi, mazingira safi na usafi kwa wote barani Afrika na duniani kote. Katika kukamilisha mpango wake huu Wash United imeungana na wadau mbalimbali duniani, kwa hapa Tanzania shughuli zinaendeshwa kwa msaada wa shirika la maendeleo la Ujerumani (GIZ).
Kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF)
Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania limekubali kushirikiana na mpango wa Wash United katika kuhamasusha tabia ya kutunza mazingira na usafi kwenye timu za vijana kupitia mradi timu za vijana wa shirikisho hilo. Katibu mkuu wa TFF Ndugu Angetile Osiah, leo amesaini mkataba wa makubaliano kati ya TFF na Wash United. “Ushirikiano kati ya Taasisi ya Wash United na Shirikisho la mpira wa Miguu ni mpya na wa kujitolea katika sekta ya mpira wa miguu Tanzania. Akiongea kuhusu Wash United, mratibu wa Wash United nchini Tanzania Ndugu Femin Mabachi alisema “Kupitia mpira wa miguu na kwa kushirikiana na TFF, tunaweza kutunza mazingira na usafi ‘salama’ na kuongeza uwiano katika kushughulikia mambo haya katika jamii yetu.
Taifa Stars Kuongoza mpango wa Wash United
Kwa kuungana na Wash United, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litakuwa limejiunga na zaidi ya mastaa 100 wa mpira wa miguu kama Didier Drogba, Michael Ballack, Arjen Robben, Bayern Munich, Taasisi za Real Madrid na ile ya Barcelona na pia zaidi ya wananchama 30,000 wa Wash United duniani kote. Nahodha wa Taifa Stars Juma Kaseja atawaongoza wachezaji wenzake kuwa washiriki kwenye mpango huu wa Wash United na kushiriki katika kampeni nchini Tanzania na duniani kote. Zaidi ya yote wachezaji wa timu ya Taifa watashiriki katika shughuli za mchezo wa mpira wa miguu mashuleni zitakazofanyika hapa nchini zitazokuwa zikiendeshwa na taasisi hizi.

Friday, November 16, 2012

WACHEZAJI 20 WALIOITEKA ULAYA KWA KUZISAIDIA TIMU ZAO




Kabla ya kuwataja wachezaji bora 20 ambao wameiteka Ulaya, napenda kuthamini mchango wa wachezaji hawa katika timu zao Yaya Toure, Xavi, Mario Gotze, Wayne Rooney, na Hazard. Hawa wamekuwa kwenye viwango bora kabisa msimu huu huku wakiziwezesha timu zao katika kupata matokeo bora.

Frank Ribery (20)

Mfaransa huyu amekuwa akijitolea kila kitu kwa ajili ya klabu yake ya Bayern Munchen. Licha ya matatizo yake ya kugombana na winger mwenzake wa Bayern, Arjen Robben mara kwa mara, Ribbery amekuwa bora mara zote anapoingia ndani ya uwanja. Hivi karibuni Ribbery alikaririwa akisema kwamba anaipenda Bayern kuliko timu ya taifa ya nchi yake, Ufaransa. Ribbery anashika nafasi ya 20 katika viwango hivi.

Edin Dzeko (19)

Amekuwa akitokea pale anapohitajika. Edin Dzeko amekuwa bora zaidi msimu huu hasa pale anapotokea benchi, watu kama Edin huitwa Super Sub. Yeye ndiye mtu ambaye amekuwa akiipa matokeo mazuri Manchester City mara kwa mara pale inapoonekana kushindwa. Huku akiwa na kiatu cha ufungaji bora cha ligi kuu ya Ujerumani pia mchezaji bora wa wachezaji wa ligi kuu ya Ujerumani, Dzeko ameendelea kumuonesha Roberto Mancini yeye ni mchezaji wa aina gani. Dzeko amekuwa wa 19.

Demba Ba (18)

Huu ndio ulikuwa usajili bora wa msimu wa 2011/2012 kulingana na makocha wa timu za ligi kuu ya Uingereza. Baada ya Papiss Cisse kusajiliwa January, 2012, Ba alifunga goli moja tu, tangu msimu huu kuanza imekuwa kinyume chake, Cisse hafungi na Ba amerudi kuwa roho ya timu. Kama akiendelea na kiwango hiki Ba anaweza kuwa mfungaji bora wa ligi kuu ya Uingereza. Ba anashika nafasi ya 18.

