Wachezaji wa timu
ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 ya Serengeti Boys wakishangilia bao
lililofungwa na Mudathiri Yahaya Abbas wakati timu hiyo ilipopambana na Congo
Brazzaville katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika kwa
vijana wenye umri huo, zitakazofanyika mwakani nchini Morocco. Serengeti Boys imeshinda 1-0. (Picha zote na Habari Mseto Blog)
Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Jacob Michelsen na msaidizi wake Jamhuru Kihwelo wakipongezana baada ya mchezo kumalizika.
Mshambuliaji
wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 ya Serengeti Boys, Hussein
Twaha akiwatoka mabeki wa timu ya Congo Brazzaville katika mchezo wa
kufuzu kwa fainali za Afrika kwa vijana wenye umri huo zitakazofanyika
mwakani nchini Morocco. Mchezo huo ulifanyika leo kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam. Serengeti Boys imeshinda 1-0.
Mshambuliaji wa timu ya Srengeti Boys, Faridi Mussa (katikati)
akiwania mpira huku beki wa Cpngo Brazzaville, Tmouele Ngampio akijaribu
kumzuia. Kulia ni Golipika wa Congo Brazzaville, Ombandza Mpea akijaribu
kuokoa hatario langoni mwake.
Waamuzi wa mchezo huo wakitoka baada ya kwisha kwa pambano hilo
Mshambuliaji wa Serengeti Boys, Tumain Baraka akichuana na beki wa Congo Brazzaville, Okombi Francis
Heka heka katika lango la Congo Brazzaville
Wachezaji wa Serengeti Boys, Hussein Twaha (shoto), Joseph Lubasha na
Selemani Hamis Bofu wakibadilioshana mawazo wakati wakitoka mapumziko
Tusubiri kichapo tu kwaoo sioni kama tutapita
ReplyDelete