Marco Reus (17)

Moja ya vipaji kutoka Ujerumani vinavyokuja kwa kasi ni huyu Marco Reus. Akisajiliwa kutoka Borussia Monchengladbach kuja kuziba pengo la Shinji Kagawa, Marco ameweza kushirikiana vyema na Mjerumani mwenzake, Mario Gotze pia mshambuliaji Lewamdowski katika kuiboresha timu ya Borussia Dortmund. Marco Reus ndiye mchezaji bora wa Ujerumani kwa mwaka huu, 2012. Reus anashika nafasi ya 17.

Thomas Muller (16)

Mchezaji bora kijana wa kombe la dunia, 2010. Baada ya kuwa akitokea benchi msimu uliopita wakati Mario Gomez alipokuwa katika kiwango cha juu. Thomas Muller amekuwa akitengeneza chemistry nzuri na mshambuliaji mwingine wa Bayern Munich, Claudio Pizzaro. Mara nyingi Muller amekuwa hatajwi sana midomoni mwa wapenda kabumbu lakini yeye amaandelea kutunza kiwango chake vyema na sasa yupo kwenye kiwango cha hatari. Amekuwa wa 16.

Klaas-Jan Huntelaar (15)

Wenyewe humwita Hunter, amekuwa akifananishwa na Ruud van Nistelrooy na Marco van Basten kutokana na jinsi anavyouchezea mpira. Kocha wa zamani wa Barcelona Louis van Gaal aliwahi kusema kwamba huyu ndiye mchezaji bora katika dimba la penalti. Tangu ajiunge na Schalke 04 akitokea Milan, Huntelaar amekuwa kwenye kiwango bora na ndiyo mhimili wa Schalke. Hivi sasa ana ushirika mzuri kabisa na Mholanzi mwenzake aitwaye, Ibrahim Affelay. Amekuwa wa 15.

Oscar (14)

Kipaji cha ajabu kutoka Brazil. Uwezo wa kumiliki mpira, nguvu, pasi na jinsi anavyojitoa uwanjani haipingiki kwamba Oscar atakuja kuwa moja ya wachezaji hatari sana katika timu ya taifa ya Brazil. Oscar ndiye mchezaji wa Chelsea anayeng’ara zaidi katika ligi ya mabingwa Ulaya msimu huu kuliko mchezaji yeyote mwingine ndani ya klabu. Goli la pili aliloifunga Juventus katika mechi yake ya kwanza ya ligi ya mabingwa Ulaya halitafutika kirahisi katika vichwa vya wapenzi wengi wa soka. Alipoulizwa atoe maoni yake kuhusiana na goli lile, kipa wa Juventus, Gigi Buffon alisema hivi, “Siwezi kusema ni vizuri kufungwa goli lakini ni vizuri kuwa sehemu ya goli bora kama lile. Hongera kwake”. Oscar ni wa 14.

Maroune Fellaini (13)

Mchezaji ghali zaidi wa klabu ya Everton. Huyu ndiye alikuwa gumzo zaidi wakati ligi ya Uingereza ilipokuwa katika wiki za mwanzo mpaka sasa. Akiwa ni mzaliwa Ubelgiji na asili ya Morocco, Maroune Abdellatif Fellaini amekuwa kiwango bora zaidi msimu huu kuliko msimu mwingine wowote katika maisha yake. Watu wengi wamekuwa wakiifuatilia Everton kwa sababu ya huyu mtu na yeye ndiye ubongo nyuma ya mafanikio ya Everton kwa msimu huu. Anazivutia klabu kubwa nyingi huku Chelsea ikiongoza mbio za kumnyakua, si ajabu kuona akihamia kwenye timu inayoendana na kiwango chake. Amekuwa wa 13.

Gonzalo Higuain (12)

Mtambo wa magoli kutoka mzaliwa wa Ufaransa. Huyu ndiye patna wa Cristiano Ronaldo katika kupasia mipira nyavuni pale Real Madrid kwa sasa. Mafanikio ya Gonzalo msimu huu yamechangiwa zaidi na kuumia na kiwango cha Karim Benzema kushuka. Katika siku za hivi karibuni Higuain amekuwa akishirikiana vyema na Lionel Messi katika kutengeza nafasi za magoli katika timu ya taifa ya Argentina. Amekuwa wa 12.

Luis Suarez (11)

Mchezaji ambaye amekuwa akiandamwa na mikasa ya kutosha tangu adake mpira uliokuwa ukiingia nyavuni katika mechi ya robo fainali ya kombe la Dunia pale Afrika Kusini dhidi ya timu ya Ghana. Pamoja na mikasa mingi kuwa upande wake Luis Suarez hajashuka kiwango na msimu huu tofauti na misimu mingine amekuwa akifunga magoli mengi ingawa timu yake ya Liverpool bado mambo hayajawa mazuri. Ndiye mchezaji anayeng’ara zaidi kwa majogoo wa jiji. Amekuwa wa 11.

Andrea Pirlo (10)

Ule usemi wa ng’ombe hazeeki maini uhalisia wake huonekana hapa. Watumiaji wa mvinyo humfananisha Andrea Pirlo na kinywaji hicho, kadri kinywaji kinavyozidi kukaa ndivyo ubora wake unavyoongezeka. Kadri umri wa Pirlo unavyoongezeka ndivyo kiwango chake kinavyoongezeka. Huyu ndiye chachu hasa ya mafanikio ya Juventus katika kumaliza msimu uliopita bila kufungwa na Italia kufika kwenye fainali ya kombe la Ulaya. Amefunga 10 bora.

Juan Mata (9)

Pamoja na kwamba Didier Drogba ndiye aliyeiwezesha Chelsea kushinda kombe la FA na lile la ligi ya mabingwa Ulaya kwa kiasi kikubwa katika mechi za fainali, Mata ndiye aliyekuwa mchezaji bora wa Chelsea kwa msimu uliopita. Msimu uliopita Mata alikuwa kwenye kiwango bora lakini sasa hivi amekuwa zaidi ya alivyokuwa msimu uliopita. Juan Manuel Mata Garcia anaendelea kuwa mchezaji bora wa Chelsea mpaka sasa. Huyu ndiye mchezaji bora wa ligi ya Uingereza kwa mwezi wa 10, mwaka 2012. Amekuwa wa 9.

Bastian Schweinsteiger (8)


Roho ya timu ya Bayern Munchen, akifunga magoli na kutoa pasi za mwisho za kutosha. Basti kama marafiki zake wanavyomwita ametengeneza chemistry katika timu ya Bayern hasa katika sehemu ya kiungo ya timu. Uwezo mkubwa wa kukota aliokuwa nao, pasi kali ‘zenye macho’ , uwezo mkubwa wa kukaba, uwezo mkubwa wa kumiliki mpira, na mwisho wa yote ni uwezo wake mkubwa wa kupiga mipira iliyokufa unamfanya awe mchezaji wa kipekee. Schweinsteiger ana nafasi kubwa ya kuingia kwenye FIFA FIFPro World XI ya mwaka huu. Amekuwa wa 8.

Andres Iniesta (7)

Mchezaji bora wa Ulaya kwa mwaka 2012, siku zote amekuwa kwenye kiwango bora. Iniesta kwa sasa yupo kwenye kiwango cha juu cha soka katika maisha yake. Yeye ndio mtu anayeng’aa zaidi kwenye timu yenye vipaji lukuki ya Spain. Sababu ya Iniesta kushika namba 7 katika listi hii ni kutokana na makali kupungua kidogo tangu mashindano ya Ulaya kuisha pia ni kutokana na watu waliopo juu yake viwango vyao kuongezeka kwa kiasi kikubwa. Kitu ninachoamini ni kuwa lazima Iniesta atajwe kugombania FIFA Ballon d’Or katika wale watu watatu wa mwisho.

Stephan El Shaarawy (6)

Mashabiki wake humwita ‘The Pharaoh’ kwa sababu amezaliwa na wazazi wenye asili ya Misri pale Savona, Italia. Huyu ndio nguzo ya Milan kwa sasa katika upachikaji mabao baada ya Zlatan Ibrahimovic kuondoka. Akivaa jezi yenye namba ya mwaka aliozaliwa, # 92 (1992), na ikiwa ndio kwanza katimiza miaka 20 juzi tu mwezi October, Firauni huyu amekuwa tishio sana kwa mabeki wa timu pinzani zinazopambana aidha na Italia ama A.C Milan. Nimempa namba 6 kwa sababu anastahili.

Zlatan Ibrahimovic (5)

Mtaalamu huyu mwenye mkanda mweusi wa mchezo wa karate amekuwa mkubwa kuliko ligi ambayo anacheza ndani yake. Tangu kuhama kutoka AC Milan na kutua PSG mambo yamekuwa rahisi sana kwa Ibracadabra. Kutokana na aina yake ya mchezo na kipaji chake watoto wa mjini wanakwambia, Ibra sio wa leo wala kesho wakimaanisha, Zlatan ataendelea kung’aa kwenye medani nzima ya soka kwa kipindi kirefu kidogo mpaka pale atakapoamua kustaafu. Huyu ndiye mfungaji anayeongoza katika ligi kuu ya Ufaransa kwa sasa. Tarehe 14 mwezi huu wa 11, 2012, goli la 4 aliloifunga Uingereza linasemekana kuwa goli la karne. Zlatan Sefik Ibrahimovic ni namba 5.

Radamel Falcao (4)

Ukiwa ni msimu wake wa pili katika ligi kuu ya Spain, Radamel Falcao ameibuka ghafla na kuwa gumzo katika bara lote la Ulaya. Falcao ndio mpinzani mwenye nguvu wa Ronaldo na Messi ambaye alikuwa akinghojewa katika kugombania kiatu cha dhahabu cha ligi kuu ya Spain. Akiwa tayari ameshinda kombe La UEFA akiwa na Porto ya Ureno pamoja Athletico Madrid aliko sasa ambako pia majuzi alishinda UEFA Super Cup pale alipoichabanga Chelsea goli 3 peke yake katika ushindi wa 4-1, Falcao ameendelea kuwa mchezaji wa kutumainiwa katika kila timu anayoitumikia. Falcao anastahili nafasi ya 4.

Robin van Persie (3)

Huyu ndiye mchezaji bora wa ligi kuu ya Uingereza kwa msimu uliopita, 2011/12, huku akiwa hana muda mrefu tangu ajiunge na mashetani wekundu akitokea kwa mahasimu wao wakubwa, Arsenal, RvP amekuwa ndio nguzo katika mashambulizi ya United msimu huu akiwa ameifungia goli 8 tayari na pasi za magoli 3 kwenye ligi kuu, van Persie ameendelea kuwa moja ya nembo za ligi kuu ya Uingereza kwa wakati huu. Hivi karibuni wakati Sir Alex Ferguson alipochaguliwa kuwa kocha bora wa mwezi October alimshukuru Robin kwa kutoa mchango mkubwa sana katika tuzo yake hiyo. Robin van Persie anakuwa wa 3 nyuma ya Ronaldo na Messi.

Cristiano Ronaldo (1)

CR7 kama anavyopenda kujiita. Yeye kaiteka dunia ndani ya uwanja na nje ya uwanja. Cristiano Ronaldo ni moja ya wachezaji adimu sana katika kizazi hiki cha leo. Uwezo wake wa kupasia ‘kamba’ umekua ukiongezeka siku baada ya siku. Ronaldo ndiye mchezaji anayetawala vichwa vya habari vya magazeti kila kukicha pamoja na ‘fundi’ mwingine kutoka Italia aitwaye Super Mario Balotelli. Mtupia mabao huyu ambaye ndio anaongoza magoli katika ligi ya mabingwa Ulaya msimu huu akiwa na goli 5 katika mechi 4 alizocheza amekuwa akisifika kwa bidii yake ya kujituma mazoezini na kwenye mechi. Kutokana na yote haya Cristiano pia anashikilia namba moja pamoja na Leo Messi. Ronaldo ndiye mchezaji bora wa mwaka huu, 2012 wa Goal.com, mtandao wa soka wenye heshima kubwa zaidi.

LIONEL Messi (1)

Ameendeelea kuiteka dunia kutokana na kipaji chake ambacho kinawashangaza wadau wengi wa soka. Huku akishikilia rekodi ya kufunga magoli mengi duniani katika msimu mmoja, magoli 73 katika msimu wa 2011/12 na magoli 76 mpaka sasa kwa mwaka huu akiwa nyuma ya Gerd Muller, urafiki wa Messi na nyavu umezidi kudumishwa siku baada ya siku ikumbukwe kwamba kila goli analofunga Messi kwa hivi sasa ni rekodi katika klabu ya Barcelona kwa sababu yeye ndiye mfungaji bora wa klabu kwa wakati huu. Kwa sasa mchezaji huyu bora wa dunia yuko katika kiwango sawa na mshindani wake wa karibu wa siku zote, Cristiano Ronaldo ndio maana wote wamekuwa vinara kwa kushikilia namba moja.



Imeandaliwa na Stephen Samuel, napenda kutumia jina la PodoBest zaidi.


Twitter: @iPodoBest